MWANZO WA ANGUKO LA WAKRISTO KWA ULIMWENGU WOTE NI UBATIZO
WA WATOTO WADOGO
UFUNUO 13: 16,18
UFUNUO 19: 20
UFUNUO 13: 16, 18. Naye
atawafanya wote wadogo kwa wakubwa na matajiri kwa maskini na walio huru kwa
watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume au katika vipaji vya nyuso zao,
hapa ndipo penye hekima, yeye aliye na akili na aihesabu ya mnyama huyo. Maana
ni hesabu ya kibinadamu na hesabu yake ni mia sita sitini na sita.
UFUNUO 19: 20 Yule mnyama
akakamatwa na yule Nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara
mbele yake ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya
huyo mnyama nao walioisujudia sanamu yake, hao wawili wakatupwa wangali hai
katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti.
Ndugu msomaji wa blog hii ya Nabii Hebron, mwanadamu uliyeumbwa na MUNGU kwa kila jinsi
ya rangi zake tofauti apendavyo yeye. Ujumbe huu ni kwa ajili ya wanadamu wote,
ujumbe huu nitakaoelezea jinsi wakristo walivyoangukia kwa idadi kubwa katika
ulimwengu huu kwa kupigwa chapa ya Namba 666 bila kujua na kazi hiyo ikifanywa
na watumishi wa uongo ( Nabii wa uongo) Ni mtumishi afundishaye mafundisho ya
MUNGU asiyejulikana ikiwa ina maana hayapo katika Biblia, tofauti na Biblia ina
maana yanatoka kwa MUNGU asiyejulikana yaani ( Baali).
Jinsi usomavyo wewe ujumbe huu ,
ndivyo na mimi Hebron nilivyoelezwa na YESU wa Nazareti uso kwa uso kwa hiyo
kazi kwako usije ukalia siku ile ya mwisho au endapo utakufa kabla ya
kutengeneza na yeye muda huu .
Anguko kwa wafuasi wanaompenda
YESU lilianza kwa jinsi hii, kwa kuanza kubatiza watoto wadogo , badala ya mtu
mzima na akili zake akubali mwenyewe abatizwe kwa maji mengi tena mtoni kijito
cha utakaso wala siyo kisimani.
Nitaelezea kwa ufupi lakini
utapata picha. Mtoto mdogo anatoka kwa MUNGU, ndipo anakuja ulimwenguni na
akizaliwa na anapokuja ulimwenguni anakuwa anao malaika kutoka kwa MUNGU ambao
humlinda na kuhakikisha yale yote yaliyo kusudiwa na MUNGU kwa kiumbe hicho yani mtoto yanatimia katika
ulimwengu huu na ule mwisho wake mtoto huyo anarudi kule alipotokea yani
mbinguni.
Mfano halisi ni YESU WA NAZARETI
alitoka mbinguni na akarudi mbinguni na hata Herode alipotaka kumuua wale
malaika waliokuwa na YESU walimlinda na kuwaongoza wazazi wake, pia hata mama jusi walionywa wasirudishe ripoti
kwa Herode.
Huu ni mfano tu nimekupatia uzidi
kuelewa na ufunguke ufahamu wako, hakika utaona jinsi watu walivyopotea na
wanavyoendelea kupotea na kazi hii ya kuwaharibu wanadamu inafanywa na Nabii wa uongo (
mtumishi au watumishi wanaofundisha tofauti na Biblia na kuibadili na
kukushirikisha mapokeo yasiyojulikana yalipotokea hayo ndiyo ya MUNGU
asiyejulikana yaani ( Baali).
Nitaelezea kinachofanyika kwa
mtoto mdogo anapopelekwa kanisani na kumwagiwa yale maji, kinachofanyika
kupitia yale maji na anayefanya hayo ni mtumishi wa uongo kwa sababu Biblia
haijaruhusu mtoto mdogo abatizwe.
