NABII HEBRON: Karibu tena ndugu mtazamaji na msikilizaji katika kipindi cha
mahojiano kati ya Isaya na Nabii Hebron wa kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI
WA MATAIFA YOTE ambapo siku ya leo ndugu mtazamaji na msikilizaji kwa mara ya
kwanza kabisa mwaka 2014 akiwa atashirikiana na wanadamu wenzie katika Krismas.
Sasa leo tutahojiana kuhusu Krismas alivyoisherehekea miaka yote huko kuzimu na
ilivyokuwa inafanywa na ilisherehekewaje; BWANA YESU asifiwe.
NABII HEBRON: BABA ninawakomboa fahamu zao
na akili zao, naondoa kila aina ya upingamizi katika jina la YESU KRISTO wa
Nazareti. Asante baba yangu, kstiks jinsi la YESU amen. Karibu sana. Karibu
Isaya.
NABII HEBRON: Supai...
ISAYA: Eeephva..
NABII HEBRON: Eeephva..
NABII HEBRON: Haya, nataka uwaeleze
watazamaji na wasikilizaji na wana wa MUNGU, ukikumbuka Krismas, maana mara ya
mwisho mwaka 2013 ulikula kuzimu si Ndio?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Haya, leo nataka uwaeleze
wanadamu, mimi nayajua lakini nataka nikuhoji kwa faida ya watazamaji na
wasikilizaji. BWANA YESU asifiwe.
ISAYA: Amen.
NABII HEBRON: Karibu
ISAYA: BWANA
YESU asifiwe, kwa jina naitwa Isaya; kutoka kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI
WA MATAIFA YOTE, nimeokoka na ninampenda YESU, napenda kumshukuru MUNGU kwanza
kwa sababu mwaka huu nasherehekea Krismasi nikiwa duniani na wanadamu
wenzangu, ninachopenda kuwaambia ni
kwamba shetani hafai, na hata siku moja msije mkakubali hata kujaribiwa na
shetani imani zenu, maana shetani hana akili wala adabu. Leo nitaeleza kwa
upande wa Krismasi kuzimu huwa inafanywaje,
na inakuwaje na ni nani anasimamia
Krismasi kule kuzimu, ambayo inakuwa inafanyika tarehe ngapi muda gani.
Krismasi ya kule kuzimu inakuwa ni kila mwaka tarehe 23 Desemba mpaka tarehe
27, katika hizo tarehe, Krismasi zao kwanza huwa wanaonana na tammuz mwenyewe.
NABII HEBRON: Mwelezee tammuz
ISAYA: Tammuz
ni ule mti, ambao watu walikuwa wanauita ni "Chrismas tree", lakini
yeye ndiye mtu ambaye anaonekana kabisa kuzimu, wanamwona kabisa tammuzndiye
ameenda, na pia, nitapenda kuelezea siku ya leo kwa sababu hata kule kuzimu
siku za krismasi sherehe zao huwa wanatoa sadaka, huwa wakunywa damu za watu;
sadaka zao ni damu na nyama za watu, na pia wapo washirika ambao wanashiriki
kule kuzimu kila Krismasi, ambayo pia wanasherehekea kuzaliwa kwa yesu wao kule
kuzimu,
NABII HEBRON: Yesu wao?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Labda Isaya tungeeleza kitu
kimoja kimoja maana vitu ni vingi sana. Hiyo ni dondoo tu ndugu msikiliza ya
yale yatakayokuwepo, lakini yapo mengi. Haya bwana, tueleze ilikuwaje mara ya
mwisho.
ISAYA: BWANA
YESU asifiwe; mara ya mwisho kula Krismasi kule kuzimu, walifanya sherehe,
nakumbuka ilikuwa ni sherehe kubwa sana, sidhani hata huku duniani kama watu
huwa wanafanya sherehe kubwa kama ile, waliitana viongozi wote wa kuzimu na
kila mtu ambaye anahusika na kuzimu alikuwepo hiyo siku, walifanya mavurugu
masherehe yao, wakatoa sadaka, wakaua watu, kwa sababu huwa wanapenda sana
kuuwa watu na kutoa sadaka kila inapofika mwezi wa kumi na moja na mwezi wa
kumi na mbili, wao inakuwa ni mwezi wao wa kutoa sadaka. Walifanya sherehe,
tammuz alienda; walialikana walisherehekea vizuri, lakini ndio hivyo mwishoni
na mimi nikaja kutoka.
NABII HEBRON: Ilikuwa ni mji gani huo
mlikuwa mnasherehekea Krismasi?
ISAYA: Freeman
village
NABII HEBRON: Kwa joka kuu kabisa
ISAYA: Ndiyo
NABII HEBRON: Uliniambia kwamba tammuz
katika krismasi iliyopita ulikuwa umekaa naye pamoja mnaongea. Mlikuwa mnaongea
nini wakati wa krismasi?
ISAYA: Tulikuwa
tunapanga mipango ya kuingiza vitu vingine tena ili watu waendelee kumwabudu tammuz,
na pia tulikuwa tunaongea maongezi ya kule kuzimu, kucheka, kufurahi,.. basi.
NABII HEBRON: Mlikuwa mnacheka mnafurahi?!
ISAYA: Ndiyo
NABII HEBRON: Na ubabe ubabe
ISAYA: Ndiyo
NABII HEBRON: Haya, jambo lingine ambalo
ningependa kuuliza uwaeleze watazamaji na wasikilizaji, mtu anapokuwa anaweka
huu mti wa krismasi nyumbani kwake, ina madhara gani?
ISAYA: Kwanza
anakuwa anafukuza baraka za MUNGU haziwezi kuingia nyumbani kwake hata mara
moja, na pia anakuwa anamkaribisha mungu tammuz na anakuwa anamkaribisha kwa
hiyo hata siku za krismasi anakuwa na uhalali na yeye, na hata akitaka kwenda
kwake anaenda na anafanya chochote anachokiamua. Na pia unakuwa unakabidhi
kuzimu maisha yako, na unakuwa unaingia maagano na shetani mwenyewe kwamba
umekubali kila kitu chake, na upo tayari kufanya kila kitu ambacho tammuz
atakuamuru. Sio kwamba atakuamuru kimwili, atakuwa anakuamuru kwenye ulimwengu
wa roho, nafsi yako anaiamuru ifanye chochote pasipo wewe mwenyewe kuelewa.
Unaweza kuwa unalalamika MUNGU hanioni lakini ni kwa sababu ya huo mti ambao
umeuweka nyumbani kwako.
NABII HEBRON: Na jambo lingine kule
kuzimu mkiwa mnaangalia huku duniani
mkiona nyumba zimewekwa miti mlikuwa mnajisikiaje?
ISAYA: Raha.
NABII HEBRON: Raha?
ISAYA: Ndio.
NABII HEBRON: Kabisa? Mnaona kwamba
mmeshinda?
ISAYA: Ndiyo
NABII HEBRON: BWANA YESU asifiwe; nitakuja
jambo lingine sasa kuhusu "father christmas" na yeye umuelezee.
