2 Wafalme 23:15
Katika ulimwengu huu kuna aina mbili ya madhabahu ipo
madhabahu ya MUNGU aliye hai na ipo madhabahu ya miungu au ya shetani na
madhabahu hizi huwa katika ulimwengu wa roho na katika mwili madhabahu hizo
hukaa ndani ya mwanadamu na mwanadamu huyo huwa ni kuhani. Madhabahu hizi ili
ziingie ndani ya kuhani huyo kwa mfano madhabahu ya MUNGU aliye hai ili iingie
ndani ya kuhani ni mpaka MUNGU peke yake aamue na hivyo hivyo na madhabahu ya
shetani, mpaka shetani aamue kuingia kwa kuhani katika kanisa, na kwa shetani
katika madhabahu yake ipo njia nyingine, ni pale mtumishi anapojiita, kujifanya
au kuwa freemason, mchawi au kuwa mtumishi wa mshahara au atakapomsaliti YESU,
hapo ndipo shetani huipanda madhabahu yake na ndipo wengi mnaona watumishi
wengi ni wachawi hii ni sababu ndani yao ipo madhabahu za shetani (miungu) na
hata wewe muumini kama unaongozwa au kusali katika kanisa la jinsi hiyo au mtumishi
wa jinsi hiyo uelewe na wewe ndani yako unapandikiziwa pasipo kujijua maana
jinsi alivyo kuhani ndivyo na picha ya kanisa lilivyo.
A.
MADHABAHU YENYE USHIRIKA NA MUNGU ALIYE HAI
§ Hii ni
madhabahu ya MUNGU mwenyewe inayotenda kazi ndani ya mtumishi, nitaelezea kwa kifupi upate picha. Kwanza haionekani kwa
macho ya nyama na damu ila kitakachokujulisha ni madhabahu ya MUNGU aliye hai
inatenda kazi, chunguza tabia za kuhani, kanisa liwe lina wokovu wa kweli siyo
wokovu halafu kanisa linachangisha.
§ Lazima
kuhani awe ameitwa na MUNGU na pia asiwe msaliti atende yaliyo ya MUNGU tu.
§ Neno la
MUNGU halibadilishwi, watu wanafunguliwa pasipo kutoa pesa au kuchajiwa malipo
yeyote kama vile katika hospitali za kibinadamu.
§ Lazima
ubatizo wa maji mengi na yanayotembea ndiyo yanayotumika kubatiza, hakuna
ubaguzi kwa watu wote ni sawa. Majibu ya waumini wanayapata kila waombapo
katika madhabahu ya kuhani huyo. Kanisa hilo halichangishi pesa au harambee,
bali hujitegemea peke yake maana madhabahu ya MUNGU aliye hai inajibu kwa moto,
na madhabahu ya MUNGU milango ya kuzimu hailiwezi milele. Madhabahu ya MUNGU
ina nguvu kuliko madhabahu zote za aina yeyote ile.
2 Wafalme 23:15 Neno linasema “tena zaidi ya hayo, ile
madhabahu iliyokuwako Betheli, na mahali pa juu alipopafanya Yeroboamu, mwana
wa Nebati, aliyewakosesha Israeli,madhabahu hiyo aliibomoa; na mahali mahali pa
juu alipateketeza, akapaponda-ponda hata pakawa mavumbi, akaiteketeza ile
Ashera.”
Katika neno hili utaona kuwa zilikuwepo madhabahu za
kuwakosesha watu wa Israeli ili wapotee na hata leo zimejaa na madhabahu hizi
zinaongozwa na mungu mke na ndizo zilizopo kwa idadi kubwa katika ulimwengu huu
ili kuwaangamiza watu roho zao ili ule mwisho wasimuone MUNGU, maana kazi ya
madhabahu ya MUNGU ni kuhakikisha watu wanavunwa na MUNGU na madhabahu ya
shetani ni kuhakikisha inawavua watu wapelekwe jehanamu, na jinsi ifanyavyo
kazi haitaitwa madhabahu ya shetani, ili msifunguke ila siri anakuwa anaijua
kuhani peke yake, ila nakufundisha uelewe vizuri maana watu wanashindwa
kutofautisha madhabahu ya kweli na mfu.
