Pages

Friday, May 31, 2013

KANISA LA SASA 98% LIMEKUWA PANGO LA WANYANG’ANYI.

KANISA LA SASA LAMFANYA YESU AITWE MNYANG’ANYI 98%


Ndugu msomaji wa makala hii, ninao ujumbe tena kwa ajili ya ulimwengu wote na watu wote na aliowaumba MUNGU aliye hai, na ambaye aliyemtuma mwanae YESU KRISTO WA NAZARETI kuja kuukomboa ulimwengu huu, akaja akatufundisha njia ya ukweli na uzima ambaye yeye ndiye uzima huo. ( YOHANA 14:6 ) na pasipo yeye hakuna atakayemuona  MUNGU au kufika kwake, au kwa maana nyingine bila YESU hauwezi kufika kwa MUNGU, au bila wokovu hautamwona, na tena uwe ni wokovu safi siyo wokovu wa jina tu, nikiwa namaanisha kwamba watu wengi wakisha okoka wanabakia wokovu jina tu na siyo kimatendo, au kumsaliti YESU kama Yuda alivyomsaliti YESU.

Huyu YUDA alikuwa ameokoka ila alifuata njia tofauti na ndiyo maana aliangamia, hivyo ukiokoka na ukaacha  kwenda  sawa sawa na YESU wewe unaitwa Yuda, nikuulize swali je kwa nini wale mitume wa YESU (11) hawakuachwa na YESU? Jibu walimpenda YESU kiukweli na siyo kinafiki na YESU hakuwaacha.

Ndugu msomaji ninanukuu NENO LA MUNGU katika  baadhi ya vitabu kuonyesha kwamba yale yote aliyoyakataa  YESU akiwa hapa ulimwenguni katika nyumba ya sala yamerudishwa katika makanisa  na makanisa kutumia jina la YESU kufanya biashara ndani ya nyumba ya ibada na YESU kuitwa mnyan’ganyi japo yeye alikwisha yakataza  yasifanyike na ukisoma katika  kitabu cha Marko 11: (15-17) wakafika Yerusalemu,naye akaingia ndani ya Hekalu, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakiuza na kununua ndani ya Hekalu, akazipindua meza za wabadili fedha na viti vyao wauzao njiwa, wala hakuacha chombo kati ya Hekalu, akafundisha akasema, Je? Haikuandikwa nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi! .

Ndugu msomaji wa makala ya Nabii Hebron, kwa picha  halisi  iliyopo makanisani kwa sasa inaonyesha wazi kanisa la sasa 98% limerudi kuwa pango la wanyang’anyi, unyang’anyi inamaanisha pesa na hizo mali haziendi kwa MUNGU zinaenda kwa shetani na shetani ndiye mnyang’anyi, ila unyang’anyi huu unafanyika makanisani kwa kivuli cha kutumia jina la YESU. Japo YESU alishakataa na kama alishakataa YESU, basi kanisa hilo haliongozi YESU, ni roho ya kumpinga YESU na MUNGU , ndiyo inayoongoza  mahali hapo, na mahali kama hapo, MUNGU haonekani kwa sababu ni machukizo kwa MUNGU, nitaelezea kwa ufupi mambo ambayo yamerudishwa na kanisa na kanisa kuwa soko na siyo nyumba ya ibada tena.

  1. Kuhusu sadaka ya mavuno – sadaka hii watu huleta mazao kanisani; ni kuleta sadaka na kisha watumishi huanza kufanya mnada au kuvinadia vitu hivyo, hapo tayari siyo kanisa hilo na hivyo siyo sadaka tena, na haipokelewi na MUNGU aliye hai. Jambo hili ni machukizo kwa MUNGU. Zaidi uelewe kuwa sadaka ya mavuno ni fungu la kumi la kiasi cha mazao uliyoyapata, wewe cha kufanya,  kauze halafu peleka hiyo pesa kanisani  haijalishi ni pesa ndogo umeuza MUNGU anaijua na anaithamini, na zaidi sadaka yako inapojulikana na mtu unatoa kiasi gani hiyo tayari siyo sadaka tena . Imeandikwa utoapo  hata kushoto isijue, sasa embu angalia mazao yako yanavyonadiwa. Madhara ya kufanya kanisa soko unalaaniwa  na MUNGU na haubarikiwi, unazidi kufilisiwa. Hivyo kufanya mnada kanisani ni dhambi kubwa kwa MUNGU, ila kama ni YESU wa kweli analiongoza kanisa hilo mnada haufanywi na kanisa hilo, maana ni machukizo kwa MUNGU.