Maanake kuna "christmas tree" na "father christmas" huko
kuzimu. si ndio?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Haya, hebu sasa tuelezee na
"father christmas"
ISAYA: Father
christmas, yeye kwa jina anajulikana kama saint Nicholas kule kuzimu, lakini
yeye kule kuzimu ameshakufa na anatumikishwa na mapepo na majini pamoja na watu
wengine ambao wanahusika na kuzimu. Na pia father christmas unapokuwa unaweka
ule mdoli wake nyumbani kwako unakuwa kwanza tayari wewe umeshamtukuza yeye
yamekuwa baba wa maisha yako siku zote.
NABII HEBRON: Baba wa maisaha.....
ISAYA: Yako.
NABII HEBRON: Kwa hiyo watu wanaoweka midoli
inafanya fanya hivi na madevu yake huyo ndio baba wa maisha yako kwenye
ulimwengu wa roho. Unasikia ndugu msikilizaji na mtazamaji? Mambo yameharibika.
Huyu niliyeko naye hapa alikuwa nafasi ya tatu katika ufalme wa shetani.Huyu
ndie ngazi kubwa sana ya siri za shetani. BWANA YESU asifiwe; lakini sasa
anatuelezea habari za huko kuzimu, ili wanadamu mzikatae. Zimeingizwa
unaposhiriki tu, na wewe uko kuzimu. Sasa ndugu mtazamaji na msikilizaji,
unapenda ule mdoli kuwa ndio baba yako? Jibu unalo. Karibu endelea.
ISAYA: Na
pia unapokuwa na huyo mdoli nyumbani kwako, kwanza anakuwa na uhalali na wewe,
kwa sababu ni baba yako, basi anaweza kukuamuru ufanye kitu chochote. Kwa hiyo
pia anakuwa na uwezo wa kuchukua baraka zako, anabeba nyota yako, anabeba
ufahamu wako, moyo wako anateka na nafsi, na anakuwa anakutumikisha kwenye
ulimwengu wa roho na unakuwa umeshafunga naye ndoa pia.
NABII HEBRON: Na hawa wanaokuwa wameweka hii
midoli makanisani, inakuwa inaashiria nini kwa kanisa?
Wanakuwa wanamkaribisha baba yao aje kuingia washiriki ibada.
NABII HEBRON: Wanamkaribisha nani?
ISAYA: Baba
yao.
NABII HEBRON: BWANA YESU asifiwe. Ashukuriwe
MUNGU wa Ibrahimu na Isaka; kama nilivyokwisha kuwaambia, ulimwengu ulikwisha
tekwa na shetani. Na angalia Krismasi kwenye makanisa, hayo mamidoli ndio yamekaa.
Je, ndiyo baba yenu hiyo? Ndiyo YESU huyo? BWANA YESU asifiwe. Ni wakati wa
kufunguka. Ni wakati wa kuyakataa. Kama unataka kushiriki Krismasi nzuri,
usiweke hiyo midoli wala huo mti. YESU sio mti, YESU sio mdoli. Hafanani na
yeyote hapa duniani. BWANA YESU asifiwe. Haleluya..
NABII HEBRON: Jambo lingine ambalo
ningependa kuulliza kazi aliyokuwa anaifanya father christmas kule kuzimu maana
kule kuzimu ulikuwa una meli kubwa sana. Na hiyo meli ulikuwa unazunguka nayo
dunia nzima. Hebu nataka ueleze, japo navijua; kwa faida ya wasikilizaji na
watazamaji. Wewe ulikuwa na meli kubwa sana hapa duniani hakuna, na dreva wake
alikuwa ni nani?
ISAYA: Father
christmas.
NABII HEBRON: Ndio mdoli mnaoubeba huku.
Alikuwa dreva wake huyu. BWANA YESU asifiwe. Haya, hebu tuelezee kwa ufupi
kidogo kuhusu hiyo meli. Ulikuwa unafanya nini, lengo lake, unazunguka, na umefanya nini?
ISAYA: Hiyo
meli, nilikuwa nikitumia kufanya safari mbalimbali, kama labda nikihitaji
kwenda kuangalia kitua au kwenda kutembelea manabii wa uwongo, kuangalia kazi
zao; na pia hiyo meli ilikuwa na maana yake. Maana ya ile meli ni ule utatu
mtakatifu wa kule kuzimu ambao ni joka kuu, lusifa na maxwel. Ukiwa umeitwa
mtakatifu kule kuzimu, hata hawa ambao mnasikia wa madhehebu ya wenzetu, ukisikia
mtakatifu ujue kwamba tayari yeye alishafanya kazi ya shetani kama inavyotakiwa
kwa sababu amefanya kazi ya baba yake vizuri.
NABII HEBRON: Mmh,
ISAYA: Na
anakuwa amefanya kile ambacho baba yake amemtuma.
NABII HEBRON: Mmh,
ISAYA: Kwa
hiyo sasa, yule father christmas akawa ananiendesha mimi kwenye meli,
NABII HEBRON: Mh,
ISAYA: Na
ile meli ilikuwa ina rangi saba.
NABII HEBRON: Rangi saba? Mmh..
ISAYA: Rangi
ya kwanza ya ile meli ilikuwa ni blue, rangi ya pili ilikuwa ni njano, rangi ya
tatu ni kijani, rangi ya nne ni zambarau, rangi ya tano ni nyeupe, rangi ya
sita ni nyekundu, na rangi ya saba ni nyeusi.
NABII HEBRON: Unaweza kuelezea maana ya hizi
rangi?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: MMh...
ISAYA: Rangi
nyeusi maana yake ni giza ambalo wana wa MUNGU wanakuwa wanarushiwa kwenye
ulimwengu wa roho, na ile rangi nyekundu ni agano ambalo shetani ameingia na
wana wa MUNGU huku duniani pasipo wao wenyewe kuelewa, na manabii wa uwongo na
watu wote wanaohusika kule kuzimu,
NABII HEBRON: Mmh...
ISAYA: Na
maana ya ile rangi ya njano ndio vitu ambavyo wana wa MUNGU wanalishwa; yaani
tuseme ni makufuru.
NABII HEBRON: Mmh...
ISAYA: Ambayo
wana wa MUNGU wanakuwa wanalishwa usiku, na ile rangi ya blue ni rangi ya mto
wa kule kuzimu ambao unakuwa umefanana na hiyo rangi ya blue,
NABII HEBRON: Ambao unaitwa timberland?
ISAYA: Ndiyo...
NABII HEBRON: Kwa hiyo hapa duniani watu
wanasema navaa chata ya timberland, kiatu timberland, ndio mto wa nani? Kuzimu.
Karibu endelea,
ISAYA: Kwa
hiyo hiyo rangi ya blue inakuwa inatukuza mto wa kule kuzimu ambao watu
wanakuwa wanabatiziwa bila wao wenyewe kujijua. Ukibatizwa ubatizo wa kikombe,
au ubatizo wa kisima ujue wewe tayari umeshabatiwa katika ule mto bila wewe
kujielewa, kwa sababu unapobatizwa pale
unakuwa na connection na kule kuzimu, na unapokuwa unabatizwa pale unaacha
nyota, unaacha ufahamu, unaacha nafsi, unaacha kila kitu unatoka boksi wewe
mwenyewe; Unatoka boksi!
