Pages

Wednesday, June 29, 2016

JINSI HUKUMU YA MWISHO WA DUNIA ITAKAVYOKUWA!!!

BABA katika jina la YESU, ninakushukuru ninakutukuza. Ninawaombea wasikilizaji na watoto wako na mimi ninaomba nguvu zako na uweza wako, Uweze kuniwezesha kuelezea jinsi  ulivyonielekeza “Jinsi hukumu itakavyokua.” Na ulivyonionyesha maandalizi uliyoyaandaa na serikali ilivyojiandaa kwa ajili ya hukumu ya mwisho. Nikaweze kueleza watoto wako, wakapate kufunguka na wengine wakurudie wewe maana unawapenda. Amen

Haleluya. BWANA YESU ASIFIWE! Katika mda huu nitakwenda kuelezea jinsi  hukumu itakavyokua na jinsi MUNGU alivyonionesha na YESU alivyonielekeza na kile kitengo cha hukumu ya mwisho kilivyoandaliwa kwa sababu  kila kilichoandikwa kwenye biblia ni kweli kabisa mbinguni kinavyofanyika. BWANA YESU ASIFIWE! Nikaonyweshwa watakao ingia mbinguni ni wale walioalikwa harusini. 

Waliompokea BWANA YESU na kuishi maisha ya kuolewa na BWANA YESU na kuishi maisha ya kumkubali YESU kuwa ni BWANA  na kuishi maisha matakatifu. Itakua ni siku ya kutisha lakini mbinguni ni shangwe, shetani itakua ni siku  ya kuuzunika, kwa Malaika itakua ni shangwe na furaha na kwa serikali ya Mbinguni itakua ni shangwe. Mbinguni watapiga mpaka matarumbeta, kutakua kuna sherehe ya ajabu kwa ajili ya kuwapokea walio mkubali BWANA YESU watakaokua wameshinda. Nitawaelezea kwa kifupi ni mambo mengi sana lakini yale ambayo ROHO MTAKATIFU atakayokua ananiongoza ndani yangu nitasema.

Kama unavyofikiri kwamba YESU atakuhukumu hivi , aha ! Yeye atakaa mbali sana. YESU anao wasaidizi wake ni kama hapa duniani Raisi alivyo na watu wake. Muundo ni kama huu lakini kwa YESU  kuna vitu vingine vinaongezeka zaidi. Nataka kuwaeleza kila kitu unachokifanya hapa duniani kuna mtambo unaokurekodi Mbinguni. Matendo yako matakatifu,  masafi, toka siku unazaliwa mpaka sasa. Na hata waliokufa mpaka sasa walikufaje? Rekodi zao ziko kule. Umekaa katika Utakatifu? Siku ile ya mwisho utaonyweshwa Utakatifu wako. Sikukatishi tamaa na kutia moyo utakapotubu na kuacha lile faili linafutwa unakua safi.

Haleluya.Itakavyokua ni hivi; kutakua na Mawakili upande wa MUNGU kutakua na “advocates” upande wa shetani. Haleluya. Itakua kama vile mahakamani unavyoona watu, majaji wanavyo ulizana maswali na wewe mtakatifu, shetani atakavyo kushtaki. Kama kweli hauna kosa wale majaji ”advocates” upande wa MUNGU watakutetea kama ilivyoandikwa kwenye biblia kwamba “mshtaki wenu halali ana washtaki kila wakati.” Ni kweli mpaka siku ya mwisho atakushtaki. Niliona akishatki watu katika majibishano watu wenye dhambi, wasio na dhambi, wakristo, ambao hawajaokoka na wengineyo. 

Ni watoto wadogo tu ndio niliona wana neema hawana dhambi lakini huku duniani tukaambiwa kwamba abatizwe akiwa mtoto mdogo mana atakufa akiwa na dhambi hataenda Mbinguni. Ujiulize pia, kwa nini  YESU  alisema “Waacheni watoto wadogo waje kwangu mana ufalme wa mbinguni ni wao?” Bado wana asili ya ufalme wa MUNGU  hawajachafuka.

Utakapokua mtu mzima ndio utapata alama za shetani .Haleluya. Itakua ni mara ya tatu, mara ya pili sasa anakuja kulichukua kanisa. Atakaa miaka saba halafu atakuja mara ya mwisho sasa ambapo patakuwa kuna vita. Haleluya.Vita hivyo MUNGU  ndiye atakayeshinda lakini nakuja kwenye kuhukumu, kila mtu atahukumiwa kwa matendo yake. Hakutakuwa kuna hongo, hakutakuwa kuna upendeleo. Shetani yupo macho, MUNGU yupo macho.

Shetani anakudanganya usiokoke na siku ile ya mwisho atakushtaki hakukukubali wewe alisema anakula maisha, alisema next year na siku ile ya mwisho itaonyweshwa hivyo. Wengi watalia sana kwa sababu watakataliwa na MUNGU. Matendo yako yataletwa pale kama hujashinda utasogezwa kushoto,ukishinda utapelekwa kulia. Mpaka sasa nikuulize kama ni hukumu inafanyika sasa hivi utashinda? Kama utashinda ubarikiwe! Lakini wengi hawatashinda kwa sasa hivi.

Kila ambaye hajaokoka haendi. Ambao wamebatizwa kwenye ubatizo wa kisima, kwa jina la mchungaji , kwa tenki, kwa dramu hawataenda. Wanaishi kiutakatifu nimeomba sana, nimekutolea sadaka, kabisa siku ile ya mwisho, nilionyeshwa kitengo hicho  akaniambia nenda uwaeleze wakabatizwe upya hapo watakamatwa na shetani. Shetani ameungana na wanadamu watumishi baadhi yao amewawekea nembo za shetani.