Sababu wapo watumishi ambao kweli baadhi yao waliitwa na
MUNGU na watu mnayajua hayo ila mbeleni walimgeuka MUNGU wakawa mbwa mwitu
(ninamaanisha madhabahu ya MUNGU ikaondoka na shetani ndiyo akaingia na
kuendeleza hilo kanisa pasipo watu kuelewa, ila wengi mtaona sasa tofauti. Kwanza
nguvu za MUNGU zinaondoka, shida zitaanza kujaa kwa waumini, hakuna uponyaji,
inabakia ni story tu na kupoteza muda. Ukiona hivyo ondoka maana uelewe tayari
MUNGU ameondoka na MUNGU akiondoka ni nani anayebakia? Jibu ni shetani.
B.
MADHABAHU ISIYO NA USHIRIKA NA MUNGU ALIYE HAI
Madhabahu hii kwanza zipo za aina mbili lazima uelewe. Madhabahu
ya kwanza uelewe kimwili ni ya waganga wote wa kienyeji hawa wanazo madhabahu
za shetani, pili katika kanisa na inakuwa ipo ndani ya mtumishi. Kiongozi na yeye
anawaambukiza wote wanakuwa katika ushirika na shetani, jinsi alivyo kuhani
ndivyo na kanisa lake lilivyo!!!
§ Kwanza wanabatiza
ubatizo wa maji ya kikombe, na wengine wanabatiza ubatizo wa maji mengi ila
kuhani anakubatiza kwa jina lake halafu anachanganya kwa jina la BABA na MWANA
na ROHO MTAKATIFU. Hii ni madhabahu ya miungu na inaongozwa na mungu aina ya
mungu mke.
§ Kanisa linaloabudu
sanamu, kufanya ibada za wafu, kubatiza watoto wadogo, kubariki watu wazima
kinyume na biblia, haijalishi wanaimba nyimbo za kumsifu YESU, uelewe yupo yesu
wa kuzimu na wanapotenda hayo uelewe ni kristo wa uongo ndio anainuliwa na
miungu. Madhabahu hiyo haina ushirika na MUNGU aliye hai ni ya miungu (mke).
§ Lazima iwe
na mapartiners na lazima ili ufunguliwe lazima utoe pesa kama vile kwa mganga,
wapo walioambiwa MUNGU anataka damu ya kuku au pesa kwanza, na wewe unao akili
ukisoma neno la MUNGU linasema nimewapa bure, toa bure, sasa uelewe hiyo ndiyo
formula ya madhabahu ya MUNGU aliye hai hachaji pesa sababu damu ya YESU
ilishalipa kila kitu. Ila ya shetani hakuna bure na zaidi hauponi unawekewa
pepo lingine la kupona tu kwa muda fulani shida inakurudia pale pale, belzebuli
hawezi kumfitini belzebuli mwenzake.
§ Katika kanisa
hilo waumini humuabudu kuhani kama yeye ndiye MUNGU na hata kuimba nyimbo za
kumsifu kuhani ndani ya kanisa. Ukiona hayo elewa ni shetani ndiye atendaye
kazi.
§ Hakuna majibu,
uponyaji, ni shida tupu. Waumini wanafunga na kuomba hakuna majibu, hiyo ni
dalili hiyo madhabahu ni ya baali. Tazama kipindi cha Eliya na baali, madhabahu
ya Eliya ikajibu lakini ya baali haikujibu na ndivyo ilivyo leo hii makanisa
mengi yanaabudu baali.
§ Inafanya
biashara, kuhani ni mchawi au anaongozwa na mizimu, kuhani ni mzinzi ni mlevi,
anavunja ndoa za waumini na matendo ya ufisadi, uonapo hayo uelewe ni madhabahu
ya shetani.
§ Ukiona unatoa
sadaka na unafilisika elewa hiyo madhabahu imekufa na kazi ya madhabahu mfu ni
kuua maendeleo ya watu na kuharibu na kufilisi, wewe utabakia kutiwa moyo tu,
siku ukishtuka umeishiwa hata pesa ya chakula hauna tena. Na hata kuhani na yeye
akiishiwa ataanza kukopa benki, au kukopa pesa waumini na wala harudishi
anakuwa na yeye ni mzimaji na ukisha ishiwa utaona kuhani hana muda na wewe
hata kama alikuwa anakuja nyumbani kwako au kukupigia simu mara nyingi utaona
simu zake zimekatika hakuna mawasiliano na wewe. Ameshajua hauna kitu tena,
amejipanga kuwatafuta wengine, tena anawanyanganya akitumia jina la yesu aliye
naye wa uongo.
