(ALL OVER THE WORLD)
Ndugu msomaji ya makala ya Nabii Hebron, natumaini hautakuwa
na ubishi kabisa kuhusu watumishi wa makanisa, iwe Nabii, Mtume, Mchungaji,
Mwinjilisti, Mwalimu na watenda kazi wameacha kazi ya YESU WA NAZARETI ya
kueneza injili ya kweli na kutoa bila malipo sawa sawa na mwenye kanisa ambaye
ni YESU WA NAZARETI alivyoagiza. (Mathayo 10:8 mmepewa bure, toeni bure) hii
inamaanisha kuwa mpango wa MUNGU kuwapona wanadamu haiitaji ulipie pesa yeyote
kama vile unavyolipia hospitali maana yeye ni MUNGU na vyote ni vyake.
Ukisoma katika kitabu cha Mathayo 9:9-13 YESU anamuita Mathayo aache kazi aliyokuwa anaifanya ya utoza ushuru
amfuate yeye awe mwanafunzi wake. Huu ni mfano mzuri ambao tulionyeshwa njia na
hivyo kabla ya kuwa mtumishi lazima ulikuwa na mambo yako kama Mathayo. YESU
alimwambia wacha maana kazi ya kutoza ushuru ni ya Kaisari na ya Kaisari mpe
Kaisari na ya MUNGU mpe MUNGU.
Sasa watu wote mfunguke ufahamu ya kuwa sasa hivi kanisa 98%
siyo kanisa tena bali ni kitengo cha dini na watumishi baadhi yao cha kukusanyia
kodi kwa waumini wakiwadanganya ni sadaka. Nakueleza MUNGU amechukia sana. Nilipokuwa
naongea na malaika Gabriel mtumishi wa MUNGU katika habari aliyokuwa ametumwa
na MUNGU anieleze ambayo ni siri yangu. Alipomaliza akaniambia rafiki yangu
nakupenda sana na sisi sote tunakupenda mbinguni na tunafurahi jinsi unavyomtii
MUNGU aliye BABA yetu, sisi tupo na wewe milele. Na malaika huyu ndiye malaika
achukuaye roho (ndiye akataye uhai) sasa ogopeni MUNGU na muache uovu, na yeye
anawaangalia tu ila akitumwa lazima atende. Akaniambia Hebron MUNGU aliwaita
watumishi wachache tu siyo kama inavyoonekana leo hii walivyo wengi. Wengi wamejiita
na kujifanya na wengine ni wachawi na wengine ni wafanyakazi wa mishahara tu. Hao
wote MUNGU hawatambui wala hayupo nao. Ila katika wachache aliowaita nao
wamebakia 2% katika ulimwengu wote, hao 98% ni wachawi, freemason, na ni watoza
ushuru wa leo hii.
Niliogopa kujua tena kumbe watumishi sasa hivi mpaka malaika
Gabriel anawaona na anawajua wamekuwa ni watoza ushuru. Akanieleza harambee
zote na sadaka za ujenzi, ahadi, collection na nyinginezo tofauti na fungu la
kumi na shukurani hizo zote hazina mahali pake mbinguni. Huo ni mchomeko wa
shetani wa kulifanya kanisa badala ya kuwa nyumba ya sala imekuwa ni nyumba ya
watoza ushuru. Waeleze wote wa mataifa yote, hizo sizo sadaka ni ushuru au kodi
unayochajiwa na watumishi au tax collectors kama ilivyo hapa duniani kwa MUNGU
hakuna kulipa kodi wala yeye siyo mnyang’anyi. Huduma yake ni bure ila ukikuta
unaambiwa utoe malipo yeyote yakupewa jina la sadaka hicho ni kiini macho, huo
ni ushuru kama walivyofanya mafarisayo na masadukayo enzi zile alipokuwepo YESU
hapa duniani. Na walimchukia YESU kwa sababu moja wapo alikataa mambo yao
likiwamo la ushuru na ndiyo maana YESU akasema muwe makini na mafarisayo na
masadukayo ambao hupita sokoni na kusimama wakiwa na mavazi yao marefu ili watu
wawaheshimu.
Ndugu msomaji YESU alimaanisha sokoni siyo masoko ya
matunda, nguo, magari au supermarket, anamaanisha watumishi ambao katika
makanisa yao watu wawaelewe ya kuwa mahali walipo au hata katika ibada hizo
hapo MUNGU hayupo ni sokoni pa wanyang’anyi au watoza ushuru. Na hata hapa
ulimwenguni kwa kweli si watu wanawaheshimu sana hawa watumishi wenye tabia za
uwizi na kuchafua jina la MUNGU na kuchangisha harambee na kutoa huduma za
kiroho mpaka ulipe pesa. Sasa hawa ndio watoza ushuru na YESU watumishi wake
yeye hawachaji pesa ndio wakuombee bali watoza ushuru. Sasa wametawala makanisa
98% ulimwengu wote.
MIFANO
MIDOGO YA USHURU MAKANISANI
1.
