Ni jambo la aibu kwa waimbaji wa miziki ya injili,
wanalitumia jina la YESU kulichafua kwa matendo yao ambayo hayaendani hata na
nyimbo wanazoimba na kumtaja YESU na walijifanya wanaeneza injili. Nawaeleza
watu wote katika ulimwengu wote, huu ni wakati wa kulitetea jina la YESU,
msikubali kabisa watu wavitende maovu yao halafu wanajihusisha na jina la YESU,
huku ni kumchafua YESU.
Katika Tanzania waimbaji wengi maarufu ni wala unga na
katika nchi mbali mbali na mabara yote. Ninachowaeleza hawa siyo watumishi wa
MUNGU katika uimbaji hawa ni watenda kazi wa shetani ambao ndani yao ipo roho
ya kuchafua jina la YESU, japo na wao wenyewe wanajijua 100% hawamtumikii YESU
kabisa. Na wenye tabia hizo nimekuta ndio waizi wa huduma za wenzao na kuwaua
kiroho waimbaji wenye wito wa kweli wa kutoka kwa MUNGU. Na ili uamini kwa macho
embu serikali zote kila nchi muwapime afya zao, majibu utayasikia. Wengi ni
wala madawa ya kulevya. Sasa waimbaji wenye matendo hayo unaposikiliza nyimbo
zao tu tayari na wewe kuna roho ya kukua roho yako usikue kiroho urudi kwenye
dhambi hata kama umeokoka.
Nyimbo hizo zina nguvu za giza, japo hauwezi kujua mpaka uwe
na macho ya rohoni. Kwa urahisi chunguza muimbaji yeyote wa nyimbo za injili,
ukikuta mkao wake ni mchafu tayari elewa hapo ni sifuri. Anatumika kumwaga roho
za kuwavuvia watu wadumae kiroho. Na shetani ndiye anayewapa hizo nyimbo.
Nyimbo hizo hazina mvuto, ni makelele matupu, na pia chunguza staili zao katika
kuimba, ukikuta kazi yao ni kukata kiuno (kama staili ya uzinzi) hiyo ni dalili
nyingine tena uelewe. Hivi kibinadamu unaweza katika kiuno mbele ya Baba yako?
Jibu siyo. Hii ni kukosa adabu, na MUNGU anakosewa sana na waimbaji hawana
heshima kwake, wanakatika kiuno?! Hii ni staili ya kuzimu wala hawamuimbii
MUNGU bali wanamtukuza shetani. Nyimbo za waimbaji wa namna hii unapokuwa nazo
na wewe unanajisika na unadhoofika roho yako, maana ni roho ya kuuwa ipo ndani
yao.
YESU hashirikiani na waimbaji wala madawa ya kulevya, wala
wauza madawa ya kulevya, walevi, wazinzi, wachawi, freemason, wafisadi.
UFUNGUKE UELEWE NA ROHO YAKO IPONE.
NABII HEBRON.