Haleluya, karibuni sana katika kipindi tena siku njema ya
leo ambayo siku ya leo ninakuletea habari njema, habari njema kutoka kwa YESU,
habari njema kwa mataifa yote, habari njema kwa anayemjua na asiyemjua. Lengo
langu na lengo la MUNGU ni habari mjema ifike kwako. Amenituma habari njema
ifike kwako. Amenituma niwaeleze habari njema kuhusu habari za ufalme wa
mbinguni. Hajanituma nieleze habari mbaya.
BWANA YESU asifiwe. Haleluya; Baba ninawaombea watoto wako
tayari kwa kusikiliza habari njema kwa siku ya leo, ninafuta ndani ya mioyo yao
wale wote waliopokea habari mbaya wakajulishwa kama ni Injili kumbe sio Injili
wakapokea habari mbaya. Na ndio maana wanateseka, ndio maana wanahangaika, ndio
maana wamechanganyikiwa, ndio maana hawana mbele,ndio maana wanajuta na
wanahangaika, hii yote ni kwa sababu hawakupokea habari njema, walipokea habari
mbaya. BABA ninakutukuza, ninakuinua, ni kwa utukufu wako, Amen.
Watoto wa MUNGU, siku ya leo nitakwenda kufundisha habari
njema aliyoileta YESU alipotumwa kutoka mbinguni. Yeye hakuleta habari mbaya,
alileta habari njema. Ni habari njema kwa sababu pasipo hiyo habari njema
hauwezi ukamwona MUNGU hauwezi ukafika alipo yeye, hauwezi ukafanikiwa. BWANA
YESU asifiwe. Haleluya, utafungua na mimi katika kitabu cha WAGALATIA 1 : 6-9.
Neno la MUNGU linasema hivi; nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi ili yeye
aliyewaita katika neema ya Kristo na kuigeukia Injili yanamna nyingine, wala si
nyingine lakini wapo watu wataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo.
Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubirie ninyi injili nyingine
isipokuwa hiyo tuliyohubiri na alaaniwe. BWANA YESU asifiwe. Kama
tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena mtu awaye yote akiwahubi ninyi
injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe. Tutafungua nawe kitabu
cha WARUMI 1 : 16, nitaendelea kuisoma, neno la MUNGU linasema hivi; kwa maana
siionei haya injili kwa sababu ni uweza wa MUNGU uletao wokovu kwa kila
aaminiye kwa Myahudi wa kwanza na kwa Myunani pia. Haleluya; BWANA YESU asifiwe.
Umesoma katika kitabu cha WAGALATIA neno la MUNGU linasema ambaye atakayeleta
habari tofauti na neno la MUNGU na alaaniwe. BWANA YESU asifiwe. Alaaniwe kwa
sababu MUNGU anasema hivyo kwa sababu sio habari njema. Kwa hiyo Biblia
ikibadilishwa ikaenda kinyume au anayefundisha, tayari amelaaniwa. BWANA YESU
asifiwe. MUNGU alipokuwa akinifunulia somo hili ili kuwafunulia watoto wa MUNGU
na kuwafundisha, kwanza alinifundisha mimi kwa faida yangu kwa miaka mika mingi
japo yalikuwa yamekaa ndani ya moyo wangu ila wakati wake ukifika nitafundisha
kama sasa ilivyo. Haleluya. Sasa watu wengi wanajua kwamba wanapokea habari
njema ila wanapokea habari mbaya. Nitakufundisha tofauti ya habari mbaya na
habari njema. Habari njema zinatoka mbinguni. Habari njema ni habari ya ufalme
wa MUNGU, kusimamia neno la MUNGU kama lilivyo bila kulibadilisha kunyooka
straight kama MUNGU anavyotaka yeye. Ikiwa ni tofauti tu, ni habari mbaya.
Mfano imeandikwa, usiabudu sanamu. Sasa kanisani wanahubiri Biblia kidogo
ukweli halafu wanaabudu sanamu. Hizo zote ni habari mbaya ninawaeleza watoto wa
MUNGU. BWANA YESU asifiwe. Unapovunja amri za MUNGU tayari umepokea habari
mbaya, na unapopokea habari mbaya inakaa ndani yako inakujengea mabaya unazidi
kulaaniwa na kulaaniwa. Lakini nitazungumza katika kipengele cha watumishi.
Maana watumishi wengi nimekuta katika maombi na MUNGU alivyokuwa ananifundisha
wameshalaaniwa. Yamkini hata ni wewe unayeangalia hapo umelaaniwa kama ulikuwa
hujui. Kama unachangisha pesa kanisani, MUNGU amesema hivi, atakayefundisha
tofauti na MUNGU anavyopanga na alaaniwe. Sasa wewe utabisha wapi hujalaaniwa?
unaabudu sanamu umelaaniwa, unachangisha watu pesa kanisani umeshalaaniwa. Ni
freemason halafu unajifanya mtumishi umelaaniwa. Umejiamkia tu kwa kutafuta
pesa kwa kudanganya watu kwa kujifanya wewe ni mtumishi kumbe MUNGU hajakuita,
umelaaniwa. Utabisha hujalaaniwa? Na kama umelaaniwa, tayari mbinguni huendi.
Sasa madhara yake na wale wote ambao mnasikiliza mmeshalaaniwa kwa sababu
mwenye laana hana baraka, anatoa laana, na laana, na laana. Mfano YESU
alipokuja, alileta habari njema ya ubatizo wake wa maji mengi akasema kila mtu
afuate njia yake. Sasa watu watu wanabatizwa ubatizo wa maji ya kikombe
nikuulize swali, hiyo ni habari njema au mbaya? Kama ni ni habari njema ina
maana ubatizo huo umetoka mbinguni. Kama ni habari mbaya hauko mbinguni, hauko
kwnye Biblia. Anakubatiza kwa jina lake mtumishi. Hiyo ni habari mbaya.