NABII HEBRON: Mmh,
ISAYA: Na
majini ndiyo yanakuwa yanakupelekesha na pia unakuwa umeshaingia maagano pasipo
wewe mwenyewe kuelewa na shetani.
NABII HEBRON: Ahaaaa... Na kwa nini ulikuwa
una-survey na hiyo meli unazunguka? Umeniambia ulikuwa unaenda kuangalia
mipango mbalimbali; sasa ukiwa kama mshiriki namba tatu wa shetani kwa hiyo
ukapewa na mamlaka ya kuzunguka?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Na dereva wako alikuwa huyu
ambaye wanamwita father christmas?
ISAYA: Mmhh,
NABII HEBRON: Ambaye wanadamu ndiye
wanamuweka ndani?
ISAYA: Mmmh.
NABII HEBRON: Kwa nini sasa walikupa mtu
mkubwa hivyo kule kuzimu akuendeshe wewe?
ISAYA: Ni
kwa sababu mimi nilikuwa mkubwa wake, nilikuwa juu yake kwa hiyo alikuwa
akifanya chcochote nilichokuwa nakitaka mimi.
NABII HEBRON: Huyo ni wewe ulimwajiri, au
ulipewa na joka kuu akuendeshe?
ISAYA: Ni
mimi mwenyewe nilimwajiri.
NABII HEBRON: Sasas ulimwajiri mtu ambaye
leo hii watu wanamueka ndani wanamuita father christmas?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: ALikuwa ni mfanyakazi wako
tuseme?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Sasa wanadamu wanamuweka na
madole, wanamuweka ananyoosha nyoosha na vidole na madevu. Najua anafanana
hivyo hivyo. Sasa watoto wa MUNGU na wasikilizaji, shetani alikwishawateka wana
wa MUNGU na hawajielewi, na anawatengenezea mashtaka kila wakati. Lakini
amenituma kuleta habari njema, kueleza siri za shetani na kuzifichua na
kuzibomoa. Sasa utakapoacha tu, utakuwa
umepona.
Tukija kwenye habari ya utatu mtakatifu, huyu ni mmoja wa
utatu mtakatifu. Utatu mtakatifu namba moja ni joka kuu, namba mbili ni lusifa,
namba tatu ni huyu ambaye ni maxwel. BWANA YESU asifiwe. Haleluya; Na hapa
nitakuonyesha picha kidogo ya huyo max ambaye watu wanasema utatu mtakatifu.
BWANA YESU asifiwe. Kwa ufupi ili ukaweze kujua. utaona ni mambo ya ajabu na ya
kutisha. BWANA YESU asifiwe. Sasa hawa hapa wako watatu, wa kwanza ni joka kuu,
ambaye picha yake sina hapa, wa pili ni lusifa, ambaye pia sina picha yake
hapa, na wa tatu ni max ambaye ni mwanadamu saa hizi ni mwana wa MUNGU. Haya ni
manyoka yalikuwa yanamzunguka. Huyu ni mtoto wa nyoka, huyu ni mtoto wa
yezebeli, BWANA YESU asifiwe. Ndio wanamzunguka. Alikuwa ni mwanadamu mwenye ma
vyeo vyeo yake. Alikuwa ni mwanadamu mwenye mikono minne, na huku minne, ina
maana ni nane. BWANA YESU ASIFIWE. Alikuwa na jicho hili hapa ndilo alikuwa
anaangalia nalo dunia nzima, alikuwa ana pembe, BWANA YESU asifiwe. Maxwel alikuwaje?
Alikuwa ana pembe hapa lakini nimekwisha kuzikata. Hapa allikuwa na jicho la
kuangalia dunia nzima. BWANA YESU asifiwe. Hayo mengine endelea kufuatilia
katika vipindi, na karibu katika KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA
YOTE utafundishwa. BWANA YESU asifiwe. Huyu ndiye mwanadamu mnayemwona sasa
hapa, lakini ameshakuwa mtoto wa MUNGU ametulia. BWANA YESU asifiwe; Hebu
tuendelee. Kama wanadamu wanamuweka huyu mdoli wanamuita father christmas
alikuwa ni mfanyakazi wako, je, hamuoni wanadamu mnapotea kumwabudu mwanadamu?
Hamuoni mnamuudhi MUNGU? Yako wapi makanisa ya kusema ukweli? Makanisa yenyewe
ndio yamejaza midoli, hata sasa hivi wanaiandaa kwa ajili ya kuiweka.
Ninawaambia, itoeni katika jina la YESU KRISTO wa Nazareti. Kama mnampenda YESU
itoeni, kama mnamchukia YESU iacheni. Huo ndio ukweli, na muitupe. Kama
unampenda YESU achana na kuweka mti wa krsimasi.Kama unamchukia, weka. Zaidi
nimekwishafundisha, fuatilia katika makala na katika wesite ya
www.prophethebron.org ingia katika blog na vitabu, uyatafute haya masomo.
nimeyaelezea vizuri sana. Amenituma YESU kuupindua ufalme wa shetani.
Nilichofanya, nilimchomoa kwanza huyu. BWANA YESU asifiwe. Ilikuwa ni vita
kubwa sana kumchomoa huyu, sasa shetani hana chake tena. Lakini usiogope. Karibu
tena tuendelee msikilizaji. Enhe, hebu tuelezee, hiyo meli wakati mkiwa
mnazunguka, mlikuwa mnavua samaki?
ISAYA: Hapana
NABII HEBRON: Ndani ya meli kulikuwa kuna
nini na nini?
ISAYA: Kulikuwa
kuna mapepo, kulikuwa kuna majini na kulikuwa na nguvu za kuwapa manabii wa
uwongo.
NABII HEBRON: Nguvu za nini?
ISAYA: Nguvu
za giza na nguvu za kufanya miujiza huku ulimwenguni ili kuchukua pesa za wana
wa MUNGU, na mali zao, na pia kulikuwa na mapepo mbalimbali ambayo yangeweza
kuwasaidia hao manabii wa uwongo.
NABII HEBRON: Ahaaa... Sasa baada ya wewe
kuondoka, ile meli ilibaki inafanya nini?
ISAYA: Haikuwepo
tena.
NABII HEBRON: BWANA YESU asifiwe. Unakumbuka
katika watumishi, (lakini usitaje jina) ambaye alikuwa mwenyekiti wa manabii wa
uwongo dunia nzima ambaye ulimpa hicho cheo? Na utataja mmoja ambaye alikuwa ni
rais wa nchi, utuitaja hiyo nchi ambaye alikuwa msaidizi wake wanashirikiana?
ISAYA: Huyo
rais aliyestaafu katika hiyo nchi alikuwa ni rais wa America, yeyendiye alikuwa
amesimama pia kama kwenye uongozi wa namba mbili kwenye hicho chama, cha
kuwasimamia manabii wa uwongo, na pia alikuwepo huyo ambaye ni mwenyekiti wa
manabii wa uwongo, naye pia alikuwa anahusika kuwapa nguvu manabii wenzake, ili
kufanya maajabu mengi, ndio maana mnasikia watumishi wengi wanakwenda Nigeria,
wanakwenda wapi, lakini wanachokwenda kukifanya huko wanakwenda kuchukua nguvu
za giza, kama vile ambavyo Mtume na Nabii Hebron amekwisha kueleza kwamba ziko
nchi ambazo kuzimu inapatikana chini ya hizo nchi.
