Pages

Wednesday, March 10, 2021

 

NALIVUNJA HEKALU LA SHETANI (BREAKING THE TEMPLE OF THE DEVIL) YEREMIA 7:1-4 YOHANA 2: 19-21

Haleluya! Baba nakushukuru, Yehova ni wakati wako tena, MUNGU sema na watoto wako tena, ufurahie nao, tenda mapenzi yako kwa utukufu wako, navunja kazi za ibilisi katika jina la YESU Kristo wa Nazareti Mwana wa Mungu uliye hai, Mungu wa Ibrahim, Isaack na Yakobo wewe ni Mungu unayestahili kuabudiwa, zaidi yako hakuna, Naombea amani, ninafungua mioyo ya watoto wako, nakata kamba za ibilis, nakata cheni za miungu, katika jina la YESU na kwa damu ya YESU. Fahamu na Masikio ya watoto wako MUNGU yaendelee kufunguka. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Bwana YESU asifiwe, Nalivunja hekalu la shetani, wachawi, mizimu, wanadamu, na nalijenga hekalu la Mungu. Yeremiea 7:1-4, Yohana 2.19 -21 - Bwana YESU asifiwe, hebu tujiulize kwanini YESU alimwambia Petro nalijenga Hekalu langu ndani yako na jambo jingine jiulize kwanini YESU alisema atalibomoa? Jiulize Je! Lilikuwa libaya?  Kama lingelikuwa lizuri asingelibomoa ila wakati alipokuja yeye hapa dunia yeye ndiye aliyekuwa amelijenga kanisa na kabla ya kuondoka akalijenga kwa mtume wake Petro. Ndipo likaendelea kuhubiri habari ya kweli lakini ilifika mahali wakamuua Petro na akafa kimwili ili kuua lile kanisa alilokuwa amelijenga YESU, kanisa ambalo misingi ya kuzimu haikuliweza. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

  Kabla YESU hajaja kulikuwepo na makanisa lakini makanisa yenyewe yalikuwa na  misingi ya kuzimu na mengine yalimpinga YESU na YESU alipokuja wakawa hawamtaki YESU kwa sababu alikuja kuvunja misingi hiyo na kujenga kanisa ambalo MUNGU alimwambia alijenge, na kanisa ninalokwenda kuzungumza na kulibomoa sasa hivi ni kanisa  la shetani, kubomoa kanisa la malango ya kuzimu, kubomoa kabisa hekalu la  kila namna ambalo ni tofauti na lile la MUNGU na kulijenga hekalu la MUNGU na sio kuwa naenda kubomoa majengo maana YESU  akija hatachukua majengo atachukua kanisa alilolijenga, kanisa ambalo ni wewe ambaye  unasikiliza, umejengwa katika misingi ya kweli, umemwamini YESU umempokea YESU na kama umempokea basi yeye ndio atakateyekuchukua siku ya mwisho, maana  kila mmoja atachukua kile ambacho amekijenga yaani YESU atachukua kanisa alilolijenga na Shetani hivyohivyo na mwenye uamuzi wa mwisho ni wewe, kwenda kwa YESU au kwa shetani. Unaweza ukawa na hekalu la mpinga kristo utachukuliwa na mpinga kristo na ukiwa umejengwa juu ya hekalu la YESU KRISTO utachukuliwa na YESU. Mfano: Unaambiwa okoka hutaki na unasema wewe ni Mkristo, Mkristo wakati hutaki wokovu? Hekalu hilo litakuwa limejengwa na Mpinga Kristo hata mimi Hebron kabla  sijampokea Kristo nilikuwa Mpinga Kristo, nilikuwa mkristo ambaye hajaokoka, nasoma biblia nasema sala ya baba yetu, nasoma zaburi, natoa sadaka, nasoma zaburi, lakini nilikuwa sijaokoka, nilikuwa  mpinga kristo kwa kutokujua maana ndio nilikuta dini na nikafuata dini za wazazi wangu na ambazo ndio zilimpinga mpinga Kristo kwa kujua au kutokujua maana huko hakukuwa na wokovu, na mpinga kristo ndio alikuwa ananikataza kuokoka mpaka  mpinga kristo alipotoka yaani nilipoachana na dini nikaokoka na nikamfuata YESU na kwenye moyo wangu nikampokea YESU, na YESU ndiye aliye jenga hekalu lake, akaendelea kunikuza kama anavyoendelea kukukuza sasa  na hiyo siku ya  mwisho ndio atakuja kukuchukukua. