Pages

Tuesday, October 18, 2016

SHETANI AMEPANGA KULETA KILEVI AMBACHO KITAITWA KWA JINA LAKE KWA LUGHA YOYOTE ILI WATU WAANGAMIE.
WARNING!!!
BWANA YESU WA NAZARETI ASIFIWE SANA! Mimi Nabii Hebron, nawasalimu mataifa yote na mwenyezi MUNGU anawapenda sana, hataki muangamie kabisa. Kama nilivyoelezea, YESU aliponiita nimtumikie kuanzia mwaka 2009 aliniambia kuwa ulimwengu umeshikwa na shetani na kanisa limetekwa na shetani 98%  na 2% tu ndiyo ipo na mwanae wa pekee YESU wa Nazareti.

Shetani amebuni njia nyingine ya kuwapata watu na kuwateka kwa wepesi na hii itatokea katika nchi mbali mbali. Vitasambaa vinywaji ambavyo vitaitwa kwa jina la shetani kwa lugha yoyote na atawatumia wanadamu ambao wapo katika ufalme wa shetani. Pale tu utakapokunywa hicho kilevi au kinywaji utakuwa umemmeza shetani na ataingia kwa nguvu sana katika maisha yako na ataishi ndani yako badala ya YESU kuishi ndani ya mwili wako na mwili huo kuwa ni hekalu la shetani na kumzuia mwanadamu asiwe hekalu la MUNGU kwa njia hiyo.

Kila atakayekunywa kwa kujua au kutokujua, shetani atakuwa tayari ndiye anayeishi ndani yake na mtu huyo atakuwa ni mali ya shetani. Tayari atakuwa ameshavunwa na shetani.

Watumie ujumbe huu mataifa yote. Nimeelezwa na YESU WA NAZARETI, nami nawajulisha watu wote kwa jinsi YESU alivyonijulisha.

Zaidi muokoke; Sema, BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, uandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele. Najitenga na vilevi vyote visinitawale katika jina la YESU. Amen.


NABII HEBRON.