Upendo wa shetani ni ile hali ambayo
inakuwa ndani ya mtu kwa nje anaonyesha anakupenda ila ndani ya moyo wake anakuwazia mabaya
matupu hata kukuua, ila kwa nje akiongea na wewe anajifanya yupo yupo na wewe
na mda mwingine hujiweka rafiki wa
karibu sana na hata usimjue ila anakuwa
analo jambo lake analolijua kwa hiyo hii
inaitwa chuki na siyo upendo.
Mtu huwa anakupenda sababu anapata
vitu kwako, mfano unampa pesa, au msaada na ukiacha tu, huanza kukuchukia au
hata kukusema vibaya. (Inaonyesha ni vitu vyako ndiyo alivyovitamani).
Mtu asiyekuheshimu kama upo na hali
yako hiyo na kisha anaongea na wewe hata kukupa salamu huyo anayo chuki.
Mtu anayejifanya yupo upande wako na
pia yupo upande wa maadui wako, huyo ni msaliti wa mtu kama vilea YUDA alikuwa
pande mbili/
Upendo wa shetani ni matunda yote au
tabia zote za kinafiki juu ya mtu na mtu au pia mtu anajiita mkristo yani
anampenda MUNGU lakini matendo yake ni udhalimu mtupu. Huyo anayo roho ya
shetani na ni mnafiki wa MUNGU na ni rafiki wa shetani.
Upendo wa shetani - ni kukosa na kutenda kinyume kama
kubadilisha Neno la MUNGU kama alivyoagiza
yeye ( mfano WAGALATIA 1:5-6)
Mtu mbinafsi hajali wenzake ,
kudharau, siyo msikivu, siyo mtiifu, kwa upande wa kanisa ukiona kanisa linawapenda
wale wenye pesa na kuwajali tu! Na hao
wasio na kitu hapo ujue ni upendo wa shetani.
Ukikuta watu wanaabudu miungu mingine
tofauti na MUNGU aliyeumba vitu vyote hapo ujue kuwa hawampendi MUNGU aliye hai
wanampenda shetani , haijalishi wanamtaja YESU hata kusoma BIBLIA, huo ni
unafiki na imeandikwa MUNGU huwachukia waovu; hawa ni waovu.
Ukikuta mtumishi anakudai pesa ndiyo
akuombee huyo anao upendo wa shetani, ndio wenye tamaa, na imeandikwa nimekupa
bure toa bure, hapa tayari hakuna utii ni utovu wa nidhamu kwa MUNGU na wizi.
Upendo wa MUNGU wa kweli hauangalii vitu, hebu ona hapa sasa unaangalia pesa (vitu) hii ndiyo upendo wa shetani.
Na zaidi unadaiwa utoe pesa na kama hauna
unaambiwa leta hata mifugo yako na kiasi kikubwa cha pesa na hata ukitoa bado
shida haiishi ipo palepale au inazidi . Hii inaonyesha kama tayari huu upendo
hauna neno la MUNGU bali una uwongo wa
shetani na hamna ukweli.
Upendo wa shetani (chuki) hukaa ndani ya watumishi wote na watu
wote walio wanachama wa freemason,
zaidi wapo majina yao katika mtandao,
hawa wote tayari ni mfano halisi yakuwa
wanamchukia MUNGU na ndani yao ni udhalimu, na wauaji wa roho za watoto
aliowaumba MUNGU kwa upendo wake na
shetani huwatumia kama roho yake ya
chuki kuangamiza. Au kwa maana nyingine yeyote ametengwa tayari na MUNGU, hao
ni wafanyakazi au vibarua wa shetani, ni wakati wa wanadamu wote katika
ulimwengu kujitenga nao na kumtafuta
MUNGU wa kweli na siye MUNGU wa
unyang’anyi. YESU anarudi utakuwa wapi wewe? Jiulize na roho yako ifunguke.
Upendo wa shetani (unatamani uzinzi). Japo imaeandikwa usizini, ukikuta mtumishi anazini - ujue ndani yake amesha mchukia MUNGU na
sheria zake na ndani yake ni roho wa shetani.