  1. Ukisoma katika kitabu cha YEREMIA  (7: 11) je nyumba hii iitwayo kwa jina langu imekuwa pango la wanyang’anyi machoni penu? Angalieni, mimi, naam mimi nimeliona jambo hili, asema BWANA, lakini enendeni sasa hata mahali pangu palipokuwepo katika Shilo, nilipolikalisha jina langu hapo kwanza, mkaone nilivyopatenda sababu ya uovu wa watu wangu  wa Israeli. Na kwa sababu nimezifanya kazi  hizi zote asema  BWANA, nami nikasema nanyi nikiamka mapema  na kunena lakini hamkunisikia  nami nikawaita wala hamkuniitikia, Basi nitaitenda nyumba hii iitwayo kwa jina langu ( Yani  kanisa) mnayoitumainia na mahali hapa nilipowapa ninyi na baba zenu,  kama nilivyopatenda Shilo. Nanyi nitawatupa ninyi mbali na macho yangu, kama nilivyowatupa ndugu zenu wote, yaani wazao wa Efraimu.
Ndugu msomaji natumaini unazidi kuelewa  kuwa MUNGU hapendezwi na mahali panapoitwa kwa jina lake halafu panafanyika unyang’anyi , mahali pa hivyo MUNGU hashiriki 100% na mwisho ni hukumu na yeye ndiye ayafanye apendavyo, ufunguke ufahamu usishiriki hayo makanisani na makanisa yanayofanyaga hivyo, ni yale ya kujiita yenyewe na siyo MUNGU kayateua , kama akiyateuwa  yeye au alilolitenga yeye kwa jina lake.  Nitaeleza kwa kifupi mambo yanayomchukiza MUNGU na lakini mtu pasipokujua unayashiriki bila kujua.

  1. HARAMBEE ZA MAKANISA – Kama hilo kanisa ameliteua MUNGU    
mwenyewe kanisa hilo atafungua milango ya ujenzi, ila kama umejiita kwa jina  lako ina maana halitambui MUNGU, Harambee kufanya kwa ajili ya kanisa YESU aliniambia HEBRON, MUNGU siyo masikini, vitu vyote hapa ulimwenguni ni vyake. Akaniambia MUNGU akianzisha kazi yake tayari huwa ameandaa njia zake, tazama mimi YESU kabla ya kuja hapa ulimwenguni, MUNGU aliniandalia njia, kupitia Manabii, kusema habari zangu na nikaja. Akaniambia , ole wao wanaotumia jina la BABA kufanya harambee, au kwa lugha nyingine ni kumnadi MUNGU. Kama kanisa ni lake watumishi wamuombe yeye, alisema msisumbukie jambo lolote na zaidi katika Yohana 7:7. Ombeni atafanya ila siyo kwa namna  ya harambee na zaidi hakuna harambee yeyote iliyopokelewa mbinguni tokea ilipoanza na sasa na milele na kama haipokelewi ina maana wale watu waliotoa pesa  hizo wakijua wanamtolea MUNGU aliyehai, wameibiwa na mungu mfu, na sasa shetani analitumia nyumba ya kanisa iitwayo kwa jina la MUNGU kuwa pango la unyang’anyi.

