Ndugu msomaji wa makala ya Mtume Hebron, karibuni tena
katika injili ya kweli ya YESU WA NAZARETI aliye hai na sasa yupo mbinguni
anasubiri ule mwisho tu aje tena kwa mara ya pili kuwachukua wale walio wake. Ukisoma
katika kitabu cha Injili ya Yohana 14:6 “YESU akamwambia, mimi ndimi njia, na
kweli, na uzima; mtu haji kwa BABA, ila kwa njia ya mimi”. Maana ya njia ndio
mlango maana hata kama kuna njia ila mlango umefungwa ina maana hautapita.
Nitaelezea kwa ufupi na naamini utaelewa vizuri maana yeye
aliye lango la mbinguni ambaye ndiye YESU ndiye anayenifundisha na zaidi yeye
ni mwalimu wa tofauti sijawahi kuona wala kusikia anayefanana na yeye katika ulimwengu huu, na zaidi hata kuwepo
zaidi ya mwalimu kama YESU WA NAZARETI. Watu wengi katika ulimwengu huu
hawaendi katika kanisa ambalo ndilo lango la mbinguni bali wengi wanashiriki
katika makanisa ambayo ni malango ya kuzimu bila kujua na wengine wanajua. Ila
80% hawajui kuwa wanaabudu katika malango ya kuzimu na 20% wanajua kabisa
ukweli wakiwemo na watumishi, wanaojiita kwa majina ya Nabii, Mitume,
Wachungaji, Wainjilisti, Waalimu, Maaskofu na Mashemasi.
Kwa ufupi ukisoma katika nyaraka mbali mbali utaona YESU
anasema msiwachaji watu pesa yaani watumishi makanisani. Pengine leteni mizigo
yenu kwangu nami nitawapumzisha. Sasa nasema makanisa yamekuwa malango ya
kuzimu sababu yanayotendeka siyo ya YESU na kama siyo ya YESU ujue hapo tayari
YESU hayupo bali ni yesu wa uongo na mahali pa yesu wa uongo ni kuzimu na yeye ndiye
njia ya kwenda kuzimu, na ili uingie kuzimu ni lazima uyafuate yake ndio njia
yake, na njia yake ni kubadilisha Neno la MUNGU. Mfano wa njia zake za uongo-
ukifika kanisani mtumisi ili umuone lazima uchajiwe pesa. Au ukifika kanisani
badala ya wewe kuvuliwa mizigo yako uliyonayo ya kiroho, unabebeshwa mizigo na
mtumishi ya harambee, michango, na hata kuahidi kiasi cha pesa. Sasa jiulize,
je ungemkuta YESU WA KWELI, angekufanyia hayo? Jibu, siyo, sasa elewa hapo ni
lango la kuzimu. Watu wengi wamekata tamaa na kanisa sababu ya mambo
yanayofanyika kanisani kinyume na Neno la MUNGU. Nawaeleza ni bora mkae nyumbani
kuliko kwenda katika lango la kuzimu, unapoendelea kushiriki katika kanisa
ambalo linatenda tofauti na biblia, ujue wazi kuwa wewe unaendaga katika lango
la kuzimu na siyo lango la mbinguni. Katika lango la mbinguni hakuna mambo
hayo.
Nikuulize swali, je wewe unapoenda kanisani unamfuata YESU? Jibu,
ndiyo. Sasa kama umemfuata YESU kwa nini uiabudu sanamu? Je YESU ni sanamu? Jibu,
siyo. Sasa utabisha wewe haushiriki ibada ambazo ni malango ya kuzimu? Neno la
MUNGU linasema usiabudu sanamu, sasa makanisa yanaruhusu kuabudu sanamu, kuibusu,
na hata kuwaabudu wanadamu aliowaumba MUNGU. Na wengine hata kuabudu viungo
vyao, mfano mioyo yao badala ya kumwabudu MUNGU peke yake maana hata hivyo
mnavyoviabudu ni yeye kaviumba. Ni DHAMBI kubwa sana, na ni chukizo kwa MUNGU,
bali ni furaha kwa shetani watu kuabudu sanamu ni kumtukuza shetani na wote
wanaoabudu sanamu hawamtukuzi MUNGU aliye hai ila wanamtukuza shetani na
shetani amekuwa ndio mungu wao na anawapeleka kuzimu wote, ila elewa na upone
leo roho yako.
