Pages

Saturday, September 10, 2016

MKRISTO SHITUKA

YOHANA 3: 1-21

Amani iwe nawe mwana wa MUNGU aliye hai, nakusalimu katika jina la YESU KRISTO WA NAZARETI. Siku ya leo nataka ujifunze kitu kimoja ili upone umrudie YESU uende mbinguni usiende jehanamu.

Kwanza kabisa napenda nikufahamishe kwa mfano wa Nikodemu kwenye somo hilo juu kwenye kitabu cha Yohana 3: 1-21; maana yake ni kwamba YESU alikuja kuleta wokovu siyo dini na kwa yeyote ambaye atasema ameokoka na yuko mahali panapofanana kwa baadhi ya mifano iliyoko hapa chini ujue hujaokoka bado, uko gizani, angalia ukweli huu. Na neno la MUNGU linasema ; tokeni mkatengwe nao, hivyo unapookoka unatakiwa uondoke kabisa huko wanapopinga wokovu; kwa sababu wokovu ndiyo YESU.

·        Wengine wanaabudu na kubusu msalaba we unasema umeokoka uko kati yao hujaokoka. Uko kati ya waabudu sanamu hujaokoka. Msalaba siyo alama ya mkristo, bali msalaba ni alama ya laana na YESU alikufa kwa ajili ya laana zetu, ili sisi tupone. Na toka awali msalaba ilikuwa ikitumika kuua waliohukumiwa. Alama ya mkristo ni wokovu ndani ya mtu katika roho na kweli. Na zaidi kama msalaba ingekuwa ni alama ya YESU basi hata makaburini wachawi wasingeenda kufukua mizoga, wangekutana na YESU hapo na hata wanaovaa shingoni wasingelogeka au kuteswa na mapepo.

·        Uko kati ya ibada ya wafu au ibada ya njia ya msalaba hujaokoka, uko kati ya kuomba wana wa MUNGU walioko mbinguni ndio wakuombee na wakati YESU yuko mkono wa kuume wa BABA kutuombea hujaokoka, uko kati ya kumuomba mama fulani au kuomba kwa kutumia shanga; hujaokoka. Umebatizwa ubatizo wa kikombe, ubatizo wa  kisima (baptism of the well) haujaokoka, umebatizwa ukiwa mtoto mdogo hujaokoka, uko kati ya mahali wanabariki watoto wakubwa haujaokoka.


·        Uko kati ya wanaoabudu sanamu na wewe unasema umeokoka; haujaokoka. Uko ndani ya kanisa ambalo wanapinga wokovu ukiwa hai na wewe uko kati yao unasema umeokoka hujaokoka.


·        Unaabudu kwenye kanisa ambalo lina makaburi ndani; hujaokoka. Neno linasema ukimkiri YESU na kubatizwa maana yake kumkubali na yeye na usiwe na michanganyo toka huko leo mtafute YESU wa kweli ambaye atakuongoza na kukupeleka mbinguni. Nakufungua macho yako upate kuona na kutambua hapo ulipo siyo mahali YESU alipo, kubali kutoka sasa uokoke kweli kweli usiwe vugu vugu.

Sema sala hii; BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizozifanya kwa kujua na kutokujua. Namkataa shetani na mambo yake yote, nakukubali wewe uwe BWANA na mwokozi wa maisha yangu. Andika jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele. Asante BWANA YESU kwa kuniokoa. Amen.


APOSTLE DORCAS (Sophia) MDEE.