Tafuta kwanza kitabu cha mwanzo
mpaka mwisho. Jibu hakuna, tunatakiwa
tumfuate YESU yeye ambaye ndiye njia ya uzima na kweli kiimani na kimatendo, na
hakuna pa kumlaumu YESU yeye alionyesha njia na mfano akasema afuatwe yeye ndio
kweli katika mambo yote sasa imebadilika, imekuwa kinyume ila imeandikwa Neno
lake lazima litimie na halitarudi bure na imetimia kwa kupigwa chapa usoni
ya namba 666. Hii namba 666 ni
roho, usifikiri utaandikwa usoni kimwili, maana hakuna apendaye aangamie ila
mambo haya hutendeka kwa roho, na hii roho ni ya shetani, ambayo huwekewa mtoto
mdogo akiwa anabatizwa kama tunavyo au
tulivyokuta katika makanisa unaitwa ubatizo na kumbe siyo ubatizo, maana ya
ubatizo ni kuzamishwa, hii yenyewe kibinadamu pamoja na akili yako ukiangalia
maana yake utajua ni uongo mtupu. Ila
imebadilishwa kwa kufungwa fahamu za wanadamu ikaitwa ubatizo badala ya chapa
666 ya mpinga Kristo.
Ukisoma katika Ufunuo 13:16, 18
na Ufunuo 19: 20. Utaelewa vizuri. Sasa kinachofanyika mtoto mdogo akimwagiwa
yale maji ndani yake yanakuwa na hiyo roho ya shetani kwa sababu siyo mpango wa
MUNGU anayejulikana watoto wadogo wabatizwe, ila watoto wadogo inatakiwa
wawekwe wakfu tu yani kubarikiwa kama ilivyofanyika kwa YESU WA NAZARETI akiwa na siku nane. Mtoto huyo anapobatizwa
hayo maji kama nilivyokwisha kukueleza
pale tu anapowekewa kichwani, wale malaika kutoka kwa MUNGU waliokabidhiwa
mtoto huyo,huondoka na kumwacha, maana yale maji yanakuwa na roho ya shetani na mtoto huyo huwekwa
alama ya namba 666 bila ya watu kujua, na afanyaye hayo imeandikwa katika ufunuo 19 :20 ya kuwa ni Nabii wa uongo ndiye atakayefanya
hayo akishirikiana na mnyama ambaye ndie shetani, na haya hufanyika katika roho
siyo mwili ndio maana Neno la MUNGU linasema vita vyetu siyo katika mwili bali
ni katika roho na ndivyo pia imeandikwa usiziamini kila roho bali zichunguzeni
kama kweli zatoka kwangu, roho kutoka kwa MUNGU haziwezi kumpinga MUNGU ila ambazo
zimetokea kwa Mungu asiyejulikana hizo ndizo za shetani, mfano kuabudu sanamu,
ubatizo wa watoto wadogo.
Ndugu msomaji haya ninayokuelezea
mimi Hebron siyo maneno yangu ni maneno aliyonieleza YESU na mimi nakufundisha
ili watu wapone wasiangamie ila ni kwa wale tu watakao tii ila watakao kaza
shingo zao kuwa ngumu hukumu ipo tayari juu yako, na wote wanaobatiza watoto
wadogo ubatizo tena ambao haupo katika Biblia yaani MUNGU anayejulikana na
kuleta ubatizo ambao haupo katika Biblia yaani haujulikani ulipotokea, ( Ndiyo
MUNGU asiyejulikana) na wewe ukafanyika uunganishwe kwa Mungu asiyejulikana na ile
siku ya mwisho utapelekwa huko huko pasipo julikana.
Wote tunajua mtoto mdogo anaitwa
malaika wa MUNGU, hii ni sababu hajui kutenda dhambi na anakuwa yupo na malaika
kutoka kwa MUNGU na ndiyo maana humlinda, na zaidi mtoto mdogo hata mchawi akiwanga ndani ya nyumba huanza kulia ila
watu hawaelewi, anaona adui, hii yote ni sababu bado malaika wa kumlinda wapo
na yeye ila mara anapowekewa yale maji
tu kanisani malaika humuacha, maana anakuwa siyo mali ya MUNGU tena
amekabidhiwa shetani, na jinsi hii ilifichika sana na watu hawakujua ila YESU
amenifunulia siri hii na zaidi soma kitabu changu cha UBATIZO WA KWELI KWA
ULIMWENGU WOTE. Utaelewa zaidi.
MARKO 10: 42
NOTE:
- Kuanzia sasa utambue unapompeleka mtoto mdogo abatizwe kwa maji yale ujue mtoto wako anaenda kuwafukuza malaika aliotoka nao kwa MUNGU, na shetani kummiliki na kumpiga chapa 666.
