WANAOJIITA WAO NI YESU
HAO NI MASHETANI 100%
YOHANA 1:14
Naye Neno
alifanyika mwili, akakaa kwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa
mwana pekee atokeaye kwa Baba amejaa Neema na kweli.
Ewe
mwanadamu uliyeumbwa na MUNGU aliyeumba dunia hii na sayari zote na vitu vyote
ni mali yake. Tarehe 5.08.2013 muda wa saa nne za usiku kwa saa za Afrika
Mashariki (Tanzania), Bwana YESU aliye mwana wa pekee wa MUNGU alikuja kusema
na mimi kuhusu ulimwengu ulivyoharibika na utakavyoendelea, akaniambia Hebron
usiogope kwa ajili ya machafuko yanayotokea sasa, na majanga katika nchi mbali
mbali Neno la MUNGU lazima litimie na hizi ndizo dalili za ujio wangu. Ila machafuko
haya hayatawaathiri wale waliopo na yeye, ila wale ambao hawapo na yeye yatawahusu;
huo ni mpango wa MUNGU. Akanieleza na mengine ambayo hakuniruhusu niyaseme
popote kama vile alivyomzuia Ezekiel kusema lolote.
Ila
akaniambia waambie wanadamu wote mimi
YESU wa Nazareti nipo mbinguni kwa Baba yangu na nitarudi hapo duniani siku ile ya mwisho (Nitarudi
kimwili kama ilivyoandikwa). Akaniambia wameibuka watu wanajiita wao ni YESU
akaniambia hao ni mashetani. Akaniambia je, huyo anayejiita yeye ni YESU
alishinda mauti? Nikamjibu hapana,
akaniuliza je alisulubiwa msalabani? Nikamjibu hapana, je alikufa na kufufuka? nikamjibu
hapana BABA, akaniuliza je yeye alipaa kurudi mbinguni? Akaniambia sasa angalia
je anafanana na mimi sasa, nikamjibu hapana, akaniambia waambie watu ukweli
wapone haijalishi upo nchi gani, taifa
lolote.
Ujumbe huu
sio wangu mimi Hebron, ninanukuu kama alivyoniambia YESU wa Nazareti. Amesema
msishiriki kumwita YESU, hivi mnajua uthamani wa jina la YESU? Niliogopa sana,
maana aliongea kwa ukali. Wanadamu wanajifananisha na mimi na kushiriki utukufu
wa MUNGU? Akaniambia ndani ya anayejiita
YESU mwanadamu, ndani yake ni shetani anakaa ili kuwapoteza watu, someni
BIBLIA mtaona YESU anarudi ule mwisho wa dunia. Je, kama mtu anasema yeye ni
YESU na yupo hapa duniani ina maana mwisho wa dunia ndiyo tayari? Jibu bado.
Akaniambia akishuka YESU kwa mwili wake
yeye siku hiyo ya mwisho, hakuna kitu kitakacho salia hata milima itakuwa
tambarare sababu ya nguvu zake na uweza wake.
Ndugu uzidi
kufunguka anayejiita yeye ni YESU huyo ni muongo anawapoteza watu, na wote
wanaomwamini huyo hawamwamini YESU, ni shetani amejipa jina hilo akamtumia huyo
mwanadamu. Mnapo enda kwake mnaenda kujikabidhi kwa shetani 100%. Mrudieni YESU
wa Nazareti na mtubu. Yeye anatafutwa kwa njia ya roho na kupitia msaidizi wake
ambaye ni roho mtakatifu tu. Na zaidi uzidi kuelewa YESU hakuwahi kuoa, wala
kuzaa watoto, na alizaliwa kwa njia ya ROHO MTAKATIFU, na alizaliwa kwa njia
hiyo ili atuokoe kutoka katika dhambi ya asili.
Kila
mwanadamu anadhambi ya asili isipokuwa YESU tu! Je huyo anayejiita YESU yeye
hana dhambi ya asili? ( jibu anayo), na kama anayo je, huoni ni muongo huyo?
YESU amesema ole wake shoka lipo tayari kwenye shingo yake na hukumu tayari.
Imeandikwa wakati wa mwisho mkiambiwa yupo kule au kule msiamini, YESU alikuwa
anayo maana. Yupo mbinguni tu mkienda
hamtamkuta, sasa angalia wengi walioenda je hawajaambulia patupu?
NOTE:
YESU YUPO
MBINGUNI NA HAKUNA MTU MWINGINE ANAYEFANANA NA YESU. YESU MWANA WA MUNGU NA MWOKOZI
WETU.
NABII HEBRON