Ndugu
msomaji wa makala ya mtume na nabii Hebron, siku ya leo napenda kukufundisha
tena kuhusu ndoa zinazofungwa na makanisa jinsi zilivyotekwa na Yezebeli au
Malkia wa kuzimu ambaye ndiye mama wa makahaba wote katika ulimwengu huu, au
kwa maana nyingine ili uelewe zaidi, nitakupatia mfano katika ulimwengu huu,
unajua nini maana ya kahaba na mpaka mtu kufikia kuitwa kahaba.?
(Mfanya
uzinzi wa kujiuza mwili wake, au kuvaa nguo na kuonyesha maumbile yako badala
ya kuyasitiri.)
Sasa
anayesababisha wanadamu wawe hivyo ni
huyu malkia wa kuzimu au kwa jina jingine anaitwa mama wa makahaba.
Anachokifanya
anamwaga roho yake kwa wanawake ili wamkosee MUNGU na wawe wafauasi wake hata
pasipo kujua na wengine wanajijua.
Ukiona
mtu mwanamke anavaa mavazi ya kuonyesha uchi wake mfano mapaja, tumbo(kitovu),
matiti yake anavaa (transparent clothes) Hilo utambue moja kwa moja ndani yake ipo roho ya huyo mama wa makahaba aliyepo kuzimu na unapovaa hivyo
tu tayari na wewe unaunganishwa katika mtandao wa makahaba wa kipepo.
Utakuta
mwingine hazini kimwili ila anaolewa na majini, yanakuwa ndiyo mume wake na
watu waliolewa na majini, huota ndoto za zinaa sana na pia huota wananyonyesha watoto na hawawaoni ,
ukiona hivyo ujijue umeshikiliwa na malkia wa kuzimu (YESEBELI) soma Ufunuo
2:20-24 ,
Lakini
nina neno juu yako ya kwamba wamridhia yule mwanamke YESABELI, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na
kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa
sanamu.
Nami
nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake. Tazama nitamtupa juu
ya kitanda na hao wanaozini pamoja nae, wapate dhiki kubwa wasipotubia
matendo yake.
Nami
nitawauwa watoto wake na makanisa yote
yatajua ya kuwa mimi ndiye nichunguzaye
viuno na mioyo , nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo
yake. Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wowote wasiyo na
mafundisho hayo wasiyo zijua fumbo za shetani
kama vile wasemavyo, sitaweka juu yenu
mzigo mwingine.
Na
ukisoma tena 2Wafalme 9:22, ikiwa Yoramu alipo muona Yehu, akasema je ni amani
Yehu ? Yehu akajibu ni amani
gani, maadamu uzinzi wa mama yako Yesebeli na uchawi wake ni mwingi? Hesabu 25:1 Basi Israeli akakaa Shitimu kisha watu wakaanza
kuzini pamoja na wanawake wa Moabu.
Katika
vitabu nilivyo vinakili hapa na mistari
yake inaonyesha waziwazi ya kuwa
Yesebeli hutumika kwa wanawake ili kuwaangusha wanawake /
watumishi katika uzinzi hiyo ndiyo kazi
yake kubwa.
Ila
nitaelezea kwa kifupi hasa katika ponti;
Ndoa zanazofungwa makanisani na
makanisa kupitisha hayo mavazi ya ajabu
na aibu huko ndiko watumishi kuzini na huyo Yesabeli (kitendo cha kuruhusu hayo
mavazi ya uchi tayari hata aliyevaa hilo gauni , tayari ameshakuwa mama wa kahaba katika ulimwengu wa roho na
kama ameshakuwa kahaba katika ulimwengu wa roho, hata ndoa hiyo MUNGU haiungani na yeye sababu tayari yale mavazi
aliyoyavaa ya kipepo yasiyo na heshima na watumishi hawasemi lolote mnaendelea
kuangamia.
Hii
ni sababu wameshazini na Yesebeli na amewashika fahamu zao wakapigwa upofu na
kuruhusu binti bibi harusi uvae mavazi ya uchi, mbele ya BABA yako MUNGU.
Nitaelezea
mavazi ya bibi harusi ambayo ni ya mitindo iliyo dizainiwa na malkia huyu Yesebeli. Shela au gauni ambalo bibi
harusi huvaa huku mabega yake na mgongo
vikiwa havijafunikwa , pia matiti yake yanaonekana kifua, gauni la transparent,
na nyingine yeyote ambayo siyo ya heshima inayoonyesha maumbile ya bibi harusi
hizo zote ni za kahaba na bibi harusi anapozivaa hizo ina maana na yeye amekuwa mama wa makahaba, kutokana na
mavazi yasiyo ya heshima, japo wengine
wanasema ndiyo mtindo wa kisasa siku hizi.
