NABII HEBRON AKIWA NA BABA YAKE WA KIROHO ALIYEMZAA- MOSES KULOLA.
Ndugu msomaji wa makala hii, habari hizi ni za kweli. Mnamo tarehe 3.8.2013, BWANA YESU alipokuwa akinifundisha kuhusu kazi yake na jinsi ilivyoharibika, watumishi wameshabadili neno lake na kuwa kinyume na yeye alivyopanga yeye ambaye ndiye njia ya uzima na y a kweli, wengi wamekuwa wachawi na kujiingiza kwenye chama cha freemason cha shetani. Ila shoka lake tayari lipo juu yao, maneno haya nimemnukuu, kama alivyonieleza ukiamini sawa ukikataa shauri lako, utakuja kulia kama hao viongozi . (Marais na wafalme wa n chi mbalimbali katika ulimwengu huu wanateseka sana kuzimu), wakiwamo wanajimu wote katika dunia hii, wote waliokufa wamekataliwa na MUNGU wanateseka mateso yasiyoelezeka maana niliwaona kwa macho yangu japo na viongozi wa dini wengi 99 % waliokufa wamekataliwa na baadhi ya wanamiziki maarufu duniani waliokufaga wote wapo kuzimu, wanateseka mateso yasiyoelezeka wanatamani hata kuja huku duniani wa waonye msitende dhambi na kila miziki yao ikipigwa huku duniani ndivyo wanavyoteseka zaidi.
Ila mlango nulishafungwa na malaika Mikaeli hakuna kutoka.
YESU akaniambia nimekuonyesha ili uone hali halisi jinsi watu wanavyoangamia
kwa dhambi, wameacha kutengeneza maisha yao wanajidanganya wakifa watafanyiwa
ibada za wakfu na maombezi , YESU wa Nazareti akaniambia anayenitaka sasa hivi
ndiye ninaye mtaka mimi. ( Akaniambia
anitafutaye kwa bidii ataniona ) na
anayesema muda bado atanitafuta baadaye na mimi huyo simtaki.
Akaniambia ndivyo ilivyo kwa hao marais wa nchi
mbalimbali nimekuonyesha uone hali halisi. Akaniambia hawa maraisi walio nikataa mimi walikuwa
wamejieleza kuwa wakifa wataombewa na watapokelewa , na ni makanisa kupitia
watumishi watumishi wasio sema kweli na
kuwapoteza watu wasitengeneze maisha yao kwa kunirudia mimi kwa kunirudia mimi YESU, akaniambia soma katika kitabu cha Waebrania 9:27-29
Imeandikwa hivi , kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja , na baada ya kufa hukumu, kadhalika KRISTO naye, akiisha kutolewa sadaka mara
moja azichukue dhambi za watu wengi atatokea mara ya pili,
pasipo dhambi kwa hao watazamiwao kwa wokovu (Hapa utaona Neno linasema
ukishakata roho tuu, kama hujatengeneza
na y eye kinachofuata ni hukumu).
Sasa ndugu msomaji wa
nchi yeyote , taifa lolote na bara lolote, kilicho waponza hawa viongozi au watu maarufu kukataliwa na MUNGU
walivyokuwa hai walitegemea ibada
za wakfu, na ibada za mazishi yao wataombewa
na watumishi wengi na watu wengi
hivyo watapokelewa. Kwa
MUNGU siyo hivyo, hizo ibada za wakfu ni
ujanja wa shetani kuwapumbaza watu ili
wasiurithi ufalme wa MUNGU. Niliogopa sana akanionyesha, embu angalia
mazishi na ibada kubwa zisizo elezeka za kufana
wakati marais hawa na wafalme wakizikwa. Je ! kwa nini hawajapokelewa
paradise,? Si kuwa na jibu, akaniambia muda wa watu kunifuata mimi YESU na
kunipata ni sasa, hawa wengine wanategemea wataombewa na watu wengi na nyimbo zitaimbwa na makaburi ya kifahari na wengine
hata wanakaushwa ili wasioze, lakini MUNGU haangalii hayo.
