Ø KUPITIA
KAPU LA SADAKA LA MAMA MCHUNGAJI
Ø KUPITIA
KAPU LA SADAKA LA BABA MCHUNGAJI
Nawasalimu kwa jina la YESU KRISTO WA NAZARETI aliye mwana
wa pekee wa MUNGU na ni mtakatifu wala siyo mnyang’anyi. Siku ya leo nawafungua
watu ufahamu sababu uwizi na unyang’anyi umekithiri katika makanisa mengi ulimwenguni
na ni uwizi wa kisayansi unaibiwa pesa zako ukijua ni sadaka kumbe umenyang’anywa
na watumishi walafi na walioibadilisha biblia.
Kwanza kabisa mchungaji hatakiwi kujitengea chombo maalum
cha sadaka yake, sababu yeye siyo MUNGU, ila anayetakiwa kutolewa sadaka ni
MUNGU peke yake. Na zaidi ukiona kanisa lina kikapu cha sadaka ya mchungaji au
mama mchungaji uelewe hao wanampinga YESU neno lake bali kwa midomo wanakiri
wanampenda YESU ila ndani ya mioyo ni wanafiki. Ni wanafiki sababu biblia
inasema mtu hutenda lile lililomjaa moyoni mwake, sasa hilo kapu la sadaka
ndilo lililomjaa moyoni mwake. YESU alisema msisumbukie mtakula nini mtavaa
nini? Ndugu msomaji akili yako ielewe kauli ya YESU. Sasa kama katika kanisa si
kuna sadaka ambayo watu humtolea MUNGU? Jibu ndiyo, sasa na hii sadaka ya
kikapu cha mama mchungaji kimetoka wapi wakati neno limekataa asisumbukie
chochote? Sasa anaposumbukia hilo kapu
la sadaka tayari amebuni mbinu kuwanyang’anya watu pesa akitumia jina la YESU.
Na zaidi watu wengi wanalia sababu waumini wanalazimishwa
kutoa pesa ya kapu la sadaka ya mama pastor na usipotoa unachukiwa. Sasa nawaeleza ukweli kama unatoa ujue
unaibiwa na wala MUNGU hatakubariki kamwe sababu biblia haijaeleza pawe na kapu
la sadaka la mchungaji. Hivi jiulize unatakiwa umtolee MUNGU sadaka au
mchungaji au mke wake? Jibu ni MUNGU tu. Sasa madhara ya kutoa pesa na ikaitwa
sadaka ya kapu la mchungaji ina maana huyu pastor na yeye amejiinua kama miungu
na shetani na yeye anatolewa sadaka kama
vile MUNGU. Muulize pastor wapi imeruhusiwa katika katiba ya MUNGU yaani biblia
kumtolea sadaka mtumishi badala ya MUNGU au wapi biblia imeruhusu sadaka iitwe au
mchungaji atolewe sadaka? Jibu hana. Haya ni machukizo makubwa sana ukitoa
sadaka hizo unakuwa umetoa kwa mashetani na zaidi sadaka hii ya kapu la pastor
au mke wake hii ni kutoza ushuru. Sadaka haipaswi mtu adaiwe wala aandikwe
jina, amelipa ngapi na hiyo nyingine ataleta lini. Ukiona kanisa lipo hivyo
ujue hilo ni kanisa la watoza ushuru na siyo YESU WA NAZARETI. Hapo ni makao ya
pepo mfilisi.
Kataa kushiriki katika sadaka hizo za unyang’anyi na ni
machukizo mbele za MUNGU. YESU amechukia sana watoto wake wanafikiri wanamtolea
yeye kumbe wananyang’anywa kwa njia hiyo sasa elewa ili upone. Ni marufuku
kutoa sadaka ya mchungaji wala mke wake. Kanisani ni mahali pa kutoa sadaka ya
fungu la kumi na shukurani tu na iwe ni siri yako. Hizo sadaka za kapu ni za
unyang’anyi na kuwafilisi na mtaendelea kufilisika mpaka utakapo acha. Zaidi
soma vitabu vya mafundisho ya Nabii Hebron na makala utaujua ukweli.
·
Maswali ya muhimu muulize huyo anayetenga kapu
la sadaka ya pastor na mkewe je yeye ni MUNGU? Jibu hana.
·
Je unakwenda kanisani kupeleka sadaka yako kwa
pastor au MUNGU? Jibu MUNGU.
·
Je kama haujatoa sadaka ya kapu ni dhambi? Jibu
ukitoa ndiyo dhambi.
NOTE:
Kila mtumishi anayefanya hivi ujue yeye ni mwizi, mnyang’anyi
na amemkufuru MUNGU na zaidi amegeuka badala ya kutenda atakavyo MUNGU amekuwa
mtoza ushuru.
NABII HEBRON.