Sawa sawa na neno la MUNGU katika kitabu cha Yohana 17:17,
inaelezea kuhusu neno la MUNGU la kweli ndilo litakalo. Mamilioni ya watu
katika ulimwengu wote wamepotea na kupigwa upofu wasijue kweli ya neno la MUNGU
na ndiyo maana wanakubali maneno yasiyotokana na biblia na kuyapokea na kama
ukiyapokea ina maana hayo siyo maneno ya MUNGU ya kweli ni ya uongo na kama
uliyakubali tayari udhihirisho wa kutakaswa na neno la MUNGU haitokei milele
sababu tayari inakuwa ni kinyume na hao watendao maneno tofauti na biblia hawa
ni adui wa YESU 100% na ndio mpinga kristo, sababu ya kuitwa ni wapinga kristo
ni kuwashirikisha wanadamu mafundisho ya uongo wakichanganya na biblia.
Sasa mfunguke mataifa yote, YESU ni mzuri na yeye ni mkweli milele
na ahadi zake ni kweli tupu, akiwa pamoja na BABA yake na ROHO MTAKATIFU wao
wote wanasema kweli, na mpaka sasa wapo na umoja na hawajagombana na
hawatagombana milele au kutengana. Hivyo na watu wote wanatakiwa wafuate umoja
wao na kweli yao ndipo watafika mbinguni. Amenituma niwafungue macho yenu na
akili zenu wale mliofungwa na hamjijui; mmebakia kujitia moyo na kusimama na mstari
huu wa Yohana 17:17 wakati nyie ni waongo na siyo wa kweli, kivipi?
Ø Kila anayeshiriki
au kubatiza ubatizo wa maji ya kikombe au kubatizwa kwa jina la mchungaji au
katika kisima, usitegemee kuwa neno la MUNGU litawatakasa, sababu nyie
mmeshiriki uongo, tafuta hakuna katika neno la MUNGU haya yameruhusiwa.
Ø Mnaoabudu
sanamu, kufanya ibada za wafu, kuabudu kina Mathayo, Musa, Eliya na Maria na wengineo.
Mjue mmejichafua na mnaharufu mbaya mbele za MUNGU na mnajipachika harufu ya
dhambi Isaya 45:20, Isaya 44:6-9. Msitegemee maombi yenu yatasikiwa na MUNGU
aliye hai wala damu ya YESU iwatakase, wala neno la MUNGU liwatakase, hata
mnavyokariri na kusoma biblia na ungali hayo unayatenda ujielewe umekuwa adui
wa MUNGU hivyo utarajie mapigo kutoka kwake na hukumu ile siku ya mwisho, au
ukitaka kupona uokoke sasa na usishiriki hayo yasiyopo katika neno la MUNGU na
kweli yake ikutakase uwe na akili timamu.
Ø Kanisa likichangisha
pesa au harambee msitegemee kubarikiwa sababu neno la MUNGU lililokweli
haliruhusu kuchangisha au kuomba omba na kumfanye YESU ni masikini, hata kama
mnaelezwa mnamjengea MUNGU kanisa, fuatilia neno lake. Usijisumbue kwa kila
jambo bali ombeni na yeye atafanya. Sasa mmeacha kuomba ili MUNGU ajitukuze
peke yake mnageuka kumuaibisha. Hii ni dhambi na siyo neno la MUNGU, habari za
michango makanisani (hayo ni maneno ya shetani).
Ø Ukipewa
huduma yeyote ya kiroho ukalipia pesa kama vile hospitali ya kibinadamu. Na hata
anayekudai pesa hizo ndio akuombee, elewa hilo silo neno la kweli kutoka kwa
MUNGU hivyo hautakaswi na MUNGU bali unanajisiwa na maneno ya uongo. Sasa funguka
maana wengi wanafarijika na neno hili, lakini wapo katika kambi ya kanisa au
watumishi wanaosema au kutenda maneno ya uongo.
Nawaeleza hautakaa utakasike sababu hayo myatendayo siyo neno
la kweli bali mnaposhiriki unajijengea njia ya jehanamu. Fuata neno kama
lilivyo usibadilishe lolote na hata kanisa ambalo linabadilisha neno la MUNGU
uelewe hilo ni pando la shetani lipo hapa ulimwenguni kwa lengo la shetani au
mpinga kristo na ndiyo maana lipo kinyume. Ingekuwa lipo na limeletwa na YESU
lingefuata kweli yake na kuitenda peke yake.
Na wengine wanasema shika neno au tenda neno, hili ni neno
zuri, ila uchunguze pia isiwe ni shika neno kwa mdomo halafu kimatendo ni
unafiki kivipi? Mfano unabatizwa kwa jina la kiongozi huyo badala ya jina la
YESU, je nikuulize huku ndiko kushiriki neno? Au ni kulitupa neno na kupokea
uongo? Wakristo mfunguke ufahamu zenu, sasa hivi bwana mchunguze iwe ni Nabii,
Mtume, Mchungaji, Mwinjilisti, mwalimu wapo wenye neno la kweli ila 95%
wamechanganya maneno ya uongo, na hadi iwe hivi ina maana wametekwa na shetani
full sababu ya kukataa kumsikiliza YESU atakavyo. Haiwezekani hivi hivi mtu kwa
akili zake kama hajatekwa na shetani aibadilishe biblia na kutenda tofauti,
hiyo ni dalili kuwa ndani yake hata ROHO MTAKATIFU hayupo na ndiyo maana kazi
yao ni kusaliti neno la MUNGU na kusema kinyume. Na waumini mnatengenezewa na
njia ya jehanamu pasipokujua, toka utengwe na huko uokoke leo hii ili
akusafishe na kuyaondoa mapando ya uongo.
SALA YA TOBA:
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU UNITAKASE MOYO
WANGU NA UUONDOE UONGO WA MANENO YA UONGO NILIYOINGIZIWA KWA KUFUNDISHWA
MAKANISANI, BILA KUJUA. UZITEKE NA AKILI ZANGU ILI NISITEKWE TENA, UNIANDIKE
JINA LANGU KATIKA KITABU CHAKO CHA UZIMA WA MILELE UNIONGOZE SASA MAHALI SALAMA
ULIPO WEWE.
NABII HEBRON.