Ndugu
msomaji wa makala ya Nabii Hebron, Tokea YESU wa NAZARETI aniite kumtumikia
muda mwingi kila mahali nilipokuwa ninasali
katika makanisa mbalimbali nilifikiri hao watumishi ndio walionizaa
kiroho.
Na
nilipokuwa katika huduma zao, nilikuwa nashangaa kwa nini wananiogopa hata
kuniita majina ya muovu na wakati
sifanyi uovu , nilivumilia nilimuomba MUNGU
anichukue nirudi alikonitoa mbinguni maana napigwa kwa maneno mabaya na
wachungaji, kwa kunisema vibaya mara nikiwa sipo ibadani siku hiyo , ile siku nikija hata mchungaji au
kiongozi wa kanisa hilo, hukaa na mimi
karibu sana kana kwamba ananipenda sana, ili nisiweze kuelewa au kuambiwa na waumini jinsi alivyonisema.
Ila
baadaye waumini waliniambia kila kitu,
nami nilimwachia YESU tu yeye ndiye aijuaye mioyo ya wanadamu, na ilifika mahali hata mmoja wa kiongozi
mkuu mwenye cheo cha Askofu katika kanisa la mwisho nililoabudu,
kiongozi huyo nilimshangaa na yeye ananiogopa na angali nilikuwa mtoto mdogo
kiroho tofauti na sasa.
Siku
moja alikuja katika kanisa lake la mkoani kulikuwepo na ujenzi, akaniona
nikamsalimia, kumbe moyo wake ulikuwepo na wivu kwa sababu aliona huduma yangu
aliyonipa YESU, akamwambia mchungaji wake, hivi aisee kwa nini hadi leo hii
hujamfukuza huyu Hebron ?
Akamwambia
huyu Hebron ni
hatari hafai kuwepo katika kanisa langu, yule mchungaji hakukubali kunifukuza
akaniambia “ achana naye wewe mwangalie YESU tuu.”
Nikaendelea
kusali kama miezi minane hivi, na ilipofika
September 2009, siku hiyo nilikuwa katika ibada ni siku ya Jumapili wakati wa
kutoa sadaka akaja YESU mbele yangu bila mtu yeyote kumuona akaniambia leo ndio mwisho wako kuja katika kanisa hili, tena uondoke sasa hivi
nitakuongoza cha kufanya.
Niliogopa na kustuka sana, siku hiyo nilikuwepo na
mmoja kati ya waumini anaitwa Charles nilikuwa nimeketi naye karibu, na yeye baada ya kutoa sadaka alitoka, alikuwa anaenda moshi mjini na mimi nilitoka nikaenda nae na ibada ilikuwa
inaendelea.
Katika
kuongea nakumbuka nilimwambia ila sikumueleza yote kwa undani, nikamwambia,
nimesikia sauti imeniambia usirudi tena katika kanisa hili, wala
usikanyage hata mguu wako. Na ndivyo
ilikuwa mwisho wangu na itakuwa milele kama
ilivyo na nilionywa na YESU WA NAZARETI.
Baada
ya muda nikawa siendi kanisani nasali nyumbani na baadhi ya watu waliopenda
kusali na mimi na kuwaombea, maana jambo hili la kuwaombea watu na kufunguliwa
nilianza siku nyingi, na pale muumini alipokuwa akiombewa na mchungaji, akishindikana akija nikimwombea anapata jibu hapo kwa hapo.
Nilichukiwa
sana ,
nilifikiri ningetiwa moyo au waniinue huduma niliyonayo, lakini walitaka kuniua kiroho ila kwa neema
ya MUNGU, nilikuwa najua kabla ila hakuna neno kwa ujanja wakijua mimi sijui
lolote kumbe najua kila kitu.
Ikafika
muda nikawa nasema sasa YESU nitakaaje bila ya kuwa na Baba wa kiroho,
akaniambia mimi ndiye Baba yako wa kiroho, achana na hao wewe mwenyewe ni
shahidi kwa ajili ya hayo waliyokutendea, hao siyo Baba yako wa kweli wa
kiroho, hawajui uchungu kuhusu wewe akaniambia, hao nilikupitisha tu huko
ukaekae hadi wakati wangu ukifika nikutoe, hao ni Baba wa kambo wa kiroho.
Akaniambia,
kama ilivyo kibinadamu mzazi wa kambo hawezi kupenda kiukweli mtoto asiye mzaa yeye, akaniambia Hebron hivyo ndivyo
ilivyokuwa. Basi nikapata amani nikasonga mbele na YESU akaendelea kunitunza na
kunilea na kunifundisha kwa ajili ya kazi yake, mpaka ukafika wakati nikaacha
kazi August 2011. Nikabaki kuifanya kazi
yake kama ilivyo sasa. Na ilipofika July 2012,
akaniambia Hebron sasa
nataka nikuonyeshe Baba yako wa kiroho aliyekuzaa wewe na ndipo
ulipopokea huduma uliyonayo, nilishikwa na butwaa, akaniambia,
Huyu
Baba yako wa kiroho amekuwa akiniomba sana kwa muda wa miaka mitatu analia na kuomba kwangu kuhusu wewe,
japo hajakuona kimwili ila anakujua hadi sura yako, ila YESU akaniambia nilimwambia subiri nianamtengeneza ikifika wakati wake
nitakuletea na kukukabidhi, hapo bado hakuniambia ni nani?