  1. Jambo lingine ni chukizo zaidi ( Mathayo 21:13 ). Akawaambia imeandikwa,       
Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala, Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi. Unyang’anyi huu unafanywa na watumishi, Kwa hapa YESU anasema ninyi? Ina maana viongozi wa kanisa. Na (14) mstari na vipofu na viwete na wenye matatizo walipomuona YESU hekaluni wakamwendea, akawaponya. Inamaana hawa viwete, na wenye matatizo walikuwepo tuu katika kanisa ila hawakufunguliwa mpaka YESU  alivyokuja. Hapa unajifunza kwamba YESU hakai katika pango la unyang’anyi na waumini waliopo hapo wataendelea kuteseka tuu.. Na ukuu  wake hauonekani. Sasa hivi kanisa kwa kupitia watumishi kazi imekuwa ni unyang’anyi tuu, mpaka wamebuni kuwaita watu partners na kuwapangia kila mwezi watoe kiasi fulani na ni lazima. Na kuchagua watu wenye pesa tu ndio  huwaambia eti MUNGU ameniambia nyie kwa majina yenu,  Hapa swali jiulize kwa nini hawachagui partners asiye na pesa? Je, huyu MUNGU ni mbaguzi? Wakati tunajua kwamba wote ni wafuasi wa YESU sasa haya matabaka  ya masikini na matajiri  ni mpango wa MUNGU kanisa lifanye  hayo?  Jibu ni mpango wa shetani, kuwaita waumini baadhi wenye pesa kuwa partners huo siyo mpango wa MUNGU, huo ni wizi ni unyang’anyi wa mali zao nao hawabarikiwi, na MUNGU hafurahii jambo hili, na jambo hili limekuwa kero hata kwa waumini maana wamejiingiza mpaka kwenye madeni ili kutafuta hiyo pesa. Na wewe ufunguke ufahamu wako haiwezekani umtolee MUNGU na aipokee halafu ubakie na madeni. ( Madeni ni roho ya shetani)  Embu ona sasa kanisa lilivyokuwa pango la unyang’anyi, YESU aliyakataa na sasa yamerudishwa na shetani na kama yamerudishwa na shetani,  je, hili pango sasa linaongozwa na shetani na siyo YESU tena, imebakia kutaja jina la YESU tu kama kitu cha kunyang’anyia waumini pesa, mali na vinginevyo na siyo tena kuujenga ufalme wa MUNGU na watu wamjue MUNGU aliye hai na sheria zake, au kwa luhga nyingine kanisa limerudi  Misri, au kurudia matapishi.

5. YOHANA 2: (14-17 ) Akaona pale hekaluni  watu walivyokuwa wakiuza        
    ng’ombe  na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi, akafanya 
    kikonyo cha kitambaa akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng’ombe  
    akamwaga fedha za wenye kuvunja pesa, akazipindua meza zao, akawaambia  
    wale waliokuwa wakiuza njiwa, yaondoeni haya. Msiifanye nyumba  ya BABA  
    yangu  kama nyumba ya biashara. Hapa Neno la MUNGU linazidi kuonyesha wazi   
    kuwa MUNGU amekataa nyumba yake isiwe nyumba ya biashara na kama hizi
    biashara zinafanyika basi siyo nyumba zake za ibada, maana yeye hashirikiani na
    biashara katika  nyumba yake ya ibada. Ila asili ya kuchafua kusudi la MUNGU  
    katika kanisa ni shetani. Na kama haya yanafanyika utambue hapo kanisa limeacha   
    njia ya kweli na mafundisho ya kweli ya NENO la MUNGU, na kufuata    
    mafundisho ya uongo, na kulitumia jina la YESU kunyang’anyia mali waumini na  
    kumbe YESU  hahusiki hata ukisoma katika kitabu cha Injili YESU amekataza.  
    Sasa kama mwanzilishi wa kanisa alishayakataa, na kanisa limeyarudisha
    Hii inamaana kanisa linalofanya mambo haya limemkataa YESU na
   YESU naye amelikataa na waumini wanaoshiriki wanaunganishwa na mapigo hayo  
   na hakuna pa kujitetea maana imeandikwa marufuku kanisa kufanya biashara.