Akaniambia waeleze
watu wote habari hii hata wasiokujua
wote ni watu wa MUNGU anayetaka
kupona apone atakaye kaza shingo yake kuwa ngumu shauri yake, ( KUZIMU
NA JEHANAMU INAWASUBIRI). Ni mekuonyesha
hayo ili ujue namna ya kuueleza ulimwengu wote na ole wake atakayejaribu
kukuzuia, kwanza hataweza na pili itakuwa ndiyo mwisho wake kuishi katika
ulimwengu huu ni yeye YESU ndiye atakaye
mshughulikia haijalishi upo mwenyewe
kimwili.
Mwanadamu ni nani hata ashindane na mimi MUNGU? Mimi ndiye
niliyemuumba na nikitaka muda wowote naweza
kumuangamiza. Akaniambia Eliya kipindi kile alikuwa mwenyewe kimwili na
mabaali walikuwa 450, ila Eliya aliwaangamiza. Akaniambia naelewa na ninaona
kila kitu hapa duniani. Na ndivyo itakavyokuwa songa mbele waeleze watu ukweli usiogope mtu yeyote,
shetani amewateka watu wengi sana na hawajijui. Tazama ni miaka 64 imepita toka mwaka 1949
hakuna Rais aliyeenda paradise wanasubiri hukumu siku ya mwisho.
Enyi wanadamu
tengenezeni maisha yenu msije
mkaangamia mkidhani mkifa mtafanyiwa
ibada mtakubaliwa, nakupa mfano je wewe, uliye mtu wa
kawaida hutaki kutengeneza maisha yako
je wewe utaombewa na watu wengi kama inavyofanyikaga kwa marais au wafalme?
Jibu hapana, wao waliombewa na watu
wengi na siyo ajabu maombi ya nchi nzima
ila wamekataliwa! Je wewe unayeombewa na watu wachache utapokelewa? Jibu
hakuna.
Alipomaliza kusema na mimi akaniaga akaniambia mwanangu,
mimi ninarudi kwenye kiti cha enzi nitakuja tena wakati mwingine.
Niliduwaa nikarudisha picha za mazishi
ya viongozi wa nchi mbalimbali pamoja na
maombezi yote, hakuna kitu na jumla ya miaka 64 imepita katika ulimwengu huu hakuna RAIS au mfalme aliyepokelewa na MUNGU hata
wale walionyongwa au kuuwawa. Kweli MUNGU ni wa haki
upandacho ndicho utakacho vuna, ukipanda dhambi utavuna hukumu, ukipanda
mema paradiso.
Nawasihi wanadamu wote huu ni wakati okokeni tengenezeni maisha yenu ukisha
kata roho tu basi, haki yako inakusubiri
kama ni hukumu au paradise. Msidanganyike
eti mazishi yalifana na maombezi. MUNGU
anaangalia yule aliyekufa. Kila
mtu atasimama mbele za YESU kusomewa
mashitaka yake na hakuna wa kukutetea
hivyo ndivyo fomula ya MUNGU.
Hesabu hizi za
kipindi cha miaka 64 tokea mwaka 1949 hadi tarehe 3.8.2013 hakuna Rais yeyote
aliyefariki aliyepokelewa paradise.na ni wengi sana . MUNGU haangalii cheo,
utajiri wako ni uhusiano kati yake na wewe tu.
Mwisho wa nukuu , Nukuu ya YESU wa Nazareti.
NOTE:
Miaka hii yote 64 ni ulimwengu wote , ukitaka kujua Rais
aliyekufa au mfalme chunguza kama alikufa kati ya kipindi hiki 1949- 3.8.2013.
utaujua ukweli.
Mrudieni YESU watu wote wa ulimwengu, kuitwa mkristo tu jina siyo tiketi yako ya kwenda mbinguni.
Ni Wokovu na Utakatifu tu.
NABII HEBRON.