NABII HEBRON: Ahaaa.... BWANA YESU asifiwe,
sasa baada ya yale majini kuuawa, na wewe kutoka, watapata wapi tena?
ISAYA: Hakuna
NABII HEBRON: Kwa nini hakuna?
ISAYA: Kwanza
kabisa, yele aliyekuwa anawapa nguvu aameshatoka, na pia kile chombo ambacho
kilikuwa kikitumika kimeshalipuliwa.
NABII HEBRON: Nani kalipua?
ISAYA: Ni
Mtume na Nabii Hebron
NABII HEBRON: Mambo yalikwisha kuharibika
watoto wa MUNGU, kanisa ikawa ni mazingaombwe, ni kutafuta pesa, na bado tu
inaendelea, makelele tu yanapigwa kwenye ma tv, kwenye maredio. Ingekuwa kweli
ni MUNGU, ninawaeleza kuzingekuwa kuna shida katika dunia hii. Wengine
wamejiita mungu wa majeshi, mnatakiwa muelewe wana wa MUNGU. Hivi toka lini
mwanadamu akajiita MUNGU wa majeshi? MUNGU wa majeshi ni huyu mmoja. Lakini
wengine walikuwa wanafikiri wanazo nguvu za shetani, hizo nguvu za shetani
walipewa na joka kuu, ila nimekwisha ziondoa. Sasa huyu ni mwanadamu kama wewe.
Anajifunza sasa kula kama watu, anajifunza sasa kukaa na wanadamu, anajifunza
sasa kucheza na watoto, vitu vingi alikuwa havielewe, maana alikuw aanaelewa
vitu vya huko chini. BWANA YESU asifiwe. Lakini MUNGU anamtengeneza. Haleluya;
Hebu elezea kuhusu miziki ya injili ambayo inaimbwa na wanadamu ambao
hawajaokoka. Maana sasa hivi unakuta yaani mtu hajaokoka kabisa, lakini anaimba
nyimbo za injili, watu wanakuwa wanasikiliza, lakini anakuwa ni mlevi, ni
mzinzi, zinakuwa zina maana gani? maana wewe ulikuwa unatoa hicho kitengo.
Amen?
ISAYA: Amen.
NABII HEBRON: Sawa ero? BWANA YESU asifiwe,
ISAYA: Amen.
Hawa wanaoimba hizi nyimbo, kwanza wanakuwa wanamwimbia baba yao ambaye ndiye
joka kuu, na wanakuwa wanatukuza umoja wa freemason, na wanakuwa wananitukuza
mimi ambaye ndiye niliyekuwa nafasi ya tatu kwenye ufalme wa shetani,
NABII HEBRON: Ngazi ya tatu?
ISAYA: Ndiyo.
ISAYA: Na
pia unaposikiliza hizo nyimbo zao, kwanza wanakunajisi kiroho na kimwili, na
pia unakuwa unachukuliwa vitu vyako pale pale pasipo wewe mwenyewe kujielewa
unapokuwa unasikiliza hizo nyimbo zao tu. Ndio maana unakuta hata wengine
wanaimba wanakatika, wengine wanaimba wanafanya vurugu,
NABII HEBRON: Wanakatika?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Kukatika kupo kwa aina nyingi,
mikono, kiuno au miguu?
ISAYA: Kiuno.
NABII HEBRON: Wanakatikaje? unaweza
kuonyesha kwa ishara ya mikono? BWANA YESU asifiwe.Utakuta mtu anakatika kiuno
hivi (akionyesha kwa mikono), ile ni kama matusi. BWANA YESU asifiwe, hivi wewe
utafanya mbele ya baba yako mzazi umkatikie hivi? Lakini kwa shetani ndio
hivyo. Sasa watu wanaona waimbaji duniani wanakatika viuno kama vile sangoma,
au sangoma dance wanasema ni za YESU, aaaaa, zina mambo mengine. Hebu elezea
madhara yake.
ISAYA: Na
pia unapokuwa unaendelea kusikiliza hizo nyimbo zao, wanakuwa wanakuvuta
wanakuingiza kwenye kitabu cha uzima wa shetani, na wanakuwa wanakuingiza
kwenye mafaili ya kule kuzimu ambayo kwa sasa hayapo tena, na pia wanakuwa
wanakuteka wewe mwenyewe ufahamu wako, moyo wako na nafsi yako na kumkabidhi
baba yao na wanakuwa na uhalali kwa sababu tayari wewe ulishawafuata tayari. Na
pia waoimba zile nyimbo wanakuwa hawaimbi wanadamu, yanakuwa yanaimba mapepo
ndani yao ambayo ni mapepo muziki, ndio wanakuwa wanaimba miziki yao, wanaitoa
kule kuzimu, huku duniani nyie mnakuwa mmepigwa upofu, mnakuwa mnaona mtu ana
kipaji, lakini ndani yake ni mapepo ambayo yanakuwa yakimtukuza mungu wao kwa
furaha.
NABII HEBRON: BWANA YESU asifiwe, wana wa
MUNGU na wasikilizaji, madhara ya kusikiliza nyimbo za mtu ambaye hajaokoka
anayeimba nyimbo za Injili, anakunajisi
wewe anakuunganisha na kuzimu. Na katika dunia hii, waimbaji wengi hawajaokoka,
na hata wale wachache waliookoka, wengi wao ni wachawi, ni freemason, ndio
maana ukiimbiwa ujumbe wa MUNGU hausikii chochote inakuwa ni matakataka. BWANA
YESU asifiwe. Ndio maana hata leo hii utasikia nyimbo za injili zinachezewa
disco. Mnajua, ziko nyimbo za kiingereza zinachezewa disco, zimefanywa kama
blues lakini si blues, BWANA YESU asifiwe. Wanamtaja MUNGU, lakini yakupasa
uelewe shetani naye pia ni aina ya MUNGU. BWANA YESU asifiwe. Lakini msiogope,
unakwenda kufunguka. Amen.
ISAYA: BWANA
YESU asifiwe, zipo hata product makanisani ambazo hata tulikwisha kuelezewa na
Mtume na Nabii Hebron, na hizo product zipo chache zake ambazo tumeshaelezea
kwa upande wa vitenge, kwa upande wa mavazi, kwa hiyo zile product unapozivaa
zinakuunganisha wewe na shetani na pia na umoja wa kule kuzimu ambao ndio joka
kuu, lusifa na maxwel, na unakuwa na ukaribu nao vile vile, na pia nitaelezea
wachawi, mapepo na majini wana ushirika gani na wanakuwa wanafanya kazi gani,
na kazi zao zinafanyika saa ngapi na kila lini, na muda gani na wanakuwa
wanapata kitu gani.
NABII HEBRON: Enhe, hebu tudili na hiyo kwanza, maana ma,bo ni mengi
sana. Hata tukirekodi masaa mia sita haviishi. Twende hatua kwa hatua.
