Pepo imani linaitwa pepo imani sababu imani hii ni yeye
ndiye muasisi, pepo huyu hutoka kuzimu katika serikali ya joka kuu. Kama vile
MUNGU mbinguni alivyo na utatu mtakatifu, hivyo hivyo na shetani anao utatu
mchafu. Nitaelezea katika kipengele cha pepo imani, pepo imani ndiye roho
mchafu ambaye ni moja kati ya nafsi tatu
za shetani. Kazi ya pepo huyu ni kuwaingizia wanadamu roho wake ili ROHO
MTAKATIFU asipate nafasi, haijalishi
mkristo anasema ana ROHO MTAKATIFU au anamtaja ROHO MTAKATIFU kimwili ila
katika ulimwengu wa roho ni pepo mchafu. Watu wamepigwa upofu na ni baada ya
imani zao kutekwa na pepo huyu hapo utashangaa mtu anasema anamuamini YESU
lakini hataki kuokoka na kumkiri, au mtu atasema yeye ni mkristo safi ;alini
anatenda ukristo mchafu kwa kuabudu sanamu, au utakuta mtu anajiita mhubiri au
mtumishi wa MUNGU lakini ni mlevi, mzinzi, mchawi, na hata ni freemason, hii
yote ni kazi ya pepo imani.
Pepo huyu wa imani yeye jinsi amuingiavyo ni kwa kupitia
kwenda kinyume na biblia, au kwa kupitia elimu inayoongezwa na wanadamu katika
kulipunguza neno la MUNGU au kuugeuza mafundisho tofauti na kuwapiga upofu watu
wajione wapo na ROHO MTAKATIFU ila kumbe wapo na pepo imani. Aliponituma YESU
WA NAZARETI hapo mwanzoni nilikuwa nashikwa na butwaa sababu nilirudisha
ufahamu katika ulimwengu wote na nikifanya uchunguzi kimwili niliogopa sana
mimi Hebron, niliona wasi wasi kama vile ilivyo wewe utakavyoona wazi wazi imani
za watu wanasema wapo na ROHO MTAKATIFU kumbe tayari ni pepo imani mfano kanisa
linabariki pombe na kusema imehalalishwa na MUNGU wakati ukija katika neno la
MUNGU linasema ole wake yeye ampaye mwenzake kilevi (hili ni onyo la ROHO MTAKATIFU
ambaye yeye yupo kulishuhudia neno la
MUNGU kwetu).
Ila roho mchafu yeye kazi yake ni kuleta na kupindua na
kujiingiza katika neno la MUNGU kama vile malaika wa nuru pasipo watu kuelewa. Pepo
imani huyu hukaa kwa watumishi ambao YESU hajawaita au waliojiita au walioasi kasha
hukaa ndani yao na kuua imani za watu kwa kuwafundisha tofauti mfano andika
sadaka majina, kuweka kikapu cha sadaka ya mchungaji na mke wake, kulazimisha
watu kutoa ahadi, kanisa kuwa na benki na kuchaji riba, wakati neno kupitia
imani ya MUNGU inasema usimchaji mtu riba, sasa kama kanisa linalo benki
ujiulize je ndiyo imani takatifu hiyo? Jibu ni imani ya pepo huyo na kazi zote
ni za mapepo na shetani na watu wanaoshiriki, wanafikiri wanaujenga ufalme wa
MUNGU kumbe wanaujenga ufalme wa shetani na majina ya watu yanawekwa katika
kitabu cha mauti ya shetani.
Mtumishi mwenye pepo imani siku zote yeye na kanisa lake ni
michango tu ili hilo kanisa liendelee na unyang’anyi zaidi, soma kitabu cha
Nabii Hebron JINSI KANISA LILIVYOTEKWA NA SHETANI, utamjua zaidi jinsi huyu
pepo imani alivyo na alivyoteka kanisa akishirikiana na mpinga kristo. Ukibatizwa
ubatizo wa maji ya kisima, ubatizo wa maji ya kikombe, ubarikio wa watu wazima,
kubatizwa kwa jina la mchungaji, na kushiriki katika kanisa ambalo lina sanamu,
au mtumishi ni mtu wa mshahara au ni mchawi au amemsaliti YESU, hapo utaipokea
hiyo imani ya pepo imani hata pasipo wewe kujua. Pia pepo imani hilo ndilo
kiongozi wa wachawi, manabii wa uongo, watumishi walioasi, wanaotafuta pesa,
biashara, waizi wa nyota, wafufua misukule au mazingaumbwe.
TUBU:
BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, uitoe imani
ya pepo ndani yangu, uiweke imani ya ROHO MTAKATIFU ndani yangu. Unitoe jina langu
katika kitabu cha mauti ya shetani, na mapango yake. Najitenga nao kiroho na
kimwili, niongoze ROHO MTAKATIFU siku zote za maisha yangu. Amen.
Nawakaribisha nchi zote na watu wote katika kanisa la YESU
NI BWANA NA MWKOZI WA MATAIFA YOTE, hili ni kanisa alilolipa jina YESU peke
yake kwa kinywa chake ikiwa ni kwa ajili ya nchi zote ili awakomboe na
awafungue na awapeleke peke yake mbinguni. Sababu aliwatuma wachache na
wamemsaliti sasa anafanya kazi peke yake na ndipo lile neno limetimia utukufu
wa kanisa la mwisho ni mkuu kuliko ule wa kwanza. Hii ina maana yeye sasa
atafanya hayo na ndivyo ilivyo.
NABII HEBRON.