Ndoa
zote za kufunga na mimba kwa wakristo, hizo sizo ndoa za mpango wa MUNGU, hizo
ni ndoa za uzinzi au mshahara wa dhambi , au matunda ya shetani halafu
mnamshirikisha MUNGU na kusema eti ameunganisha yeye. Huo ni uongo mtupu hata
nyie mnaofungiwa nawaeleza hata ripoti za majina ya ndoa zenu hazipo katika
kitabu cha ndoa mbinguni.
Na
laumu siyo ya waumini, mngeambiwa ukweli
msingezini, ila kwa sababu ya maadili mabaya
ya makanisa ya sasa yaliyoacha njia ya MUNGU, na pia hofu ya MUNGU imeondoka kwao wamekuwa
na roho ya kuasi na kuzibariki dhambi makanisani, kwa waumini mkawa na mimba.
Hivi
inaingia akilini kweli,? eti MUNGU atabariki kazi za shetani? Jibu ni haiingii
akilini, na kama haiingii akilini je ni kwa nini
sasa watumishi wanaruhusu kufungisha ndoa hizo? Jibu, hata wao ndani ya mioyo yao hofu ya MUNGU haipo
tena ni roho ya kuasi kabisa.
Tena
wanamtaja ROHO MTAKATIFU na BABA na MWANA katika kuubariki uzinzi, ukweli ni huu, haijalishi harusi
imefungwa kwa gharama gani, uwe umebeba mimba kabla ya ndoa(harusi) hilo ni
tunda la dhambi na mtoto atakuwa na hiyo roho ya dhambi ya uzinzi ambapo alipatikana katika njia
hiyo.
Apandacho
mtu ndicho avunacho. Na hata
wanaofungisha ndoa hizo tena binti anaonekana tumbo kubwa anaingia
kanisani bila aibu na eti YESU
anaunganisha huo uzinzi?
Ndoa
hizo hazija unganishwa na YESU WA NAZARETI . wala hazina baraka za MUNGU. Hii inamuhusu binti
aliyebeba mimba , na kijana aliyemzinisha
na pia dhambi hii inamuhusu mtumishi aliyeruhusu kumfungisha au
kuhalalisha dhambi hiyo na pia dhambi hiyo ya uzinzi inalikamata kanisa lote.
Maana
alivyo kuhani na afanyavyo ndivyo na kanisa lake. Je, ndivyo MUNGU awaagiza
hivi? Soma amri 10 za MUNGU ! je,
haijavunjwa (Usizini) halafu eti huyo huyo MUNGU awe kigeu geu
aukubali uchafu huo na aubariki? Je , ni
kweli ? msidanganyike, acheni uzinzi
tiini mpango wa MUNGU.
NOTE:
NDOA ZOTE ZA JINSI HII HAZIPO KATIKA
KATIKA KITABU CHA NDOA ALIZOZIFUNGA MUNGU. Na hajazifunga yeye na hazina
baraka za MUNGU, wala mkono wake haupo juu yake, na ndoa zote zinazofungwa kwa
agano la shida au laana na raha, MUNGU halaani, ndoa anazozifungisha baali
anazibariki, na wewe kwa kuwa umekiri shida na raha, shida itakufuata milele,
shida ni roho na hukua mahali ilipo kubaliwa
kama watu wanavyozikiri katika makanisa kinyume na mpango wa MUNGU.
UFUNUO 22:18 -20
Tazama
Rebeca alibarikiwa tuu na hakulaaniwa Mwanzo
24: 56-61.
NABII HEBRON