ISAYA: Wachawi
na mapepo na majini wana ushirika wao ambao unaitwa MPW, na wao wanakuwa
wanafanya vikao vyao lakini wao hawapatani na shetani. Na kisa cha kutopatana
na shetani ambaye ni lusifa ni kwamba yupo mmoja ambaye alitumwa hapa
ulimwenguni aje kuchukua nyota za watu, lakini akaja huku akashindwa akaanza
kuloga, kwa hiyo akawa amepindua amri za shetani akaamua kumuua kabisa.
NABII HEBRON: Kwa hiyo historia ya kuanza
kuloga ni kwamba shetani mjumbe wake mmoja alimuasi.
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Alimtuma kuiba nyota za watu.
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Apeleke kuzimu, yeye akaanzisha
kuloga wakakosana na shetani.
ISAYA: Ndiyo
NABII HEBRON: Kwa hiyo na wachawi wameasiana
na shetani.
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Sasa kama wameasiana kuna
uhusiano gani, wanasaidiwa bado na shetani? Au ni nini kinaendelea?
ISAYA: Wachawi
hawasaidiwi na shetani, ila nguvu ambazo majini na mapepo wanazo wanakuwa
wanawakabidhi wachawi, mapepo na majini wanaunda umoja wao na wana nguvu ndio
maana wanakuwa wanarukaruka usiku, ndio maana wanafanya vitu vya ajabu ajabu,
lakini hutakiwi kuogopa mwana wa MUNGU, kwa sababu kwa sasa ule uchawi haufanyi
tena kazi katika nchi ya Tanzania, na hata hakuna nguvu yoyote kutoka kuzimu
inayoweza kusimama juu ya mwana wa MUNGU yeyote.
NABII HEBRON: Haya, tunakuja, kwenye swali
lingine, umesema kwamba, chanzo cha uchawi ni mjumbe aliyetumwa huku duniani,
akaibe nyota.
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Yeye akaamua kuloga, hakurudi.
Sasa alikuwa anaitwa nani? Unaweza kumkumbuka?
ISAYA: Ndiyo,
alikuwa anaitwa Matiku.
NABII HEBRON: Anaitwa Matiku?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Mjumbe wa shetani anaitwa
matiku.
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Ndiye alitumwa huku duniani
kuiba nyota akabadilika akaanza kuloga.
ISAYA: Mmmh.
NABII HEBRON: Sasa huyu Matiku yupo bado hai
au ameshakufa?
ISAYA: Ameshakufa
tayari.
NABII HEBRON: Na huko kuzimu alikuwepo
alipokufa?
ISAYA: Ndiyo.
Ndio mzimu wake ulikuwa unasaidia wachawi wengine.
NABII HEBRON: Kwa hiyo ndio kazi anayofanya
huko?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Haya sasa Isaya, nataka
unieleze maana ya zile rangi saba na kadi za krismasi na vitu vyenu vyote
mnavyoweka, na wanadamu wanaponunua kadi za krismasi bado wanakuwa wameshiriki
tena. Hamkuchoka, mkaendelea kuwabana.
ISAYA: Bwana
yesu asifiwe, nitaelezea kuhusu hizo rangi saba zinazokaa kwenye kadi za
krismsi, au kadi za bethidei (bithday), na kwenye kadi za vitu vingine vingine,
hizo rangi kwanza tayari zinakuwa zinatukuza zile rangi ambazo tayari nilikuwa
nimeshawaeleza
NABII HEBRON: Rangi saba hizo?
ISAYA: Ndiyo,
na pia hiyo kadi unapoitumia ina maana wewe tayari umeshashiriki katika utatu
wa kule kuzimu, na unapompelekea mwingine ina maana unamsajili kwenye chama cha
kule kuzimu bila yeye mwenyewe kujijua.
NABII HEBRON: BWANA YESU asifiwe. Ndugu
mtazamaji na msikilizaji, kadi ile yenye
rangi rangi, unapompelekea mtu au kuletewa ina maana mnasajiliana wenyewe kwa
wenyewewe kwenye vile vyama pasipo kujua. BWANA YESU asifiwe. Kwa hiyo kadi ya
Krismasi inatakiwa iweje?
ISAYA: Kwa
kweli hakuna kitu kinaitwa kadi ya krismasi, kwa sababu hata hicho ni shetani
alianzisha.
NABII HEBRON: Hahahahaaaa... Dunia
imepinduliwa. Hakuna kadi ya nini?
ISAYA: Krismasi.
NABII HEBRON: Ila zipo salamu za krismasi na
baraka za krismasi. BWANA YESU asifiwe. Hebu elezea tena kuhusu kadi ya
krismasi. Shetani hakuchoka tena. BWANA YESU asifiwe. Kinachotakiwa wakati wa
krismasi, ni unampa mwenzako zawadi kamili. Au sio?
Kama vile YESU alivyozaliwa, watu walimletea zawadi. Watu
wapeane zawadi. Lakini shetani akaanzisha nini? Kadi. Kadi ina zawadi? Ina hizo
rangi saba, au mbili au tatu. BWANA YESU asifiwe. Na wewe unaletewa! Unakuwa
umeshiriki vilevile. Makanisani zimejaa, Kwa watu zimejaa, hata mimi nilikuwa
sijui, mpaka nilipopelekwa huko na BWANA YESU nikaonyeshwa? Krismasi inatakiwa
watu wanapeana zawadi, wanakula, wanashiriki, wanafurahi. Sasa utasikia
nitakutumia kadi ya krismasi. Kwenye internet ndio zimejaa, BWANA YESU asifiwe.
Ni heri umtumie mwenzako kwenye meseji heri ya krismasi. Inatosha. Amen, MUNGU
akubariki. Sasa hebu elezea bwana Max wa zamani, sasa wewe ni Isaya wa Hebron
kuhusu hizi kadi.
ISAYA: Na
pia hizo kadi zinakuwa na ushirika na mzimu wa mtu anayeitwa maxwel kule kuzimu
ambaye tayari baba yetu wa kiroho ameshatuonyesha, kwa hiyo unapoituma hiyo
kadi kwa mtu yeyote, ina maana kwamba tayari wewe umeshamtumia max kadi yako,
kwa hiyo inaonyesha kwamba unampenda sana. Unapomtumia kule labda umeandika
MUNGU akubariki, na yeye anasema safi. Kumbe kazi ya tammuz inafanya kazi
vizuri, unakuwa unamkaribisha sasa tayari.
NABII HEBRON: Hebu ngoja ndugu watazamaji na
wasikilizaji, napenda kuwaonyesha huyu sasa, ukishamtumia mtu yeyote kadi ya
krismasi, huyu ndio maxwel, ana mikono nane, ana jicho kubwa hapa, ana mapembe
na kuna linyoka linazunguka pembeni yake. Na ndivyo ilivyoandikwa lakini hapa
tumechora rafu rafu BWANA YESU asifiwe. Ana manyonyo kama mwanadamu, lakini
nyonyo lake moja ni kubwa sana. BWANA
YESU asifiwe. Ni vitu vinatisha sana. BWANA YESU asifiwe. Haleluya. Sasa
unapomuandikia mtu kadi ya krismasi, huyu na yeye umemuandikia, anafurahi,
umejiconnect. Je, unapenda kujiconnect na jitu kama hili, hawa ndio wameanzisha
kadi ya krismasi. YESU hajaanzisha kadi ya krismasi. MUNGU alichokianzisha,
mtoto wake alipozaliwa nyota iling'aa na watu wakampelekea zawadi na watu
wanatakiwa wapelekeane zawadi.BWANA YESU asifiwe, lakini zawadi sasa ikaongezwa
na nini? na kadi ya krismasi. No kadi ya krismasi katika jina la YESU. Amen.?
