1. WANAO
WAUMINI WENGI (ALL OVER THE WORLD)
2. WANAO
MAJENGO MENGI
MWANZO
4: 3-7
“ Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa
BWANA. Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona
za wanyama. BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake; bali Kaini hakumtakabali,
wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana. BWANA
akamwambia Kaini, kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
Kama ukitenda vyema hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea
mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.”
Ndugu msomaji wa makala ya Nabii Hebron na wa mataifa yote,
kazi yangu aliyoniagiza YESU WA NAZARETI niwaeleze ukweli kuhusu yeye ili watu
wote mumjue yeye alivyo na siyo baadhi yenu. Mmeona mpo sawa katika kumjua yeye
na kumbe tayari mmeshapotezwa na viongozi wa makanisa na madhehebu wakitumia
jina lake tofauti na kanuni za MUNGU alivyopanga. Ukienda tofauti tu haijalishi
unamtaja MUNGU aliye hai tayari wewe umeshapotea na umelaaniwa.
Mfano halisi; ukitazama Habili na Kaini wote hawa walimtolea
MUNGU aliye hai sadaka na siyo MUNGU tofauti ni wa kweli. Sasa jiulize kwa nini
ni sadaka ya Abeli tu ndiyo ilipokelewa tu na ya Kaini ikakataliwa? Jibu, ni
sababu Kaini hakufwata fomula ya kumtolea MUNGU na madhara yake mpaka leo hii
Kaini akalaaniwa na anazunguka tu katika dunia hii akiwa hana Baraka na
kuzunguka mahali pasipojulikana.
Kaini ni mtoto wa Adamu wa kwanza aliyelaaniwa na MUNGU sababu
hakutenda vyema kwa ajili ya kutomtolea MUNGU kwa moyo safi na biblia inasema
usipotenda vyema ujue dhambi inakuvizia, sasa yakupasa uishinde. Ila makanisa
ya leo na pia watumishi idadi kubwa isiyohesabika, hawatendi vyema kama Abeli,
bali wanatenda vibaya katika swala la sadaka. Kivipi? Kwa sababu wao wameacha
kufuata haya yafuatayo nitakavyo yaorodhesha baadhi kama wameacha kutenda vyema
na wao wote alichokipata Kaini na wao
hiyo roho ndio ipo ndani yao inafanya kazi ndani yao na katika ulimwengu wa roho,
na roho hiyo imeambukiza hata waumini na majengo yao na kila kitu, hii sababu
ya kwenda kinyume na atakavyo MUNGU. Na watumishi wanafikiri MUNGU
anadanganyika au hana akili au hawaoni kama vile Kaini alivyomtolea MUNGU kwa
udanganyifu na kukataliwa sadaka yake.
Imeandikwa utoapo sadaka yako hata mkono wako wa kushoto
usijue, ila makanisa yameacha kutenda vyema. Waumini wameambiwa andika jina na
pia hupewa risiti. Ndugu msomaji wa makala ya Nabii Hebron, nakujulisha rasmi
sadaka zote hizo hazipokelewi na MUNGU sababu tayari siyo vyema sadaka yako
ijulikane na mtu, na MUNGU anataka aijue yeye peke yake. Sasa funguka hapa embu
ona huu utahira ulivyolishikilia kanisa na waumini? Na ona jinsi wanadamu
wanavyotupa pesa zao chini wakijua wanamtolea MUNGU na MUNGU amezipokea. Na
kama unafanya hivyo ujue roho ile ile iliyokuwa ndani ya Kaini ndiyo ipo ndani
ya sadaka hizo na hayo makanisa. Na sababu ipo ndani yao basi hayo ni makanisa
ya Kaini, na watumishi wake katika ulimwengu wa roho wao ni Kaini na waumini
waliopo hapo nao ni watoto wa Kaini, na kama hawa wote ni (Kaini family)
inamaana yaliyompata Kaini muasisi na wao yapo kwao.