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 Kuna baadhi ya watu mpaka sasa hawataki kuokoka hawamtaki Bwana YESU wanasema sisi ni wakristo tu, tunaenda kanisani tu, tunaomba, tunatoa sadaka, tunasali katika dini za mapokeo, na sio kuokoka ni kweli kwa kujua au kutokujua utaona sawa tu, lakini ni kanisa ambalo sio la YESU. Ukitaka kujengwa katika kanisa la YESU, Lazima umpokee YESU na YESU ndio akalijenge hekalu lake ndani ya Moyo wako,   Kwa maana biblia inasema mtu akiliharibu hekalu hili nami nitamaribu na  shetani alitangulia kuyajenga mahekalu, ukiona watu wanaenda kwa waganga, kwenye matambiko ni hekalu la matambiko,  inawezekanai ni mahekalu ya ukoo unaenda kutambika haifai, inabidi mahekalu yote ambayo sio ya YESU yabomolewe na Hekalu la YESU wa Nazareti lijengwe Roho Mtakafu ajae, YESU ajae, MUNGU ajae, na baraka zake zijae, ndipo utakapoweza kuyashinda. Jinsi mtu alivyo ipo nguvu ya hekalu ndani yake, kama ni mchawi au mshirikina ndani ya mwili wake yapo majini na mapepo ndio yamejaa ndio yanayomuongoza. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 MUNGU anataka mwili wako uwe hekalu lake na shetani nae anataka mwili wako uwe Hekalu Lake. Wanadamu wengi wanakuwa hekalu la MUNGU kwa midomo, wanajifariji lakini matendo yao  hayaendani na yale ambayo MUNGU anataka lakini MUNGU anataka uwe hekalu lake kwa matendo, msipumbazwe upo moto  umeandaliwa wa kuchomwa,  Elia alikuwa hekalu la MUNGU ndio maana alipomwomba MUNGU,  na Roho Mtakatifu alikuwa ndani yake akifanya connection, Mungu alikuwa anafanya connection ndani yake na kufanya kazi, watu wengi baadhi  yao ni wakristo na wanafunga sana,  lakini ni  mahekalu ya shetani,  imeandikwa usiabudu sanamu, sasa kama MUNGU amejaa ndani yako, Roho Mtakatifu na Bwana YESU hawezi kukukubalia uabudu sanamu  atakuambia acha lakini kama ndani yako imekaa Miungu ya sanamu,  wewe utaabudu tu, utaabudu tu, sasa wengi watachomwa moto, watalia na siku ile ya mwisho YESU atawaambia sikujui, sikujui,  kwa sababu hekalu hilo halikua la Bwana YESU lilikuwa la majini, mapepo, mapokeo ya wanadamu,  unatakiwa  uyavunje mahekalu yote ambayo sio ya Bwana YESU, ndio maana baadhi ya wafalme hawamsikilii MUNGU, wala hawamsikilizi, kwa sababu baadhi yao, mioyo yao ni mahekalu ya mashetani, majini, miungu, kama ilivyokuwa kipindi kile cha Farao mpaka alipopigwa ndio akaacha kumtii huyo mungu wake na akamtii MUNGU ambaye alimwagiza Musa Kwake ila ilikuwa baada ya mapigo na ndivyo itakavyokuwa  hata sasa. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 Hata sasa MUNGU aliniagiza kwa wafalme na wakuu wa Nchi, Baadhi wamelipokea na baadhi wamepuuzia, inashangaza sana na wewe pia utashanga, ujiandae kusikia hayo ambayo nimeyaandika hapo juu, nimeshakuambia maana ni order imeshatoka Mbinguni, wengi hawasikilizi sasa, msisubiri kusikiliza kutoka kwa mhubiri mwenye jina kubwa, magorofa, ndenge,  maana ndio wanadamu wako hivyo wengi hutaka kusikiliza  maagizo ya MUNGU toka kwa wenye Pesa na Mamlaka, au tajiri ndio  wakisema wanawasikiliza sasa mjue kuwa  hakuna tajiri kama MUNGU na MUNGU aliyeniita  ni tajiri hasa na anakila kitu sasa ninachokuambia sikiliza na ukifanyie kazi. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