Karibu endelea.
ISAYA: BWANA
YESU asifiwe, na pia katika kadi hizo hizo unakuwa unatii utatu mtakatifu wa
kule kuzimu pia, na unakuwa unanyweshwa damu, unanyweshwa kila aina ya makufuru
kwenye ulimwengu waroho bila wewe mwenyewe kujijua, na kazi ya makufuri ni
kukuvuta uli uingie kwa shetani bila wewe mwenyewe kuelewa. Na kazi ya yale
makufuru ambayo unapewa, ni ili uweze kuvutwa vizuri kwenye serikali ya
shetani, ili aweze kuharibu vizuri maisha yako, abebe nafsi, abebe na maisha
yako, zipelekwe kwa baba yao ambaye ni joka kuu pamoja na shetani na juo mzimu
ambao umebaki kule ambao ni max. Na pia unaweza kukuta ile kadi ya krismasi ina
alama crown imekaa, ile taji, ndio hiyo ambayo imeshaonyeshwa hapo na Mtume na
Nabii Hebron, ambayo max ameiweka kichwani kwake.
NABII HEBRON: Hii hapa. Haya mapembe ambayo
mnayaona hapa ndugu watazamaji na wasikilizaji, crown ndio hizo pembe, kwa hiyo
na wewe unakuwa umejivisha limwili lake. Enhe.
ISAYA: Na
pia unakuwa tayari umesahaunganishwa ule ufalme wake ambao yeye mwenyewe anao
kule kuzimu, na hiyo ndio serikali yake kule kuzimu kama ilivyochorwa, na yeye
ameonyeshwa amekalia kitu cha duara, bna
hicho kitu cha duara ni kwamba amekalia dunia ya kule kuzimu yaani ulimwengu wa
kuzimu, upo chini yake yeye yupo juu yake, na hivyo vidude viwili vimekaa chini
yake ni kishikizo cha dunia ya kule kuzimu, na hao nyoka ndio nyoika ambao
alikuwa akilala nao na kutembea nao kila muda. Kwa hiyo unapokuwa unamtumia mwenzako
kadi ambayo ina mojawapo kati ya vitu hivyo hapo, ni kwamba unakuwa umemconnect
mwenzako na maxwel na wewe mwenyewe umejiconnect na maxwel pasipo kujijiua, na
unapojiconnect naye maxwel anajiconnect na familia yako yote mkaingia kwake
mpaka na ukoo mzima, akajiunganisha na mizimu ya kwenu, akajiunganisha na watu
wote ambao wameshakufa, ndio wanaanza kuchafua maisha yako bila kuelewa.
NABII HEBRON: BWANA YESU asifiwe, zaidi
ingia katika blog ya prophethebron.blogspot.com, YESU aliyonituma ni kufichua uovu.
Angempata nani? angemshika nani? watoto wa MUNGU mnampenda sana YESU, lakini
kila mahali wameshikwa. Ni maamuzi yako, heri ya krismasi tu inatosha. Heri ya
Krismasi kwa mdomo, hiyo hela anayotaka kukunulia kadi akupe zawadi basi. YESU
hakuletewa kadi. Nikuulize, kadi ina chochote, si karatasi? Kwenye ulimwengu wa
roho unakuwa umeunganishwa huko. BWANA YESU asifiwe. Na kadi ya pasaka vivyo
hivyo. Hebu elezea kuhusu kadi ya pasaka. Happy Eater...!!
ISAYA: Hiyo
kadi ya pasaka unapokuwa umemtumia mwenzako au unapokuwa umeitumia wewe
mwenyewe, unakuwa umejiconnect na pepo linaitwa lukman, anakupeleka kwenda
kuhiji, anakuuwa kulekule, unaporudi unakuwa umerudi boksi.
NABII HEBRON: BWANA YESU
asifiwe. Labda jambo lingine nikuulize kuhusu hizi kadi watu wanatumiana,
darling, my wife, congratulations, na hizi zina maana gani?
ISAYA: Unapomtumia
mtu yeyote kadi za namna hii unakuwa tayari umeshamtumia mtoto wa yezebeli kule
kuzimu, na pia unakuwa umemtumia maxwel, na pia unakuwa umemtumia pepo ambalo
linaitwa abubakari, maimuna na sharifu, ndio wanakuwa na uhalali na wewe, kwa
hiyo unapowatumia wanaona kumbe unatupenda, wanakuwa na uhalali na
kukufuatilia, na ukituma tu hiyo barua, wanahakikisha usiku lazima wakufuatilie
wakuzinishe wao wote na umoja wao.
NABII HEBRON: BWANA YESU asifiwe, Haleluya.
Sasas ninapenda kukukuliza, wewe hizi kadi ulikuwa unazifaidi vipi ukiwa kule?
Maana hata mimi nilishatuma hizi kadi kwa watu wengi sana, kwa hiyo nikituma
ulikuwa unaipokea?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Hebu waelezee tena watu kuhusu
hizi kadi, maana wengi wanatumiana hizi kadi, my love, my lover, my honey, my
dady, my mum, my best friend, zina maana gani? Lakini kwanza kumbuka sio
kumwambia mwenzako my best friend au my honey, my love, my dad, my mum. Sio
mbaya kwa kinywa. Lakini ile kadi iliyotengenezwa, wafaidikaji ni hawa.
ISAYA: BWANA
YESU asifiwe, Hizo kadi kama nilivyokwisha kuwaeleza, kwamba unakuwa unamtumia
mtoto wa yezebeli, maimuna, makata, sharifu, abubakari wa kule kuzimu, wanaona
wanapendwa na wengi, na katika wewe mtu mmoja kutuma hiyo kadi kumtumia mtu
mwingine, wao wanaweza wakaharibu familia yako nzima au ukoo wako mzima kwa
sababu wanakuwa wanajua wote wanatupenda. Kwa sababu chimbuko la ukoo ni bibi
na babu, kwa hiyo bibi na babu wanapokuwa wanachimbuliwa, ile mizimu yao
inakufuatilia wewe na maisha yako na wanakuwa wanakuzinisha kila usiku. Kila
mmoja wa majini anakuwa anakuzinisha kwa sababu anakuwa ana uhalali na
wameshakupenda na wanajua tayari huyu anatupenda. Kwa hiyo kila wakikufuata
wanajua nafsi yako haitalalamika kwa kuwa unawapenda, na pia ile kadi
unapoituma kule kuzimu wanachokuwa wanakifaidi wanaona ulimwengu wao unapendwa
na watu wengi, na pia wanakuwa wanaona watu wamemkubali shetani kuwa mwokozi wa
maisha yao, na wao wanakuwa wanajipongeza kana kwamba kama mtu mmoja akituma
kwa siku moja, wanafanya sherehe, na shetani anajua kwamba tunapendwa,
anawaongezea vyeo kwa sababu anajua kazi yao wamefanya vizuri na imeenda
sawasawa kama alivyokuwa anataka.