Jambo lingine lipo wazi kabisa, ili ujue makanisa mengi
hayawapeleki watu mbinguni bali yamekuwa ndio njia ya mauti ya milele. Alichokifanya
shetani alilibadilisha Neno la MUNGU na ikawa ni kinyume. Mfano ukiona au
kusikia mtumishi anakuchaji pesa ndio akupe msaada wa kiroho au kukuombea na
kukubariki ndugu msomaji hilo silo Neno La MUNGU wa kweli hata ukisoma katika
biblia halipo, na kama unashiriki na wewe umeifuata njia ya kuzimu either kwa kujua au kutokujua. Sasa
uelewe umepewa neno la shetani na hata huyo mtumishi upate picha kabisa
kilichojaa ndani ya moyo wake ni maneno ya shetani na ndiye anayemuongoza
haijalishi anataja jina la YESU. Yeye alisema watakuja Makristo wa uongo. Mtawatambuaje
angalia matendo yao na kuzichunguza roho zifanyazo kazi ndani yao, je ni za
YESU WA KWELI au wa uongo. Ukisikia mtumishi anatenda tofauti na biblia
ilivyoandikwa ujue tayari huyo mtumishi ni muongo, anasambaza maneno ya lusifa
au sumu ya kuangamiza roho za wana wa MUNGU, na zaidi yeye ndani yake ni njia
za kuzimu zimejaa na siyo njia ya mbinguni. Japo hata sema anawapeleka kuzimu
kimwili ila katika ulimwengu wa roho tayari mmeshakuwa mateka wa shetani. Hii ni
sababu ya kufuata njia za maneno ya uongo au kuipindisha Neno la MUNGU
MFANO
WA NJIA YA KUZIMU
Ø Mtumishi
akiwa ni freemason, mchawi, mwizi wa nyota za waumini na zaidi 80% ya watumishi
wote katika ulimwengu wote ni waizi wa nyota za watu na zaidi wanaiba za
waumini wao na hata katika mikutani ya injili wanaoifanya au katika vipindi vya
Television au Redio. Ukiangalia au kusikiliza tu nyota yako inaibiwa maana
wanayo majini ya kufanya kazi hiyo na utashangaa mtumishi ghafla na yeye anakuwa
na utajiri wa ghafla usiokuwa na mwanzo na umaarufu, ila hawa siyo watumishi wa
YESU wa kweli hawa ndio makristo wa uongo. Hufanya biashara, huchaji riba (kuwa
na benki), ubatizo wa maji ya kikombe, huomba pesa kwa njia ya Television hata
Redio ya kusapoti huduma zao na unapoitoa hiyo pesa tu, tayari unaibiwa
uthamani wa maisha yako na nyota yako, ni lazima wawe na partners.
Sasa YESU ukisoma Neno lake
haya yote amekataa, sasa anachokifanya shetani ni kuhakikisha sheria za MUNGU
zimevunjwa kwa kubadili yale ambayo ameyapanga MUNGU. Tazama mfano halisi, Adam
na Eva pale bustanini Edeni, MUNGU aliwapa Neno lake, msile mti ule wa katikati
ya bustani, ila shetani akamdanganya Eva wewe kula, Eva na Adam wakala na
walivyokula wakajikuta wapo uchi na kujuta. MUNGU akatamka mume utaishi kwa
jasho lako yaani ufanye kazi ngumu na mke utazaa kwa uchungu na ikawa mpaka leo
hii ndivyo ilivyo.
