Imeandikwa
sisi sote tu viungo vya Kristo, yaani wakristo wote., Ndugu msomaji pata shule
hii usipotee, kwa sasa usemi huu,wa Neno la MUNGU umebadilika siyo mwili mmoja
tena sisi sote.
Nitakufundisha
uelewe vizuri na utapata jibu kamili 100%. Watu katika ulimwengu huu wamebakia
kujipa moyo na kusema sisi sote tu viongo vya KRISTO, hii siyo kweli,
nitaelezea kumuhusu YESU huyu wa Nazareti jinsi alivyo na jinsi alivyo na
ushirika na MUNGU BABA na ROHO MTAKATIFU, hawa tu ndio wanao umoja na umoja wao
upo milele. Isipokuwa wanaadamu ambao tunamwamini YESU 98% imebakia YESU jina
tu wala siyo viungo vya Kristo tena ila utaujua ukweli endelea kusoma ujumbe
huu nikupatiayo mimi Nabii Hebron .
Jambo
la kwanza ili ujue sasa hivi kweli hili Neno la MUNGU la ya kuwa sisi sote tu
viungo vya Kristo imekuwa kinyume siyo wote tena ni mwili au katika viungo
vyake angalia haya yafuatayo halafu uyalinganishe utaona tofauti kabisa na siyo
tena wote ni viungo vya Kristo.
Ø Wakristo wengine wanaabudu sanamu ( Siyo kiungo cha
YESU)
Ø Wakristo wengine hawabatizwi ubatizo aliouagiza MUNGU
ubatizo wa Yohana (siyo kiungo cha YESU)
Ø Kubatizwa kwa jina la chungaji (Siyo kiungo cha
Kristo)
Ø Kanisa kufungisha ndoa za ushoga(siyo kiungo cha
Kristo)
Ø Makanisa kuwa na mabenki na kudai riba (siyo kiungo cha Kristo), madhara ya riba ni
mfilisi au kunyang’anya YESU alisema usidai riba kwa kanisa maana anajua
madhara ya riba mtu akishindwa kulipa anafilisiwa na kama
Benki ni ya kanisa inamaana YESU ataitwa mfilisi wakati yeye siyo mfilisi.
Aliyajua haya mambo hayo yafanywe na taasisi zisizo za kanisa tu. Kwenye riba
kuna kudhulumiwa.
Ø Wakristo wengine wanaacha kumuomba MUNGU aliye hai
wanarudi kuwaomba wanadamu kama yeye ambao
waliumbwa na MUNGU wakati imeandikwa umuabudu MUNGU peke yake tu,(siyo kiungo
cha Kristo)
Ø Watumishi wote ambao ni freemason (siyo kiungo cha
Kristo)
Ø Wakristo wanaopinga wokovu (siyo kiungo cha Kristo)
Ø Makanisa yanayokopa benki halafu waumini wanalipa riba
(siyo kiungo cha Kristo)
Ø Watumishi wanaofanya zinaa hao wote (siyo kiungo cha
Kristo)
Ø Ibada za kushiriki ibada za wakfu (siyo kiungo cha
Kristo)
Ø Wakristo wanaofanya mitambiko (Mila) (siyo kiungo cha
Kristo)
Ø Makanisa yote yanayowaambia watu waandike majina
katika sadaka zao na namba za simu, wakati imeandikwa utoapo sadaka yako ni
siri yako kati yako wewe na MUNGU tu. Hapa utaona tayari Neno la YESUwa
nazareti limekufuriwa na kupuuziwa. (tayari siyo kiungo cha Kristo)
Ø Wakristo walio wachawi au washirikina,au walevi au
watendao maovu na wanajiita ni wakristo na ni mwili mmoja huu ni uongo mtupu.
Watu wa namna hii siyo kiungo kimoja na YESU maana YESU siyo mlevi, mchawi, na
siyo muovu. Ili uwekiungo kimoja na YESU fuata
ya YESU wa Nazareti kiimani na kimatendo. ( walio kinyume siyo kiungo cha YESU
haijalishi unalitaja jina lake.
NOTE:
Mpaka
sasa kwa mifano michache umezidi kuelewa, embu nikuulize swali sasa je kwa
mfumo huu sisi sote ni viungo vya Kristo? Jibu
ni siyo kweli.
Na
wengi hushiriki tu tukijua sisi sote tu pamoja
mwili wake, ndugu msomaji, mwili wa YESU siyo huo na hii yote ni sababu
ya kukataa kulishika Neno la MUNGU na kwenda kinyume na kimatendo, na watu
wakijijua kweli wapo katika umoja wa mwili wa Kristo na kumbe wameshaachwa,
funguka ufahamu wako hii yote imetokana na mapokeo ya elimu ya wanadamu wakaacha kufuata ya MUNGU.
Na
wanadamu kujikuta ni wapumbavu mbele za MUNGU. Na shetani ili amwangamize mtu
yeyote mlango mkubwa anaoutumia ni kumfanya awe mpumbavu halafu ndipo
hummiliki na MUNGU huondoka, matokeo
yake ni kuishi katika mapigo na zaidi kwa picha hii kanisa limegawanyika na
kuwa siyo makanisa yote ni mwili wa Kristo tena.
Jichunguze
utapata jibu lako upo wapi wewe?
NABII
HEBRON