NABII HEBRON: Ndugu watazamaji, ni wangapi
mmetuma? Ni wangapi mnazo kumbukumbu? Ashukuriwe YESU. Alikosa mtumishi wa
kumtuma miaka yote wala msimlaumu. Ndio maana watu wakazidi kuangamia. Na yeye
kwa uchungu wake na hasira, akiwa na BABA yake (MUNGU) akaamua atumie njia
nyingine alikomboe kanisa lake. Utukufu wa kanisa la mwisho ni mkubwa kuliko wa
kanisa la kwanza. Na ndio huu sasa alionituma unatenda kazi. Yale
yasiyojulikana yanafichuliwa, na utakapoelewa utapona. Yamkini hutendi dhambi,
unayakimbia lakini umekamatwa. BWANA YESU asifiwe. Na zaidi, karibu katika
kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE utaupata ukweli. Na jambo
lingine ambalo napenda kukuelezea, shtani akawa bize "(busy)" kuhusu
kadi; ukiingia kwenye internet, kadi ni nyingi sana. Eee namba tatu ya ufalme
wa shetani wakati huo, maana ulitoka tarehe 02.06.2014. Hizi kadi kwenye
internet mnazifaidi kivipi na mbona mmeweka nyingi sana?
ISAYA: Kwanza
tunatakiwa tuzisambaze ili watu mzione, muendelee kzitumia ili muendelee
kuwatukuza zaidi na ili wao wapate vyeo bila nyie wenyewe kujijua, na pia hata
manabii wa uwongo wanatumia zile kadi kuvuta nyota za watu ili watu waende
kwenye makanisa yaoili mmkaibiwe huko vitu
vyenu pamoja na nafsi zenu.
NABII HEBRON: Kivipi wanaibaibaje kupitia
hizi kadi?
ISAYA: Kwa
sababu kwanza wanakuwa wameweka pepo la tamaa na pepo la kivutio katika zile
kadi.
NABII HEBRON: Pepo kivutio, pepo tamaa....
ISAYA: Ndiyo.
Kwa hiyo unavyoangalia zile kadi mapepo yanavuta macho yako unaona hizi ni
nzuri.
NABII HEBRON: Mmh..
ISAYA: Unaposema
hii ni nzuri, ujue kabisa wewe umeshavutwa na upo katika ufalme wa shetani. kwa
hiyo shtani mwenyewe ndio anakuwa anakumiliki bila wewe mwenyewe kujijua kwenye
ulimwengu wa roho.
NABII HEBRON: Sasa unaelezeaje kuhusu
makanisani maana ndio unakuta zimejazwa kwenye miti tena, na waumini, au kwenye
nyumba za waumini kadi zimejaa mpaka chini. Hii ina maana gani?
ISAYA: Kwanza
unapokuta nyumba ya mtumishi ina hizi kadi, ina maana kwamba kwanza yeye
anatukuza ule ufalme uliopo kule kuzimu, sio watumishi wote, ni wachache ambao
unakuta wanatukuza huo ufalme wa shetani ambao unakuta wanamshangilia mungu
wao, kwanza wamefanya kazi vizuri, na wamekaribia kuumalizia mwaka bila
matatizo, na wanajua kabisa krismai ikiisha wanaenda kupata vyeo kule kuzimu.
NABII HEBRON: Isaya, unaweza kuelezea hizi
zawadi za krismasi, maana nyingine unakukuta zina viboksi, vi-ball na taa
zinawakawaka. Hizi taa zinawakawaka ndio zile rangi saba, kwa hiyo kila mahali
unakuta tu zinafanya hivi... Ukiingia kwenye madisco, kweye miti unazikuta,
zina maana yake; si mpango wa MUNGU. BWANA YESU asifiwe. Lakini hebu eleza
isaya maana wewe ulikuwa navyo huko bwana mimi sikusaidii kazi. Japo mimi
nilishaagaliaga huko nikaviona kila kitu, na YESU akanionyesha jinsi ulimwengu
ulivyopinduliwa.
ISAYA: Kwanza
zile taa zinavyokuwa zinabadilika zinakuwa ndivyo shetani anapindua maisha
yako, kwa hiyo maisha yako yanakuwa yanacheza cheza, unaenda mbele unarudi
nyuma, na vile vidude vimekaa kama vibomu (viduara) ndio dunia ya kuzimu ambayo
wewe unakuwa umetekwa umekaa ndani yake, ndani ya kile kibomu.
NABII HEBRON: Unapokuwa navyo tu nyumbani
kwako?!
ISAYA: Ndiyo.
Na kile kidude ambacho kinakuwa kimekaa juu kwa ajili ya kuchomekea kamba, ndio
bomu ambalo linakuwa limetoka kule kuzimu linakuja kukutungua wewe ambaye
umekaa kwenye dunia ya shetani, kwa hiyo hata shetani akitaka kuwaua watoto
wake, akkishachoka akiona kazi imeenda vibaya, kwa hiyo shetani akiona kazi
yake imeenda vibaya anakuwa na hasira kiasi kwamba anaweza hata akaua watu wote
wanaohusika na kuzimu.
NABII HEBRON: Hana upendo yeye?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Watoto wa MUNGU mnazidi
kuelewa. Ni wangapi wana hizo taa? Maisha yanakuja, yanarudi.. Hiyo siyo nuru.
Jua likumulike. BWANA YESU asifiwe, pia katika hizi taa unakuta za rangi rangi,
labda brown, nyekundu, watu wanasema "night light", wakati wa kulala
wanawasha taa labda ya rangi ya zambarau, labda ya kijani, zote hizo ni mbaya.
labda hebu elezea. Lakini wana wa MUNGU hawajui. Na hata katika mambo haya ya
kadi, watumishi wengi hawajui kwa sababu kanisa limetekwa na shetani.
Wangejulia wapi? Hawapendi lakini watoto wa kiroho ndio wanawaletea. Mimi
sitaki katika jina la YESU. BWANA YESU asifiwe. Hata nikiletewa mimi napiga
kiberiti tu.. Nilishazichoma, miezi mitatu iliyopita. nilishazichoma. Maana
nilikuwa nazo nyingi sana, lakini hata walioniletea hawakuniletea kwa nia mbaya
lakini walikuwa hawaelewi.. Na mimi nilikuwa nawatumia watu. BWANA YESU
asifiwe.
NABII HEBRON: Ni wakati umefika wa kusema
ukweli, anayetaka kupona apone. BWANA YESU asifiwe. Hata makanisa hayataiwi
kupambwa na yale mamiti, mataa, makadi, yote yamekwisha kuelezwa hapa. BWANA
YESU asifiwe. Haleluya. Labda Isaya endelea kidogo kuelezea vingine.
ISAYA: BWANA
YESU asifiwe, nitaelezea kuhusu zile nyota ambazo zinawekwa kwenye ile miti
ya krismas tree, ile nyota ndiyo nyota
yakowe inakuwa imekamatwa na tammuz ndio anakuwa ameishika mwenyewe, lakini
bila kuelewa kwenye ulimwengu wa roho nafsi yako ndio unaona ni nyota yake ni
ile pale. Tammuz ndio anakuwa anakufanyia nyota yako hii hapa, kwani utanifanya
nini. Lakini wewe mwenyewe unaona ni kama kipambo bila kuelewa wewe mwenyewe
kuwa nyota yako imeshikiliwa na tammuz. Mpaka uje upate mtu wa kuirudisha nyota
yako, na zaidi labda ufike Moshono katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA
MATAIFA YOTE ndio nyota yako inaweza ikarudishwa.
