JE
UNAJUA yesu ASIYEJULIKANA KUWA ANAO WAFUASI WENGI ZAIDI YA YESU ANAYEJULIKANA??
BWANA YESU ASIFIWE, watu wa
mataifa yote, nawaandikia ulimwengu wote kuielewa habari hii ya yesu
asiyejulikana ili watu wasiomwelewa wamjue na wamkatae na wamrejee YESU anayejulikana
na ambaye ndiye Mwana wa pekee wa MUNGU aliye hai ambaye yuko mbinguni. Wakati
wake YESU wa kurejea kulichukua kanisa umefika, ni wakati wowote, hii ni siri
ya MUNGU peke yake ambaye anaijua siku hiyo. Habari hii mimi Hebron nilielezwa
na MUNGU peke yake nami nawaeleza mataifa yote kwa sababu yeye ni MUNGU wa watu
wote na mataifa yote zaidi yake hakuna mwingine. Ukisoma kitabu cha Matendo ya
Mitume 19: 14-16
“14 walikuwako wana
saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu waliyofanya hivyo. 15
Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, YESU namjua na Paulo namfahamu, lakini
ninyi ni nani? 16 Na yule mtu aliyepagawa na pepo
mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika
nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa.”
Nitaelezea kuhusu huyu yesu
asiyejulikana yukoje. Nitaelezea katika neno la MUNGU na siyo katika sura. Jina
la YESU ni jina mashuhuri kuliko majina yote ya viumbe vyote duniani na
mbinguni na popote pale. Huyu YESU alipokuwepo hapa ulimwenguni alisema
watakuja watu watakaotumia jina lake na hata kuwapoteza wengi hata wateule na
yawezekana wewe ni mteule lakini pasipokujua au kujua tayari na wewe upo katika
ufalme wake, shetani amekuteka na amekuwa ndiyo kiongozi wako na tegemeo lako.
Nitaelezea kwa ufupi jinsi ya
kumjua huyu yesu asiyejulikana na anafanya kazi kubwa ya kuuangamiza ulimwengu
au kuwavuna wanadamu wawe mazao ya shetani au kwa lugha nyingine ni mpinga
kristo.
Kila mtu anajua kuwa Yohana
mbatizaji ndiye aliyetumwa amtengenezee njia huyu YESU, soma katika Matendo ya
Mitume 19:4, Yohana akambatiza YESU kama alivyotumwa na MUNGU mbinguni yeye
aliyetuonyesha njia ya kweli kiroho na kimwili na akasema tuifuate njia yake
kama alivyoonyesha, na katika kitabu cha Ufunuo 22: 18-19, akasema, mtu yeyote
akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki mtu huyo ataondolewa
sehemu yake ya uzima, na je ikiondolewa kinachobakia basi ni sehemu ya mauti,
hukumu au jehanamu ya milele.
Alivyosema watatumia jina langu YESU alijua na aliona mbele
na ndivyo ilivyo na imekuwa na mnayaona kwa sababu kila alilolisema YESU neno
lake lazima litimie yeye ni MUNGU.
NOTE:
Huyu
yesu asiyejulikana na kama hajulikani ina maana yeye hajazaliwa na Maria hapa
duniani wala hakufa na kufufuka wala hakuonekana akitenda miujiza yeyote wala kuhubiri
hapa duniani.
Huyu yesu asiyejulikana hutumia
biblia kulichanganya neno la MUNGU wa kweli na mafundisho ya uongo ambayo
hayapo katika biblia. Kama angetumia kitabu kingine tofauti na biblia watu
wangekataa, hivyo alibuni njia hiyo na akafanikiwa kuwateka wengi zaidi na watu
waka amini wapo sehemu sahihi kabisa wakijua wataenda mbinguni na kumbe katika
ule mwisho wataenda jehanamu iwapo hawatabadilika leo na kumrejea yeye YESU wa
kweli ili watengwe na huyo yesu asiyejulikana.
YESU anayejulikana yeye alisema
tubatizwe kama yeye katika maji mengi yanayotembea. Sasa huyu yesu
asiyejulikana yeye ana viapo vyake na unapovipokea tu na wewe unakuwa mfuasi wa
yesu asiyejulikana bila kujua wala kupenda japo wapo wengine wanaopenda.
