Pages

Saturday, August 30, 2014

PEPO MSALABA



Katika ulimwengu huu, tunajua kabisa asili ya msalaba ilitumiwa zamani hizo katika uyahudi na misri pale mtu anapokosea atauliwa na katika kumuua mtu kitu kilichotumika ni msalaba, sasa hata YESU WA NAZARETI alipokufa pale msalabani au kuuliwa yeye hakutenda kosa bali alisulubiwa kwa ajili yetu ili kupitia damu yake tupone na kufutiwa mashtaka na wakati YESU alipoubeba ule msalaba alifika mahali alichoka na akasaidiwa na mtu aliyeitwa Simoni. Simoni huyu alibeba kwa niaba yetu sisi ili tusije tukabeba msalaba tena, sasa kwa kipindi hiki cha nyakati za mwisho mamilioni ya watu wametekwa na shetani imani zao wameweka katika misalaba badala ya YESU peke yake, biblia watu wameshindwa kuitafsiri hata kuelewa maana yake na matokeo yake watu wanaenda kinyume, mfano 1 Wakorintho 1: 18 “ kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya MUNGU.” (nitafafanua  mstari huu ili upofu utoke watu na wamrejee MUNGU wa kweli na kuachana na imani ya pepo msalaba).

Hapa neno linamaanisha hivi kupitia mateso na kifo cha YESU pale msalabani tulifunguliwa wokovu, na siyo msalaba ambao unaotuokoa hapana, ni nguvu za MUNGU. Tazama msalaba ulimuua YESU je iweje leo tena msalaba uitwe ndio nguvu ya MUNGU? Na je jiulize je YESU kilichomfufua ni nguvu ya msalaba? Jibu siyo ni nguvu ya ufufuo kutoka kwa MUNGU. Sasa watu wengi wameacha kuzielekeza imani zao kwa YESU na kuzipeleka imani zao katika misalaba, na wengine wanathubutu kusema msalaba mtakatifu. Nawaeleza hakuna msalaba mtakatifu katika ulimwengu wote bali aliyemtakatifu ni MUNGU, ROHO na MWANA peke yake, na zaidi imeandikwa usiabudu kitu chochote kwa mfano wowote ule tofauti na MUNGU, YESU na ROHO MTAKATIFU peke yake. Je niwaulize mnapoita msalaba mtakatifu hamuoni mnamkufuru ROHO MTAKATIFU? Na je hamuoni mnaabudu sanamu, tayari mnatenda dhambi? Na zaidi hata YESU alipokufa alizikwa bila msalaba, hii ni sababu ameshaondoa laana kwetu, na zaidi hata katika makaburi ya manabii wa zamani mfano Daudi, Ibrahim, hata kina Yohana na wale wanafunzi fresh wa kwanza wenyewe hawakuzikwa na misalaba sababu unapozikwa na msalaba katika ulimwengu wa roho mapepo ya kiyahudi yanakusulubisha tena na hii ndiyo sababu YESU alipokufa hata yeye hakuwekewa msalaba na kama ungekuwa tena katika kaburi lake shetani angepata cha kushtaki kwa MUNGU kupitia msalaba uliopo juu ya kaburi lake hivyo YESU angesulubiwa tena kuzimu. Amenituma YESU niwaeleze ukweli mamilioni ya watu waliokufa sasa hivi wanasulubishwa sababu ya hilo shtaka la msalaba tena, na shetani anawacheka wanadamu sababu wanajibebesha tena wakati YESU alibeba kwa ajili yako.

Sasa katika msalaba ambayo ni nguvu ya kuua roho, kutesa, na nguvu hii ndani yake lipo pepo linaishi na kazi yake kila aubebaye, awekaye nyumbani, lile pepo linamtesa na kumfanya asiende katika ufalme wa MUNGU bali abakie katika ufalme wa mateso tena. Na zaidi ujiulize kwa nini makanisa yenye MUNGU wa kweli au ya watu waliookoka hawaweki misalaba? Hao ni wajanja, siyo alama ya mkristo, ni alama ya laana. Ina maana kama zamani hizo watu wangekuwa wanachinjwa kwa kukatwa shingo leo hii tungesema kisu kitakatifu? Hii ni kazi ya mpinga kristo. Nakusihi achana na ibada hizo, hizo ni system za mpinga kristo, YESU yupo mbinguni, hayupo katika msalaba. Na zaidi, watoto wa MUNGU katika ulimwengu huu tunaona misalaba mingi sana hata haihesabiki, swali kama ingekuwa na nguvu za MUNGU kwanza isingeoza, pili kila aliyezikwa hiyo nguvu ya msalaba ingemfufua, tatu kusingekuwa na wachawi wanaoendaga makaburini kula nyama za watu, na nne, ingekuwa ukishiriki tu shida zote zinakuacha sababu una nguvu za MUNGU. Fungukeni, nawaeleza msalaba ni machukizo makubwa sana, hata kusema msalaba mtakatifu haifai. Ndani ya msalaba huo ni roho ya pepo ndiyo inayoishi na kama ukiletewa kwako uelewe unaletewa pepo nyumbani kwako na siyo MUNGU.

TOBA:
BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu za kuabdu msalaba na kuwa kibega pasipo kuelewa. Naukataa misalaba najitenga nao uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele. Amen.

NABII HEBRON.