SANTA CLAUS
AU SAINT NICHOLAS HUYU NDIE MWANADAMU ALIYEMUIBIA YESU UTUKUFU WA SIKU YA
KRISMASI (BIRTHDAY).
BWANA YESU WA NAZARETI ASIFIWE. Nawasalimu watu wote
mnaompenda YESU au kwa jina lingine anaitwa Nabii Issa. Nabii ambaye ndiye aliyeteuliwa
na MUNGU kama njia ya kutupeleka mbinguni bila yeye haufiki sababu hakuna aijuaye
njia hii ya kwenda mbinguni hata mitume waliopo na waliopita. Ndiye Nabii
ambaye mpaka sasa katika ulimwengu huu jina lake ndilo lenye nguvu kuliko
majina yote na ndiye Nabii katika ile siku ya mwisho yeye ndiye aliyeteuliwa
kuja kuwanyakua wale watakatifu na ndiye atakayehukumu ulimwengu huu, na zaidi
hata biblia imemtaja yeye ndiye mwana wa pekee wa MUNGU aliye hai, hivyo ni wa
kuheshimiwa kuliko chochote katika ulimwengu huu na kupendwa.
Ila cha ajabu shetani katika miaka ya nyuma akawaingia
wanadamu kupitia Santa Claus au Saint Nicholas wakawaita wao ndiyo Father
Christmas badala ya YESU WA NAZARETI aliye BABA yetu iwe ni siku yake maalum na
kumtukuza MUNGU kwa kutuletea mkombozi ikabadilishwa na wapinga kristo na
waliompinga MUNGU na matokeo yake sasa kila Krismasi watu wamewachanganya Santa
Claus na Saint Nicholas kama ndiyo siku yao badala ya kuwa ni siku maalum ya
YESU. Watu walitekwa fahamu zao na kanisa ambalo halikumsikiliza MUNGU au
kulitetea jina la YESU na lenyewe
likajiunga katika upande wa Santa Claus na Nicholas. Ila sasa aliyonituma mimi
Hebron katika ulimwengu wote niwaeleze ukweli, utakayesikiliza utapona, utakaye
kataa kusikiliza utaangamia. Wakristo wamepotea kiasi kwamba ile siku ya
mkombozi wao ambaye ndiye YESU hakuna mpaka sasa aliye thubutu kutaka siku ya
kuzaliwa YESU kuwa ni siku yake wala haipaswi kushirikishwa na chochote. Ila YESU
amedharauliwa sana hata MUNGU aliye BABA yetu na aliyeumba vitu vyote
amedharauliwa na huu ndio ukweli lazima watu wafunguke ili wasijewakapelekwa
jehanamu.
Siku ya Krismasi ilipoingiliwa na huyu mwanadamu anayeitwa
Santa Claus au Nicholas shetani ndiye aliyeandaa jambo hili sababu hakufurahia
YESU kuzaliwa na ili kuivuruga ile siku akawateua Santa Claus na Saint Nicholas,
na watu wakaamini mpaka sasa na imekamata dunia yote. Sasa kinyume chake
unapomtaja Santa Claus au Nicholas unakuwa unaabudu aina ya mungu anayeitwa
Claus na unapokuwa unamtaja Santa Claus inakuwa yeye ndiye anayekutawala katika
ulimwengu wa roho wala MUNGU hakupati sababu unakuwa unalo shtaka ambalo
shetani analinyanyua kwa MUNGU juu yako kuwa huku duniani una vitu vyake mfano
father Christmas, kadi zake, picha zake na hata unapiga picha na yeye. Sasa muelewe
watoto wa MUNGU, hii ndiyo njia nyingine pia aliyoitumia shetani na akafanikiwa
kwa liasi kikubwa kuiteka dunia, hakuna mahali ambapo Santa Claus hatajwi
wakati wa Krismasi.
Sasas jiulize je ilikuwaje na ina maana gani yeye atajwa
kama ndiye mhusika wa siku hiyo? Natumaini umeelewa na utapona. Yapo mengi
aliyoyafanya Santa Claus katika ulimwengu wa roho japo alishakufa sasa hivi ni
mzimu na hajaenda mbinguni nimemuona kuzimu na nilimfanyia kile alichonieleza
YESU sababu huyu ni adui wa YESU. Tazama Petro hakukubali YESU achezewe alikata
sikio la yule Myahudi, na wewe usikubali kabisa jina la YESU lichezewe kwa
kutumika kwa uongo sema kweli tu siyo upige mtu. Vita vyetu ni vya kiroho siyo
vya kimwili. Sasa na wewe unaposhiriki katika Krismasi na Santa Claus na wewe
unakuwa umeungana kuiba utukufu wa MUNGU na kuwapeleka watu wampatie shetani
utukufu eiza kwa kujua au kutokujua. Sasa tazama kanisa lilivyotekwa na shetani
lenyewe ndiyo kiongozi wa kumtaja huyu Claus na Nicholas ambaye hana tofauti
hata na wewe.
Sasa uache ili upone na wewe unayetaka kwenda mbinguni
inakubidi umkatae kuanzia sasa huyu Santa Claus ili ile siku ya mwisho usiwe na
shtaka ulilowekewa na shetani na wewe haujui ukakutwa unayo hatia. Na kama
mpaka sasa unavyo vitu vya Clause au
Nicholas ujijue unalo shitaka ambalo shetani analificha pasipo wewe kujua ili
ile siku ya mwisho atasema na wewe au yule alishiriki kuifanya siku ya kuzaliwa
YESU kuwa ni siku ya Santa Claus pia na ukaiunganisha na yeye. Hilo ni kosa na
ni dhambi na ujue unakuwa unamtukana MUNGU unapoifanya siku ya mtoto wake
kuzaliwa na kuiita Santa Claus, hata kutengeneza mdoli anaitwa father Christmas.
Hii ni sawa na huyu father Christmas (mdoli) eti ndiye MUNGU, je MUNGU ni
mdoli? Ili mpone achaneni na mambo ya Santa Claus na father Christmas kabisa. Zaidi
ingia katika YouTube ya Prophet Hebron nimeelezea zaidi kuhusu father Christmas
na pia katika blog hii ingia kupitia website www.prophethebron.org.
NOTE:
Je, Huyu Santa Claus ni mwana wa pekee wa MUNGU? Je, Yeye ni
Emanueli? Je, yeye alizaliwa na Maria? Je, yeye alizaliwa kwa uwezo wa ROHO
MTAKATIFU? Je, yeye ndiye Kristo? Je, yeye ndiye Masiya? Je, yeye alikufa na
kufufuka. Mpaka hapo umepata picha ya kuwa huyu ametumiwa na shetani kuiba
utukufu wa siku ya BWANA YESU kuzaliwa na kuwapoteza watu wote wanaomuamini
yeye.
Sema BWANA YESU WA NAZARETI, naomba unisamehe niliabudu
miungu, nikashiriki kuchafua siku yako ya kuzaliwa, naomba uniponye sasa. Sitaki
tena mambo ya Santa Claus nakutaka wewe
tu hata vitu vyake sivittaki tena milele. Amen.
NABII HEBRON.