Imeandikwa ubatizwe kwa jina la YESU tu basi. Sasa haya yametoka wapi?
Amenituma niwaeleze habari njema. Utakaposikiliza utapona na utabadilika, maana
watu wanafikiri mtumishi akishasoma Biblia hivi tu basi, huyo ndie anayeeleza
habari njema. Soma Zaburi ya 23 Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na
kitu lakini anakunywa pombe; anakueleza habari njema gani? Watoto wa MUNGU ni
wakati wa kufunguka. Sasa hivi kuna mikuno mingi sana, utaambiwa semina, injili
inapelekwa lakini sio habari njema. Hata kama wanasema habari ya wokovu,
wanayoyatenda ni biashara, kutafuta pesa, wamechanganya na uchawi na wana wa
MUNGU ndio maana matatizo hayaishi yamejaa kwenye nchi mbalimbali wala hayaishi
kila siku asubuhi mchana na jioni kwa sababu wamekuja wajamaa sasa hivi, badala
ya kuendeleza habari njema wanaleta habari mbaya. Unataka kumwona mtumishi,
utapita kwa sekretari, utaandika jina, utatoa hela, utapewa kuponi ili upewe
appointment hiyo habari njema au mbaya? Hiyo ni mbaya. Imeandikwa utoapo sadaka
yako mtu yeyote asijue. Leo makanisa yanakuambia andika namba ya simu na kiasi,
unapewa risiti. Hiyo ni habari njema au mbaya? Jibu ni mbaya. Sasa kama
wanafanya hivyo, wamelaaniwa, na wewe unayeshiriki laana imekuhusu ndio maana
hakuna baraka. Unafilisika. Ni mahali pa kukimbia wala usishiriki. Hizo ibada
ni makelele mbele za MUNGU, na MUNGU siku moja nilikuwa naongea naye,
akaniambia Hebron sipendi mtu mwenye dhambi hata kusikia sauti yake, hata kuona
mahali anapolala. Sasa pata fahamu, kama watu wanakuwa na roho ngumu, wanaenda
kinyume na MUNGU, ukienda kinyume na MUNGU ni laana unaitafuta. Ukiabudu sanamu
umefuata laana. Ukiabudu Mathayo, sijiu Eliza umefuata laana. Wewe mwabudu
MUNGU peke yake. Ukiabudu haya maua, ukiniabudu mimi umeshalaaniwa. Umeabudu
ng’ombe, umeabudu miti umeshalaaniwa. Ninawasihi mfunguke. Ndio maana maisha
hayaendi. Mje kwa YESU siku ya leo.
Haleluya. Na msidanganywe kwa sababu MUNGU kama amewatuma
watumishi waeneze neno lake, ni habari njema, sasa hivi habari ni michango,
michango, michango mitupu, support redio, support TV. Hizo ni habari mbaya.
Kama MUNGU amemtuma huyo mtumishi habari njema amesema asifikiri nini wala
nini, yeye aende atafungua milango mambo yaanyooka. Lakini hayanyooki kwa
sababu ni habari mbaya. Hivi kanisa lina benki. YESU amesema hivi; msichaji
riba, lakini mtumishi ana benki. Amesema msiwe na mabwana wawili. Sasa hizo ni
habari njema au ni habari mbaya? Sasa msingi tayari umekwisha haribika, na mti
ukishaharibika, na matawi yameharibika yote. Watu wanamsubiri YESU, atarudi,
mnatazamia wengine wanakwenda kumbe hamuendi. Hizo ni habari mbaya. Sababu
iliyopo ni hawa wajamaa wamelaaniwa. Kwanza mimi siwawaiti watumishi niwaite
wajamaa. Tena bora ni bora nisiseme wajamaa, maana jamaa wengine ni watu wazuri
tu, mfano jamaa yako jamaa yangu, jamaa yule, lakini watumishi wameoza. Ndio
wauza madawa ya kulevya, wauza bangi, wauza pombe, ni washirikina, wanatoa
makafara. Sasa atakuleteaje habari njema mtu kama huyu? Mtu kama huyu ambaye
anakuambia ili ubarikiwe au akuombee lete pesa, hiyo ni habari njema au ni
habari mbaya? Amenituma niwaombee bure, hiyo ndio habari njema. Amenituma niwafundishe,
niwaongoze ili mumwone yeye. Hiyo ndio habari njema. Lakini mambo ya sheria
sheria ili iwe hivi, fanya hivi, kuangalia vitu vyako, ni wezi hao.
BWANA YESU asifiwe. Alisema watakuja makristo wengi, hata
sasa ni wengi, na wamejaa; Tanzania na dunia nzima. 99% watumishi wamelaaniwa,
wana laana, hawana baraka. BWANA YESU
asifiwe. Huo ndio ukweli. Ukitafuta mtu wa kukubariki sasa hivi ni shida,
humpati. Atakuambia tu BWANA atafakunyia, haleluya, haleluya, lakini mchunguze;
ana laana kuanzia mguuni. Sasa watu walionaga MUNGU yeye haoni, wanamdanganya.