  1. BAADHI YA BIASHARA ZINAZOFANYWA NA MAKANISA NA  KUMFANYA YESU AITWE MNYANG’ANYI.

  1. Kanisa kuwa na Mabenki – YESU alishasema ukimkopesha mtu usitake akulipe 
Riba, sasa kazi ya benki ni kukopesha na kuchaji faida ya ziada, na zaidi mtu huyo anaposhindwa  kulipa fedha hiyo-hiyo benki humfilisi au kumnyang’anya mali zake zote. Kwa kanisa kushiriki biashara hii ni kwenda kinyume na YESU alivyoagiza, na jina lake kuzidi kutukanwa, maana kama benki ni ya kaknisa, lazima jina la YESU litajwe hapo. Je YESU anafilisi watu, na kunyang’anya mali zao? Je, ndilo kanisa alilolijenga YESU hapa ulimwenguni lipo hivyo? Jibu siyo; Imeandikwa usichukue chochote cha mtu, na je YESU anadaigi riba? Wakati alishakataa yasifanywe na kanisa, kubadili fedha na dhahabu, sasa leo hii kiasi kikubwa ulimwenguni mwote kanisa linafanya haya. Ninachokuambia YESU  hana biashara ya benki, hao wanafanya  biashara hizo wamemsaliti YESU  na YESU hayupo nao na wanaongozwa na yesu wa kuzimu, ambaye alisema  watakuja makristo wa  uongo na mtawatambuaje?  Mtawatambua kwa matunda yao, mfano matunda ya YESU wa Nazareti kama au hufanana kabisa na YESU kisura na hamna tofauti. Ila matunda kinyume na YESU kimatendo, mfano mambo aliyoyakataa MUNGU yasifanywe na kanisa na ukiona kanisa linayatenda haijalishi linatajwa jina la YESU, ujue tayari ni kanisa la uongo. Na kanisa la uongo mwisho wake ni hukumu na wote waliopo katika ushirika wa kanisa hilo hawatamuona MUNGU milele.

  1. Makanisa kukopa benki ili wamjengee kanisa? Siyo kanisa lake na yeye YESU
halipi riba maana – pesa inapokopwa na kanisa benki ni lazima kanisa lirudishe na riba. Na pesa hizi huchangishwa waumini kupitia jina la YESU na kupeleka marejesho, na waumini pesa zao zinapopelekwa kulipia deni ina maana wanatoa kwa ajili ya YESU! Na huyu huyu YESU wa kweli ameyakataa hayo!  je YESU analipa riba? Jibu hapana na yeye siyo masikini vitu vyote ni vya baba yake. Ila yesu wa kuzimu au kristo wa uongo huyo ni masikini na yeye kazi zake huziandaa kwa kupitia wanadamu na hazina njia. Ila njia za YESU wa kweli tayari MUNGU hufanya maandalizi yake peke yake na siyo kwa njia ya kukopa  na  kutumia jina lake kwa kunyang’anya na kufilisi.

  1. KANISA KUWA NA BIASHARA ZA BAR

Biashara hizi ni kumtukana YESU na kumdhalilisha kabisa na pia kumdharau MUNGU aliye hai na kumuinua shetani, kila mtu anajua kuwa MUNGU hashirikiani na bar. Ila unakuta makanisa baadhi yana bar na yanauza vileo na ile faida wanaipeleka kanisani, nikuulize swali je YESU WA NAZARETI aliruhusu kanisa lake lifanye biashara ya bar? Au biashara yeyote ile?  Jibu hajaruhusu. Na kama yametokea makanisa ya namna hiyo, makanisa hayo ni ya yesu wa uongo, kristo wa uongo utamjua kwa matendo yake mabaya kama mfano mmojawapo, mfunguke maana mahali hapo panaongozwa na roho ya ukristo wa uongo na kristo wa uongo kazi yake ni kuziangamiza roho zote ziende jehanamu. Jichunguze je upo wapi wewe kwa kristo wa kweli au kristo wa uongo?

  1. SADAKA 98% NI UNYANG’ANYI

  1. Jambo lingine kubwa zaidi kanisa hutumia njia ya sadaka kuwanyang’anya waumini wakitumia jina la YESU. Sadaka  ni ibada yako wewe mwenyewe kati yako na MUNGU na  ni siri yako hapaswi mtu yeyote kujua umetoa kiasi gani, na sadaka ya kweli ni sadakaya fungu la kumi na shukurani kwa jinsi upendavyo moyo wako unatoa na siyo upangiwe kiasi cha kutoa. YESU anahuzunika sana moyo wake na hana furaha na yeyote yule anayewaibia watoto wake pesa kwa njia ya sadaka. Akaniambia siyo mpango wa MUNGU aliye hai, watu waandike majina kwenye sadaka zao, na kiasi, na namba za simu na pia upewe risiti baada ya kutoa sadaka. Huo ni wizi na sadaka hizo hazipokelewi na MUNGU aliye hai, inapokelewa na mungu mfu , hivyo ndivyo kanisa lilivyotekwa na shetani na kanisa linalotekwa na shetani ni lile inalochukua sadaka kinyume na mpango wa MUNGU aliye hai.

