UBATIZO WA
MAJI YA KISIMA NI UBATIZO WA KABURI.
Ubatizo aliobatizwa YESU ulitoka kwa MUNGU wala haukutoka kwa
mwanadamu. Ukisoma katika kitabu cha injili ya Yohana 3:1-36, inaelezea vizuri
kabisa jinsi YESU alivyobatizwa, na inaelezea YESU hakubatizwa katika kisima
bali ni katika mto ambao maji yalikuwa yanatembea yakiwa yamejaa mto tele,
ikiwa inayomaana hii unapobatizwa katika mto ni lazima maji yawe yamejaa kiasi
kwamba unaweza ukazamishwa mwili wako. Na pia kama YESU duniani alienda mpaka
mahali penye mto? Jibu, alijua ubatizo unayotakiwa ambao ulitoka kwa MUNGU ili
afanye agano na mwanadamu awe mtoto wake, sasa nawauliza swali, je mnaamini
ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni? Jibu, ndio. Je ubatizo wenyewe ukoje? Ni wa
maji mengi katika kijito cha utakaso yaani maji yanayotembea, siyo yaliyochotwa
au kuhifadhiwa, yakajazwa kwa mikono ya wanadamu badala ya yeye MUNGU kuyaleta
akisjirikiana na umbaji wake na siyo kwa kujenga kisima.
YESU alikwisha onyesha njia, sasa yeye ndiye njia salama,
sasa hamuoni tayari hiyo siyo njia salama? Ubatizo umebadilishwa. Ila kama
alivyonituma YESU mimi Nabii Hebron ni lazima niufikishe ujumbe wake na
niufichue ushetani ulioingilia katika tendo la ubatizo na kuwafanya mabilioni
ya watu waweke agano na shetani badala ya MUNGU na kufanyika kuwa ni wakristo
wa kuzimu hawaendi mbinguni. Swali lingine, imeandikwa MUNGU analihakikisha
neno lake na alisema lisibadilishwe na atakaye liongeza au kulipunguza hataenda
mbinguni (soma Ufunuo wa Yohana 22: 18-19). Hapo jambo la kwanza unaona wazi
wazi huu ni uongo wa shetani sababu siyo kijito yaani maji yanayotembea bali
yamesimama haijalishi yamejaa tele. Swali, je yanatembea? Jibu, hapana. Je hicho
kisima ni kazi ya MUNGU kulitengeneza au ni kazi ya mwanadamu, jibu ni wanadamu
wamejenga. MUNGU angetaka watu wabatizwe katika kisima angemtuma Yohana, lakini
hakutaka.
Sasa niwaulize mnataka aliyotumwa Yohana au ubatizo wa kazi
za wanadamu? Taka wa Yohana ili upone. Ila ipo siri kubwa sana ambayo shetani
ndiye na yeye alimtuma mjumbe wake ambaye anaitwa Yohana wa kuzimu na yeye
ndiye aliyeuleta huo ubatizo wa maji ya kisima akawapiga upofu watu ili waone
wamebatizwa katika maji mengi kama ilivyo katika biblia lakini mpaka sasa
umeelewa. Hivyo nakushauri ubatizwe upya wewe umepokea ubatizo wa agano la
shetani. Ubatizo wa maji ya kisima unazo siri za shetani na mimi Nabii Hebron
nitakueleza sababu ninataka kusudi la BABA yangu aliye mbinguni tu ndio litimie
na hili la shetani nilibomoe na watu waende mbinguni.
Ubatizo wa maji ya kisima unapokuwa umezamishwa pale
unaingizwa katika kaburi katika ulimwengu wa roho, umezikwa na vitu vyako na
kufungiwa katika hilo kanisa lenye agano la ubatizo ambao haujatoka mbinguni.
Jambo lingine, katika makanisa ya kiroho 99.9% ya watumishi
wanaotumia ubatizo wa kisima huwa tayari ni wachawi na huwa ni watenda kazi wa
shetani kabisa ila wanajificha kwa kujiita watumishi na hata ndio sababu
nyingine hawa katika makanisa ya kiroho wanawabatiza waumini kwa majina ya
wachungaji. Lile ni agano la shetani na unapobatizwa hivyo unakuwa wewe ni mali
ya shetani na hata kama mpaka sasa na wewe umebatizwa hivyo uelewe mbinguni hauendi
sababu unalo au uliingia agano la ubatizo wa kisima au la kuua roho yako na
kufungwa utumikishwe na mchungaji huyo badala ya YESU siku zote za maisha yako
na siku ya mwisho YESU ataliangalia agano la ubatizo ataona ni tofauti basi
utatupwa katika ziwa la moto.
Asilimia 1% ndiyo makanisa yameiga huo ubatizo pasipkujua
ila nawaeleza hata wewe uliyeiga haukuiga katika biblia bali umeiga kutoka
katika kazi za wanadamu hivyo shetani bado yupo na wewe sababu ananyanyua
mashtaka kwa MUNGU si amebadilisha ubatizo, na MUNGU ananyamaza sababu ni
kweli. Tubu mkabatizwe upya, bado hauna agano na YESU wa mbinguni bali lipo
agano la shetani kwako.
Maji hayana uhai ni maji mauti.
Ubatizo huo ndio agano la freemason, illuminati, na mpinga
kristo na kwa wale watumishi wanaobatiza hivyo nao hupewa nguvu na shetani ili
kuweza kuliendesha kanisa hilo na kuwafanya watoto wa MUNGU misukule au vitega
uchumi vyao. Ili amkamate muumini awe teka wake ni lazima akuzike kwa njia ya
ubatizo wa kisima. Na ndiyo sababu wengi wanateseka na mambo kuwa shida,
kumbuka ulipobatizwa, ulizikwa na haiwezekani ufufuke ni mpaka uje ubatizwe tu
ndipo ufufuke na uingie agano na YESU, na pia ubatizo wa kisima unakufukuzia
mbali na YESU na kukukaribisha katika ufalme wa shetani.
NOTE:
Batizo zote tofauti na ubatizo wa Yohana ni batizo za
shetani alizozituma huku duniani na zimepokelewa na ule wa mbinguni umekataliwa
ili wanadamu wasiwe watoto wa MUNGU. Amenituma YESU kwa sauti ya uchungu, Ole
wao wanaowapoteza watoto wangu. Nenda uwaeleze, watapona wale watakao tii,
shetani anajua ile siku ya mwisho wapo wengine hawatendi dhambi ila atawahstaki
wanalo agano la ubatizo wa shetani. Sasa nawaeleza wakati ndio huu sasa, uje
utolewe hilo agano, ili ile siku ya hukumu usiwekewe shtaka na shetani. Zaidi soma
masomo ya ubatizo katika blog ya Nabii Hebron, na pia sikiliza mafundisho
katika YouTube ya Prophet Hebron, na watumie na wengine ili wapone. YESU
anarudi, usikutwe na agano la shetani na usishiriki hata kuabudu katika sehemu
wanayobatiza ubatizo wa kisima, hapo ni makao ya shetani na huo ni mlango wa
shetsni. Na pia kisima hicho ni lango la kuzimu, wewe ulipelekwa huko.
Sasa sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote,
uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele. Uniongoze nikaondolewe
hili agano la lango la kuzimu, katika nafsi yangu ili niingie agano na wewe
YESU sababu mpaka sasa halijatoka. Amen.
Ufanye haraka ubatizwe upya na ukatengwe nao. Karibu katika
kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE ubatizwe uwe huru.
NABII HEBRON.