Ni sawasawa na mtoto mdogo analamba sukari halafu imebaki mdomoni, baba yake au
mama yake anamuuliza kwa nini umelamba sukari? Yeye anajibu “mimi sijalamba
mimi”. Ndio watumishi wa sasa hivi, lakini MUNGU anaiona na MUNGU anaona
mnataka baraka lakini mna laana. Sasa mtapata wapi? Mtamwonaje MUNGU? BWANA
YESU asifiwe. Kanisa limeacha njia ya MUNGU. BWANA YESU asifiwe. Limekwenda
kinyume kabisa, badala ya habari njema sasa hivi ni habari za laana, habari
mbaya. Sasa hivi habari kanisani ni pesa, michango michango michango. Hayo
majengo ni mapango ya laana. Na ndio maana hata mliojenga hambarikiwi kwa
sababu mmedanganywa hamkutoa kitu ambacho kinajenga ufalme wa MUNGU, bali
kimejenga ufalme wa laana. Ndio maana unadaiwa sana kanisani. Hizo ni habari
njema? Makanisani sasa hivi habari ni madeni tu. Watu wengi mna madeni. YESU
hakutuma habari za kuchukua pesa zenu bwana. Na kama unatoa pesa ujue hizo ni
habari mbaya. Pesa inauma, ukitaka kumtolea MUNGU, toa ukiamua, kwa moyo wako,
tena usitake ujulikane. Iwe ni siri yako, maana kuna watu wengine wanasema
nikitoa nikionekana ndio MUNGU ataniona; rudi kwenye neno la MUNGU; ficha mtu
asijue. MUNGU anaona kama unamtolea bwana. Sasa hawa jamaa wamekuja na saikolojia
ya kukuchezea chezea, andika jina, sasa mtu akiandika jina anaona aibu kutoa
mia mbili, masikini ya MUNGU atatoa elfu, kumbe elfu ndio bajeti yake ya kula
siku nzima. Sasa huyu MUNGU akunyang’anye mpaka uishiwe ni mungu gani huyu? Na
zaidi wakiona hivi kuna kitabu askofu anatakiwa aje akisome hapa, ni saikolojia
tu ili udanganywe askofu ataona nimetoa ngapi ataiona vizuri kweli. Taka MUNGU
akuone, usitake mwanadamu akuone wala mchungaji akuone, hao wamelaaniwa. Ukweli
ndio huo; katika nchi utasikia kuna semina nyingi sana. Hivi kweli wangekuwa
wanapeleka baraka kuna watu wangekuwa na shida? Sasa hivi ukipita katika
Tanzania ukipita kwenye kijiji kimoja makanisa labda mia mbili au mia tatu.
Yote yanaeleza eti habari njema. Habari gani watu wana shida? Habari gani nchi
haifunguliwi? Habari gani mpaka nchi ikafilisika? Kama kweli serikali inatoa
vibali, ili hao jamaa waiombee nchi, na MUNGU aibariki nchi. Miaka yote nchi
hainyanyuki, wachawi nfio wanaitesa, shetani ndio anaitesa mnabaki kulaumu
viongozi; siri iko wapi? Hawa jamaa wana laana. Kwa sababu mahali palipo na
nabii au mtumishi wa MUNGU wa kweli lazima baraka zishuke, lazima kuwe kuna
njia, lazima kuwe kuna upenyo, upenyo uko wapi? Watu sasa hivi wanatafuta
majibu baharini; baharini ni kwa waganga wa kienyeji. Na siwacheki kwa sababu
watumishi wenyewe nimekuwa nikifungua watu wengi sana wemeniambia mimi
nimekwenda kwa mganga zamani hizo nashangaa namkuta mchungaji naye amepaki na
suti, mganga ananiambia namtengeneza na huyu jamaa bwana, si anaenda kuhubiri
huko? Sasa mganga atakupa nguvu gani wewe ya kwenda kupeleka habari njema?
Zaidi unaenda kumwaga makufuru, makafara. MUNGU awaaibishe, MUNGU awashushe
wote mnaotumia uchawi. Nimetamka neno hili halirudi kama vile mvua inavyonyesha
inagonga chini, mazao yanatokea. Ndivyo ilivyo, watu wamechoka, watu wanakata
tama, watu wanalala njaa sababu pesa zao mnavyozichukua mnaenda kupeleka kwa
mashetani, wanalaaniwa, watoto wa MUNGU linda sana ulicho nacho, pesa yako mtu
asiizoee. Wengine mpaka watumishi wanajua akaunti ya mtu Fulani ina shilingi
Fulani. Yeye ametumwa huko wewe? Kama MUNGU amekutuma, kahubiri, nenda mbele.
Fungua mtu aende zake. Acha kuangalia ana suti, acha kuangalia ana gari, acha
kuangalia ana nyumba. Mwenye ghorofa ndio unafuatwa mpaka nyumbani. Wewe mwenye
kinyumba cha majani hawakufuati, kwenda huko huna kitu. Sasa hiyo ndio habari
njema? Ni wakati sasa hivi injili ifanyike kama vile YESU alivyofanya. Hiyo
ndiyo injili. YESU alilala kwenye mapango, YESU alilala chini, YESU alilala
barabarani, yaani mahali popote. Kwenye shida yupo; leo hii YESU alichukua pesa
za watu? YESU alinyang’anya? Sasa wanachukua jina la YESU wamebadilisha injili
ya namna nyingine, Na Biblia inasema mtu wa namna hiyo au nyingine na alaaniwe.
Sasa wengi wana laana. Ukishakuwa na laana mbinguni huendi, ni kitanzi.