  Wanaopambana na wewe hawatakuweza hata mimi walijaribu wakashindwa  na hawatakaa wasimame,  hekalu lako likijengwa na MUNGU, na Roho Mtakatifu atakuwa amejaa na Serikali ya Mbinguni itakuwa imejaa,  napenda nikufundishe, YESU akakutana na yule mgerasi  mwili wake ulikuwa umejaa mapepo, yamkini mwili wako umejaa shida, umejaa roho chafu za kila aina na za kishetani, zinatesa maisha yako na ndani ya yule Mgerasi kuliluwa na Mapepo na alikutana na YESU  na ndani ya YESU,  kulikuwako na Roho mtakatifu na ndani yake kulikuwa na MUNGU amejaa  kwa level yake  wakamwambia YESU tuna nini na wewe? Utuache! Na mimi nakuambia MUNGU amejaa kwangu nataka wakuache lakini na wewe ukubali na useme siwataki, siwataki, haijalishi wamekupigaje waambie siwataki hekalu likajengwe usifikiri ukiomba sana na kufunga wakati wewe mwenyewe umefungwa utafunguliwa? hapana, nakurudisha nyuma kidogo, MUNGU anaangalia hekalu lake ambalo ni wewe ashamiri ndani yako masa 24, anafurahishwa na wewe lakini huenda ukawa unajiita Mkristo lakini ni hekalu la Wachawi, kwa waganga, kwa washirikina upo, hapo unakuwa mwenye mapepo kama yule Mgerasi sio lazima upige kelele kama yeye na kama pia una mawazo machafu, mabaya, hilo ni hekalu baya lazima livunjike na lijengwe la MUNGU. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 Watu wanataka kupokea ya MUNGU lakini baadhi yao ni mahekalu ya mapepo na ya mapokeo ya wanadamu kwa kujua na kutokujua ukiwa u hekalu la MUNGU, na MUNGU amejaa, serikali ya Mbinguni imejaa, na ipo ndani ya maisha yako, ipo ndani ya Moyo wako huwezi ukawa na chuki au fitina, maana ni hekalu la MUNGU, kama umeokoka huwezi ukawa kijana au binti unatamani, tamani kila  umwonaye kwa nia ya uzinzi, au kutamania au kufanya dhambi fulani na kama uko hivyo hekalu hilo linashida mwambie YESU alivunje hekalu ambalo si lake ndani yako na utaona MUNGU akijaa na kupwa ROHO Mtakatifu na Bwana YESU akikuombea na mzigo wake ni mwepesi na anapokaa kwenye Moyo wako yeye anafurahishwa Tazama kipindi kile cha Musa MUNGU ndiye aliyekuwa amejaa ndani ya Musa, akamwambia Musa nyoosha mkono wako, watu wakajua ni Musa, nachokuambia ujue kuwa ni MUNGU na sio Musa, MUNGU ndio aliyemwongoza Musa mtumishi wake na MUNGU ndiye aliyesema na bahari ikatii na maji yakagawanyika ni nguvu za MUNGU hizo. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Kama ulikuwa umekufa kiroho utafufuka, wamekuharibu utanyanyuka na yule MUNGU wa Ibrahimu MUNGU ashushaye moto ndiye aliyeniweka hapa ndie aliyenituma kwako kuvunja hekalu nataka ukachanue, ziko ahadi nyingi kwako  lakini yawezekana  kuwa u hekalu la ibilisi hutazipata hata mimi ni mchungaji  lakini pia kuna baadhi ya wachungaji / wahubiri wengi ambao ni mahekalu ya shetani kwa sababu Roho Mtakatifu hawezikuwa na ubaguzi kusema leta pesa za maombezi, akawambia mna sh ngapi mje niwaaombe,  ukiona hayo jua kuwa huyo ni hekalu la mapepo na shetani, YESU anakuja, ataangalia kanisa lake na kanisa lake ni wewe na mwingine, angalia mama atakuwa jikoni,  baba atakuwa darini, baba  au mama atanyakuliwa, hata kama mnasali pamoja  kwa jina la YESU  ataangalia alichokijenga yeye ambacho ni wewe unayemkubali sasa, huwezi kuwa hekalu la MUNGU ukategemea waliokufa kwa sababu MUNGU aliyeumba Mbingu na dunia anasema yeye si wa wafu. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