- Usidanganyike eti akifa akiwa mdogo hataenda mbinguni, kabla hajabatizwa huo ubatizo wa maji ya kichwani. Jambo la kwanza atakuwa bado yupo na wale malaika aliotoka nao mbinguni watamrudisha alipotokea na hatapotea. Ila ubatizo huo wa Mungu asiyejulikana na wewe ukifa utaenda huko kwa Mungu asiyejulikana. Amua leo umtake uende kwa Mungu anayejulikana? Au asiyejulikana uamuzi unao mwenyewe ndani ya moyo wako, maana kila mtu atasimama peke yake kujitetea siku ile ya mwisho.
- Madhara yake kuwabatiza watoto wadogo ndiyo maana wakristo wanakuwa
waovu hata hawafananishwi na jina la
Kristo ambaye ni Mtakatifu, inabakia jina
tu bila uthamani wa nguvu za YESU ndani
ya mkristo.Na pia hofu ya MUNGU
inakuwa haipo ndani yao na matendo maovu huwa ni jambo la kawaida
kwao.
Sasa
ninayokueleza uelewe wala mimi siogopi kusema kweli na hakuna atakaye jaribu
kunizuia kusema kweli ya YESU wa Nazareti na kama yupo ajaribu, atakutana na
MUNGU mwenyewe asifikiri anapigana na Hebron ni MUNGU hakuna atakaye weza
kumpinga wala yeye hashindwi na lolote
ni MUNGU mwenye uwezo wote, yeye ndiye aliyeagiza watoto wadogo wabarikiwe tu!
Sasa kwa nini watumishi wa uongo wanawabatiza watoto wadogo? Wanatumika
kuwapiga watu namba 666.Tambua mtu yeyote katika ulimwengu huu aliyebatizwa
ubatizo wa kichwani huyo tayari anayo alama ya namba 666 na tayari hao wanadamu
wamepewa shetani bila ya wanadamu hao kujua. Sasa mfunguke watu wote wa
ulimwengu wote YESU wa Nazareti ameniambia msikubali tena huo uchafu hilo ni kaburi au
jehanamu, ile siku akija YESU
atawaangalia wote wenye alama yake tu ndio atakao wachukua je nikuulize swali?
Sasa kama unayo alama ya 666 atakuchukua? Jibu hapana.
- ONYO:
1. Ole wao wawawekeao wanadamu aliowaumba
MUNGU namba 666. hukumu
ipo tayari juu yao ,
2. Hao wanaobatiza ubatizo watoto wadogo
ubatizo huo YESU kawaambia
haujatokea kwa BABA yake ambaye
ndiye MUNGU anayejulikana. Ila umetoka
kwa MUNGU asiyejulikana wala kujibu
( Mungu Baali) na wote mnaoshiriki
ibada hizo hamwongozwi na MUNGU
aliye hai, mnaongozwa na Mungu asiyejibu
na asiye julikana yaani ( Baali)
na nyie kufanyika watoto wa Baali bila
kujua,
badala ya kufanyika wana wa MUNGU
anayejulikana.
- Shetani aliifunga hii siri 98% katika ulimwengu wote na makanisa yakawa siyo
makanisa tena ni pango la unyang’anyi
(Baali ndiye kiongozi ). Sasa YESU
amenituma niufichue uovu wote ili watu
wapone, maana baadhi ya watumishi
aliniambia aliwatuma wakakataa kusema na yeye amewakataa
tayari. Ila
NOTE: Usikubali
kubatizwa ubatizo usiotoka kwa MUNGU anaye julikana, hata hao wanaobatiza
ubatizo huo hawajulikani na YESU na siyo wanafunzi wake 100 %. Wangekuwa
wanafunzi wake wa kweli wangefanya kile alichofundisha mwalimu YESU wa
Nazareti. Sasa wanafundisha yale ambayo siyo yake na kama
siyo yake yaani yeye njia ya uzima na
kweli utafika alipo yeye? Jibu hapana.
Imeandikwa watu
hawa huniabudu kwa midomo tu ila ndani yao
ni mbwa mwitu na mimi sipo nao. Tokeni huko mkatengane nao hao ni mbwa mwitu
watumiwao na shetani katika kanisa ili kuziua roho za watoto wa MUNGU. Ndiko
huko kuwapiga chapa hasa katika mwisho wa mwaka ndipo hufunga hesabu yao na kumpatia shetani
ya kuwa mwaka huu hawa ndio wamewapiga chapa ya namba 666 ni wake. Usikubali
ewe mwanadamu huo ndio ukweli na haitabadilika. Neno lake lazima
litimie na haya niliyokueleza ni ya MUNGU anayejulikana.
NABII HEBRON