v HUDUMA
YA UASKOFU SIYO MOJAWAPO YA HUDUMA TANO ALIZOZIANZISHA YESU.
v HUDUMA
YA CHEO CHA JINA LA ASKOFU NDIO AWE KIONGOZI WA KANISA NI MPANGO WA SHETANI
SIYO MPANGO WA YESU ALIOACHA.
v HUDUMA
YA UASKOFU NI HUDUMA YA NAMBA YA 6 KUTOKA KWA SHETANI ALITEKE.
Zaidi Soma Hapa!!!
Watu wote wa mataifa yote nawasalimu kwa
jina la YESU KRISTO WA NAZARETI aliye hai ndiye aliyelijenga kanisa linaloitwa
kwa majina ya Kristo. Amenituma niwaeleze mataifa yote mumrejee yeye na
mumrejee yeye sababu mamilioni ya watu wameshatekwa na shetani wala hawajielewi
ni njia ipi wanayoiendea kivipi endelea kusoma makala haya ya Nabii Hebron.
YESU WA NAZARETI alipokuwepo hapa ulimwenguni nawauliza swali je alilijenga
kanisa lenye huduma ngapi? Jibu ni huduma tano tu ili wakamilishe kulijenga
kanisa lake. Ukisoma Waefeso 4: 11-12 Naye aliwatoa wengine kuwa mitume na
wengine kuwa manabii na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na
waalimu kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu hata kazi ya huduma itendeke
hata mwili wa Kristo ujengwe mpaka umeona kanisa alilolijenga katika msingi wa
Manabii na Mitume, hii ina maana kuwa viongozi wa kanisa ni Mitume na Manabii,
peke yake.
Na ukisoma katika Ufunuo 22: 18-19, inasema
hivi “namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, mtu ye yote
akiyaongeza, MUNGU atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Na
mtu yeyote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, MUNGU
atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima na katika ule mji mtakatifu,
ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.”
Mpaka hapa unazidi kufunguka hata biblia
inasema maneno yote ya injili ni ya kinabii wala haisemi ya kiaskofu. Na zaidi
inasema mtu yeyote atakayeyaongeza maneno atahukumiwa, sasa angalia hapa hili
neno Askofu wewe hauoni limezidi ni la sita, na YESU alichagua huduma tano tu
katika kanisa. Je umeshawahi kujiuliza ilikuwaje mpaka mtu akaitwa Askofu,
ndiye aliongoze kanisa? Najua ulimwengu hauelewi ila amenituma niwaonyeshe njia
sahihi na atakayeifuata atapona roho yake atakaye kaza shingo yake iwe ngumu
ajijue asahau habari ya mbinguni ajijue yeye ni wa jehanamu. Na zaidi hata
ukiangalia wale wanafunzi wake ambao ndio mitume wa kwanza hawakuitwa Askofu,
na zaidi neno Askofu au shemasi, hayana tofauti hawa ni watumishi watenda kazi
ndani ya kanisa na ni watu wadogo, ni sawa na waimbaji, viongozi wa vijana, wa mama,
wa baba au wapiga bendi na hawa wote wapo chini ya Nabii, Mtume, Mchungaji,
Mwinjilisti na Mwalimu.
Sasa cha ajabu kazi alioifanya YESU na
wanafunzi wake baada ya kuuwawa na watu wa dini nyakati hizo, wakaingiliwa na
shetani na yeye akakopi hizo huduma tano akaongezea yake ya sita ambayo ni jina
la wahudumu wa chini ndiyo akawapachika watu ya kuwa badala ya kanisa kiongozi
wake awe ni Nabii na Mitume, akalipindua kwa jinsi hii na akalijenga kanisa
lake akateua mwanadamu aitwe Askofu au Bishop ndio aongoze hizo huduma tano na
hapa ndipo kanisa lilikosa mwelekeo sababu zile huduma tano ziliongozwa na
askofu, na YESU hakuteua Askofu ndio aliangalie na kuliongoza kanisa. Natumaini
unazidi kufunguka na kama YESU hajateua maaskofu katika huduma zake tano, sas
jiulize hii huduma ya sita ndiyo mapenzi yake MUNGU? Najua hamjui ila amenituma
niufichue uovu wa watu, mpone, hata wewe uliye na cheo cha Askofu nikuulize
swali je Askofu ni moja ya huduma tano? Jibu hauna, kubali umetekwa na kama
YESU hajaanzisha elewa sasa na wewe dhambi ya kuongeza neno la MUNGU imekushika
kama ulikuwa haujui leo achana nacho ni machukizo mbele za MUNGU. Mpaka sasa
unazidi kufunguka ufahamu wako.