Mfano siku hizi unakuta mtumishi
amekufa na na ukimwi au anao ukimwi, Je
aliupata akiwa na MUNGU wa kweli au shetani ambaye ndie mungu wa uongo? Je
angekuwa anampenda MUNGU kiukweli
angeupata ukimwi? Jibu hampendi MUNGU, mshahara wa dhambi ni mauti. Na zaidi
hata akifa na ukimwi kanisa linaficha na kusema uongo katika taarifa ya sababu
ya kifo, je, MUNGU wa kweli ni muongo? Jibu
husema kweli. Hii ni dalili tosha kuwa hamna MUNGU wa kweli, utawajua watu kwa matendo yao. Ni aibu! na kama
viongozi wanakufa kwa ukimwi sasa hilo kanisa linaenda
wapi? Mbinguni au jehanamu? Jibu linaenda jehanamu, na mahali pa namna hiyo ni
chukizo kwa MUNGU na ndiyo maana adui
anawauliza watumishi wake.
Ukikuta mtumishi anazini na muumini au hata mwanadamu
yeyote yule iwe ni mtumishi wa kike au wakiume, hao wote siyo rafiki wa MUNGU ni rafiki wa shetani na anayo roho ya namna ya shetani. Huyo siyo mtumishi anayetumiwa na MUNGU
mtakatifu je MUNGU anashiriki na uzinzi? Jibu hapana. Hivyo ni namna ya
kuelewa kuhusu MUNGU wa kweli na watu wapone roho zao.
Ukiona michango makanisani, ujue hapo
tayari MUNGU hayupo ni roho ya tamaa ya
kwenda kinyume na upendo wa MUNGU . soma
1WAKORINTHO 13 yote. Halafu uangalie na uchunguze utaona ni matamaa tu, na kukosa utiifu kwa MUNGU aliyekataa. Nyumba yake ni nyumba ya Ibada (yani sala tu) soma MARKO 11: 15 -18 YESU
alikataa, ila kwa ajili ya watumishi kumpenda shetani na tama zake wameamua
kuwa wanyang’anyi, kama majina yao wakitumia jina la YESU. Watumishi wa namna
hii wameshikiliwa na upendo wa shetani ndiyo maana wanafanya ya shetani. Na ibada hizo na kila kifanywacho ni unafiki
mbele za MUNGU na MUNGU hawasikilizi wanafiki au wasaliti wa amri zake. Mwisho
ni hukumu na jehanamu ipo tayari, na MUNGU amaeniambia
hukumu ipo tayari inawasubiri. Amua mwenyewe Jehanamu
au Paradiso.
UPENDO
WA MUNGU NDANI YA MWANADAMU.
Upendo huu ni roho ile ya upendo ndiyo inayofanya
kazi ndani ya mwanadamu kwa kusudi la kuujenga mwili wa Kristo. Bila upendo wa
MUNGU ndani ya mwanadamu kanisa la YESU
halijengeki, ikiwa ina maana Utiifu hautakuwepo na roho ya kumpenda MUNGU
kiukweli, mfano wanaoabudu sanamu huo sio mwili wa Kristo ni mwili wa shetani
au yasiyofuata BIBLIA na sheria zake tayari huo siyo mwili wa Kristo maana ndani yake haipo kweli yake na
upendo ni kweli tupu ya MUNGU na kama
kweli tupu ya MUNGU imeondolewa na yeye
hayupo siyo anayeaujenga huo mwili. Na hata ule mkate wa kimwili
unaoliwa kanisani na ile damu kama kanisa limeacha sheria za MUNGU mkate ule unakuwa ni mwili wa shetani na damu
ya shetani na waumini wanakuwa na afya ya kiroho ya shetani, wanaumizwa tu.
Hebu jiulize itawezekanaje ulishwe mwili
wa YESU na huyo ambaye yeye anaabudu
YESU 100% waabudu sanamu, au Miungu
mingine, na hata ukikataa ubatizo wa
maji mengi ambao ndio wa MUNGU,
eti akuunganishe na mwili wa YESU. Hii
ni uongo ni mkate ambao ni yesu wa uongo
na mkate wake ambaye yupo kuzimu
(Kristo wa uwongo) utaona jinsi
watu wanavyolishwa mwili wa Yesu wa
kuzimu. Na zaidi hata mgonjwa akikata roho
hupelekwa mwili huo ikiwa ni chakula cha shetani anaangamia zaidi .
Mwili wa Yesu hautokei au kutumika
katika watu wasiofuata sheria za
MUNGU. Huo ni feki tupu! Swali ! Je,
mwili wa YESU na damu yake inatumiwa na sanamu au na dini zisizofuata
ubatizo wa kweli wa maji mengi?
Huo
ni mwili feki kabisa ndiyo maana mtu anakula
huo mkate miaka 40, karibu anafikisha hata debe hamna matokeo zaidi ni
mapepo yamejaa ndani ya mwanadamu na matatizo badala ya kuwa na uzima tele ni
mauti tele.
- Mtume na Nabii Hebron Wilson Kisamo