BWANA YESU ASIFIWE, YESU WA
NAZARETI ambaye ndiye kristo wa MUNGU au mwana wa pekee wa MUNGU aliyetumwa
kuja kulikomboa ulimwengu. Katika somo hili nitafundisha uelewe na utofautishe
ukristo wenye asili ya shetani au uliotoka kuzimu ukoje na hata sasa upo hapa
ulimwenguni kwa kiasi kikubwa sana na ukristo huo umeshikiliwa na kupokelewa
kwa kiwango kikubwa na pasipo watu kuelewa kuwa ukristo huo walio nao siyo wa
MUNGU bali ni ukristo wa mpinga kristo.
Ukristo huo unaitwa mpinga
kristo sababu upo kinyume na YESU, ROHO MTAKATIFU pamoja na MUNGU aliyeumba
kila kitu. Ukisoma 1 Yohana 4:1-6. Nabii Yohana alisema wapenzi msiziamini kila
roho bali zijaribuni kama zimetoka kwa MUNGU. Hapa ndipo watu wametekewa na
mpinga kristo hata na kujiunga na umoja wa mpinga kristo japo najua idadi kubwa
zaidi inampenda YESU ila alilolituma adui hapa wakaleta roho yao ya kristo wa
uongo, ikaja duniani na ikafanikiwa kuanzisha makanisa wakitumia jina la YESU ili
kuwateka wengi hata wale wateule wa MUNGU wakajiunga nao vizazi na vizazi. Pia kumbuka
YESU alishasema wengi watakuja kwa kutumia jina langu na watawateka wengi, hata
sasa imetimia, ila YESU alishatupa ishara zote, yeye hapaswi kulaumiwa sababu
alishayaweka yote wazi wazi.
Cha kujiangalia zaidi ni
kuzichunguza hizo roho, je wanachokifanya kimetoka mbinguni au zimeruhusiwa
katika neno na ukiona ni kinyume uelewe ukristo huo siyo ukristo wa mbinguni ni
ukristo ambao asili yake ni kuzimu na unaposhiriki basi na wewe tayari
umeshakuwa mfuasi wa kristo wa kuzimu na hata katika ibada zote uelewe
unamuabudu kristo wa kuzimu kabisa, na hata kama ni kanisa linajiita ni la
kiroho na unaona umeokoka lakini lipo kinyume na biblia tu uelewe unazidi
kujiimarisha katika ufalme wa mpinga kristo wala wewe siyo wa YESU wa mbinguni.
Nitaelezea machache ili upate
picha uelewe na ukatae ukristo wa kuzimu:
Ukristo unaobatiza watu kwa
ubatizo wa maji ya kikombe, kubatiza kwa maji ya kisima, kubatiza kwa jina la
mchungaji, kubatiza watoto wadogo. Tafuta katika biblia ya MUNGU, haya hayajaruhusiwa
na kama hayajaruhusiwa sasa uelewe ukweli huo ni ukristo wa kuzimu na siyo wa
mbinguni.
Wakristo wanaoabudu sanamu.
Kubariki watu wazima, badala ya
watoto wadogo.
Ukristo unaoongozwa na huduma 6
na zaidi badala ya zile tano alizozianzisha YESU.
Ukristo unaoruhusu pombe,
ushoga, unazuia watu kuokoka, kutolea sanamu sadaka, kufanya ibada za wafu,
kuandika sadaka majina, kumuabudu mcungaji.
Ukristo wenye viongozi
freemason, illuminati, mchawi na mengineyo, ikiwemo kuweka misalaba katika
nyumba za ibada.
NOTE:
Nimeeleza, naamini utakuwa sasa
umepata picha na wewe utafunguka na uwatumie na wenzako ili wawe nao wakristo
wa mbinguni kama wapo katika ukristo wa kuzimu watoke wasije wakaangamia. YESU
aliye mwana wa MUNGU yeye yupo mbinguni, na ili uwe mkristo wa mbinguni ni
lazima uifuate biblia ilivyo na siyo uchanganye ukweli na uongo, inapokuwa
tofauti tu uelewe umeshakuwa mkristo wa kuzimu, na kama upo hivyo basi uelewe
ukifa utaenda huko kuzimu ambako na wewe umeyashika mafundisho yao. Ila ipo
neema ya YESU, amenituma mimi Hebron niwafundishe muujue ukweli na utakapo
upokea utakuweka huru kama unavyoelewa sasa kuwa ulishapotezwa upo katika njia
ya yesu wa kuzimu. Yesu huyu wa kuzimu njia yake ni uongo na ili kuujua uongo
chunguza mafundisho yake hapo utapata jibu, tena bila ubishi.
YESU aliponieleza mimi mwenyewe
niliogopa sana sababu hata mimi nilibatizwa ubatizo ambao haujatoka mbinguni
yaani ubatizo wa maji ya kikombe nikafanywa niwe mkristo wa kuzimu, lakini YESU
WA NAZARETI aliniokoa na kunitoa katika kambi ya ukristo wa kuzimu ili siku
moja niwepo mbinguni na yeye alipo. Nawasihi muokoke sasa enyi watu wa mataifa
yote, na kama upo katika ukristo wenye asili ya kuzimu nakusihi utoke huko
sababu wakristo wa jinsi hiyo wanaandaliwa moto wa kuwachoma milele sababu
wamekuwa wapinga kristo. Ila wengi wametekwa hawajijui na wengine wanajijua
kabisa wanafanya kazi ya shetani kabisa ya kueneza umissionary wa yesu wa
kuzimu ili shetani awateke watu kwa kutumia jina la yesu wa uongo.
Sema BWANA YESU WA NAZARETI
uliye mbinguni naomba unisamehe dhambi zangu. Najitoa kwa yesu wa kuzimu na
sasa mimi uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele. Sikutaki
tena wewe kristo wa kuzimu kuanzia sasa. Amen.
Mpaka hapo umeokoka na wewe ni
mkristo wa asili ya mbinguni. Sasa usirudi katika nyumba za ibada za jinsi hiyo
tena, wala usishiriki tena, ukiingiza hata mguu wako tu tayari unatekwa tena na
shetani. Zaidi fuatilia masomo katika website ya www.prophethebron.org
NABII HEBRON.