Ili umuone mtumishi kwa appointment unadaiwa
pesa (huyo ni mtoza ushuru).
2.
Kuchajiwa ada yeyote katika kanisa (ushuru huo).
3.
Kuchaguliwa kuwa partners (umekuwa wewe ni mlipa
ushuru maalum).
4.
Sadaka zote tofauti na fungu la kumi na shukurani,
hizo nyingine zote kwa majina yake ni kodi mbali mbali unachajiwa kama vile
katika ulimwengu huu unalipa kodi ya serikali mfano mafuta, nauli, vifaa mbali
mbali. Hii yote ni mpango wa shetani kuharibu maisha ya wanadamu, waangamie na
wafilisike bila ya MUNGU kuwabariki na ndiyo maana wakristo idadi kubwa ni
maskini na hata waliomatajiri utakuta wanatumia nguvu za shetani ni
washirikina, hii husababishwa na roho ya mfilisi na michango ndani ya
makanisa,na watu wakijua wanamtolea MUNGU kumbe siyo ni wanatozwa ushuru na
MUNGU hapokei ushuru; ya Kaisari mpe Kaisari na ya MUNGU mpe MUNGU.
NOTE:
Kama wametoa huduma za kiroho mpaka ulipe pesa basi hakuna
ujanja wa kukwepa, wao siyo watumishi wa kweli wa MUNGU, hao ni watoza ushuru
wanaowaibia watu mali zao kwa kutumia kivuli cha jina la YESU, wakati YESU hana
tabia hizo, hao wanamchafua BWANA YESU.
Mfano halisi ulitokea katika nchi ya Tanzania, alitokea
mtumishi (Mchungaji) akasema ametoa huduma ya maji ya kikombe eti MUNGU
amemwambia achukue (TSH 500) hataki zaidi. Nawaeleza watu wote muwachunguze
watumishi maana wengi mnaona mnaongozwa na mtumishi wa kweli kumbe mnaongozwa
na watoza ushuru. Mchungaji huyu amemchafua MUNGU na ni muongo anamsingizia
MUNGU. Soma Mathayo 10: 7-9. Toa bure huyo ndiye MUNGU. Ila kuchaji pesa hiyo
ni roho nyingine ya mtoza ushuru ya kuzimu ndiyo ipo ndani yake. Watu wengi
walikwenda kwa mtoza ushuru wakifikiri wamekwenda kwa YESU WA NAZARETI na ndiyo
maana hakuna kitu watu wamepata huko zaidi ya vifo na mateso zaidi.
Na katika makanisa 98% katika ulimwengu huu watu wanafikiri
wanaenda katika majengo ya makanisa kumbe ni kinyume, wanaenda kwa watoza
ushuru. Ndiyo maana mateso na vifungo vinajaa kwa watu sababu watumishi 98%
siyo watumishi tena wa YESU bali wamekuwa ni watoza ushuru. Na kwa watoza
ushuru hakuna uzima wa milele, bali ni mfilisi na kufa kiroho na kuzubaishwa
ukae hapo hapo mpaka akija YESU kuchukua kanisa lake asikukute katika kanisa
lake bali upo kwa watoza ushuru na wanyang’anyi. Soma vitabu vya Mafundisho ya
Nabii Hebron utapona roho yako na kufunguka. MUNGU amesingiziwa uongo sana kama
enzi zile za Adam na Hawa, shetani alichafua jina la MUNGU kwa kumsingizia
uongo. Hivyo na watumishi 98% hawana tofauti na shetani wa leo. Ila mwisho
unakuja, tubu wacha uwizi na kazi ya utoza ushuru maana hicho ni cha Kaisari
siyo cha YESU.
Ni ajabu hata serikali zote katika uliwengu huu zina hofu ya
kumchaji MUNGU kodi, mpaka makanisa hawachaji kodi. Sasa cha ajabu hawa
wanaojiita ni watumishi, kwa nini wanawachaji watu ushuru? Je ni halali? Na hayo
makanisa yote hayapo chini ya serikali ya kila nchi? Je nyie serikali zote
hamyajui haya? Ina maana hizi serikali ni MUNGU ndiye anaziongoza, na haya
makanisa yanaongozwa na shetani kupitia
watumishi hao watoza ushuru.
Basi kama makanisa baadhi yamekuwa watoza ushuru basi
yamekuwa Kaisari na yenyewe yalipe kodi yasimuibie Kaisari yaani hizi serikali.
Kila mahali panapofanyiwa michango, au ulipe ada ya kanisa, nawaeleza
nilivyoelezwa na MUNGU mwenye ulimwengu huu, hao ni wezi na MUNGU hajawatuma
kutoza watu ushuru maana yeye siyo mtoza ushuru. Anawapenda wote mrudieni yeye,
wakati wowote atarejea muda wa YESU kurudi ameniambia umefika ila hajui muda
wala siku ya kuja. Ishi katika utakatifu, msikubali kutozwa ushuru kanisani.
NABII HEBRON.