Nabii Hebron:
Hebu tulia
Ndugu wa Emmanuel:
Haongei na asemi chochote
Ndugu wa Emmanuel: Anaitwa
Emmanuel Njau
Nabii Hebron: Muda
gani sasa?
Ndugu wa Emmanuel: kama
siku tatu hivi
Nabii Hebron: Huyu
wamemlipua aisee, sawa?!
Nabii Hebron: Sasa
ngoja niuzime huu moto. sawa sawa?
Nabii Hebron: Anaitwa
nani?
Ndugu wa Emmanuel: Anaitwa
Emmanuel
Nabii Hebron: Emmanuel
niangalie
Nabii Hebron: Niangalie
Nabii Hebron: Huyu
wamemlipua. Sawa?!
Nabii Hebron: Na
wewe uliyemlipua muachie haraka. Muachie Emmanuel.Emmanuel nakuchomoa kwenye
kichaa, na nyota narudisha na nafsi, njooooo...
Nabii Hebron: Niwekeeni
pale basi.
Nabii Hebron: Askofu
fanya kazi.
Nabii Hebron: Sasa
wengine wanakuambia tu hawataki kuwaleta. waweke hapa
Nabii Hebron: Huyu
walishamuua aisee. sawasawa?! Wameshamuua, wamechukua nyota, walitaka kumtoa
kafara.
Nabii Hebron: Baba,...
Emmanuel narejesha akili yako sasa ukapate kunielewa, ukapate kunisikia, hiki kinachokunyonga hapa ninakichomoa.. Jini
liko hapa. Sasa haya mafuta hata kama umelishwa kitu gani hakibaki, ninaondoa
na tiketi ya mauti. Anakuja Sasa hivi na kichwaa hakuna bwana.
Nakomboa kichwa, majini yaliyoharibu kichwa chake, na mbuzi
waliyoichinja na kumzika, ninatupa,... achia haraka.
Emmanuel: (Anakoroma)
Nabii Hebron: Jini
hilo.. Piga kelele kwa mara ya mwisho bwana...
Emmanuel: Khanikiiiiiiii...
Nabii Hebron: eee
Emmanuel: Khanikiiiiii......
Nabii Hebron: Wewe
muweke chini hapo. Mwache, funika tumbo. Hii ni imani yenye nguvu ndio inatoa
hii kitu. Sawa sawa? Sasa
Nabii Hebron: kuambiwa
imani leta hela hiyo imeku....
Waumini: imekufa.
Nabii Hebron: Lakini
YESU hana makosa, alituma watumishi
Nabii Hebron: Acha
kuweka hivi bwana wewe, furahi , unaondoka na mtu wako, mnaenda kula nyama sasa
hivi. sawa sawa?
Nabii Hebron: Wakamfanya
kichaa..
Nabii Hebron: Sasa
huyu, kwa yule anayetaka kuona sasa, kwa somo nililofundisha; Emmanuel, mapepo
yaliyokuwa yanakuzuia sasa, mpaka umefika kwa YESU, YESU anamwamsha Emmanuel,
amka, Emmanuel amka ukiwa na akili zako, na ukichaa ukiwwa hamna tena.
Nabii Hebron: Eeeeee...
Muacheni
Nabii Hebron: Hebu
mwacheni bwana.
Nabii Hebron: Leta
maiki (mic)
Nabii Hebron: Emmaneul
Nabii Hebron: Emmanuel
Nabii Hebron: Vipi?
Emmanuel: Niko
wapi?
Nabii Hebron: Hapa?
Nabii Hebron: Hapa
kanisani
Nabii Hebron: Anaangalia
hela yake iko wapi au ni nini?
Nabii Hebron: Pesa?
Emmanuel: Pesa
na Simu
Nabii Hebron: Nini
unatafuta?
Emmanuel: Pesa
na Simu
Nabii Hebron: Imeenda
wapi?!
Nabii Hebron: Enhe...Imeenda
wapi? Umeiona?
Nabii Hebron: enheee...
hebu Simu unayo aisee? sasa unaona amerudi na akili!
Ndugu wa Emmanuel: Nimempa
mama, mke wake
Nabii Hebron: sasa
unaona amerudi na akili, alikuwa hakumbuki hata simu. njoo mama hapa.
Nabii Hebron:
Alikuwa na kichaa sasa hamna kichaa tena.
Nabii Hebron: Enhe,
vipi mama, unaonaje sasa?
Nabii Hebron: Ukichaa
umetoka anachukua mtoto wake
Nabii Hebron: Si
alikuwa kichaa sasa hivi?
Nabii Hebron: Emmanuel,
Huyu ni mtoto wako?
Nabii Hebron: Ni
mtoto wangu huyu.
Nabii Hebron: unamependa?
Emmanuel: Nampenda.
Nabii Hebron: Hebu
mbusu.
Nabii Hebron: Na
huyu ni mke wako?
Emmanuel: Ni mke
wangu
Nabii Hebron: Mke
wako?
Nabii Hebron: Unampenda?
Nabii Hebron: Hebu
mbusu na yeye
Nabii Hebron: Aisee
walitaka kukumaliza. Sawa sawa? Simama hapa, hawakupati tena.
Waumini: Amen
Nabii Hebron: Haya
kakae
Nabii Hebron: Anadunda,
haya mchukue mtu wako bwana
Nabii Hebron: BWANA
YESU ASIFIWE. hiyo ni imani yenye
Waumini: Nguvu
Nabii Hebron: BWANA
YESU asifiwe, endelea kuimba, nyoosha mikono
Nabii Hebron: Huyu
alikuwa amebakiza masaa matatu afe sasa, mmesikia? Masaa matatu.
Nabii Hebron: Eheee..
mtasema huyu ni kichaa? Mtasema huyu ni kichaa sasa anafuta mtoto wake? eeeh?!
ana upendo. Analea baba mzuri.
Nabii Hebron: Hebu
muangalie aisee, si unamjua wewe?
Ndugu wa Emmanuel:
Leo ni siku ya tatu hajui mtoto wake, mama yake yani hata kuongea alikuwa
haongei, hata hanijui mimi niliyekuja naye.
Nabii Hebron: Wewe
ni nani wake?
Ndugu wa Emmanuel:
Mimi ni mdogo wake
Nabii Hebron: Eeeeeh...
aisee anashukuru. Yani anakupa mkono. Mwambie asante
Emmanuel: Asante
aisee.
Nabii Hebron: Ulikuwa
wapi Emmanuel? Ulikuwa unajua?
Emmanuel: Mimi
sijui. sijui.
Nabii Hebron: Tena
nikuambie alikuwa amebakisha masaa matatu. Hesabu sasa hivi masaa mangapi bado?
Tena kesho abatizwe ili wasimuweze tena.Mmesikia?
Nabii Hebron: Nabii
Hebron unamfahamu? wa Arusha?
Emmanuel: Eeeh
Nabii Hebron: Wewe
Umetoka wapi?
Ndugu wa Emmanuel
& Emmanuel: Kondoa
Nabii Hebron: Umetoka
Kondoa?
Nabii Hebron: Kondoa?
Ndugu wa Emmanuel:
Yani leo ndio tumetoka huko.
Nabii Hebron: Mlijuaje
habari ya hapa?
Ndugu wa Emmanuel:
Ndio hivyo MUNGU mkubwa..
Nabii Hebron: Redio?
Nabii Hebron: Au
ni mtu amewaelekeza?
Ndugu wa Emmanuel:
Tumeelekezwa, na,... na yani yote ni mipango ya MUNGU.
Nabii Hebron: Ilibakiza
masaa matatu. Hafi tena.
Waumini: Amen