Utasema nimeokoka,YESU nimekupokea. Shetani atasema “BWANA MUNGU wewe ni mwenye haki  wewe unaliangalia Neno lako angalia huyu amebatizwa ubatizo wa wapi? Na wewe YESU ulisema wewe ni mwalimu na wewe ulionyesha njia kabisa. Je, wewe ulionyesha njia hii? Hawajatimiza Neno lako. Huyu hastaili kwenda mbinguni anastahili kubaki na mimi.” MUNGU  ataanaglia Neno lake ataona ni sawa sawa; nenda kushoto. 

Nakuambia wewe unapotezwa sitaki ukaja ukalia mambo yatakua ya ajabu maana wengi wanampenda MUNGU,wanajitunza, lakini shetani anakutafuta mahali pakukushikia. Nchi mbali mbali wanasema kuna baridi, kuna barafu, hatuwezi kubatizwa mtoni; subirini maji yatakapo yeyuka mkabatizwe. Na wengine huko kwenye nchi za baridi, wanachemsha maji yanapata moto ndiyo wanabatizia kwenye kisima. Umepotea, maji YESU aliyobatiziwa hayakuchemshwa.Yalikua na uasili wa MUNGU mwenyewe. Maji yanapokuwa yamechemshwa, unaanza kuungua hapa duniani maisha yako kiroho unaungua  hapa na shetani atakushtaki siku ile ya mwisho.

Watu wengi  wanasema wameokoka, wamebatizwa, wamemaliza haki zote lakini siku ile ya mwisho shitaka litakuja. Ninawapenda wote na YESU amenipa uwezo wa kuwapenda, uwezo wa kusema ukweli, uwezo wa kuhubiri ukweli, nami  nakueleza .Kama unanipinga, unanichukia hunichukii mimi unamchukia MUNGU na ndivyo ilivyo siku ile ya mwisho katika hukumu utashtakiwa tena, ni mashtaka niliyokuwa naona .Shetani atasema  “huyu hakukuamini wewe, hakuamini neno lako, ni mnafiki anayejiita mkristo. Kwa nini hajabatizwa kama wewe?” Tazama na huyu Mtumishi ni wa kwangu. Je, wewe ndiye uliyewafundisha wakabatize watu kwa kikombe? Kwa kisima? Kwa jina la Mchungaji? Kwenye tenki? Sawa ameishi maisha matakatifu, je wewe ndiye uliyemtuma? Ni kama vile mahakama ya hapa duniani. Atafungua tena sehemu nyingine.Ulisema “ole” wake anayezuia watu kwenda mbinguni huyu si amezuia? Huyu aungane na wale. Haleluya.USIOGOPE.  Fanya mabadiliko umrejee BWANA YESU. Hukumu ile usifikiri kwamba kutakua na mafaili. Huko wana digital za kisasa zaidi kuliko za hapa. Nikaona mtambo, ile unakuja tu pale vitu vyako vinatokea vyenyewe wala hawa click. Na pembeni kutakua na malaika wakija kukukamata na wale watu laki moja na arobaini na nne na wazee ishirini na nne wakiwemo, wakishuhudia kinachoendelea.

Haitakua siku moja itakua ni mda mrefu sana, maana watu ni wengi sana. Mimi nilifikiri itakua siku moja 24hours, hapana. Itakua ni mda mrefu yakusubiri, lakini wewe ambaye utakuwa na YESU sawa sawa  utakuwa na neema  hautasogea katika kuhojiwa .Wewe utakua katika mahali panaitwa “Rest house” umepumzika  kwa ajili ya kwenda Mbinguni. Halleluya. Lakini wale wote wenye dhambi hautahukumiwa bila kupita mbele ya kiti cha judge. Ni kama hapa duniani huwezi kufungwa kifungo magereza bila kuingia kwa jaji. Ndivyo itakavyokua kila mtu atahukumiwa sawa sawa na matendo yake na Neno linasema hivi, “Na shetani anataka wengi wahukumiwe.” BWANA YESU ASIFIWE! 

Ninaelezea kwa kifupi, ni mambo yanatisha Malaika watakua na hasira na kitengo kilichoandaliwa Mbinguni kwa ajili ya hukumu tayari kimeshaandaliwa. Kila kitu kipo tayari. YESU anarudi mbinguni wameshamaliza kazi zao wanasubiri tu kuambiwa lini waje .Sio kwamba MUNGU  yeye atakuja huku.Hapana! Yeye anatuma watu .Nilishangaa sana, wale watakao shinda  watamsogelea kule mbinguni na kumuona lakini wenye dhambi hata siku ya mwisho hawamuoni MUNGU uso wake.

Watakutana na watoto wake na wako tayari. Watakua wanaingia kwa shift, kuna ndege mbinguni zitakuwa zinawaleta na wanaingia wanarudi kukamilisha kazi hiyo waliyopewa na YESU.

Huu ni wakati wa neema, mrejee YESU ili uingiee rest houe na usihukumiwe. Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, naomba uniongoze mahali sahihi ili niweze kubatizwa katika mto kama vile ulivyobatizwa wewe, naomba uniongoze kwa mtumishi wako wa kweli ili aweze kunifundisha njia ya kuenenda ili niweze kuurithi uzima wa milele na ile siku ya mwisho usiniache. Nakupenda BWANA YESU.

MUNGU awabariki na awalinde. Tutaonana katika kipindi kingine. Amen.


NABII HEBRON.