MUNGU amenituma kwa mataifa yote na akaniambia  “niangalie mimi” yaani nimtegemee MUNGU peke yake, hata wa shetani humwangalia shetani na lakini hata ambao wanamwangalia shetani  wana mbinu zao za kunyang’anya watu  lakini ni bora ujue kuwa hichi ni kipindi cha ngano na Pumba  kupepetwa na sijui kuwa wewe upo  upande upi? U hekalu la MUNGU au la shetani? Bado una mawazo mabaya? Bado unawatakia watu mabaya? Bado unampinga MUNGU? Unashindana na MUNGU?  Alichokijenga MUNGU hakishindani na MUNGU?  Lakini yawezekana ulikuwa na MUNGU na kwasababu ya tabia zako shetani naye akalibomoa hilo kanisa ambalo YESU alilijengwa ndani yako.  Kama Yuda ambavyo alikuwa amejengwa na alikuwa hekalu la MUNGU kwa kufungua milango Ibilisi akapata mlango akalibomoa  watu wengi wameokoka kwa kujua   na kutokujua  kwa hiyo wanabakia  kudhoofika na  kulia acha nikufundishe MUNGU alikuacha, MUNGU aliondoka, ila  nina habari njema kwako  ukatubu na ukubali ili akujenge upya,  Unajua hata ukienda mahali kama MUNGU  yuko ndani yako kila ufalme unanywea si unanywea kwa sababu yako  wewe ni kwamba ufalme huo unamwogopa MUNGU wanaokupiga wewe wanampiga MUNGU, wanaokutukana, wanamtukana MUNGU, Je! Watavuna nini? www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Napenda nikwambie ukweli wewe ambaye unasema naenda disco, kasino, bado unatenda dhambi hilo ni hekalu la shetani, hata kama unajichanganya nusu kwa MUNGU, nusu kwa shetani, Amua, kisha badilika ili hekalu la Shetani  likavunjwe  na MUNGU ajenge la kwake  ndani yako, maana MUNGU amenituma nijenge hekalu lake sio nijenge majumba, nikujenge wewe ili  YESU akatukuzwe,  YESU akaonekane na Roho wa MUNGU akajae kwako. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 Bwana YESU asifiwe, kwa sababu wewe ni kanisa na ahadi zake zikatimie kwako maana amesema nitakulinda, nitakuchunga, nitakushika mkono, Wengi ni mahelaku ya wachawi, wapinga kristo, wamepunguza au kuongeza Neno la MUNGU, na wanatenda dhambi na bado wanataka MUNGU awashike mkono, nakuambia hatawashika mkono tunaelewana? Mmejifunza kitu hapo na kikae ndani yako.  si wakati wa kuomba maombi ambayo hayamfikii MUNGU na kupoteza mda si wakati wa kuongozwa na mahekalu ya shetani, labda nikufundishe Biblia imetoka Mbinguni na ni maagizo ya MUNGU na katika kitabu hiki kimeandikwa ombea watu bure, lakini hapo hapo mhubiri / mchungaji anashika kitabu hichi hicho na anakuja mbele za MUNGU kwa jina la baba, mwana na roho Mtakatifu na atataka utoe hela kwanza kama hospital, sasa ulienda kwenye hekalu la MUNGU au la shetani?  