MATHAYO 10: 8 -9.
Pozeni wagonjwa, fufueni wafu,
takaseni wenye ukoma, toeni pepo;
mmepata bure toeni bure. Msichukue dhahabu,wala fedha, wala mapesa mishipini
mwenu.
Ujumbe huu siyo ni kwa
watu wa nchi za Afrika Mashariki tu ni pmoja na sehemu nyingine zote za
ulimwengu huu. YESU wa Nazareti amechukia
sana kwa ajili ya watumishi ambao wameibadilisha kazi yake na kuwa ni huduma kama ya hospitali isiyotolewa bure na zaidi
hata hospitali za kibinadamu baadhi siku hizi zinatoa huduma kwa watu
bure.
Ila kwa ujumla YESU
anasema msidanganyike na hawa watumishi ambao
ili akuhudumie au akuombee lazima utoe pesa kwanza au ili akupe appointment
umueleze shida zako utapita kwanza kwa
cashier unalipa kiasi fulani na unapewa
risiti ndipo umuone akukubali.
Hao sio watumishi
wanaoongozwa na MUNGU wa kweli, maana YESU aliwaambia nimewapa bure toeni bure,
muwapende watu na msichukue pesa wala
dhahabu za watu. Sasa funguka, sasa hivi watumishi 98% ni matapeli, 45% ni
wachawi kiwango cha kutisha na ni wanachama wa chama cha freemason wanatumia
nguvu za giza kuendeshea makanisa, na makanisa haya siyo makanisa tena imebakia kanisa jina tu mwenye kanisa yani
YESU wa Nazareti ameshaondoka amebakia yesu wa uongo ambaye nyumba yake ya
ibada huitwa pango la unyang’anyi wa kitumia jina la YESU na kumfanya YESU
mwana wa MUNGU aitwe mnyang’anyi, wakati yeye siyo mnyang’anyi kabisa.
Ninawaandikia waraka huu
mimi Hebron
kwa kila mtu atakaye usoma amshuhudie mwingine
ili watu wasinyang’anywe mali
zao na shetani. HAO NI WEZI,
Soma MARKO(11:15-18). Na zaidi BIBLIA
INASEMA NI WATUMISHI WA MATUMBO YAO .
WARUMI 16:17-18.
Ndugu zangu nawasihi waangalieni wale wafanyao fitina na
mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho uliyojifunza mkajiepushe nao. Kwa
sababu walio hivyo hawamtumikii BWANA WETU KRISTO
BALI MATUMBO YAO WENYEWE, NA KWA MANENO LAINI NA YA KUJIPENDEKEZA WAIDANGANYA
MIOYO YA WATU WANYOFU.
Mtu mnyofu ni wewe unayeambiwa toa pesa ndipo YESU
atamaliza shida zako, na wana maneno laini mpaka utatoa pesa tu, ukiambiwa eti,
huduma hii haina mfadhili yeyote, hapo funguka utambue hajatumwa aifanye hiyo
kazi na YESU ndiyo maana, YESU hamfadhili anaangalia kwa watu , zaidi YESU
akimtuma Mtumishi humtengenezea njia ili aifanye hiyo kazi
na njia yenyewe siyo ya kuchangisha watu pesa au kuomba omba watu pesa kwenye Radio na TV pesa
za kuendesha vipindi .
YESU ni tajiri na sio
omba omba kama kazi hiyo ni yake ataifanya mwenyewe na siyo kwa njia ya kuomba
omba, na YESU ameniambia ole wao watumishi wafanyayo hayo, shoka lake tayari
lipo shingoni mwao. Wamekuwa watumishi wa shetani japo wanasimama makanisani,
ka nisa limekuwa kama soko, habari inayozungumzwa ni sadaka tu, ndio wimbo , badala ya rehema.
Kama hauna pesa
hauonekani wewe ni mtu katika kanisa , wenye pesa ndio wanaopendwa. Nikuulize
swali hilo
ndilo kanisa alilolijenga YESU? Jibu
Siyo.
Soma vitabu vyangu
katika Blog yangu; KANISA ALILO LIJEANGA YESU NA JINSI KANISA LILIVYOTEKWA
NA SHETANI, MPINGA KRISTO NI NANI? NA VINGINEVYO ILI UPONE, NA KAMA NI MTUMISHI UNAYEFANYA BILA KUJUA UPONE
UACHE KUTOZA WATU PESA MAANA NI DHAMBI.
Unapotoza watu pesa
unapata dhambi, hivyo tambua kuwa mtumishi yeyote anayetoa huduma ya kiroho kwa
kutoza au kuchangisha mtu pesa huyo
anayo dhambi na anatenda dhambi. Ila
wale walio wanachama wa freemason kazi
yao ni kuomba omba tu pesa kwa waumini
maana hawana mfadhili na mfadhili wao ni masikini na sababu ni shetani hana
kitu hivyo kazi yao ni kuomba omba tu
kila siku kwa Radio na TV, semina na mikutano.
Hivyo ufunguke ujue
ukweli matokeo yake utaibiwa baraka zako na nyota yako na ndiyo maana shida
haziishi kwa wakristo makanisani wakati YESU ndiye jibu. Shida ni mafarisayo na masadukayo wamejaa.
Usiogope fanyia
kazi nakuombea hata kama sijakuona,
usiteswe tena. Kama wameitwa na
YESU wamuombe YESU awape pesa, siyo
kuwatumikisha watoto wake.
Imeandikwa amelaaniwa
amtegemeaye mwanadamu, amebarikiwa
amtegemeaye MUNGU, ona sasa watumishi wanamtegemea mwanadamu badala ya
kumtegemea MUNGU, na zaidi nchi zinabeba laana kwa ajili ya watumishi
wanaofanya mabaya tofauti na MUNGU. Mnabakia kulaumu viongozi wa nchi
shida ni wako wapi watumishi wa kweli
ambao MUNGU huwasikiliza? 98% ni wa uongo, 2% ndiyo ya kweli na mara nyingine
hata 2% haipo katika nchi ni 0%.
NOTE:
Usidanganyike tena,
MUNGU amekupa wewe pesa ukipenda mtolee na uangalie mahali pa kutoa ili
ubarikiwe, na usilazimishwe kutoa na kupangiwa kiasi cha kutoa. Na utoe
ukipenda moyoni mwako. Ila usitoe kwa shetani na kwa mpinga Kristo. Roho
akuongoze.
Ujumbe huu ni wa YESU wa
Nazareti kwa ulimwengu wote, Ila nchi 4 nilizozitaja watu wanalia hata
wamenitafuta niwasaidie walikosa pesa za kulipa ndio wasaidiwe na watumishi
hasa KENYA na RWANDA, huu ni wizi umejaa, na TANZANIA .
NABII HEBRON