Ubatizo wowote ambao ni tofauti
na YESU alivyobatizwa unakufanya kuwa mfuasi wa yesu asiyejulikana kwa sababu
ni viapo visivyo kuwepo katika kitabu kitakatifu cha neno la MUNGU.
Ubatizo wa maji ya kikombe, je ubatizo
huu utasema ni wa YESU anayejulikana? Jibu siyo. Unapompokea tu na wewe
unafanyika kuwa mfuasi wa yesu asiyejulikana. Kama unabisha tafuta ni wapi YESU
alibatizwa kwa maji ya kikombe? Na zaidi neno kubatiza maana yake ni
kuzamishwa, je huoni kufanya tofauti ni uongo mtupu.
Umemwagiwa maji matone
wakati miguu, mikono, mgongo, haujaingia katika maji! Hivyo usipinge, acha kutetea
uongo, unapoutetea na wewe unapokea dhambi ya kuiharibu injili ya kweli na
kuimarisha uongo, huyo ni yesu asiyejulikana, hivyo hata ibada zako, maombi
yako, sadaka zako, uelewe unampatia yesu asiyejulikana.
Hivi nikuulize wewe unamjua
yesu aliyebatizwa katika maji ya kisima?
Sema ukweli, jibu lake ni haumjui!
Hivi unamjua yesu aliyebatizwa
kwa jina la mchungaji? Huyo hajulikani, huyo ni pepo.
Hivi unamjua yesu anayetoza
watu pesa za maombezi? Mimi Hebron simjui wala siyo YESU aliyezaliwa na mama
Maria wala siyo YESU ambaye ndiye mwana wa pekee wa MUNGU, na wewe mkatae huyo
yesu asiyejulikana na mambo yake. Namfahamu YESU aliyesema “nimekupa bure, toa bure” huyo
ndiye YESU anayejulikana. Ukikutana na maombezi ya pesa uelewe unakutana na
yesu asiyejulikana au yesu wa wanyang’anyi au wezi.
Yesu asiyejulikana yeye hufufua
misukule kwa mazingaombwe bali YESU anayejulikana yeye alifufua kina Lazaro na
wengineo waliojulikana na jamii na watu wakawaona kwa macho ya nyama na
wakafufuka. Hao wanaofufua misukule ni wachawi, wapeleke hospitali maiti
zimejaa mortuary hawatafufua, watakimbia. Hao wanafanya miujiza ya kichawi.
Ili uwe na YESU anayejulikana
ni lazima uokoke, ila huyu yesu asiyejulikana utajiita ni mkristo na wala
hautaki wokovu. YESU anayejulikana yeye alileta wokovu ili kila atakayempokea
awe mfuasi wake na asiyempokea hatakuwa mfuasi wake. Sasa huyu yesu wa uongo
yeye anaaminiwa na watu wengi zaidi katika ulimwengu wote na mataifa wamepigwa
upofu wanaona wapo sawa sawa wanampendeza MUNGU wa mbinguni kumbe wanamchukiza
MUNGU wa mbinguni kabisa na kumkana kwa hayo matendo.
YESU anayejulikana katika
kitabu kitakatifu cha BABA yake (Biblia) amesema usitoze riba, ila huyu yesu asiyejulikana
yeye huweka benki na kutoza riba. Hapa sasa mnaelewa tofauti ya YESU
anayejulikana na asiyejulikana na yapo mengi utazidi kufunuliwa ili hili giza
liondoke katika maisha yako na kwa wengineo.
Imeandikwa nyumba ya BABA yangu
ni nyumba ya sala, YESU anayejulikana alipoingia katika nyumba ya ibada
akayakuta yameletwa mambo ya yesu
asiyejulikana, aliyatupia nje. Sasa yamerudishwa na kutawala, mfano harambee,
michango, mwenye pesa anatoa ndiyo anaombewa, kulazimishwa kuahidi utatoa pesa
ngapi na mengineyo. Mimi Nabii Hebron nawaeleza huyo ni yesu asiyejulikana,
mimi simfahamu na simtaki kabisa, na wewe mkatae, ni mnyang’anyi 100%.