www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Unajua kwanini YESU aliingia kanisani akakuta wanauza njiwa na Meza akavuruga vuruga, aliingia kimwili maana rohoni hawakusikia na mimi nawafundisha  kimwili na kiroho kuwa sanamu hazitakiwi kuabudiwa maana zimetengenezwa na wanadamu,  MUNGU hafananishwi na chochote ni ukosefu wa adabu mbele za MUNGU mimi Nabii Hebron, nasema hivyo niko na MUNGU na hakuna kitakachonitikisa maana  hakuna kitu kinachoweza mtikisa MUNGU, shetani na majeshi yake na Malango ya Kuzimu hayawezi kunitikisa maana wote wapo chini ya miguu yangu kwa sababu MUNGU amejaa, YESU amejaa, baadhi ya wanadamu ndani ya mioyo yao, imejaa umbea, hila, wivu, viburi na mambo kama hayo, Je!  MUNGU atakaa wapi? www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 Namshukuru MUNGU, katika Nchi kiongozi wa Nchi anaomba Neema ya MUNGU itunusuru na majanga ambayo yapo na yanapita, na anawahimiza na kuwahamasisha wananchi wake wamtegemee MUNGU na kuwatia MOYO wasiogope kwani MUNGU anaweza na kuhimiza kuwa tutegemee Neema yake kwani MUNGU pekee ndio anaweza kutuvusha. (Kumbuka wana wa Israel walivyovushwa na bahari iligawanyika wakapita kwa wepesi, lakini kibinadamu wangeliambiwa bahari ingeligawanyika wasingeliamini - akili za mwanadamu lakini kwa MUNGU iliwezekana) lakini baadhi wa watumishi wamekata tamaa, wamekuwa waoga, wanaona mauti hawauoni uzima ambao ni YESU, ni kweli kila mmoja ana siku yake ya kufa lakini katika jambo hili kweli watakufa maana wamekukiri kwa vinywa vyao kuwa wanaogopa, inatia moyo pale ambapo kiongozi wa Nchi anamtegemea MUNGU lakini inashangaza endapo au pale ambapo baadhi ya wale ambao tunawajua wanatuongoza katika nyumba za ibada wanaogopa kufa, wamekata tamaa kama vile MUNGU hawezi, kweli yamkini mungu wao hawezi ila MUNGU wa Ibrahim, Isaack na Yakobo anaweza.  Simama imara usitishwe kwa kuambiwa kuwa hatutakuombea ukiwa mfu (maana baadhi ya makanisa mtu akiokoka wanamtenga na kumtishia kuwa endapo atakufa hawatamfanyia ibada) fikiria faida ni ipi kuombewa ukiwa mfu na kwenda kwa shetani au kuamua kuokoka ukiwa hai na ukaurithi uzima wa milele? Amua sasa.  Unapenda kufanyiwa kumbukumbu duniani ya wafu wakati umeshakufa na kwenda kwa shetani Kuzimu au ufe katika Bwana YESU, YESU akuchukue ukaishi milele kwenye ufalme wa MUNGU? Msiwe na Imani za kufa kufa utakufa ona uzima na hata ukifa basi ufe katika YESU, siku na saa ambayo Bwana MUNGU atataka. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 Jiulize u hekalu la nani wewe? Majini wamejaa ndani yako kwanini usiwaambie ondoka? MUNGU anasema mtakuwa kichwa bado mnakuwa mkia, najua wengi mu hekalu la MUNGU lakini sio kwa kiwango kile cha kuridhisha, mimi nakujenga sasa hivi uwe hakalu la MUNGU ili nikikuambia utafika kwa sababu ni hekalu la MUNGU utafika.   Lazima umpokee YESU wanaokuambia usiokoke waambie nimewatambua kuwa sio wa YESU na walikuwepo toka zamani na ndio maana wakamkataa YESU na walikasirikia YESU maana walijua kuwa alikuja kuharibu mahekalu yaliyokuwa yamejengwa na shetani ndani yao. Na mimi Hebroni nimekuja kuharibu kazi za Ibilisi maana ninyi ni mali na ni watu wa MUNGU amua, amua, amua, nakwenda kulivunja hekalu la shetani, na ujue kama ndani yako liko hekalu ambalo sio la MUNGU tambua kuwa majini, na mapepo, shetani na mawakala wake wamefunga ndoa na wewe kiroho kwa kujua na