NABII HEBRON AKIWA NA BABA YAKE WA KIROHO MOSES KULOLA.
Basi kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu, hali akijua ya kuwa saa yake imefika, atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba, naye ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo. Hata wakati wa chakula cha jioni; naye Ibilisi amekwisha kumtia Yuda, mwana wa Simon Iskariote, moyo wa kumsaliti; Yesu akijua ya kwamba Baba amempa vyote mikononi mwake, na yakuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu, aliondoka chakulani; akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa, akajifunga kiunoni. Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga. Hivyo yuaja kwa Simon Petro. Huyo akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi? Yesu akajibu, akamwambia, nifanyalo wewe hulijui sasa; lakini utalifahamu baadaye. Petro akamwambia, wewe hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia,
Basi alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa
mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia je! mmeelewa na hayo niliyowatendea?
Ninyi mwaniita, mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo. Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na mwalimu,
nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi. Kwa
kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, ninyi mtende vivyo.
Ndugu msomaji jambo hili sio jambo geni la
kuoshwa miguu makanisani ila nataka uelewe kusudi la YESU na ni nani wanaopaswa
kuoshwa miguu na ni kwa jinsi gani? Hali YESU akijua ya kuwa muda wake
umekaribia kuchukuliwa aliwaita wanafunzi wake akawaosha miguu ikiwa ni ishara
ya utayari kwa ajili ya kazi yake, akachukuwa kitambaa akajifunga kiunoni
wakati akiwanawisha miguu - hii ina maana aliwaachia ujasiri kwa ajili ya kazi
yake ili wayaendeleze yale aliyowafundisha kwa wanadamu wote, na ukisoma utaona
Petro alikataa asioshwe miguu ila YESU akamwambia usipokubali nikuoshe
hautakuwa na shirika na mimi, hii yote ilikuwa ni maandalizi ya kuwaandaa wale
mitume wake au wanafunzi wake kwa ajili ya kazi yake. Na akasema ikiwa mimi
mwalimu nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi
kwa kuwa mimi nimewapa kielelezo ili kama mimi
nilivyowatendea nanyi mtende hivyo hivyo.
Ndugu msomaji, natumaini umesoma huu waraka
niliokuandikia hapo juu Yohana 13:1-15. Yesu anasema mtawadhane ninyi kwa ninyi
na kufuata kielelezo alichowaachia na kwa jinsi ile ile na akasema ni ninyi kwa
ninyi inamaana ni watumishi kwa watumishi. Na zaidi nikuulize swali; je, kwa nini
Yesu hakuwatawadha miguu watu wengine tofauti na wale mitume?
Hii ni kwa sababu hawa mitume waliandaliwa
kwa kazi yake tu, na ni tofauti na wafuasi wa Yesu, ndiyo maana anasema ninyi
kwa ninyi na nimeshawapa kielelezo na ukisoma mstari wa 15 inaelezea, na
kielelezo hicho ni wale mitume / watumishi sasa swali nakuuliza, ndugu msomaji,
je wewe unayeoshwa miguu wewe ni mtumishi? Au ni mfuasi wa Yesu? Soma utaona
imeandikwa ni watumishi kwa watumishi ili kuifanya kazi yake, ila siku hizi
Neno na maagizo aliyoyaagiza Yesu na kutoa mifano imepuuzwa, watu wote
wanaoshwa miguu kanisani je nikuulize
swali kwa nini Yesu amesema ninyi kwa ninyi tu? Ina maana ni watumishi peke yao kwa ajili ya kazi
yake. Na kama ingekuwa ni kwa watu wote, basi ingeandikwa kwa watu wote kama ilivyoandikwa mkawabatize watu wote.
Na ili uzidi kufunguka ufahamu wako je, ni
mtumishi anayebatiza au ni muumini? Jibu ni mtumishi, hii ni sababu yeye
ameshatofautishwa na kondoo. Ndiyo maana ni mtumishi tu ndiye anayetakiwa
kuoshwa miguu tu, na sio waumini japo hata mimi niliwahi kuoshwa miguu, bila
kujua ila nitakueleza hasara zake, kwa hiyo tayari hili ni kosa kubwa na
kufanya kinyume na Yesu alivyoagiza. Na ukisoma
katika Yohana13: hakuna mahali Yesu amerudia kuwaosha hawa mtume wake miguu ni mara
moja tu, hao wawafanyie wengine kwa
kufuata kielelezo alichokifanya Yesu. Leo hii hakuna cha mtumishi wala muumini
wote mnaoshwa miguu. Hebu someni Neno na kuelewa. Na utashangaa kila mara
ibada za kuoshwa miguu. Ni kuulize swali
wewe unayeoshwa miguu wewe ni mtumishi? Jibu siyo na kama
wewe ni mtumishi kwa nini na wewe kila mara unawanawisha miguu? Hauna jibu,
umepotea.
Ndugu msomaji leo nakupatia siri kubwa na ufunguke
kuhusu ibada za kuoshwa miguu na hili ni
kwa Dunia yote na mataifa yote, Yesu
kaniambia siyo mpango wake watu wote waoshwe miguu ni kwa watumishi tu, ila
watumishi wengine wanaiga wenzao wafanyavyo ila 95% ya Ibada zote za “foot washing” kwa waumini, hutumia
nguvu za giza na kuyanenea yale maji
wanapokuosha miguu wanakushika utayari wako unakuwa wewe ni wa hapo hapo
tu hata kama mnamjua kabisa mtumishi ni
mchawi hauondoki hapo, hata kama mambo yako hayaendi unaangamia hauwezi kutoka, maana miguu
imeibiwa utayari na zaidi ule utayari unabakia katika kitambaa na vile vitambaa huviweka kwenye
kiti na begani, kwenye kiti ni
kukukalisha wewe hapo hapo tu, na begani anakubebesha mizigo ushindwe kuondoka.
Funguka Yesu anawapenda mpone, unayesikia, sikia, unayekataa utajuta. Na watumishi hao wakiona waumini
wameanza kumshtukia mtumishi hayupo sawa na MUNGU haraka sana huitisha ibada ya kuoshwa miguu, na
waumini wanafikiria ni jambo jema kumbe unaenda kumalizwa kiroho na kimwili,
waulize swali, hawana jibu zaidi ya kukukimbia, na zaidi waulize wapi Yesu aliwarudia kuwaosha mitume miguu wale aliowaosha? Jibu
hawana. Huu ni mpango wa kwenda kinyume na Yesu. Amesema ninyi kwa ninyi tu,
watumishi na kielelezo ni kama hao mitume na
watumishi tu. Na zaidi ufunguke ukisoma katika Neno lake Yesu alifunga kitambaa
kiunoni, akawafuta, sasa kwa nini hawa hawajifungi kiunoni kitambaa? Jibu
umelijua.! na je, ndicho kielelezo alichokiacha YESU cha kuweka kitambaa kwenye kiti na begani? Huu ni
mfano halisi hiyo ni feki tu. Na waumini siyo watumishi waoshwe miguu ni mtumishi anaoshwa tu
pale anapopakwa mafuta. Ufunguke ufahamu ili mtumishi akukamate kipepo, njia
mojawapo ni hiyo na ujiulize swali kwa nini hurudia ibada ya footwashing kila
mara? Na
je wewe muumini ni mtumishi? Kataa na usishiriki na waulize swali na uangalie
kwenye BIBLIA utaona ukweli mtupu, usishiriki dhambi na zaidi unaangamia,
umeshiriki Neno la MUNGU kinyume na alivyopanga YESU.