Pages

Wednesday, February 18, 2015

KILA ANAYESHIRIKI KUWA BABA WA UBATIZO AU MAMA WA UBATIZO AJIELEWE ANAMKUFURU ROHO MTAKATIFU AU ANAMTUKANA MUNGU.

Nawasalimu watu wote wa mataifa yote kwa jina la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE yeye ambaye alikuja ili tupone kupitia yeye. 
Ukisoma katika kitabu cha injili ya Mathayo 3: 16-17 “16 Naye YESU alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona ROHO WA MUNGU akishuka kama hua, akija juu yake. 17 na tazama, sauti kutoka mbinguni ikasema, huyu ni mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.”

YESU alipobatizwa kwanza alienda peke yake katika maji hakusindikizwa na mtu ili abatizwe, na alipotoka katika maji baada ya kubatizwa alilakiwa na ROHO MTAKATIFU ambaye ndiye aliyemsimamia YESU katika ubatizo. Na ndivyo inavyotakiwa unapobatizwa hakuna kusimamiwa na mtu yeyote awe ni mwanamume au mwanamke, ni ROHO MTAKATIFU peke yake na hauwezi ukamuona hata ROHO MTAKATIFU kwa sura yake, japo wengine wamewadanganya watu ROHO MTAKATIFU ana sura kama ya njiwa, huo ni uongo. MUNGU alitumia njia ya kuwajulisha wale kwa kutumia kiumbe chake aina ya njiwa kutoka mbinguni, sababu nataka mjue pia mbinguni wapo wanyama na mimi niliwaona. Ila nilishangaa san asana huku duniani watu wakabadili kuwa ROHO MTAKATIFU ndio njiwa, hilo ni somo lingine tena, ila hapa naelezea jinsi shetani kupitia roho wake mchafu ambaye anaitwa MAXWELL aliwapoteza wanadamu wakabadili biblia na mpango wa YESU katika swala la ubatizo, akawakosesha wanadamu ili wamkufuru ROHO MTAKATIFU na nafasi yake ichukuliwe na mwanadamu.

Nawaeleza mimi Nabii Hebron sababu nawapenda, msiangamie, na najua ipo adhabu iliyoandaliwa kwa watu watakaomkufuru ROHO MTAKATIFU ikiwemo moja wapo ni wanadamu wanaosimamia watu ubatizo, nikuulize swali wewe ni ROHO MTAKATIFU? Jibu, siyo. Sasa nani kakuloga ukakubali uchukue nafasi ya ROHO MTAKATIFU? Jibu ni mafundisho ya mpinga kristo na makanisa yake ili na wewe uangamie. Wengi wanayo iyo dhambi lakini hawajijui ni wenye dhambi na hata hao wanaobatiza na kwa nini mtu awe na msimamizi na yeye ni mwenye dhambi vile vile anayeshiriki kusimamia na kuhakikisha ROHO MTAKATIFU anatukanwa na shetani anainuliwa katika dunia hii.

YESU aliponituma kwa watu wote aliniambia mengi na aliniambia watumishi wamemsaliti ndio sababu wanadamu wanateseka ila sasa nenda wewe Hebron nipo na wewe. Sema kweli yangu ili watu wapone, wanafikiri wapo salama kumbe 98% ilishaangamia. Hebron ninarudi ila ni watu wachache sana ndio wapo na mimi, 98% ni ya shetani na katika 98% wengi hawajui kama wameshatekwa na shetani. 45% ya watumishi wote katika ulimwengu wote ni wachawi kwa kiwango cha juu sana karibia wangefanana na shetani ila ni wanadamu. Ni marufuku kuchukua utukufu wa ROHO MTAKATIFU enyi wamama wa ubatizo au wababa wa ubatizo mnafanyika kuwa adui wa MUNGUmnaposhiriki na mnasimama badala ya shetani na hata huo ubatizo ni wa kishetani sababu haujatoka mbinguni. Kila aliyesimamia ubatizo atubu na atakayeendelea kusimamia ajielewe anamuinua shetani na huko ndiko kumtukana MUNGU, yakupasa uelewe kuanzia sasa usishiriki kuwa baba wa ubatizo, mama, kaka, babu, mjomba na wengineo, unatengenezewa kaburi na moto wa milele ili ile siku ya mwisho uangamie na roho mchafu ambaye alifanikiwa kukutumia mwili wako ili usimamie kama wewe ndio ROHO MTAKATIFU na uingie katika orodha ya kuhukumiwa.

Sasa sema BWANA YESU naomba unisamehe nikijua au sikujua nikawa msimamizi wa ubatizo tena hata huo ni machukizo sababu haukutoka kwako, ulitokea kwa wanadamu ili watu wasiwe wana wa MUNGU, nimejua ukweli ninatubu YESU, uniongoze na mimi nikabatizwe na unitenge na mahali pa ibada kama hizi na wasimamizi wa ubatizo, wanadamu wa kumkufuru ROHO MTAKATIFU. Sitaki tena na sitashiriki tena uchafu huo wa shetani. Amen.

Ukristo wenye asili ya kuzimu ndio wenye mapando ya wanadamu na kulibadilisha neno kwa njia hiyo hata unayeshiriki kama msimamizi wa ubatizo kama mwanadamu uelewe unayo mbegu ya ukristo wa kuzimu na MUNGU  hakujui sababu hata Kristo aliyopo mbinguni na yeye hakusimamiwa na mtu. Sasa uelewe kuwa ni upofu shetani aliwapiga watu kupitia roho wa kristo wa kuzimu ili kuwateka wanadamu wawe ni wakristo ambao ni wa kuzimu pasipo kujua kwa njia hiyo. Utakapotubu ndipo utakuwa mkristo wa mbinguni na usirudi katika mapango hayo au hekalu sababu huko ni mahali pa kristo wa kuzimu na wewe ukienda tena unatekwa tena.

NABII HEBRON.