Mathayo 15: 8-9
Neno la MUNGU linasema “watu hawa huniheshimu kwa midomo;
ila mioyo yao iko mbali nami, nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho
yaliyo maagizo ya wanadamu.”
Watu wengi katika ulimwengu wote mahali hapa wanashindwa
kupaelewa na kupambanua, ila sasa
ufunguke ufahamu wako na ROHO MTAKATIFU wakati unasoma mafundisho haya
ya Nabii Hebron atakufunulia zaidi uelewe ili upone roho yako na wewe utoke
katika mfumo wa kusikiliza mahubiri ambayo unasikiliza sauti ya mtu badala ya
sauti ya MUNGU. Ukisoma katika injili ya Mathayo 15:8-9 inaelezea vizuri kabisa
na maneno haya ni YESU mwenyewe ndiye aliyeyatamka, na sababu ya kuyatamka ni
hivi, katika kipindi kile pia walikuwepo watumishi wanaohubiri habari za MUNGU
ila walikuwa ni wanafiki (Mafarisayo na Masadukayo) katika midomo yao huonyesha
wanampenda MUNGU ila ndani ya mioyo yao hakuna kitu na kama hakuna kitu ina
maana wanaabudu bure na hata hao wanaosikiliza hawatapokea kitu katika mioyo
yao bali yataishia katika midomo ya wasikilizaji tu na mafundisho hayo
hayatendi lolote katika mioyo ya watu na ndiyo maana watu maisha yao katika
makanisa ni mabaya na ni ya vifungo tupu vya shetani wala hakuna mpenyo.
Japo asubuhi, mchana na hata usiku kila mahali ni mahubiri
tu na mikutano mingi lakini utashangaa watu hawabadiliki kiroho wala kimwili,
hii ni sababu hao wanaohubiri kwanza hawampendi MUNGU katika mioyo yao na
katika mioyo yao YESU hayupo na kama hayupo mafundisho yote wanayoyahubiri
sehemu mbali mbali yote ni feki na ndiyo mbegu zilizomwagwa katika mwamba
barabarani, na siyo katika udongo mzuri. Watumishi wengi 95% all over the world
ni wapigaji wa makelele tupu kupitia sauti za vinywa vyao na siyo sauti ya
MUNGU itokayo katika kinywa au ROHO MTAKATIFU. Ingekuwa kweli ni sauti ya MUNGU
ndiyo itokayo katika vinywa vyao basi hakika katika ulimwengu huu maovu
yangekuwa hakuna, na shetani angekuwa hajawapata watu wengi kama alivyowateka
sasa.
Ukiangalia Television mbali mbali au hata Radio nyingi za
injili tena ni 24 hours zinahubiri na kufanya maombezi, ingekuwa kweli hao wanaohubiria
katika hivi vyombo ndani yao ni YESU kweli yupo ndiye anayeongea kupitia hicho
kinywa hakika kila mtu angepona hapo hapo roho yake na kupokea uponyaji halisi
kutoka kwa MUNGU. Lakini cha ajabu watu wanalala hata na radio ikihubiri usiku
kucha wakitegemea ile sauti inayoongea ni ya MUNGU na itawafungua na kuwaponya,
cha ajabu ndiyo mapepo yanawanyonga kisawa sawa, sasa jiulize wewe peke yako
kwa ufahamu wako inawezekanaje wewe unafungua TV na Radio usiku kucha au
unalala karibu na TV ili upate maombi, lakini shida ipo pale pale? Jibu hayo ni
makelele tu mbele za MUNGU na pia wewe mwenyewe, na hii ni sababu wamejiita au
wanatafuta pesa kwa kutumia jina la YESU
na kumbe hao ndio wasaliti wakubwa wa YESU na kwa kutumia midomo yao watu waliwaamini
pasipokujua kupitia sauti za maneno ya vinywa vyao wakijua ni sauti ya MUNGU.
NOTE:
Ø Nitakueleza
kwa ufupi ufunguke kuhusu kujua sauti ya MUNGU na sauti ya midomo ya watu
wakati wakihubiri. Kwanza kabisa ukiona kinywa cha mtumishi kinataja michango
tu, harambee, mapatina uelewe hiyo siyo sauti ya MUNGU ni sauti yake peke yake.