kwa kutokujua ili waendelee kukutawala sasa kubali kuvunja ndoa hiyo ya kiroho waliyofunga nawe kwa jina la YESU, ili wakuachilie na kama watu wa ukoo wanaokupa masharti, (maana ukoo nao una mahekalu yake ya mila na desturi za wazee) waambiie ukoo wako ni YESU mmenielewa? www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Jambo lingine Hekalu linaweza kuharibika pia kwa sababu ya tabia za ajabu  kuna watu wana vifungo vingi na Roho Mtakatifu ananielekza kuwa kuna watu wana chain (mnyororo) ya miunganiko kwa sababu ya tabia zao za kutokuwa waaminifu wengine wanashindwa kuoa au kuolewa, binti au kijana, watu wazima au hata vikongwe anahahidi Zaidi ya watu 40 kuwa watamwoa au kuolewa; inafika wakati sada   unataka kuolewa /  kuoa au mchumba anakuja anakutana na wale 40 wote sasa yupi atakuoa au utamwoa maana  umeahidi wengi na kiroho ahadi zile zinashikilia na mbona miili yenu mmeifanya kitega uchumi? Ukiwa na tamaa hilo ni pepo.  Kama una hekalu la MUNGU MUNGU angelikuongoza kwa mtu sahihi wa kuoa au kuolewa nae,  Hatimaye unabakia mtu wa kuahidi  wanawake au wanaume mpaka siku ya kuoa unakuwa na wengi, pale ambapo unaingia kwenye ndoa na ahadi zote ulizoahidigi zinaingia na wewe (yaani mabinti au vijana ambao umewaahidi, maana huo mnyororo au chain ya hizo hekalu za uongo na uzinzi hujazivunja na hatima yeke ndoa inakuwa ngumu haidumu haina upendo na hatimeye kama hujapata neema ya MUNGU ya kutatiwa huo muunganiko ndoa hiyo huvunjika – Maana wote uliwaambia unawapenda na upendo huo umeugawanyagawanya sasa ukimpata yule ambaye ni wako hatakuwa na upendo na wewe. Hatimaye unakuwa umeteleza au kutelezateleza tu maana wako uliowaliza, uliowaumiza, uliowalaza njaa na mambo kama hayo na mbaya Zaidi unaingia kwenye ndoa bado unampigia simu mpenzi wako wa zamani wakati una ndoa mhhhh hiyo ni hatari badiliaka) www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Roho Mtakatifu amekuwekea Imani ya kuona mambo makubwa na Mazuri lakini Imani yako imekufa kwa sababu unasoma biblia ambayo imeagiza ubatizo wa Mbinguni, lakini wewe mwenyewe hujabatizwa hivyo, Je! Ubatizo wa Mbinguni ukoje? Ni ubatizo wa maji mengi ambayo yanatiririka na  wa kikombe na kisima wa vumbi wa bahari wa swiiming pool na mingineyo imetokea wapi? ni wa la hekalu la shetani  hivi kwanini MUNGU anabadilishwa? hii ni tabia mbaya nitawaambia Wachina,  Waarabu, na mataifa yote ukweli bado nipo, hii dunia itabadilika yote  na itamfuata Bwana YESU, nawaambia ila hamuamini lakini ipo siku dunia itabadilika na kumfuata Bwana YESU, shetani ametamba sana, hata hili kanisa La YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE,  hili kanisa shetani halipendi kwa sababu si la kwake  na asilipende na mimi simpendi na mawakala wake waendelee kuyeyuka tu  na wana hali mbaya ni wakati wa Bwana YESU sasa na Mwokozi anarudi,  uliyekata tamaa nyanyuka, simama imara omba Rehema, kata connection za wachawi twende mbele,  Ni kama vile vile kipindi cha Musa,  wale ambao walimsikiliza Musa walifika na wale ambao hawakumsikiliza waliishia njiani,   walimsikiliza Musa na kitu cha MUNGU kikajengeka ndani ya Mioyo yao na wao wakapata Neema ya kuvuka bahari wale ambao