Watu wengi wanafikiri MUNGU hawaoni mnavyobadilisha Neno lake yeye
hunyamaza na hata mnavyobadili Neno lake, jicho lake linaona kila kitu. Tazama hata
Adam na Eva walifikiri MUNGU hawaoni, walipomaliza kula tunda, akaja MUNGU
akawauliza mmefanya nini? Hivyo ndivyo itakavyokuwa kila anayebadilisha biblia
na yeye ataulizwa ila tofauti ya nyakati zile na sasa, kipindi hiki MUNGU
ameshatoa maelekezo ya kila atakayebadilisha Neno lake (Ufunuo wa Yohana 22:
18-19) ni HUKUMU hata wanaoshiriki ni HUKUMU, toka huko utapona roho yako.
Ø Neno la
MUNGU linasema katika Wagalatia 1:6-10, Neno limebadilishwa na kama
limebadilishwa ina maana wamemfuata yeye aliyelibadilisha awapeleke huko
atakalo yeye kuzimu. Mfano; imeandikwa utoapo sadaka yako asijue mtu, tazama
leo hii watu wanaandika majina sadaka zao na wanapewa risiti na rekodi zao
zinatunzwa makanisani ambapo ndipo malango ya kuzimu. Mtumishi anayefanya hayo
muulize je hili ndilo Neno la MUNGU? Jibu hana, bali hilo ndilo neno la shetani
unashirikishwa na wewe neno la shetani umkufuru ROHO MTAKATIFU.
Ø Makanisa
yanayoruhusu pombe na hata kuzibariki (Neno linasema usimpe mwenzako kileo)
haya ni makanisa yaliyo malango ya kuzimu na yamekubaliana na maneno ya
shetani, ndiyo yamekuwa njia yao na ule mwisho shetani atawafungulia mlango
waingie kuzimu maana wamekubali kuufuata uongo wake na wamekuwa ni wake.
Ø Makanisa
au watumishi wanaofanya biashara haramu wote hao ni malango ya kuzimu, hata
kuchangisha pesa kanisani. Tazama YESU aliingia hekaluni akasema nyumba ya BABA
yangu ni nyumba ya sala tu ila nyie mmeifanya ni nyumba ya wanyang’anyi,
akawatimua, ila leo wanayarejesha. Tayari ni lango la kuzimu.
Ø Watumishi
wote waliojenga makaburi yasiyo na maiti na misalaba, huyo ni mlango wa kuzimu,
na wanatabia za KUACT wanalia na pia muelewe huwa wanafanya re-aso za mazoezi
ya sauti kabla hajaja kanisani na hujipaka mafuta ya kipepo. Sura zao hung’aa
sana na hupenda kujichubua ngozi. Hayo ni masharti na ukimjua mtumishi
anayejichubua, mtumishi huyo katika ulimwengu wa roho yeye ni shoga ameolewa na
majini. Hivyo yampasa ajirembe kama vile mwanamke kimwili anavyojiremba ili
kumfurahisha mmeo. Na wao huwafurahisha majini yaliyowaoa na huwasaidia kufanya
kazi za miujiza ya kipepo na kuiba nyota na kuedeleza malango ya kuzimu katika
pango hilo (kanisa). Na pia wanazo perfume za kipepo ambazo akijipulizia ni
harufu za majini kila utakayenusa harufu
hiyo utaipenda na utamfuata tu (perfume ina majini kivutio), na majini mengine
yanakaa katika saa anayoivaa ukiiangalia tu ameshakuteka ufahamu na hata pete
za ajabu katika mikono yao na cheni za shingoni (hivi vyote uwe makini wanaweka
vyombo vyao vya kuwanasa wana wa MUNGU na kuwapeleka kuzimu). Na ili akuteke ni
lazima akukamate ufahamu wako, ila YESU amenituma niwafungue hata fahamu zenu
muwe huru. Sasa hivi kanisa linanuka harufu mbaya mbele za MUNGU, na kama
linanuka ina maana MUNGU amelipa kisogo. Utakavyo soma ujumbe huu, watumie na
wenzako wasome, utakuwa umemfurahisha YESU WA NAZARETI, maana wengi watapona na
shetani kuaibika.