Huyu yesu anayewapenda matajiri
tu, huyo ni yesu asiyejulikana hata hao wanaoona wanakutana na YESU kupitia
huyo mtumishi nawaeleza wamekutana na myang’anyi, ni pesa zao ndizo
zinazotakiwa tuu na si chochote.
YESU anayejulikana yeye
alianzisha huduma tano (5) zilizoongozwa na Mtume na Nabii, wala hakusema
huduma ya uaskofu ndiyo iongoze kanisa na hii ya uaskofu ni huduma ya sita na
huduma hii ya uaskofu kibiblia ni kazi ya uangalizi wa kanisa kama kufanya
usafi, kupanga viti na mengineyo.
YESU anayejulikana amesema
utoapo sadaka yako iwe ni siri yako tu. Isijulikane na mtu. Ila yesu
asiyejulikana yeye sadaka utaandika jina, utapewa risiti na hata utapewa cheti
cha hongera umetoa vizuri, zaidi huyu yesu asiyejulikana husoma majina ya watu
waliotoa sadaka kupitia mtumishi wake katika kanisa lake, kinyume cha MUNGU
alivyoagiza katika neno lake au sheria.
Yesu asiyejulikana ili
kumwelewa kwa wepesi yeye huchanganya uongo na neno la MUNGU yaani giza na
nuru, na tunajua kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya giza na nuru.
Yesu asiyejulikana na yeye vile
vile ana manabii wake, mitume, wachungaji, wainjilisti, waalimu na zaidi wale
watumishi ambao hapo awali walikuwa wameitwa na MUNGU kisha wakamuasi MUNGU wao
hujiunga na huyu yesu asiyejulikana na kuendeleza yale ya uongo wakijificha kwa
kutumia jina la YESU.
Watumishi wa yesu asiyejulikana
hutumia uchawi, mizimu, kwenda kuzimu, hutoa makafara na hata makanisa yao katika
ulimwengu wa roho hufanyika kuwa sehemu ya kuwatoa waumini kafara na sadaka kwa
shetani hiyo huwa ni siri ya kuhani na maagano yake na shetani.
Je, umeshajiuliza ni kwa nini
wakristo wengi zaidi wanateseka, wanalogwa na shetani na wachawi? Jibu ni kwamba
ndani yao hayupo YESU anayejulikana na huyo hawezi kuwapiga wachawi, kwa sababu
ufalme ulio pamoja hauwezi ukaufitini ufalme mwenzake.
YESU anayejulikana yeye
alivyokuwa mtoto alibarikiwa tu na alipokuwa mtu mzima alibatizwa, huyu ndiye
mfano wa kuifuata. Ila yesu asiyejulikana yeye hufanya kinyume; mtoto mdogo
humbatiza (tena uongo), hazami kwenye maji na akiwa mtu mzima ndiyo hubariki
sasa angalia huu upinzani unavyopewa kipaumbele na yale ya YESU anayejulikana
hayatakiwi.
Nawasihi mataifa yote mrejeeni
YESU anayejulikana, wakati ni sasa, ukifa pasipo kupata huyo YESU wa kweli
hakika utakwenda kwa huyo huyo asiyejulikana ambaye anayo mbingu yake
isiyojulikana (amabyo ni Jehanamu) na usifanye kazi ya yesu asiyejulikana
utaangamia, unapata dhambi unafanya kazi ya shetani pasipokujua.
Kwa YESU anayejulikana yeye
mkitaka kumwomba MUNGU mnapitia kwake (YESU anayejulikana) tu na siyo kwa
watoto wa MUNGU waliopita. Ila kwa yesu asiyejulikana, unapitia kwa watakatifu
waliopita ambao ni watu kama wewe tu, na kukupeleka jehanamu. Hapo unakua
unaabudu mizimu na majini ya miungu.
Sema, BWANA YESU unayejulikana
naomba unisamehe dhambi zangu zote. Namkataa shetani na kazi zake na sikutaki
tena wewe yesu usiyejulikana, toka ndani yangu. Kuanzia sasa wewe YESU unayejulikana
ingia ndani yangu wewe ndiye mwana wa pekee wa MUNGU aliye hai. Amen.
Ubarikiwe! Watumie na wengine.
NABII
HEBRON.