Sasa nitakuelezea asili ya hichi cheo japo
wengine mnalipenda ila laiti mngelijua usingekubali hilo jina ndio uitwe uwe
kiongozi hii ni sababu ya kupokea mapokeo ambayo ni ya elimu ya wanadamu badala
ya MUNGU. Sasa katika ufalme wa shetani yupo jini kubwa ambaye anaitwa NAPA,
huyu ni jini ambaye yeye hutoa nguvu za kipepo kwa kila anayejiita Askofu au
yeye ni Askofu ili awe kiongozi wa kanisa na ndio maana utashangaa maaskofu
wanazo nguvu zaidi kuliko hao walioitwa kwa huduma tano, kazi yake huyu jini anapokaa
ndani ya Askofu yeye anazivuruga hizo huduma tano na kuzidhoofisha na ndiyo
sababu utaona watumishi wanaosema ukweli ni wachache na hata baada ya muda
unakuta wamezimika na watu hushangaa ule moto aliokuwa nao uko wapi tena? Jibu unalipata
hii ni sababu mtumishi anakubali kuwa chini ya Askofu huduma ya sita badala ya
huduma tano au kwa lugha nyingine huduma ya Askofu awe ndio kiongozi wa kanisa
hiyo huduma ya mpinga kristo na ni huduma ya 666.
Na pia katika ufalme wa shetani kuna jini anaitwa
makeke, jini huyu yeye kazi yake kila aliye Askofu katika ulimwengu wa roho
yeye ni mke wake huwaoa wanadamu hao katika ulimwengu wa roho na kimwili utaona
maaskofu wamevaa pete hiyo ni maana yake uelewe. Na jini Makeke nilipokuwa
nikiombana kupambana nae alisema siwaachi sababu wamesaini kuwa wao ni Askofu,
na saini yenyewe na ile wanapo saini ili kukabidhiwa kanisa muda huo huo
wanaichukua wanakaa nayo kama kiapo chako kati yako wewe na yeye. Hivyo mliokuwa
hamuelewi sasa macho yafunguke na mpone sababu wapo waliopewa UASKOFU na
wengine wanajiita wakiona ni cheo cha kumtukuza MUNGU kumbe ni cheo cha kumtukuza
shetani, na YESU WA NAZARETI hana shirika na kiongozi ambaye siyo katika zile
huduma tano. Nikuulize swali hauoni hapa hauna ujanja na umetekwa na wewe na
umempuuzia YESU japo unalitaja jina lake, hata hiyo injili siku ile ya mwisho
atakueleza sikujui sikujui, sababu moja wapo yeye hakuiamrisha hiyo huduma ili
kulijenga kanisa sasa alichofanya shetani, akachukua jina la watenda kazi
kanisani akalifanya ndiyo kiongozi mkubwa, je hiyo kazi itakuwa na YESU kweli? Wengi
mmeshtuka ila mtukuzeni YESU ambaye ndiye mwalimu wangu, aliyenituma kwa
mataifa yote niwaeleze habari njema za kweli na kuwatoa katika giza na mkatae
kuongozwa na huduma tofauti na zile tano hata na zaidi shetani akabadilisha
majina katika baadhi ya makanisa badala ya kuwaita Nabii, Mitume, Mchungaji,
Mwinjilisti, Mwalimu, utashangaa mtu ni kiongozi wa kanisa anaitwa jina tofauti
na biblia na zaidi hata kiongozi wao badala ya kuitwa Nabii au Mtume anaitwa
jina tofauti, ukiona hivyo uelewe hayo ni mapando ya mpinga kristo, YESU
hakuzileta hizo huduma zinazoitwa kwa majina tofauti.
Kama nilivyokwisha waeleza mara nyingi
jinsi alivyoituma YESU soma makala yangu utafunguka na utubu leo. Mimi Hebron katika
kanisa langu watu wanaoitwa shemasi au askofu kazi yao ni kusubiri maelezo
kutoka kwa wachungaji, kufanya usafi, kukaribisha watu na kufanya kazi ndogo
ndogo kwa jinsi mtu apendavyo. Hivi ndivyo inavyotakiwa ili YESU ainuliwe
pamoja na kazi yake alioifanya yeye kuanzisha huduma tano. Na wanadamu muone
aibu mbele za MUNGU kuongeza neno la MUNGU, madhara yake ni hukumu na hata hiyo
kazi ya kuongeza huduma tano ni dhambi kubwa.
TUBU:
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU
ZOTE HATA NIKAWA ASKOFU NA KUKUBALI, NAOMBA NISAMEHE, NILITEKWA NA SHETANI,
NIKAPOKEA ELIMU YA MAPOKEO, NIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA WA
MILELE, NAMKATAA SHETANI NA KAZI ZAKE ZOTE. AMEN.
NABII HEBRON.