Watumishi jiangalieni, ni wangapi mna laana nyie? Mnasema baba wa kiroho au
mama wa kiroho. Unakuta mama wa kiroho ambaye ni mchungaji yeye ndio anazini na
watoto wake, ameshalaaniwa. Ni mama gani huyo? Baba wa kiroho yeye kazi yake ni
kuzini na waumini tu. Baba wa kiroho ni baba wa kimwili. Wewe utazinije na
mtoto wako wewe? Mnawajua na mnawaelewa. Wana laana. Biblia inasema na alaaniwe
anayefundisha injili ya namna nyingine. Na tena zaidi wengine nimekuta ni maaskofu
kabisa, watu wananiletea mashitaka, wanawaingizia vidole kwenye viungo vyao vya
siri watoto wa kike. Na ni wamama wenye heshima wakijua wamekuja kwa BWANA
YESU, Bwana atawatendea. Ficha watoto wa MUNGU viungo vyako vya siri
usimuonyeshe mtu huko. Ficha. Ukiona hivyo ana pepo huyo. Na wanajiita maaskofu
ni wengi sana. Kesi hizi ziejaa, waumini wamekuja kushtaki, matokeo yake
wanakuwekea mapepo na kukuharibia maisha yako. Hivi mmekuwa madaktari nyie au
manesi? Huko kwenye viungo vya siri mnafuata nini? Shika mikono, mwombee mtu.
Huko unafuata nini? Mnayajua. Msione kwamba watoto wa MUNGU wanashitaki kwa
baba yao. Wanalia, wananung’unika, wao wakiamini wanaongea na MUNGU kumbe
wanaongea na pepo. Nafungua na serikali kweli iwakamate watu wa namna hiyo, iwaadhibu
kabisa, maana huku ni kumtukana YESU. Kabisa kabisa, kutumia jina la YESU na
wanawake wakisikia habari ya YESU wanaamini kweli. Vua nguo nikuombee
wanakubali. Serikali MUNGU awafungue macho muwaone watu wa namna hii. Najua
hata serikali, viongozi wanampenda MUNGU, lakini kwa namna haikubaliki wala
hairuhusiki, hata mimi mwenyewe siikubali, sijui kama yuko ambaye anayekubali.
Ninamwomba MUNGU mtakamatwa, mtakutwa. Mnamwona MUNGU ni mjinga, lakini
nawaeleza ukweli. Ndugu msikilizaji yawezekana ni ndugu yako, au ni baba yako
au ni mama yako amefanyiwa vitu kama hivyo, wanajijua hawasemi lakini
wanapokuja kwa mtumishi kamili anafungua moyo anakuambia. Ni mambo mazito,
lakini wanafanyiwa makanisani. Kama imefika mahali mtu anamwambia mwanamke
(mtumishi), kaibe pesa za mume wako leta hapa. Ni mafundisho gani hayo
unayomfundisha? Ni waizi na wengi wameibiwa na kunyang’anywa mali. Lakini
njiani na suti na VX kumbe ni waizi wakubwa hawa. Wanachafua jina la Mwenyezi
MUNGU. Ni wakati wa kila mtu sasa hivi kuamua kumtetea MUNGU, wewe unayempenda
MUNGU, lakini kama humpendi wewe acha. Sikulazimishi, mimi nakufundisha. Iko
faida kwa MUNGU, iko hasara kwa shetani. Uzima wa milele ni mbinguni, uzima wa
mauti ni kwa shetani. Chagua leo njia utakayoiendea.
BWANA YESU asifiwe. Wengi wamekaa katika makanisa ya wokovu
wanaomba, wanaomba wanajua wanaenda mbinguni wako sawa, lakini wamejazwa
mapepo, wameibiwa nyota hukohuko kanisani. Sasa ni habari gani hizi zinaletwa?
Hizo sio habari njema, hizo ni habari mbaya. BWANA YESU asifiwe. YESU alituma
wale mitume wake wa kwanza waeleze habari njema waieneze. Sasa imekuwa kinyume
sasa hivi inaelekezwa habari mbaya. Haitaitwa mbaya, mimi ninachokufungua ujue
ni mbaya utaona iko tofauti na Biblia. Kwanza ubatizo wa maji ya kikombe, hiyo
ni habari mbaya. BWANA YESU asifiwe. Habari YESU aliyoileta, kwanza alikuja
Yohana akatengeneza njia, ubatizo wa maji mengi. Akaja YESU na yeye akasema
fuateni njia yangu. Sasa hiyo ndiyo habari njema ya mbinguni. Hii ubatizo wa
kikombe sio habari njema, ni habari mbaya na wengi mmeipokea na mmeikubali.
Hata mimi niliipokeaga, nimeikataa na kuitupa huko. Kila uliyewekwa alama hiyo,
wewe maisha yako ni habari mbaya tu. Sasa hawa watumishi ndio YESU amewatuma
kazi hiyo? Haipo. Soma Bblia, tafuta, haipo. Anasema atakayehubiri injili ya
namna nyingine na alaaniwe. Soma Wagalatia 1 : 6-9. Inaeleza wazi wazi.
Utabisha huna laana? Utabisha wewe unayesoma majina ya wana wa MUNGU waliotoa
sadaka na kuandika majina? Utabisha wewe unayetumia mizimu? Utabisha wewe ambaye
ni freemason? Utabisha? Utamjibuje BWANA? Madhara yake, kila aliye katika
kanisa hilo, laana iko nay eye. Kwani ndiyo chanzo cha laana. Hakuna baraka,
uondoke umfuate YESU, umuombe MUNGU kama siku ya leo akuongoze pa kwenda, na
usiogope, usiweke urafiki katika mambo ya imani. Wewe angalia MUNGU amekuongoza
wapi ndio uenende. Ulikuja peke yako, utarudi peke yako, BWANA YESU asifiwe.