walimkataa walikufa na zamani walikufa kimwili kabisa na hata sasa nisikilize twende mbele zamani walikufa kimwili na sasa wanakufa kiroho unakuwa maiti, unatembea lakini umekufa, Bwana YESU anakuhitajii ili chemichemi za Baraka ziwe katika maisha yako www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Mahekalu ya Ibilisi yavunjwe, hekalu la Kupinga sauti ya MUNGU livunjwe, la kupinga kweli ya MUNGU livunjwe, na hekalu la MUNGU lijengwe, hekalu la Mbinguni lazima lihubiri kweli si kuchanganya uongo na kweli navunja na nabomoa hekalu la Ibilisi na kujenga la MUNGU ni lazima maisha ya watoto wa MUNGU yainuliwe www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Baba MUNGU naomba na wengine wafunguke na wapate Neema hiyo ya kukujua wewe wasije wakawa wafalme, halafu wasisikilize sauti yako MUNGU na MUNGU ukawatandika kwa kushindwa kukusikiliza ujumbe wako, ni wakati wa kumjua MUNGU. MUNGU aneniambia Nabii wangu sema hivi, baadhi yenu mna viburi, na viburi vyenu vitawafanya muangamizwe, mtagongwa, mtapigwa na MUNGU, shukeni, nyenyekeeni kila mwanadamu akili yake si kitu mbele za MUNGU pamoja na utajiri wako, au umaarufu wako,  bado wewe ni mali ya MUNGU kwanini ujifanye una akili mbele za MUNGU?  rejea sasa, hii ni oder kwa kila mtu wa kila rangi, yeye  ni MUNGU kila mtu na kila kitu ni mali ya MUNGU, Mikoa na Serikali, Mikoa na Vijiji vyote ni mali yake ila nawapenda niwaeleze kuwa  baadhi ya nyumba za ibada ni mali  ya MUNGU ila sio zote nyingi ni mali za shetani, na watu wengi wamejiopeleka huko, wanatoa watu kafara na watu wengi wamejipeleka huko, na viongozi wake wakitaka kufa, wanambadilisha kifo kwa mwingine, lakini nimemwomba MUNGU kifo chake (mhusika) kitakuwa chake, (Mhusika) na kitamkuchukua tu, na wale ambao wameingia kwa shetani sasa nimefunga  njia zenu na mkitaka kuongeza nguvu haitawezekana tena  (No recharging any More) Wana wa MUNGU msonge Mbele. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Mnajua niyi ni wa watoto wa Mfalme, YESU Kristo ila maisha ya wengi hayako kama ya watoto wa Mfalme, lakini kuanzia sasa usikubali mtu / Shetani wala mawakala wake wakavunja hekalu la YESU ndani yako, kwa YESU kuna raha, amani, ushindi, upendo, Pumziko, Furaha Baraka za kiroho na kimwili na upenyo kumbuka shetani, mapepo na maajenti wa shetani wanakuonea wivu sema sasa nakata cheni zenu na siwataki tena. Amen. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

Sema: Bwana YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, nilizozifanya kwa kujua  na kutokujua, nakuomba Bwana ukalibomoe hekalu la  ibilisi na maajenti wake katika ulimwengu waroho, lilijegwa  ndani ya moyo wangu, ndani ya mwili wangu, mimi ni hekalu lako, ukajae Bwana ukaondoe kila takataka katika ulimwengu wa waroho, na Mwili nikaone furaha yako bwana, najitenga na mahekalu yote ambayo ni  kinyume na MUNGU nahitaji YESU ukae, Roho Mtakatifu Ukae, MUNGU baba uliyeumba Mbingu na dunia ukae,   wewe peke yako ukae,   na nguvu zako  zikae,  na Baraka zako zikae na uweza wako ukae na ahadi zako zikae,  hakika ninajua kwamba ibilisi ameanguka sasa. www.prophethebron.or.tz/www.prophethebron.org

 PROPHET HEBRON WILSON KISAMO.