Ø Ukifundishwa
kuabudu sanamu, na ufundishwe ubarikiwe ukiwa mtu mzima na ubatizwe ubatizo wa
maji ya kikombe au ubatizwe katika maji ya kisima au ubatizwe kwa maji mengi
halafu kwa jina la mchungaji, Mtume au Nabii (elewa hicho kinywa chake na hata
mafundisho yake yote hayatoki katika kinywa cha MUNGU na hamtapona roho zenu
zaidi mtaangamia roho zenu na kutumikishwa kiroho na kimwili), sababu
mtatumaini hayo maneno ya uongo na wewe ukijua kuwa upo sahihi kumbe
umeshatekwa na shetani na katika ulimwengu wa roho na kupigwa upofu usijielewe,
leo funguka.
Ø Ingekuwa
mahubiri yanayohubiriwa na watumishi mbali mbali kwa Television au radio ni
sauti ya MUNGU ndiyo itokayo katika vinywa hivyo kila anayeangalia au
kusikiliza angepona pale pale na kubadilika na sababu ni maneno ya wanadamu
ambayo ni sauti za watu, hivyo sauti hizo na zenyewe zinabakia katika midomo ya
wasikilizaji tu na haziingii katika mioyo. Mpaka sasa umepata jibu, uwe makini
sana katika makanisa na Television na Radio hao wanaohubiri ndani yao hakuna
sauti ya MUNGU bali ni sauti zao, na wewe umeumbwa ili usikilize sauti ya MUNGU
na iingie ndani ya moyo wako. Na kama unafundishwa sana na hauelewi au
hayaingii katika moyo wako uelewe hayo ni maneno yenye sauti ya mtu na siyo
maneno yenye sauti ya MUNGU, na hii inaonyesha kuwa hata watu ambao wameongozwa
sala za toba na watumishi wa jinsi hii ina maana hata hizo toba ni toba za
maneno ya midomo na hata mnaoongozwa hizo toba wokovu unakuwa ni feki tu au dini
tu pale pale na huu ndio wokovu wa mazoea umetokana na sala za toba za sauti za
watu na siyo sauti ya MUNGU.
Ø Maombezi
mengi yanayoongozwa sehemu mbali mbali ni watu wanapiga tu makelele wenyewe
sababu msingi ni sauti za watu katika midomo siyo ROHO MTAKATIFU ni kuchaji
watu pesa tu. Kila hitaji mtu analotaka aombewe leta pesa kwanza, ukiona haya
uelewe hapo ni ZERO, ni maombi ya shetani. Au ukute mtumishi au Nabii anachaji
watu pesa ndio akuone wewe PRIVATE elewa huyo na hicho kinywa chake sicho kinywa
ambacho sauti ya MUNGU inakitumia bali ni nguvu za giza au mizimu au freemason.
Ø Katika ibada
mbali mbali ule mwisho utasikia waumini wanaelezwa neema na iwe na wewe, sasa
ufunguke mbona unatamkiwa neema iende na wewe siku zote lakini matokeo yake
hambarikiwi ni nuksi, balaa na mikosi na kuteseka tu. Elewa kuwa hayatokei hayo
sababu umesikia sauti ya mtu na siyo sauti ya MUNGU ndiyo uliyoisikiliza kutoka
katika kinywa chake, ulisikiliza na kupokea maneno na wewe ukayapokea katika
mdomo wako.
NOTE:
YESU anarudi wakati wowote, amenieleza niwaeleze mtubu,
mumrejee yeye, anajua wengi mnampenda ila sala za toba mlizoongozwa hazikuwa za
sauti ya MUNGU bali ni za sauti za watu. Hivyo sala za toba zikawa ni bure na
ndiyo sababu wokovu umekuwa kama dini, na dini siyo wokovu.
TUBU:
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU, NAKUREJEA WEWE UWE
BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA
WA MILELE NA UNITENGE NA MAHUBIRI YALIYO NA SAUTI ZA WATU, MIMI NATAKA KUSIKIA
INJILI YENYE SAUTI YAKO TU, NA AKILI ZANGU UZISHIKE WEWE PEKE YAKO
NISISHIKILIWE POPOTE. NAMKATAA SHETANI NA KAZI ZAKE ZOTE NA MAFUNDISHO YA
UONGO.
AMEN.
NABII HEBRON.