Kivipi? Maisha ya watu wanatoa sadaka hawana Baraka za
MUNGU, na maisha ya kusumbuka hayataisha milele na mwisho ni jehanamu kwa
sababu kama MUNGU alivyomlaani Kaini atazunguka siku zote za maisha yake hapa
ulimwenguni ndivyo na kwa watu wote wanaomtolea sadaka tofauti na mpango mwema
wa MUNGU, na pia ujiulize je MUNGU hajaelezea jinsi ya kumtolea sadaka? Jibu,
ameeleza. Sasa jiulize hii elimu ya kuandika sadaka majina imetoka wapi? Jibu,
inatoka kwa Kaini na shetani ili Kaini apate wafuasi wengi. Hivyo kama umefanya
hivyo ujijue wewe ni Kaini, na mchungaji na yeye ni Kaini, na makanisa yaliyo
hivyo na madhehebu yote ni ya Kaini, haijalishi jina la MUNGU linatajwa. Kaini
alitaja jina la MUNGU huyu huyu akiwa na Abeli, na Abeli wa leo hii ni makanisa
yanayotenda vyema atakavyo MUNGU. Hapo hakuna ubishi 100%. Nawajulisha wazi
pesa zenu mmepoteza kama Kaini alivyovichoma yale mazao yake akabakia na majivu
tuu na ndivyo ilivyo, ni wengi mmechoma pesa zenu na mali zenu mmebakia na
majivu tupu.
Partiners wote ambao mnaitwa na watumishi nyie wote ni Kaini
kama alivyo huyo mtumishi (siyo mpango wa MUNGU kuwachagua) na ujiulize kwa
nini partiners lazima awe na pesa? Je, hao wakristo wasiyo na pesa MUNGU
hawathamini? Funguka akili, mnaibiwa na mnapotezwa. YESU WA NAZARETI ameniambia
ni machukizo tupu. Mmedanganywa na watumishi wamemuasi YESU, ni wala rushwa na
wanyang’anyi. Kama ni yeye amewaita amewatengenezea njia. Ila ukiona hayo ya
partiners mmh amejiita au KUACT kama vile cinema, na wengi ni wachawi.
Mwanzo 4:7- “ kama ukitenda vyema, hutapata kibali?
Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe,
walakini yapasa uishinde.” Je hawa wanaoandika sadaka wametenda vyema? Na kama
ni siyo vyema je watapata kibali? Jibu, hakuna kibali na ndivyo ilivyo, funguka
ufahamu.
Mambo mengine, ubatizo wa kweli ni wa maji mengi sasa hawa
wanaobatiza ubatizo wa kikombe wanatenda kama alivyoagiza MUNGU? Jibu, siyo vyema.
(Haya huu ni mfano halisi) ujijue na ujue kuwa hawana kibali, dhambi imewaotea
na ikawashinda badala ya wao waishinde dhambi, dhambi imewashinda au kwa lugha
nyingine au maana nyingine shetani amewashinda! Ni mali yake, na kilichompata
Kaini ndicho kinachofanya kazi ndani yao na hawatamuona MUNGU. Na MUNGU
ameniambia mkitaka kumuona yeye mtende vyema 100% siyo nusu au robo au kiasi au
kuchanganya. Yeye hachanganywi na dhambi hata kidogo au vyeo vya shetani kama
vile ubatizo wa maji ya kikombe, au
kubatizwa kwa jina la mtumishi. Hivyo ni vyeo vya shetani na kama unavyo
ujielewe hivyo na uchukue hatua ubatizwe ubatizo mwema na siyo ubatizo mchafu
(Soma kitabu cha UBATIZO WA KWELI KWA ULIMWENGU WOTE cha Nabii Hebron) utapona
na uchukue hatua. Ukaondolewe roho ya Kaini, ndiyo maana usumbufu na mateso
hayakuishi.
Watumishi wanaokopa pesa benki za ujenzi wa makanisa (hao ni
Kaini)
Watumishi wanaochangisha pesa za harambee na michango na
kusoma majina ya waumini wale wanaotoa sadaka na kuwapa vyeti vya hongera (hao
ni kaini FULL), maana siyo vyema mbele za MUNGU.