Ø Mtumishi
aliyopo kuzimu lazima awe lango la kuzimu na yeye ukiona anagawa stika ndizo
zenye nguvu ujue hiyo ni hirizi na unapokuwa nayo tu maisha yako yote ni Baraka
zako anazichukua yeye. Kwa kifupi kila mtumishi anayeuza stika halafu
anakueleza itakulinda huyo ni MCHAWI na hiyo stika ni MAJINI, na yeye ni lango
la kuzimu la kristo wa uongo.
Ø Na inawezekana
mtumishi mwanzoni alikuwa anatumika na MUNGU ila akaacha njia zake na MUNGU humwacha.
Mfano ukikuta kanisa linamuabudu Nabii, Mtume, Mchungaji kama yeye ndiye MUNGU
ujue tayari yeye ndiye lango la kuzimu. Imeandikwa utukufu wangu sishirikiani
na mtu au chochote, sasa ona hapo tayari amevunja amri ya Neno la MUNGU. Au anabatiza
kwa jina lake huyo tayari ni mpingaji wa Neno la MUNGU na siyo mtenda Neno bali
ni mvunja Neno la MUNGU. Hata kama anasema analishika neno, je huko ndiko
kulishika neno na kulitenda? Jibu, siyo. Pakishakuwa tofauti na Neno la MUNGU
hapo tayari ni lango la kuzimu, maana pangekuwa lango la mbinguni pangelitii
Neno la MUNGU na kulitende. (Kumbukumbu La Torati 6: 1-25).
Ø Makanisa
yote yanayofungisha ndoa za jinsia moja hayo yote ni malango ya kuzimu (1
Timotheo 1:8-10).
Ø Makanisa
yote yenye BAR, CLUB.
Ø Makanisa
yote yenye BENKI.
Ø Yenye masanamu
ya aina yeyote (Kumbukumbu La Torati 4: 15-23), lakini hili Neno la MUNGU
limebadilishwa na kuwekwa la shetani ambalo halipo katika kitabu cha Neno la
MUNGU.
NOTE:
Ndugu msomaji ninakupa shule fupi uelewe japo kiasi na
mengine ROHO MTAKATIFU akufundishe ili upone roho yako usidanganyike ukafikiri unaenda
katika lango la mbinguni kumbe unapelekwa au upo katika lango la kuzimu bila
kujua. Sasa upone roho yako, sasa hivi mambo yameharibika na shetani anajua
Anytime JESUS is coming back for the second time, anachokifanya ni kutengeneza
malango yake katika makanisa na kubadili Neno la MUNGU, na makanisa yote
yaliyobadili neno au kutenda tofauti na Neno la MUNGU hiyo ni picha halisi
kabisa tayari hapo siyo lango la mbinguni tena ni lango la kuzimu.
Hata kanisa ambalo linafufua misukule hilo ni lango la
kuzimu hayo ni mazingaumbwe full, ili ujue ni wachawi na siyo nguvu za YESU wa
kweli, waambie waende mochuari kuna maiti nyingi, watakimbia hao watumishi. Hiyo
ni njia rahisi kuwajua makristo wa uongo na wapo kuzimu na hapa ulimwenguni
kazi zao ni kuimarisha ufalme wa shetani na malango yake. Hivyo ukristo wa
kweli imebakia 2% katika ulimwengu wote. 98% yote ni ya uongo. Chunguza Neno la
MUNGU kanisa kwa kanisa na mtumishi kwa mtumishi, utapata jibu. Mike zao ndani
zina nyoka, akiongea au kukuhubiria anamwaga makufuru tupu. Hata kubarikia watu
wazima tayari ni kubadili Neno la MUNGU na kufanya maneno ya shetani.
Soma vitabu vya Nabii Hebron utafunguka. Elimu hii ni YESU
ndiye kanifundisha aliponiita nikamtumikie akaniambia Hebron nimesalitiwa na
watumishi sasa nenda uifanye kazi yangu. Wakimsaliti YESU ndiko kufanya ya
shetani na kujenga malango ya kuzimu ndani ya kanisa.
NABII HEBRON.