Akaniambia
Baba yako aliyekuzaa wewe Hebron
mtumishi wangu ni MOSES KULOLA, alikuzaa katika mkutano wa injili N.M.C 1999, ndipo ulipopokea huduma hiyo na mimi YESU nilikuwepo siku hiyo
nikahakikisha umeipokea huduma ambayo MIMI na BABA yangu MUNGU
tulipanga hivyo ila tulikuficha kama vile MUSA alivyo hifadhiwa kwa
Farao na ilipo fika wakati akatoka huko, akaniambia na wewe ndivyo ilivyo, na
wewe ni MUSA wa sasa.
Ikafika
mwishoni mwa October 2012, akaniambia nenda ukamwone Baba yako wa kiroho tayari sasa anakusubiria kwa hamu na furaha, basi
nikachukua hatua, nikamtafuta nikampata mtoto wake anayeitwa kwa jina Willy, akanisaidia
kufanya mawasiliano na alipomwambia Baba
yake ambaye kwa sasa ni marehemu yupo mbinguni amepumzika, akamwambia mwambie
aje; nikatii .
Alikuwepo
Dar es Salaam nyumbani kwa Willy. Nikafika
nikaonana naye nikamwelezea alivyoniambia YESU, kuwa yeye ndiye Baba
yangu wa kiroho, na mengine ambayo ni yangu na
MUNGU tuu, akaniambia “umesema
kweli” wewe ndiye niliomba muda mrefu , akaniambia ninakujua tena mbele ya mtoto wake Willy, basi akanibariki kama alivyoelekezwa na YESU
na akaniambia uende RWANDA sikupata mtu wa kumtuma kwenda huko watoto wa MUNGU
kule wanapotoshwa hawajui tofauti ya
shetani na MUNGU, wanaangamia.
Nikamwambia pia YESU alishaniagiza baada ya Tanzania niende Rwanda . Siku hiyo ilikuwa tarehe
9.11.2012. Na YESU akasema na yeye
akamwambia mwanangu makao yako yapo tayari ila muda na siku ikifika mimi YESU
nitakuja na BABA yangu kukuchukuwa, akamwambia tazama hata uliokuwepo nao
katika injili wameniacha na umebakia wewe mwenyewe na akasema katika ulimwengu
huu mumebakia watumishi wakubwa watatu tuu ambao hamjaniacha na katika Bara la
Afrika umebakia wewe peke yako tu,
wengine wote wamenisaliti wamejiingiza kwenye freemason, wachawi, na kuirudia
dunia japo wanalitumia jina langu, na mimi YESU nimekaa ole wao.
Akamwambia
nimekuletea yule uliyeniomba kwa muda wa miaka mitatu na nikakuahidi, ndiyo Hebron mtoto wako,
mbariki na umwongoze. YESU akaondoka, Mzee Moses akaniambia kwa mara ya pili
tena piga magoti akanibariki tena na mke wangu na watumishi niliokwenda nao.
Toka
siku hiyo ikawa ni furaha kwangu maana nililia kama
sina Baba wa kiroho. Lakini haijalishi kwa sasa hatupo naye, ninacho waambia
ukweli halisi msilie, mimi nililia nilipopata habari ya kifo chake, akaja YESU
akaniambia usilie Baba yako yupo katika mkono wa kuume wa MUNGU, yeye ameshinda
ulimwengu na yupo amestarehe anamtukuza MUNGU na kusifu, akaniambia kibinadamu
inauma ila usiogope hii ni kwa sababu ulimpenda sana, akaniambia simamia kazi
yangu na kusudi kama ulivyoelezwa na Baba yangu MUNGU na mimi YESU, akaniambia
nilijua muda wake umeisha hapa
duniani ndiyo maana nilikuagiza
uende na afanye kama nilivyomuelekeza
kuhusu wewe.
Ndugu
msomaji wa makala ya Nabii Hebron mpaka sasa umepata picha kwa ufupi jinsi
nilivyompata Baba yangu aliyenizaa kiroho.
Yeye
alinipenda,aliniombea sana na kunifundisha mengi, na wala hakunionea wivu kwa
ajili ya huduma aliyoiona ndani yangu ila alinikuza mpaka alipoondoka na sasa nimebaki
na YESU peke yake tu, na
MUNGU aliyeumba ulimwengu huu.
Najua
kuna watu wengi wanampenda MUNGU ila wanagandamizwa na Baba zao wa kiroho,
ukiona unagandamizwa ili usikue katika
huduma uliyonayo tambua huyo uliyenaye siyo aliyekuzaa kiroho, omba
MUNGU, atakuonyesha baba yako.
Angalia
mapito niliyoyapita na ukiinuliwa na
MUNGU utashangaa wanaanza kusema ni
mtoto wake wa kiroho. Usikubali hao ni wanafiki, songa mbele. Mbona kabla
hujainuliwa walikukataa na kukulaani? Akili kichwani.
Malaika
Gabriel aliniambia siku moja MUNGU
alisema na baadhi ya watumishi niliokuwa nikisali nao huko, ila mmoja
akayahifadhi, waliambiwa jnsi huduma niliyopewa ni kwa ajili ya ulimwengu wote
na hakuna atakayeimaliza kazi hii ni Hebron tu ndiye aliyechaguliwa, wao
wakaingiwa na wivu, na wakakufanyia mabaya kwa ajili ya kusudi la MUNGU.
Neno
la MUNGU lazima litimie tu na Hebron
lazima itakuwa, MUNGU hasemi uongo.
NABII
HEBRON .