NINI MAANA
YA KUBATIZWA KWENYE DRUM AU TANK?
Ubatizo huu hauna tofauti sana na ubatizo wa kisima kama
nilivyoelezea. Yale madhara yote yaliyopo katika ubatizo wa kisima na hapa yapo
vile vile. Soma katika blog yangu nimeelezea maana ya kubatizwa katika kisima,
huu ni ubatizo wa shetani pia ila umefanyika katika drum au tank na mtu ajione
yeye anabatizwa katika maji mengi lakini ni kinyume pia. Hapa tofauti yake ule
wa kisima unakuwa umejiingiza katika jeneza kuzimu ila huu wa drum au tank
unakuwa umebatizwa na ukapatanishwa na gereza alilofungiwa joka kuu ambaye
ndiye baba yake shetani, hivyo unakuwa umefungiwa katika kiwango cha juu zaidi
katika ufalme wa shetani na usitoke utakuwa unaanguka tu katika huo mdwara
maisha yako yote na siku ya mwisho utabakia na joka kuu kama mtoto wake na yeye
baba yako hivyo uelewe jinsi mambo yalivyo haribika kupitia manabii wa uongo na
mapokeo ya shetani. Wewe tafuta katika biblia hajabatizwa mtu kwenye drum au
tank ni mtoni tu, neno limebadilishwa tayari na kama limebadilishwa basi haupo
na MUNGU sasa rejea.
2010 aliponiita YESU aliniambia Hebron nataka nikueleze na
nikufundishe, mimi nimekuchagua na nilijua ikifika wakati nitakutumia na sasa
peleka injili yangu kwa mataifa yote. Nimesalitiwa na baadhi niliyowaita
wanitumikie sasa wanaleta injili za kishetani na watu hawajui ila sasa watajua
ukweli na watapona na hata sasa mnapona na kutoka kwenye mikono ya shetani. Hicho
ni kiapo cha ubatizo kati yako wewe na lile joka lililotupwa mbinguni liwe baba
yako, sasa kataa maana neema ipo sasa sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi
zangu zote ikiwemo kubatizwa katika drum naomba unitoe kwa joka kuu. Uniandike jina
langu katika kitabu chako cha uzima wa milele, shetani sikutaki tena, mpinga
kristo sikutaki tena katika jina la YESU. Amen.
Mrejeeni YESU na kubatizwa ili awe BABA yako na akunyakue
uende mbinguni siku moja.
NABII HEBRON.