SEPTEMBER 2013
Mnamo 2013, nilipokuwa katika maombi yangu binafsi na
kuombea nchi ya Tanzania na mataifa yote yamrejee MUNGU ikiwa ina maana watu
wote kwa rangi zote, ghafla nikapelekwa sehemu nyingine akaja Mama wa YESU WA
NAZARETI akaniambia amani iwe nawe! Akajitambulisha akaniambia usiogope
mwanangu mimi ni Mama yake YESU WA NAZARETI nimekuja kukutia moyo na
kukuelekeza mambo ambayo alinieleza ambayo ni yangu peke yake. Akanishika mkono
wangu na kulia na kuutikisa kwa furaha, akaniambia endelea kuifanya kazi aliyoianzisha
mwanangu YESU, sasa hivi yeye yupo mbinguni na mimi pia nipo mbinguni. Nafurahi
sana hata tunashangilia mbinguni maana wale watumishi ambao mwanangu aliwatuma
wakaseme kweli ya MUNGU wetu wamemgeuka na kumfuata shetani wamebakia kutaja
jina la mwanangu kwa mdomo tu ila ndani ya mioyo yao hawapo nae kabisa. Na sasa
kazi ya MUNGU ilisimama kwa muda maana hakuonekana aliyemkubali 100% na sasa
endeleza kazi ya MUNGU mpaka mwisho wake na kwa watu wote wa mataifa yote
uyatende yale tu anayokueleza MUNGU na kukuongoza.
Akaniambia kipindi kile alivyokuwa na mwanae hapa duniani
yeye aliangalia kusudi la MUNGU tu na alishinda na kipindi kile ilikua kimwili
ila kwako wewe ni tofauti hautasulubiwa wala kuteswa na utapenya kila mahali
atakapo MUNGU, wewe umeteuliwa uitetee injili na kuwakomboa watu wote wa
ulimwengu. Akaniambia Hebron mimi ni binadamu tu kama wewe au wengine
walioumbwa na MUNGU, mimi nilizaliwa na kufa kama binadamu wengine tu. Na mimi
ninamuabudu MUNGU wangu kama wewe na kanisa lako mnavyomuabudu MUNGU aliye hai.
Mimi niliishi maisha matakatifu na sasa nipo mbinguni na bado naendelea kumsifu
na kumuabudu MUNGU wangu ambaye pia ndiye MUNGU unayemuabudu.
Akaniambia mwanangu Hebron nipo mbinguni nikitazama wanadamu
moyo wangu unaniuma kwa ajili ya matendo wanayoyafanya, akaniambia wameacha
kumuabudu MUNGU wananiabudu mimi mwanadamu kama wao. Waeleze ni machukizo
makubwa mbele za MUNGU na waache kuniabudu mimi mwanadamu. Mimi sitaki kabisa
niabudiwe, mimi siyo MUNGU, niliushinda ulimwengu kwa kuishi maisha matakatifu
kama nilivyomfuata mwanangu njia zake hata mimi leo nipo nae huku mbinguni na bado
namsujudia. Akasema kwa sauti ya uchungu na uliingia mpaka kwenye moyo wangu,
mpaka leo hii ndio Napata amani baada ya kuandika kwa njia ya blog japo
nilishautoa katika vipindi vya redio mbali mbali katika nchi ya Tanzania na
Television.
Akaniambia imeandikwa usimuabudu au usiabudu kitu chochote
tofauti na MUNGU peke yake. Waeleze ukweli waeleze wanapotea, watu wote
wanaoacha kumuabudu MUNGU na kunitaja mimi, mimi siyo MUNGU wala sina mbingu
yangu nipo kwa MUNGU wangu, nanachukia sana watu wanaponitaja na kuniabudu
niwasaidie, niwajibu, niwaombee. Wanajiangamiza nafsi zao na kujichochea kwenda
jehanamu.
Akaniambia Hebron wewe mwenyewe umepata neema kubwa sana ya
kufundishwa na MUNGU mwenyewe, siku zote amekueleza ni yeye peke yake tu
anayestahili kuabudiwa zaidi yake hakuna mwingine. Sasa tazama mwanangu Hebron
kwa nini wanamkufuru MUNGU na ROHO MTAKATIFU? Nilikosa jibu japo nilikua najua
hata ukimuabudu mama yake YESU ni dhambi.
a.
Akaniambia haya yafuatayo nitayasema ila hayo
mengine sikuruhusiwa kuyasema. Hebron mimi nipo mbinguni nilikufa na kuzikwa
nimeushinda ulimwengu na watu wote wafuate mfano wa YESU WA NAZARETI na uwaeleze
kweli tupu maana neno lake limebadilishwa katika uliwengu wote ili watu
wasiende mbinguni kama ilivyo hao ambao wananiabudu mimi Maria wasipoacha na
kutubu tena na kuokoka wajue hukumu tayari ipo juu yao, ila wakitubu na kuokoka
watapona, ila hao wote wanaoendelea kuniabudu mimi tayari hukumu ipo juu yao.
b.