  1. Mtumishi – anakuambia ili akutabirie toa kiasi fulani cha sadaka ndipo MUNGU   
atatenda – huo ni unyang’anyi ( imeandikwa umepewa bure toa bure) ila mtumishi anayeongozwa na roho ya shetani fomula yake lazima utoe vitu, mfano kwa mganga wa kienyeji – ili ufanikiwe atakuambia mungu wake anataka pesa kiasi fulani ndipo atakusaidia na mtu hufanya hivyo .Ukiambiwa hivyo na mtumishi – jua  huyo ni mwizi anayetumia jina la  YESU kutafutia pesa, na watu mpaka wanaona YESU anapenda pesa sana.

  1. Ukikuta  mtumishi anajifanyia mnada na watu wanasaini katika nguo yake na
     kutoa pesa eti ndiyo wamesaini kwa MUNGU, nakujulisha mtumishi huyo kwanza  
     ni mchawi, unaposaini katika nguo yake, ina maana umesaini wewe peke
     yako, kwa uamuzi wako mwenyewe unampatia utajiri wako na wewe unabakia
     masikini na nguo hiyo hupelekwa kuzimu na yeye peke yake, na hii ni mfano wa  
     wana wa MUNGU wanavyonyang’anywa utajiri wao na shetani.

  1. Michango makanisani – huu ni wizi na kumfanya YESU nyumba yake kuwa soko, na kwa nini makanisa mengi katika ulimwengu huu yamebakia na shughuli ya kufanya michango madhabahuni, sababu kubwa mojawapo siyo makanisa yake, maana maagizo ya kanisa lake yeye hayajaruhusu hayo na alikwisha yakataa.( Soma MARKO 11: 15-17) (YEREMIA 7:11,) (YOHANA 2: 14-17) na kama aliyakataa YESU na pia MUNGU aliye hai anao wivu na nyumba yake kwa ajili ya kuabudiwa tu, je MUNGU huyu ni kigeugeu? MUNGU siyo kigeugeu wala habadiliki na NENO lake amelihakikisha na halitabadilika, ila ole wao waendao kinyume na yeye (Ufunuo wa YOHANA 22: 18-20).  Imefikia hata waumini hawaendi kanisani sababu sadaka zimezidi, mara majengo, umisheni, kwaya, na nyinginezo, kwani hiyo sadaka inayotolewa inaenda wapi?
Hizo zote ni unyang’anyi. Ninakuambia kwa ujasiri kabisa bila kuogopa lolote ninaye YESU  ndani yangu mwenye uwezo aliyeniteua nimtumikie, usidanganyike na michango  YESU hataki na mnaangamia, kufanya harambee na michango kanisani ni machukizo  makubwa kwa MUNGU na wewe unayeshiriki  pia. Kama kazi ni yake yeye MUNGU msumbue atafanya ajuavyo yeye ila kama siyo yeye, ni mungu wa uongo asiye weza, anawachangisha waumini. Na badala ya watu kwenda mbinguni panakuwa ni pango la unyang’anyi na zaidi utakuta watumishi wa pesa na sadaka, hii hufanyika pango la unyang’anyi. Na siyo kanisa teule la MUNGU aliye hai.


NOTE:
UWE MAKINI SANA NA PESA ZAKO, MUNGU AMEKUBARIKIA WEWE NA UTUMIE KATIKA NJIA AIPENDAYE YEYE ILI USIINGIE MATATANI NA KATIKA DHAMBI, BILA WEWE KUJUA UKIDHANI UNAMTOLEA MUNGU ALIYE HAI ,KUMBE NI MUNGU MFU. NA MATOKEO YAKE UTABAKIA KUKUMBUKA NA KUUMIA TU KWA JINSI ULIVYOPOTEZA PESA, MALI, MAGARI, NA VINGINEVYO UKIJUA UNAMTOLEA YESU NA USIONE BARAKA, MABADILIKO YA KIROHO WALA YA KIMWILI NA KURUDI KUFILISIKA, NA USITOE SADAKA YOYOTE  AMBAYO IMEKUWA DENI NA KANISA LINAKUDAI KWA KILE ULICHOKIAHIDI, KANISA NDILO LIMEKUINGIZA KWENYE MTEGO NA SIYO MPANGO WA YESU NI MPANGO WAO NA MAMBO YAO YA KRISTO WA UONGO, UFUNGUKE UPONE, YESU SIYO MNYANG’ANYI.

- Mtume na Nabii Hebron Wilson Kisamo