Nawasalimu kwa jina la YESU KRISTO aliye hai ndiye BWANA NA
MWOKOZI WA MATAIFA YOTE na ndiye mwana wa MUNGU wa pekee leo ninawafunulia
jambo jipya ambalo ulimwengu wote haujui, ila mimi Hebron kwa neema ya YESU
yeye aliyeniita nimtumikie na yeye aliyenituma niiharibu ufalme wa shetani na
ni usimamishe ufalme wa MUNGU katika dunia yote, ufalme ambao ni kweli ya MUNGU
yeye aliye hai na mwenye nguvu kuliko miungu yote. Wakati nilipotulia katika
kuomba nikiwa peke yangu mara akaja malaika Mikaeli ambaye ndiye malaika mkuu
wa MUNGU, ambaye yeye ndio kiongozi wa vita katika kuubomoa ufalme wa shetani
na maajenti wake na wote, huyu ni malaika mkubwa hata mimi katika maisha yangu
sikutegemea kama ningekuja kuwa karibu au hata na uhusiano na yeye sababu sikujijua
kama ningekuja kuwa mtumishi wa MUNGU, ila nilifichwa mpaka wakati wake
ulipofika MUNGU kwa kusudi lake likatimia.
Wakati wa kupigana akamkamata mtoto wa Adam wa kwanza kumzaa
ambaye jina lake anaitwa KAINI, ilikuwa ni vita vikubwa sana katika ulimwengu wa
roho. Akamleta mbele yangu akiwa tayari ameshamshughulikia na kumuamuru
anieleze kila kitu, na kisha nibomoe hayo yote ambayo sitayataja hapa mpaka
katika kipindi kingine nitakaporuhusiwa na YESU kuyasema. Ilikuwa ni vita
vikubwa na kilio kikubwa katika serikali ya shetani. Na mimi nikamhoji KAINI,
na kubomoa kazi zake zote. Sasa shetani alimpa KAINI cheo cha URAIS katika
serikali yake na huyu ndiye mwanadamu ambaye shetani alimpa URAIS katika
serikali yake, alimpa URAIS sababu yeye alikuwa ni mwanadamu ili aje atawale wanadamu tena na kuwamwagia roho zake
katika ulimwengu wote, ili watu wawe waasi kama Kaini. Na kila mtu yeyote aliye
au anatenda uasi au dhambi ndani yake ipo roho ya Kaini na ndiyo maana watu
katika ulimwengu huu hawaachi uasi ni sababu huyu aliyekuwa RAIS wa kuzimu yeye
ndiye aliyekuwa anafanya hayo ili na wanadamu wamkosee MUNGU na kuwa na kiburi
na kuimwaga hiyo roho katika makanisa na ndiyo maana makanisa yanaasi kila siku
na mengine ni yeye ndiye anayesimamia hayo maelekezo kabisa, mfano kubatiza
ubatizo wa maji ya kikombe, kuabudu sanamu, wakristo kukataa wokovu lakini
wanajiita wao ni wakristo.
Hii yote ni Kaini ndiye amwagaye hiyo roho ya kuasi na watu
wote walio hivyo waelewe wamejiunganisha na mtandao wa Kaini na laana zake ili
alipo yeye na hao wamfuate wakati wa hukumu. Na ukisoma katika neno la MUNGU
katika kitabu cha Mwanzo 4 chote utaona mtiririko ambao shetani aliutumia
kumdanganya Eva mama yake na shetani aliendeleza kuwafuatia watoto wa Eva na Adam
akamuingizia Kaini roho ya wivu na ukatili na kiburi, akamua Abeli na hata
MUNGU alipomuuliza KAINI ndugu yako yupo wapi utaona Kaini akijibu kwa kiburi
na kwa majibu yasiyofaa kujibiwa MUNGU, naye MUNGU akamlaani (Mwanzo 4:9-15).
Sasa hiyo roho iliyokuwa ndani ya Kaini bado ipo na inatenda
kazi na ndiye anayeisambaza kwa wanadamu wote ili kilichompata yeye na kikupate
na wewe, kama unakuwa hauelewi sasa uelewe. Unatenda dhambi, uchawi, unaua,
zini, lewa, abudu sanamu, batizwa ubatizo wa maji ya kikombe na unajua ni
dhambi, lakini unafanya tu. Hii ni sababu KANI amekushikilia na amekuwekea na
roho yake na makanisa yamewekewa hiyo roho na ndio maana kanisa imekuwa ni
nyumba ya biashara tu, neno la MUNGU linabadilishwa kweli haimo, hii ndiyo dalili
watu hao tayari Kaini amewaweka alama
yake na ndiyo maana wanatenda dhambi bila hofu na ndiyo sababu dhambi katika
ulimwengu huu inaonekana ni kitu cha kawaida. Hii ni sababu wanadamu wamejazwa
roho ya Kaini. Swali kama na wewe umejazwa hiyo roho je utaenda mbinguni? Jibu,
hauendi utafuata nyayo za Kaini.
Ni makanisa 98% all over the world yanafuata nyayo za Kaini
badala ya kufuata nyayo za YESU ambaye ndiye dereva ameshikilia stelingi
anaendesha YESU. Wamegeuka na kumfanya Kaini ndiyo dereva anayeendesha gari. Na
waumini wanaposhiriki kila ibada japo hawajui na wanampenda MUNGU, matokeo yake
wanaingiziwa hiyo roho ya Kaini na ndiyo maana makanisa kwanzia maaskofu mpaka
viongozi wa chini ni watenda dhambi tena wazi wazi na hawana hofu na kumuogopa
MUNGU hii ni sababu lipo pando la Kaini tayari na yeye ndiye aliyekuwa amepewa
cheo cha URAIS na shetani. Katika makala mengine nitaelezea zaidi habari zake
na kila mahali alipopita sawa sawa na MUNGU alivyonifunulia, habari hizi hata
utafute katika biblia hautazipata, haya yalifichwa na sasa nimewapa picha
kidogo.
NOTE:
Jichunguze je wewe hauna tabia za Kaini? Kiburi, wivu,
makusudi, mchawi, mlevi, muabudu sanamu, mbatizwa wa maji ya kikombe,
haujaokoka mpaka sasa na wala hauna mpango wa kuokoka?
TUBU:
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE NILIZOZITENDA
KWA KUJUA AU KUTOKUJUA, UNIANDIKE JINA LANGU
KATIKA KITABU CHA UZIMA WA MILELE, NAOMBA UNIONDOLEE ROHO ZA KAINI NDANI
YANGU NA NIKUTII WEWE NA KUKUSIKILIZA. AMEN.