Akaniambia mimi Maria siyo sanamu mimi ni
mwanadamu niliyoumbwa na MUNGU namtukuza MUNGU wangu, sistahili kuabudiwa wala
kutukuzwa, hapo ulimwenguni wametengeneza vitu kwa mfano wangu na vingine
vinatenda miujiza ya aina mbali mbali huo ni uongo, ni shetani wala siyo mimi. Pia
nakueleza uelewe, mimi Maria sijawahi kuwatokea
watu katika ulimwengu huu, hao wote ni waongo ni mizimu ya shetani na
mpinga kristo. Waeleze wanadamu na wamrejee MUNGU. Inasikitisha sana mimi Maria
jina langu kufanywa MUNGU au tegemeo, mimi sina kitu chochote ni kama hao watu
waliopo hapa duniani ila tofauti mimi nipo mbinguni, namuabudu MUNGU wangu.
c.
Akaniambia watu wengi wamepotezwa na shetani na
hata watumishi aliowatuma mwanangu ambao wapo hai hata sasa wamekataa kusema
ukweli, sasa Hebron usijidharau kama ulivyo, wewe siyo Yule wa zamani wewe
umebadilishwa tayari kwa safari ya mbinguni na MUNGU yupo na wewe na serikali
ya mbinguni. Waeleze ukweli, tokea nije mbinguni sijawahi kuja duniani wala
kusema na mtu kwa maono au sauti, nasubiri mpaka ule mwisho wa ulimwengu
atakapokuja YESU. Nimekujulisha uelewe na hayo mengine ni yako wewe kama wewe. Hivyo
nawaeleza ulimwengu wote hapa na kusema mama yake YESU anaonekana hapa duniani
ni uongo. Ila kinachoonekana ni mzimu wa Maria wa kuzimu siyo mama yake YESU WA
NAZARETI.
Wapo YESU wa wawili:
1.
YESU WA NAZARETI aliyekufa na kufufuka yupo
mbinguni hata na mama yake aliyemzaa.
2.
Yesu wa pili ni yesu kristu wa uongo, huyu yupo
kuzimu na anaye mama yake wa kuzimu ambaye ndiye Maria mzimu au mzuka na ndio chombo
cha mpinga kristo kuzimu, na sasa kinatawala ulimwengu.
Mama yake YESU wa kweli yeye anamheshimu MUNGU na anafuata
sheria zake kama alivyofuata za mwanae ambaye ndiye Mfalme wa Wafalme na ni
wapekee alikufa na kufufuka. Ila sasa elewa system ya mpinga kristo kuzimu
inayo yesu wa uongo na pia yupo Maria wa uongo na Maria wa uongo ndiye
anayemkufuru MUNGU aabudiwe yeye wakati yeye siyo MUNGU, tena anatengenezewa
sanamu zake na watu humtolea sadaka. Sasa nawaeleza fungukeni mambo
yameharibika.
MAMA YAKE YESU SIYO MUNGU WALA HAPASWI KUABUDIWA NA YEYE
HATAKI, ila Maria wa kuzimu yeye ni mama wa mpinga kristo na anayeendeleza ya mtoto
wake yesu wa uongo. Sasa amua leo, nakusihi usishiriki. Hiyo ni picha halisi
100% makanisa ya jinsi hiyo ni ya mpinga kristo siyo ya kuiendeleza injili ya
YESU WA NAZARETI bali ni makanisa ya kuiua injili ya Neno la MUNGU, na
kuwaingiza wanadamu wote wawe adui wa MUNGU na BWANA YESU wasiende mbinguni. Amua
leo kumjua YESU WA NAZARETI na usiabudu hilo jina tena kama unataka uiponye
nafsi yako. Kama unaabudu sanamu ujue nafsi yako ipo jela ya shetani. Mbinguni hakuna
sanamu wala MUNGU siyo sanamu, YESU, ROHO MTAKATIFU wote siyo sanamu, sanamu
haina uhai, haioni, haiongei. Ila MUNGU, YESU, ROHO MTAKATIFU wanao uhai,
wanaishi milele
SALA YA TOBA
BWANA YESU WA NAZARETI NAOMBA UNIOKOE UANDIKE JINA LANGU KWENYE
KITABU CHAKO CHA UZIMA WA MILELE MIMI NI WAKO KWANZIA SASA NA DAMU YAKO
INIFUNIKE NA NENO LAKO LIJAE NDANI YA MOYO WANGU NA LISITOKE MILELE.
AMEN.
SOMA:
Mathayo
7: 13-27
Mathayo
15: 7-9
Ufunuo
wa Yohana 22:15
Kumbukumbu
La Torati 32:39
Kutoka
20: 1- 20
NABII
HEBRON.