Pages

Tuesday, January 24, 2017

JE, INA MAANISHA NINI WATU WANAPOZIKA BIBLIA KATIKA MAKANISA, NYUMBA AU KATIKA MALI ZAO?

KWA NINI WATU WANAZIKA BIBLIA?

BWANA YESU ASIFIWE, YEYE ALIYE HAI MILELE! Katika makala hii nitaelezea kwa nini baadhi ya wakristo katika ulimwengu huu wanazika Biblia au kufukia Neno Takatifu la MUNGU katika ardhi au katika misingi ya nyumba zao wakati wakijenga na wengine hata kufukia katika ofisi wanazofanya kazi na wengine katika nyumba za ibada.

Nataka ulimwengu uelewe kuwa hili ni jambo baya sana na ni dhambi kwa MUNGU, unapofanya hivyo unakuwa umemfukia MUNGU, haumtaki aishi na wewe na badala yake unaipokea miungu ya kikristo badala ya kumkubali MUNGU aliye hai ambaye ndiye MUNGU wa miungu ambaye siku moja ataihukumu miungu na akiihukumu basi uelewe wazi kwamba atawahukumu na wafuasi wa miungu hiyo. Kipindi hiki ni cha hatari tunapomsubiri YESU katika unyakuo, shetani nae anazo mbinu nyingi za kuhakikisha anawateka wakristo katika njia mbali mbali ambazo hata watu wasizozijua ikiwemo njia hii ambayo ninaifichua mimi Nabii Hebron.

Sasa utajiuliza inakuwaje baadhi ya watumishi wanafundisha watu kufukia Biblia. Watu wengi pasipokujua na wengine wakijua wameipokea elimu hii, wakati kufukia Biblia ni kumzika MUNGU. Kila mtu  anajua kuwa Biblia ni kitabu kitakatifu kutoka kwa mwenyezi MUNGU kwa ajili ya kutuongoza wanadamu kiroho na kimwili kama  katiba takatifu ya MUNGU, hata ukisoma kitabu hicho hakuna mahali imeruhusiwa kizikwe au kifukiwe bali ukisoma katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana  22:18-19 utaona ni maonyo tupu.
Lakini msishangae iliandikwa watakuja wapinga kristo na watawapoteza wengi, huu ni mfano halisi, yamkini na wewe ni mmoja wapo kati ya wale waliozika Biblia. Nataka muelewe ulimwengu wote, asili ya kuzika Biblia imetokea kwa watumishi ambao wameletwa na miungu wafanye injili za miungu na siyo injili ya MUNGU aliye hai, wanatumia jina la YESU kuwadanganya watu wakati lengo lao ni kuwakosanisha wanadamu na MUNGU aliye hai pasipo mtu kupenda au kujua na kujikuta umepatanishwa na miugnu ya kikristo pale tu anapofanya hivyo.

Hilo linakuwa ni agano ambalo mtu ameingia na miungu ya kuwa MUNGU aliye hai asiishi katika maisha yake bali miungu wafu iishi na ndiyo atakayoiabudu na zaidi mtumishi anayeyafanya hayo ni lazima afanye maagano ya kuzika Biblia ili miungu imsaidie katika kazi hiyo ya utumishi wake japo kimwili atasema yeye ni mtumishi wa MUNGU ili watu wasimwelewe ila katika ulimwengu wa roho yeye anaiwakilisha miungu na kazi ya miungu ni kuiharibu kazi ya MUNGU aliye hai ikiwemo kuzika Biblia.

Na zaidi imeandikwa kuwa itafika wakati biblia hizi za kweli hazitapatikana basi uelewe hii ni njia moja wapo ya kuzimaliza Biblia za kweli kwa kuzifukia ardhini ikimaanisha kuwa Neno Takatifu halitakiwi bali biblia za uongo ndizo zipatikane na kwa kutumia biblia ya uongo basi ndivyo na wewe umetekwa na miungu na hicho kinakua ni kibali cha miungu kukuteka. Sasa uelewe na uepuke hizo mbinu chafu, ng’ang’ana na MUNGU aliye hai.

Cha kufanya kwa wewe ambaye umezika Biblia, tubu na uifukue popote ulipoizika ili miungu ikuachie na umrejee MUNGU wa kweli aliye hai. Na zaidi nasema hivi nikiwa na uhakika 100%, kila anayeongoza watu kuzika Neno la MUNGU aliye hai, yeye SIYO mtumishi wa MUNGU aliye hai bali yeye ni mtumishi wa miungu na baba zake ni miungu na hata akikuongoza wewe muumini hata wewe utakuwa mwana wa miungu, jinsi alivyo kuhani ndivyo na kondoo alivyo.

Zaidi ukikuta madhabahu waumini wanaambiwa waweke vitu vyao, iwe ni dhahabu (gold), pesa, picha au majina ya vitu vyao wakaambiwa vizikwe madhabahuni na vikajengewa utambue kuwa madhabahu hiyo ipo chini ya miungu na siyo MUNGU aliye hai, hilo ni agano la miungu ambalo linaipa nguvu hiyo madhabahu iweze kufanya kazi na siyo Roho wala siyo MUNGU wa mbinguni. Kwa kuzika vitu hivyo ina maana pia vitu vyao na maisha yao huzikwa na miungu au kwa lugha nyingine hivyo vitu au hao watu wametolewa kafara katika madhabahu ndiyo maana majina yao yanafukiwa chini. Kama unaabudu mahali kama hapo kimbia sasa na umrejee MUNGU aliye hai.
NABII HEBRON.