Mmepotea
! hayo ni mavazi ya uzinzi mtupu. Cha ajabu utakuta binti anakuja kanisani
manyonyo yapo nje na mgongo upo wazi, eti anaenda apewe baraka za mchungaji na
anapokwenda ni lazima mchungaji amwangalie usoni pia hata kifuani , macho huwa
yanaangalia mahali pengi, hiyo tayari umemzinisha hata mtumishi kwa
kukuchungulia matiti, na zaidi wengine
wanaovaa mavazi ya kikahaba unakuta wakati wa kusaini cheti cha ndoa mara
nyingine titi linaweza likawa size kubwa
anapoinama titi linatoka nje ya nguo
inakuwa ni aibu kwa mtumishi huyo na pia kuichafua madhabahu na
kuilaani.
Na
ndiyo maana Neno linasema, Israeli amezini na Yesebeli. Ina kuwa siyo ndoa tena hiyo ni laana tupu. Na siyo kosa la bibi harusi ni kwa sababu,
makanisa hayasemi ukweli na kuwafundisha
kipi kizuri na kipi ni kibaya.
Hivi
ndivyo mama wa makahaba alivyoziteka ndoa za wakristo kupitia mavazi. Na mwanamke huyo
katika maisha yake hiyo roho ya
ukahaba na uzinzi itamfuatilia kwa
sababu alikubali kuyavaa mavazi yake na akavalishwa hiyo roho bila kujua.
Shetani
ametumia ujanja sana
. na zaidi nitaelezea kidogo ili mabinti, na wanawake wapone kuhusu nguo za
ndani zile zinazoitwa “Bikini” Zile ni
nguo ambazo amezibuni Yesebeli ili kuharibu nguvu za kike za wanawake na
wanawake wapende kukutana kimwili
kinyume na maumbile. (yaani shoga), msivae nguo hizo, na madhara yake
mnao zivaa nguo hizo huota ndoto za zinaa sana na hawadumu katika ndoa na pia
ni shida kupata mchumba kwa sababu
anakuwa tayari ameolewa na majini na
anapokuja mchumba mwanadamu yanamvuruga akili au kuwafarakanisha
mnaachana, na hata wanazuia usizae au kushika mimba.
NOTE:
Natumaini
mmefunguka kataeni mavazi ya Yezabeli, na kama unapasali watumishi
hawawaambii ukweli ina maana tayari na
wao wameshazini na Yesebeli au Yesebeli ndio anayezifungisha ndoa hizo na siyo
YESU wa NAZARETI.
Siyo
heshima kuvaa mavazi ya uchi mbele za MUNGU hata kwa wazazi wako waliokuzaa
kimwili, umeshavunja amri ya MUNGU.
Mavazi ya uchi ya harusi ile kuyavaa tu,
kanisani na watumishi kuruhusu ina maana hilo
silo kanisa tena ni NIGHT CLUB, hayo ni ukahaba, na Yesebeli ndipo mahali pake.
Je
nikuulize swali , je kanisa limekuwa ndiyo night club? Jibu siyo ila watumishi
wanaoruhusu mavazi hayo kinyume na mpango wa MUNGU, hao ni wanachama wa Night
club, au wamekamatwa na Yesebeli na kupendelea kuona uovu ukitendeka kanisani.
(Marko 11:15-18) YESU alisema nyumba ya BABA yangu ni nyumba ya sala tu, ikiwa
inamaana ni mahali pa heshima na patakatifu.
Mavazi
ya night club ndilo kanisa linaruhusu watu waje nazo makanisani kufungia ndoa.
Je, hilo ni
kanisa la YESU wa NAZARETI? Au linakuwa pango la unyang’anyi?
Ni
pango kama ilivyo mapango ya night club
yalivyo.
Na
ndoa hizo zimeshikiliwa na Yesebeli zote na hazipo katika kitabu cha ndoa
mbinguni.
Inamaana
ni kazi bure mnafanya na mtaendelea pia, mnakuwa mama wa makahaba.
Uzinzi
upo juu yako. Uamue upone au uangamize ndoa yako.
Nawatumishi
wanaoruhusu mavazi hayo hao ni viongozi vipofu.
NABII HEBRON