Somo hili nimeamua kulitoa wazi wazi ili watu mpone imani
zenu sababu wapo watumishi ambao kwa majina kama nabii, mchungaji, mwalimu,
mwinjilisti, mtume na wana makanisa na wanatumia jina la YESU vile vile lakini
watu hamjaweza kuelewa ni wa kweli au wa uongo. Amenituma YESU niufichue kila
aina ya uovu ambao unatumika kuwapiga upofu watu wasione katika macho ya roho.
Hapa nitaelezea katika aina za mavazi za maagano ambayo utaona mtumishi hawezi
kuhubiri bila kuvaa mavazi ya aina hiyo hiyo au rangi moja kila akihubiri,
unapoona hayo uelewe ni maagano. Maagano haya niliyaona katika ufalme wa
shetani na nilionyeshwa na YESU ili nitambue njia zao sababu siyo YESU WA
NAZARETI yeye ndiye anayepanga lazima uvae nguo Fulani wakati wa kuhubiri na za
aina moja tu. Na ili shetani ampe miujiza ni lazima avae nguo hizo ambazo
nitakuelezea.
KWA
WATUMISHI WANAWAKE.
1.
Atavaa nguo za suruali na shetani haijalishi
ataishona kwa staili ya kike, na ni lazima avae, wewe chunguza utaona na akivua
tu tayari amevuruga agano na shetani hivyo hata mpatia miujiza wala mengineyo,
na cheni miguuni na pete kwenye vidole au mavazi ya kuonyesha mabega na mgongo
(mavazi ya Yezebeli).
2.
Anakuwa anavaa kofia kwa wengine kila
anaposimama madhabahuni badala ya kuvaa kitambaa cha kawaida.
3.
Anaweza akawa amevaa nguo nyeupe kila anapokuwa
katika ibada siku zote, miaka yote.
4.
Siku zote hawa watumishi wa jinsi hii ndio wanao
waoa wanaume na wanaume wao hawana nguvu yeyote juu yao hii ni sababu ndani
yao, yapo majini yanamzidi nguvu za kiutawala mwanaume.
5.
Wanajichubua sana mpaka imepitiliza.
6.
Hupenda kuvaa kama wanaume sababu katika
ulimwengu wa roho wanasagana na pepo la kike.
KWA
WATUMISHI WANAUME.
1.
Wanavaa nguo moja au suti nyeupe mara nyingi na
hupenda kujichubua na ukiona anajichubua ni sababu yeye katika ulimwengu wa
roho amekua na jini na yeye ni shoga yaani shangazi, vaa herein maskioni.
2.
Wanakuwa na perfume ya aina moja, akijipulizia,
ukipita mbele yake ile harufu ina nguvu za mapepo yanakuangusha chini na watu
wanaona ni nguvu za MUNGU kumbe ni uchawi.
3.
Wana makaburi katika nyumba zao wanayoita majina
ya watakatifu na huwaeleza watu wakasujudie hapo.
4.
Wote ni wazinzi wawe wakike na wakiume.
5.
Akipuliza mike watu huanguka chini, ile mike ni
nyoka siyo mike, na ile pumzi ni pumzi ya shetani iliyopo ndani yake anawavuvia
watu, na mavazi yenye sura za magamba ya nyoka au viatu vyenye magamba na pochi
na nguo.
6.
Hupenda kujiremba kama mwanamke hii ni sababu
katika ulimwengu wa roho ni mke wa jini.
NOTE:
Mavazi haya na tabia hizi unapoziona mtumishi anazifanya
elewa siyo wa MUNGU wa kweli ni wa miungu ya shetani ndio mkristo wa uongo.
NABII HEBRON.