NABII HEBRON: Kwa hiyo, watu wengi mnakuwa
mmeibiwa nyota, na maisha yenu. Wengine si wachawi wamewaloga, wengine si
mizimu, ni kwa sababu umeweka lile pambo lenye nyota, na crown - krismasi. Sasa
toka watu wamezaliwa, toka watu wakiwa wadogo, wana mambo hayo. BWANA YESU
asifiwe. Na hebu elezea kuhusu mwezi.
ISAYA: Ule
mwezi ndio kuwa maisha yako yanatandikwa kila baada ya miezi ambayo wewe
mwenyewe umeingia maagano na kuzimu bila kuelewa mimi kila mwezi fulani, kila
siku fulani maisha yangu nimeyafanya hivi lakini kwenye ulimwengu wa roho bila
wewe mwenyewe kujielewa. Kwa hiyo kila ule mwezi ina maana maisha yako yanakuwa
yanamulikwa, mwezi ule ukiondoka maisha yako yanakuwa tena giza bila wewe
mwenyewe kujijua. Kwa hiyo ule mwezi unakuwa na muunganiko na malango ya
kuzimu, na pia unakuwa unakata maisha yako, kwa hiyo shetani anakuwa amekaa
huku, huku amekaa joka kuu na maxwel yupo katikati, na pembeni umezungukwa na
majeshi ya kuzimu kwa hiyo hakuna pa kutokea wewe mwenyewe.
NABII HEBRON: Sasa nikuulize, wewe uliwakata
watu wangapi kipindi hicho?
ISAYA: Wengi
sana.
NABII HEBRON: Unaweza kujua hesabu yake?
ISAYA: Au
kwa hesabu tu ya rafu rafu?
ISAYA: Kama
milioni mia nane (800,000,000).
NABII HEBRON: Umeua?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Ambao ni binadamu.
ISAYA: Ndio.
NABII HEBRON: Na shetani akaingia ndani yako
kukutumikisha, lakini leo umetoka.
ISAYA: Ndio.
NABII HEBRON: Sasa ni wakati wa wewe
kuwaeleza wana wa MUNGU wapone, maana wengi hawatendi dhambi, ila hivyo vitu
vimewashikilia. Na mbinguni hawaendi kwa sababu ya vitu vya shetani pasipo
kujua. Haya, unawaelezaje sasa watu wanaoandikiana kadi za uchumba, za harusi,
unawaambia nini? Maana hapo zamani nilichokuwa nakijua mimi, watu walikuwa
wanaadikiana barua. Barua ni salama. BWANA YESU asifiwe, ooh sikuoni, ooh
nakupenda sana, na wanaweka vitu vingi
na nyie wenyewe mnajua. Lakini shetani akaingia kati katika mahusiano ya
uchumba, akaleta kadi ili ashiriki uchumba wako wewe. Unapotoa kadi. Unakuta
mabalaa balaa, mikosi mikosi. Shida ni nini? Ukiangalia wazazi wetu zamani
walikuwa wanatumiana barua wamedumu na wako katika ndoa imara mpaka leo. BWANA
YESU asifiwe, lakini hawa wa siku hizi wamekuja na kadi I love you so much; I
love you wapi? Ni pepo linakuambia linakupenda so much. BWANA YESU asifiwe.
Kuna wengine wanakuambia me & you; unajua me & you? Hebu elezea maana
ya me & you kuzimu ni nini? Mkaileta duniani.
ISAYA: Maana
ya me & you, kwanza kabisa wewe unayetumia ndio maana ya me, ambayo ni
mimi. You inakuwa ni ulimwengu mzima wa kule kuzimu, sasa anaweza kuwa
mmojawapo, jini, pepo, mchawi, nabii wa uwongo, shetani, joka kuu, maxwel, au
watoto wao ndio unaweza ukawa umewaambia you.
NABII HEBRON: Sio mwanadamu mwenzako. BWANA
YESU asifiwe, lakini msiogope, iko habari njema. Ninawatakia Krismasi njema.
Lakini sasa, sio Krismasi ya ma-father christmas, miti hiyo, na makadi.
Inatakiwa Krismasi uwe mtakatifu. Uokoke, umtukuze MUNGU. Umwabudu na kumsujudu
yeye. Kama ni mambo ya kutoa kadi, usimpe mtu kadi, mpe zawadi. BWANA YESU
asifiwe. YESU alipozaliwa hakupelekewa kadi, alipelekewa zawadi. Sasa kadi
nikuulize ndugu mtazamaji na msikilizaji, ina chochote? Si inakaa tu hapo
unaweka hapo. BWANA YESU asifiwe. Mpe mtu zawadi. Unapotoa kadi, unashirikisha
na kule kuzimu krismasi ya kwao ambayo ni ya mpinga kristo. BWANA YESU asifiwe.
Huyu hapa alikuwa anakaa nao, anatufichulia siri zote leo, mpate kuzielewa.
BWANA YESU asifiwe, Haleluya... Una jambo lingine la kuwaeleza kuhusu krismasi?
Maana Krismasi hii sasa unaenda kula na wanadamu. BWANA YESU asifiwe. Na wewe mwenyewe usingependa kula na makadi,
hataki kurudi huko! Asingependa kushiriki na ma-miti, asingependa kushiriki na
ma-midoli, BWANA YESU asifiwe. Hata wafanya biashara wote ambao wanauza hizo
kadi, ni kwamba wanatumikishwa kuendeleza kazi za shetani, pasipo wao kujua.
Haleluya; Zaidi shetani akaona YESU karibu anarudi, akabuni mtandao wa internet
kusambaza faster. BWANA YESU asifiwe. Hata wauzaji wa kadi siku hizi hawapati,
ni internet. Unakuta mtu mmoja anaweza akatuma kadi hata mia tano (500) si
bure? Lakini uelewe, ni madhara tupu, na ninabomoa katika ulimwengu wa roho
katika jina la YESU. Nawafarakanisha na hizo rangi zote saba katika jina la
YESU. Wanadamu wote. Ninaomba MUNGU Neno lako lisonge mbele. Na watoto wako
wabadilike, wakujue wewe. Na ufalme wa wachawi ninaubomoa, na manabii wa uwongo
ninawaharibu katika jina la YESU KRISTO wa Nazareti, ninasimamisha ufalme wako.
MUNGU awabariki. Heri ya Krismasi. Tutaonana muda mwingine na wakati mwingine
tena. Zaidi, karibu katika KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE,
ewe mtu wa nchi yoyote, taifa lolote, njoo ukutane na YESU. Huduma aliyonipa ni
ya mataifa yote, ina maana ni mataifa yote, kwa watu wote, niwaonyeshe njia
kama MUSA alivyotumiwa kuwapeleka wana wa Israel Kaanani. BWANA YESU asifiwe.
Mambo yamebadilika, MUNGU awabariki, Amen.