Pages

Saturday, February 22, 2014

KUHIJI ISRAEL, NA KUHIJI KATIKA KABURI LA YESU SIYO TIKETI YA MTU KWENDA MBINGUNI.


Wasomaji wa makala ya Nabii Hebron, nataka muelewe pia mimi ni kivuli tu haya makala ni ya YESU WA NAZARETI, mimi ni chombo tu cha kukufikishia ujumbe na kukufundisha uzidi kumjua MUNGU na uachane na dhambi na kukurejesha katika njia ya kweli ambayo ndiye YESU mwenyewe aliye hai na yupo mbinguni amestarehe kwa BABA yake.

Nitaelezea kwa ufupi kuhusu kuhiji. Maana yake ni kudhuru mahali fulani kwa ajili ya shughuli fulani iliyokupeleka. Nitaeleza kiundani kidogo kuhusu kuhiji Israel na kuhiji katika kaburi la YESU. Watu wengi wanafikiri YESU bado yupo pale kaburini au pale kaburini zipo nguvu zake na ukifika pale kaburini basi utaenda mbinguni. Enyi mataifa yote napenda kuwajulisha kuwa YESU hayupo pale kaburini, yupo mbinguni na ukuu wake na uweza wake hakuacha kaburini. Ila kama unaenda katika nchi ya Israel na kaburini mwa YESU ni unaenda tu kujifunza au kujionea kwa macho ambalo pia ni jambo zuri kujifunza na kutembea ili uimarike zaidi kiroho na kuzijua sehemu takatifu basi.

Ila watu wengine wanafikiri kwenda kuhiji ndiyo unaenda mbinguni, jibu silo hilo au mpaka ukahiji ndiyo utasamehewa dhambi zako. Huu ni upotofu uliowapotosha wengi. Kinachokupeleka mbinguni ni wokovu safi na utakatifu peke yake. Wokovu safi na utakatifu ndiyo tiketi ya kukupeleka mbinguni peke yake. Watu wengi imani zao zipo makaburini badala imani zao wazielekeze mbinguni alipo YESU na ambaye ni mwana wa MUNGU aliye hai.

Nawaeleza ukweli 100% kwenda kuhiji ni kujifunza tu, na kwenda kuhiji siyo kwamba MUNGU ndio anaishi huko, hapana, MUNGU anaishi mbinguni. Watu wote wamuangalie MUNGU mbinguni ndipo alipo na siyo imani zao kuziweka katika makaburi ya watoto wake waliopita. Pale makaburini ni mifupa tu ipo na hata wao waliokufaga ni wanadamu tu kama wewe wanaopitia hatua ya kuzaliwa na kufa na wameumbwa na MUNGU. Ingekuwa kweli YESU yupo pale kaburini nakueleza hawa mafreemason wasingekuwa wanaendaga. Tazama katika mitandao wanaoongoza kwenda Israeli ni watumishi wachawi wanaotumia nguvu za giza na wanaenda ili kuwazuga watu kuwa wao ni watakatifu, lakini wachunguze.

Wengi wanarudi na udongo na chumvi na kuchota mchanga katika sehemu alizokanyaga YESU kipindi hicho, na wakirudi wanapotea kiroho. Wanaanza kuabudu ule mchanga na maji ya mto Yordani. Huku ni kupotea. Imeandikwa usiabudu chochote zaidi ya YESU hata kuvisujudia vitu alivyoviumba MUNGU. Nawauliza swali, je huku siyo kupotea? Je YESU anaishi katika mchanga wa Israeli?  au bado yupo kaburini? Jibu, yupo mbinguni. Kinachotakiwa nenda ukajifunze na siyo kuviabudu hivyo vitu, mshukuru MUNGU kuwa umeweza kufika huko na ukaona vitu vya historia alivyovifanya yeye kupitia watoto wake waliopo mbinguni.

Moyo wako umwangalie YESU alipo juu mbinguni tu, ili alipo yeye na wewe ufike. Usiangalie au kuiacha imani yako pale kaburini, yeye amefufuka yu hai na wewe umwangalie yeye aliye hai, maana hata kufa tena. Na wengine wanaenda kuhiji makaburini sehemu mbali mbali ili wasamehewe, hiyo ni wrong. Unapoenda kuhiji kaburini (kuabudu) unakuwa unashirki ibada za wafu na mizimu. Nikuulize swali, je hapo kaburini ndipo anaishi MUNGU anayesamehe? Jibu, siyo. Hiyo ni dhambi. Siyo vibaya kutembelea makaburi ya mitume wa MUNGU baali ni dhambi na vibaya kuyaabudu hayo makaburi. MUNGU anataka aabudiwe yeye peke yake tu.


NABII HEBRON.