Pages

Saturday, March 26, 2016

HERI YA PASAKA….HAPPY EASTER 2016!

BWANA YESU ASIFIWE!
Nawatakia heri ya pasaka watu wote wa mataifa yote ikiwemo na kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE na waumini wote. Tunakumbuka siku ambayo YESU alifufuka miaka 2016 iliyopita bado jina lake ndilo jina kuu lenye nguvu kuliko majina yote ya viumbe vya MUNGU na hata kupita manabii wote na mitume wote walliopita na hata watakaokuja, yeye ndiye mwana wa pekee wa MUNGU ambaye ndiye aliyetumwa kuja kutuokoa. Sasa amefufuka yu hai, anasubiri kuja kulinyakua kanisa lake yaani mtu aliyeokoka akamkubali kwa imani na kwa matendo.

Nawasihi ambao bado hamjampokea mumpokee awe BWANA NA MWOKOZI wenu, upokee wokovu wenye uhai na siyo wokovu uliyokufa au ulokole. YESU alileta wokovu peke yake na ili mkristo uokoke ni lazima upokee wokovu. Kama haujaokoka bado haujakamilika kuwa mfuasi wa YESU kikweli. Sasa anarudi kama alivyonieleza, muda wake umefika ila sijui siku anasubiri apewe ruhusa ya kuja kulinyakua kanisa na mimi nawaeleza mataifa yote; hiki ni kipindi cha neema, uokoke sasa ili akija uwe mmoja wapo wa kunyakuliwa kwenda na yeye. Mwishi maisha matakatifu yanayompendeza MUNGU na mkatae uovu kabisa na mbatizwe ili muwe wanafunzi wake wa kweli wa ubatizo wa maji mengi yanayotembea siyo ya kisima, ziwa wala baharini au kubatizwa kwa jina la mchungaji.

Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, uniokoe mfalme. Uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele. Shetani sikutaki na maovu yako katika jina la YESU aliye hai. Amefufuka. Amen.

MUNGU awabariki na mzidi kusimama imara katika kweli ya neno la MUNGU bila kulichanganya na uongo au kulibadilisha. ROHO MTAKATIFU uwaongoze na MUNGU awalinde. Amen.


NABII HEBRON.