Wengi hawajarudi. Idadi kubwa wanaenda kwa shetani sasa, hawaendi mbinguni.
Ulitoka kwenye raha mbinguni, ukazaliwa, uje ushinde ulimwengu na urudi, YESU
alionyesha njia hiyo hiyo, lakini wewe wapi?
BWANA YESU asifiwe. Ni mapenzi ya MUNGU tumwabudu yeye peke
yake, si kuabudu wachawi, si mizimu, sio vibao vya waganga mabarabarani kila
mahali, yote hayo wanayoyafanya wamelaaniwa na MUNGU. Na wewe unayekwenda kwa
mganga umelaaniwa kama ulikuwa hujui, na unashiriki umelaaniwa. BWANA YESU
asifiwe. Wengine wanakwenda mpaka kwa waganga wanachanjwa miguu ili wapendwe,
hivi, upendo unatoka kwa waganga au unatoka kwa MUNGU? Lakini siwalaumu,
nawafundisha mpate kuelewa ukweli kwa sababu mambo yalikwisha kuharibika na
injili ikabadilishwa badilishwa, sasa imekuwa ni habari mbaya. Na mimi siionei
haya injili, ni uweza kutoka kwa MUNGU ambayo ninakueleza, wala sipindishi,
nakuambia vile vile ili usalama wako upone, ili ubadilike, ili uwe safi. BWANA
YESU ASIFIWE. Mimi sitaki hata shilingi kumi yako. Mimi ninamjua yeye
aliyenituma, nafuata injili yake “habari njema” usiulize watu wala usifanye
nini, wewe songa mbele kama alivyonituma. Anarudi, lakini sasa wengi wako
kwenye laana, wameshikiliwa, ni kudanganywa, makanisa yamekuwa kama ni
makampuni, ni masoko, ni biashara, ni pesa pesa pesa tu, kunyang’anya mali za
wana wa MUNGU na hata wewe mwana wa MUNGU mnaona kama mnamtegemea MUNGU.
Mmelaaniwa, hiyo ni habari mbaya, amenituma niwaeleze habari njema, mumrejee
yeye. Amenituma niwaeleze habari njema ya uzima wa mbinguni, anarudi, makao yako
tayari. Wale wanafunzi wa YESU waliokuwepo hapa ulimwenguni, wao walikuwa na
makao yao tayari mbinguni, na hata sasa wapo katika miji yao. Walishinda, na
wewe je, unategemea kwenda wapi? Kinachokupeleka mbinguni ni habari njema.
BWANA YESU asifiwe. Unajua watu wanaona kwamba injili au habari za neno la
MUNGU ni stori stori tu zisizotimia. Lazima litimie, neno la MUNGU halirudi
bure. Makao yapo mbinguni na kila mtu ana makao. Lakini yule aliyeshinda,
mwenye dhambi hatakwenda, aliyelaaniwa hatakwenda, ambaye amefundisha habari ya
injili ya namna nyingine hatakwenda. Kwa nini MUNGU anasema alaaniwe, kwa
sababu ile injili anayofundisha ni kwamba anafanya kazi ya shetani, sasa
yaliyompata shetani unakuwa umefungiwa na mapigo hayo hayo ya shetani,
haijalishi unasali sala ya Baba yetu, unasoma Biblia, mara neema, hiyo injili
itakurudi. Imani tuliyofundishwa ni kumwamini BWANA YESU, hakuna imani ya nikea
au imani ya mitume. Unatakiwa umwamini BWANA YESU peke yake. Hata mimi ni
mtume, unkisema imani ya mitume mimi imani gani itakusaidia wewe? Wewe mwamini YESU peke yake. BWANA YESU asifiwe.
Achana na injili ya imani za nikea, achana na injili za kuabudu watoto wa
MUNGU. Achana nao hata akina Petro, hao sio MUNGU, hao hawana nafasi, habari
njema ninayowaeleza mwamini MUNGU BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU peke yake. Wao
wana umoja. BWANA YESU asifiwe. Na ndio tumeongozwa, sasa hizi injili nyingine
au kanisa lina Biblia yenye vitabu vingine na wanavipa majina mengine, hizo
injili ni habari mbaya. Amua leo kuachana na habari mbaya. Amua leo kuachana na
tabia za kidunia, amua leo kuachana na uzinzi na uchawi na umrejee BWANA YESU.
Amua leo kuachana na masanamu na utoke huko, usiabudu, usibusu, leo uje kwa
YESU ambaye amenituma habari njema. Tazama nikueleze mfano YESU mwenyewe
angekuwepo ulimwenguni nikuulize wakati anafundisha; rudi kwenye ufahamu wako,
je, ungeabudu sanamu mbele yake? Jibu usingeabudu. Ungeabudu watoto wake
(wanafunzi wake)? Jibu usingeabudu. Kwa nini usifanye hivi hivi wakati ameamuru
kwamba msiabudu? Hii ni kumdharau. Na anayemdharau, laana inamhusu. Soma neno,
sio mimi nalaani, ninawafunulia muelewe.
BWANA YESU asifiwe. Watu wamekukuwa ni wachawi, sasa hivi
wakihubiri wanavaa hirizi kwanza, wanaangusha misukule, wanamazingaombwe hao.
