Kanisa na watu wote nawatakia heri ya krismasi na mwaka mpya
2018. Muwe na krismasi njema na baraka zake ziwe juu yenu katika jina la YESU
wa Nazareti. Bila kusahau katika sikukuu hii ya krismasi tunakumbuka siku ya
kuzaliwa kwake mwokozi wa ulimwengu huu na cha kujiuliza kwa anayesherekea je
unausherekea kuzaliwa kwake Bwana YESU?
Basi ingekuwa vizuri watu waokoke wamkiri yeye kama Bwana na
mwokozi wao, siyo kusherekea na kufurahia hiyo siku yake wakati haumkiri kuwa
ni Bwana na mwokozi wa maisha yako, maana pasipo yeye, kama MUNGU asingemtuma
kuja hapa ulimwenguni sijui dunia ingekuwaje? Hivyo nawasihi mataifa yote
muokoke na kumpokea yeye ukimaanisha na unapoisherekea hiyo siku yake zipo
baraka ambazo atakupatia wewe uliyeokoka na kwa yule ambaye hajaokoka hawezi
kuzipata hizo baraka zake sababu yeye hamtaki halafu anataka baraka zake; ni
sawa na mtu hakupendi halafu anataka umsaidie ni vigumu.
Sasa mfunguke fahamu na mzidi kumpenda huyu mwokozi mkimpokea
kwanza na yeye atawafurahia sana, siyo tena kubakia kuitwa mkristo halafu
hamtaki kuokoka, unajipotezea muda wako utakuwa kama msindikizaji ila kwa
safari hii okoka.
Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote uniandike
jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele.
Ubarikiwe na ufunguliwe.
Merry Christmas and Happy new year 2018.
NABII
HEBRON.