Waabudu sanamu (ni wana wa Kaini) hawana kibali mbele za
MUNGU huo ndio ukweli, toka huko. Soma kitabu cha Nabii Hebron JINSI KANISA
LILIVYOMKUFURU ROHO MTAKATIFU, utayakuta mengi na utapona ukiamua.
NOTE
Hivyo basi yeyote yasiyo mema au kutenda kinyume cha MUNGU
katika kanisa au waumini ni dhambi na shetani amewashinda. Hivyo hata ibada
mnazoenda na nyimbo mnazoimba ujue ni bora ungekaa nyumbani tuu unajichosha
kupiga makelele tuu hakuna kibali cha MUNGU na giza tupu limetanda juu yenu. Cha
kufanya soma kitabu cha Nabii Hebron LIJUE KANISA ALILOLIJENGA YESU WA NAZARETI
ALIVYOKUWEPO HAPA ULIMWENGUNI na MJUE YESU WA UONGO, hakika utapona roho yako,
vipo katika blog ya Nabii Hebron na vinginevyo vingi tuu.
Pia najua wengi hampendi kuwa Kaini japo hata mimi
nilishakuwa Kaini huko nyuma sababu nilipewa na kufundishwa mafunzo yasiyo mema
mbele za MUNGU na nikamtii mchungaji kumbe ndio kuangamia. Hakuna kitu
nilichofanya kikasimama vizuri ni mpaka nilipoigundua siri hii. Na wewe funguka
kataa ukaini. Na unaweza ukasema huandiki jina katika sadaka yako, lakini
sadaka yako unatoa katika madhabahu ya Kaini, hapo bado umepotea tuu. Huwezi kujitoa
wewe katika moto halafu ukarudisha vitu vyako katika moto ule, jibu utaangamia
tena.
Watumishi wanao omba omba pesa katika TV au Redio au MPESA
hao hawatendi vyema, wanamuaibisha YESU na MUNGU ya kuwa wao ni omba omba, ni
masikini. Na hii ni dhambi iliyowaotea na imewakamata na kama imewakamata
inamaana ni wana wa shetani sasa au wajukuu na vitukuu vya Kaini vya leo hii, maana
Kaini yupo hai mpaka leo na hayo ndiyo mazao ya ile roho ya Kaini. Na unavyotoa
na wewe unaunganishwa na mapigo ya Kaini. (hao ni Kaini). Soma kitabu changu JINSI
KANISA LILIVYOTEKWA NA SHETANI.
Kanisa la YESU wa kweli haliwezi kutekwa ila kanisa
linalotekwa ni lile ambalo halitendi vyema, dhambi inashikilia kanisa na
kuhani, na inawashikilia na waumini. Hata
mkiombaje hakuna majibu maana wote mmekuwa Kaini, sasa Kaini yupi atamtoa Kaini
mwenzake? Tafuta mahali alipo YESU wa kweli na mtumishi umechunguza tabia zake
na kama anatenda sawa sawa na biblia, akiwa tofauti huyu ni KAINI TUU hakuna
lolote.
Mpaka sasa umepata picha ya Kaini alivyojiingiza na
kulimiliki kanisa ili na ile laana yake na mapigo wamsaidie kuibeba ambayo
ndiyo dhambi ya sanamu, majina kwa sadaka, ubatizo wa kikombe, ubatizo wa
watoto wadogo; sasa jiulize utabisha wewe siyo Kaini wa leo na endapo
unayafanya kama yeye? Wacha upone. Uokoke
na umtegemee YESU WA NAZARETI, mambo yameshaharibika katika ulimwengu wote. Imefika
hata mtu anajiita yeye ni YESU? Hivi, muulize yeye ndiye MWANA WA MUNGU WA
PEKEE? Au yeye aliushinda ulimwengu? Na je
kwa kuwa anaishi hapa ulimwenguni sasa hivi wakati neno linasema YESU atarudi
siku ya mwisho yaani kimwili. Pia muulize mama yake ni Mariamu? Halafu alitabiriwa
wapi huyo YESU anayejiita sasa hivi katika ulimwengu huu? Huyo ni SHETANI,
msidanganyike.
NABII HEBRON.