Waliotumwa wanaojifanya kupeleka habari
njema hawapeleki habari njema, ni habari mbaya. Ndio mbwa mwitu. Leo utoke
katikati ya mbwa mwitu. Usikubali ukasikia mtu anatuma habari kwenye
televisheni m-pesa saidia kipindi sijui nini, hiyo ni habari mbaya. Kwa nini ni
mbaya? Rudi kwenye injili usisumbuke utafanya nini wala nini, ina maana kama ni
MUNGU amemtuma atafanya mwenyewe, kama hajamtuma ndio anakuja na habari mbaya.
Sasa habari mbaya yoyote ndio unaanza kuchangishwa pesa, kuvutwa, watu
wanajenga nyumba za watumishi wanaambiwa MUNGU ameniambia mnijengee nyumba,
mnalala njaa nyie mnanyang’anywa, habari mbaya hizo. Angalia, MUNGU amemwita,amwambie
amjengee; MUNGU atanyanyua mtu amjengee lakini sio kwa namna ya kukuambia wewe
leta, wewe fanya hivi, wewe kataa. Ndio maana mmefilisika, wengine mpaka mjenga
makanisa, mkijua kwamba mnaeneza habari njema,na mioyo yenu inajua inaeneza habari
njema lakini ni habari mbaya. Ndio maana unaumwa, umekaa hapo mpaka sasa hivi,
unaangalia, haunyanyuki, hakuna msaada. Unasema MUNGU kumbuka sadaka zangu kama
za Cornelio; wapi? Hazikutenda habari njema, zilitenda habari mbaya. Haleluya.
Hata mafundisho yote unayofundishwa sijui ya imani, sijui ya heshima, sijui ya
ndoa, lakini baba wa kiroho akishakuwa tayari ana laana, laana haitakaa iondoke
pale. Sasa wewe ninachokuambia, ni ondoka maana wako wengene wamekataa na
wamemwasi MUNGU, wako wengine wanapaa, sasa hivi ni kuruka nchi ya Zimbabwe
ndio wanakimbilia sana na Austalia. Naendelea kuvunja na kubomoa kwenye
ulimwengu wa roho makao yao yote kwa jina la YESU. BWANA YESU asifiwe. Habari
njema inakuja bure. Ni ajabu sana hata serikali inatoa kibali kwa kanisa,
ikisikia kanisa au huduma ya mungu, hawachaji kodi. Serikali yenyewe inaeneza
habari njema, lakini hawa jamaa huku wanaeneza habari mbaya. Serikali
chunguzeni hata mimi jamani. Kataeni, waulizeni hata kwenye Biblia wapi
imeandikwa jamani kwa nini mnamdhulumu MUNGU namna hii, kwa nini mnachukua pesa
za watu, kwa nini mnanyang’anya watu pesa. Kwa nini mnatumia jina la Mwnyezi
MUNGU, hata wewe uliyeko kwenye serikali MUNGU atakuuliza ulikuwa wapi wewe
watu wakatumia jina langu kunichezea chezea? Lakini kama mlikuwa hamjui
muelewe.
BWANA YESU asifiwe. Makanisa sasa hivi ni uchawi, uchafu
mtupu. Lakini mnampenda MUNGU. BWANA YESU asifiwe. Unampenda MUNGU njia ni ipi?
Wahuni wameingia huku jamani makanisani, kama vile duniani unasikia mtu fulani ni
mhuni, na watumishi wamekuwa wahuni. Ni pesa tu. Atakuja mwingine anakuambia
leta dhahabu zako zote anazichukua, anakuambia MUNGU hataki uvae, dhahabu ni
mashetani. Nikuulize swali mwana wa MUNGU. Nani kaumba dhahabu? Nani kaumba
tanzanite? Sasa MUNGU ameumba najisi hivyo? Wengine wanakatazwa hata kuvaa
dhahabu, vaeni mpendeze. Hizo sio habari njema, ni wivu. BWANA YESU asifiwe. Mmenielewa
watoto wa MUNGU? Amenituma niwaeleze mumrejee yeye, yeye sio mnyang’anyi, yeye
injili yake si ya kuwafilisi watu. Yeye injili yake si ya kuwanyang’anya watu
mali zao. Yeye injili yake anaipeleka mwenyewe, na hata watu wakimtumikia atawabariki
atawainua, hawatabki kama walivyo. BWANA YESU asifiwe. Lakini sasa hawa mbwa
mwitu, wanaitwa kwenye Biblia mbwa mwitu kwa sababu wamebadilisha neno la
MUNGU. BWANA YESU asifiwe. Watajiita majina mengi; daktari, mtume, nabii,
askofu, mchungaji, lakini YESU mwenyewe hawajui. Sasa watumishi wote walio
hivyo MUNGU hata hawajui majina yao. Sasa wewe unaenda kwa mtumishi ambaye
MUNGU hamjui unategemea nini? Lakini ni vigumu kumuelewa mtumishi mwenye MUNGU
na asiye na MUNGU mimi nakufundisha. Zaidi fuatilia masomo yangu katika redio
mbali mbali za Tanzania kila wiki na katika website www.prophethebron.org na vitabu vingi
nilivyovitoa na DVD zitakusaidia. Na zaidi ukaribie upate mafundisho ili uwe
imara usonge mbele. Mimi ninachotaka ni roho yako ipone, nataka roho yako ibadilike
umjue MUNGU, mapenzi ya MUNGU yatimie. Kila mtu aishi kwa raha, amfurahie,
taifa lifurahi. Mnaambiwa maombi, maombi, maombi yanafanyika sana lakini watu
wana laana sana hata MUNGU hawajui. Sasa maombi yamekuwa ni ya kichawi. Wachawi
wanawanga usiku. Wengine wanaenda mlimani unasikia wanaenda kwenye kuomba. Lakini
kule wanachoenda kufanya wanaenda kukutana na miungu. Hivi wewe, mtu anazini na