§ Kuhani anakuwa
na tamaa ya pesa sana, na hata huwachagua wenye pesa ndiyo huwapa vyeo vya
kanisani ili asiye na pesa hampi cheo chochote.
§ Hufungisha
ndoa kwa agano la shida, hubariki pombe, hushiriki matambiko.
§ Hubusu misalaba
na sanamu (Daniel 3:18, 28-30[soma]) utaona jinsi watu wanavyotengenezewa na
makanisa baadhi katika ulimengu huu waabudu miungu na maashera. Wewe kataa kama
Shadraka, Meshaki na Abednego, kimatendo na kiimani.
§ Huzika majina
ya waumini na vitu vyao vya thamani katika altare na wengine huchimbia pesa au
kufukia mnyama au biblia na kuzika madhabahuni.
§ Huomba omba
michango kwa njia ya TV au Redio na harambee, na pia zina mabenki, kuuza madawa
ya kulevya, hufufua misukule kimazingaumbwe, wanatumia elimu ya hekima ya wazee
kuongoza makanisa hayo badala ya ROHO MTAKATIFU.
§ Hufundisha
mafundisho potofu, soma makala ya Nabii Hebron ufunguke zaidi pamoja na vitabu
vyangu.
§ Huuza vitambaa
vya leso, stika zenye alama za vidole vyao na stika zenye saini zao kwa majina
yao. Wakikueleza ipo nguvu katika hivyo vitu, hawaelezi hizo ni hirizi amekufunga
wewe Baraka zako zinaenda kwake na ndani ya stika hizo yapo majini
yanakuangalia Baraka zako katika ulimwengu wa roho yanaiba na wewe utabakia
kuteseka siku zote.
§ Ilikumuona
mtumishi kwa private lazima utoe pesa na uandikwe jina au upewe coupon mfanyiwe
arrangement ya siku yako. Huyo siyo MUNGU aliye hai ni mungu wake unaenda
kuonana naye uelewe.
§ Mtumishi
kujiita yeye ni YESU au ni MUNGU, huyo ni pepo liko ndani yake.
§ Watumishi
wanaotoa makafara na wengine wanazika mafuvu ya vichwa kanisani au mtu.
§ Jambo lingine
ni ashera katika makanisa ambayo asili yake ni miungu ili yawapoteze wanadamu
lazima yanakuwa na maashera, mfano masanamu ndani ya kanisa, kuvaa kofia
kuhani, kubeba mkuki na majoho yenye msalaba au picha ya njiwa, hayo ndiyo
maashera, na mahali pa jinsi hiyo uelewe ni mungu mke ndiye aabudiwayo hayo madhabahu
mfu.
§ Ukisoma
2 Wafalme 23:15 utaona zinabomolewa na sasa unapoabudu mahali hapo madhabahu
hiyo inajengeka ndani ya moyo wako, na wewe unakua ni pepo sasa, mfunguke,
maashera ni misalaba makanisani. Hizo zote ni dalili ya kuwa ni madhabahu mfu.
NOTE:
Enyi watu wote wa mataifa amenituma YESU niwaeleze na
mfunguke msishiriki, shetani ameliteka kanisa, jiangalie wewe kama haujatekwa
na shetani unayobahati usimame imara, uwatumie na watu wengine ujumbe huu
wasome na wewe utakuwa unatenda vyema mbele za MUNGU, roho za watu zitapona
nyingi.
TUBU:
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE UNIANDIKE JINA LANGU KATIKA
KITABU CHAKO CHA UZIMA, UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE, NAKUREJEA WEWE, NISHIKE
MKONO, TAWALA NAFSI YANGU NA AKILI YANGU, NAJITENGA NA MIUNGU NA MAASHERA YAO,
NITOE HUKO YESU, NISISHIRIKI HATA KUINGIA HUKO KIMWILI NA KIROHO, NISHIKE YESU.
AMEN.
Endelea kusoma makala na vitabu, pia karibu sana katika
kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, nawakaribisha watu wote wa
nchi zote, karibuni, na mimi nitafurahi sana kuwaona na pia YESU WA NAZARETI
anayeishi ndani yangu.
NABII HEBRON.