waumini kanisani; ana baraka gani huyo? Hivi wewe mtuanachangisha pesa, hivi
wewe, mtu anahubiri injili tofauti na MUNGU; amechanganya mahali pengine
ukweli, pengine uwongo halafu anakuambia hili ndilo neno la MUNGU. Ninakuambia hilo
sio neno la MUNGU. Ninakueleza injili kutoka mbinguni ambayo ni uwezo wake
halisi kutoka mbinguni ambayo ni uwezo wake halisi uingie ndani yako, uujue
ufalme wa MUNGU na ukubali ubadilike. Usitishwe wala usiogope; mambo
yameharibika. Sasa hivi na wachawi, wananyang’anya watu pesa, makanisa ni
mengi, miujiza ikafanyika ya shetani lakini haitatoka tena nimeibomoa nazidi
kuiharibu kwa jina la YESU KRISTO wa Nazareti. Msiogope, mrejeeni MUNGU, yeye
anawapenda njia iko wazi. BWANA YESU
asifiwe. Usiogope cheo cha mtu, wewe muangalie. Kama ana MUNGU sawa, kama hana
MUNGU ondoka. Sasa wengi wanatumia jina la MUNGU. Hivi unajua hata ng’ombe ni
mungu? Hivi unajua hata shetani ni aina ya mungu? Si ndio miungu hao? Si ndio
mabaali? Sasa hivi imekuwa kama kipindi kile cha Eliya. Mabaali walikuwa mia
nne hamsini,yaani watumishi hao, Eliya alikuwa peke yake. Wote walikuwa
wanasema tunamwomba MUNGU. Eliya akajijua akakaa pembeni, akasema ombeni nyie
na mimi niombe. Akawaambia nyie mpo wengi, ombeni mungu wenu atajibu, hakujibu.
Eliya MUNGU akajibu. Ndivyo na picha ya makanisa ya sasa hivi yalivyo. BWANA
YESU asifiwe. Hizi Biblia watu wanazibeba siku hizi ni kusanii watu, kuibia watu,
watoto wao. Sasa hivi hata imekuwa mtu akienda kwenye maombi nakusihi iwe
mwanamke au mwanamke, hakikisha kama ni mke wako nenda naye. Na mwanaume kama
anaenda kumwona mtumishi wa kike kwa appointment, sindikiza, kaa hapo. Akimwambia
toka uje siku nyingine hapana, nyie ni mwili mmoja. Mambo yameharibika, vijana
wanalia, wamama wanalia, mambo yameharibika, serikali ikaone jambo hili. Hata wakachunguze
huko makanisani, watayakuta. Najua mnajua, MUNGU azidi kuwafungua, na azidi
kuibariki serikali ya Tanzania na kuiinua juu sana, hao wanaotuchafulia nchi
yetu MUNGU ninaomba uwaondoe maana wanapofundisha vibaya tofauti na MUNGU
alivyoagiza, tayari nchi inalaaniwa, nchi haisongi mbele, BWANA YESU asifiwe.
Laana inabaki pale pale, na MUNGU yeye anaangalia haki siku zote, BWANA YESU
asifiwe. Haleluya. MUNGU ninakupenda, MUNGU ninakuinua.
Nakwenda kuwaombea wote ambao hawajaokoka, ninawasihi mrejee
habari njema aliyonituma YESU ya wokovu, na iingie ndani yako. Yamkini yawezekana
umeongozwa sala ya toba lakini aliyekuongoza hiyo sala haijaingia ndani maana
yeye mwenyewe hana habari njema ndani yake, ana habari mbaya ila amejificha. BWANA
YESU asifiwe.
Sema BWANA YESU, naomba unisamehe dhambi zangu zote,
nilizozitenda kwa kujua au kwa kutokujua. Niondolee habari mbaya, mafundisho
mabaya kwenye fahamu zangu na akili yangu. Uandike jina langu kwenye kitabu
chako cha uzima wa milele. ROHO MTAKATIFU niongoze wewe mahali pa kwenda katika
jina la YESU. Nisidanganyike tena, nisifungwe na nguvu yoyote kwa jina la YESU.
Ninawafunika kwa damu ya YESU KRISTO wa Nazareti. Ninawaombea wagonjwa,
ninawafungua. Msio na nyota narejesha. Mlio na kesi ninafuta, mabalaa, mikosi
nafuta kwa damu ya YESU KRISTO wa Nazareti, mnaologwa kwenye nyumba zenu kila
uliyewasha TV au radio, naachilia moto mchawi hatakanyaga tena, na wewe ambaye
ni mchawi naunguza uchawi wote, nakuvua mavazi ya kichawi yote kwa damu ya
YESU. Ninakuvua mapete ya kishetani nayachoma, ya ki-freemason nayachoma,
mazindiko yote ninayachoma ninayapindua ninakamata ninachoma ninatupa gerezani kwa
jina la YESU. BABA ninainua serikali ya Tanzania juu, rais, mawaziri, makatibu,
nainua madini, BABA ninaondoa mabaya yote katika nchi ya Tanzania. Ninaombea
bunge, BABA ninaombea na katiba. Ninaomba kusudi lako likatimie, la adui
hakuna. BABA, wanaochezea wabunge fahamu zao kwa kuwaloga wasiwe kitu kimoja au
kukubaliana jambo ambalo ni jema kwa ajili ya maslahi ya nchi ninaliondoa kwa
kwa damu ya YESU KRISTO wa Nazareti. BABA, kusudi lako litimie. Tanzania ni
yako, umeiumba wewe, na watu wote ni wa kwako. MUNGU, kilichoingia au kuharibu
kiondoe. Ninakuomba kwa sababu wewe unajibu. Wewe ni MUNGU na hata siku moja hujaniambia
uwongo wala husemi uwongo. Asante kwa sababu yamekuwa.
BWANA YESU asifiwe. Nitaeleza tena mabo mengine yanayoenda
kutokea Tanzania. Naendelea kurudia, Tanzania ndio Eden. Wote watakaotumia
uchawi hawatarudi mimi nakuambia hurudi, iwe uenyekiti, iwe ubunge, iwe
ukatibu, iwe urais, hupati. Ameniambia MUNGU, kama unabisha, endelea. Tuone kama
shetani ataingiza kiongozi, au MUNGU na shetani tuone ni nani zaidi. Habari
ndiy hiyo. Toka huko, okoka, uanza upya. Mpango wa kusamehewa uko pale pale,
MUNGU ni wa rehema. Nchi hii niliwaambia, ndege zitakuja nyingi, niliwaambia
mmeona sasa kiwanja cha Kilimanjaro kimenyanyuliwa, bado; hiyo nib ado. BWANA
YESU asifiwe. Jeshi la Tanzania sio lile, na nchi ya Tanzania hitakaa ivamiwe,
jambo lingine, majira kwa nchi ya Tanzania, sasa mvua zitakuwa zinanyesha kwa
wakati wake na muda wake. Ameniambia MUNGU wakati nikimuomba, akaniambia
Hebron, nimerejesha majira ya nchi ya Tanzania sasa. yalikuwa yamefungwa na
wachawi na shetani, yameshafunguliwa. Mvua zitakuja kwa wakati wake, kiangazi
kwa wakati wake, kila mahali. Sasa zinavyokuja kuna shida tena? Lakini ni hatua
kwa hatua anaponiruhusu kusema. Ninayo mwngi sana kwa ajili ya nchi ya
Tanzania, aliyoniambia, na anayafanya na ninayajua lakini ni yangu mwenyewe kwa
utukufu wake, maana hawezi kutenda neno lolote katika nchi bila kumwambia nabii wake, nami
ameniambia tayari. Haleluya. Nchi hii ni taifa kubwa na tajiri kuliko zote. Iko
mali hapa imehifadhiwa kwanza. Lakini wakati wake ukifika itakuwa. Hata mtafuteje
hamtakaa muione. Narudia, uchawi Tanzania haufanyi kazi, viongozi mnaotaka
kutumia uchawi, MUNGU hatawatumia nyie kwa sababu hawataki wachawi, kwa sababu
MUNGU hashirikiani na mchawi. Wengi wana mapete, hayo mapete walipewa na
mashetani, ni mameneja, wana vyeo mbalimbali, hiyo imetoka kwa shetana. Kwa hiyo
inakuwa ngumu MUNGU kubariki nchi. Atapitia kwa mchawi? Atamtumia huyo? Sasa mmekaza
shingo, anawaondoa, na anavyowaondoa mimi sijui, yeye mtanwona. BWANA YESU
asifiwe. Madawa ya kulevya hakuna, pesa zilizoko nje ya nchi zitarejeshwa zote
hapa. Zinavyorudishwa mimi siju, mimi nimekueleza. Utakapoyaona hayo
usishangae. Haleluya, wala msiogope. BWANA YESU asifiwe. Elimu na matibabu kwa
rais atakayepita na matibabu yatakuwa bure. Itafika mahali hii nchi hata Afrika
kusini haioni ndani. Haina muda mrefu, na YSU atawatumia watu hawa hawa. BWANA
YESU asifiwe. Ila msiogope kwa sababu MUNGU yeye ndiye atendaye kwa jina la
YESU kwa damu ya YESU. Mtu yeyote una shida yoyote karibu katika kanisa la YESU
NI BWANA NA MWOKOZI, nitakuombea, wala usije na hela. Mimi ninakueleza habari
njema. Unaumwa moyo, moyo ufunguke hapo hapo, kilema; simama uende; hiyo ndiyo
habari njema. Mambo ya kufuata fuata hea yako wizi mtupu. Sio nguvu ya YESU, ni
nguvu ya shetani inafanya kazi hapo, ndio maana unaambiwa leta. Sasa wamebadilisha
ukienda kwa mganga utaambiwa mungu anasema leta kuku, leta bata. YESU hana
hayo. Kwa baba yake kuna kila kitu. Makao yapo tayari. Rejeeni amesalitiwa
vibaya sana BWANA YESU, injili imeharibiwa vibaya sana. Sasa hivi ni makelele,
waimbaji, kila mahali ni makelele mbele za MUNGU. Watu wamemwacha MUNGU,
wamemwasi MUNGU lakini wanatumia jina la YESU kufichia maovu lakini ni mbwa
mwitu, ni wachawi, ni freemason, hawafai, ndio wanazidi kuwaangamiza wana wa
MUNGU. MUNGU mtaonana naye mnaotesa watoto wa MUNGU. Lakini wewe uliyeteswa
uliyenisikiliza hayo mateso hayatafanya kazi ndani yako tena. Na anayekuzuia
kukufunga usije ukajua ukweli, nakuombea hapo unaposikia sauti hii malaika wa injili
watakuleta na utamwona MUNGU, utakkuwa huru. MUNGU akubariki sana, tutaonana
muda mwingine, wala usiogope, mkae kwa amani, muishi kwa amani, anayekusogelea adui
yeyote mkono wa MUNGU uwe juu yake. ninawainua juu sana. Amen.