TAIFA TEULE ISRAEL SASA KUANZA KUREJEA KATIKA NCHI YAO
Ndugu
msomaji wa blog hii ninakusalimu katika jina la YESU KRISTO wa Nazarethi, aliye
hai, BWANA wa Mabwana, Mfalme wa Wafalme, wala hakuna zaidi yake.
Leo
hii unabii wa wana wa Israel kurudi Israel umetimia, kuanzia tarehe 11-02-2013
majira ya saa kumi na mbili jioni kwa masaa ya Afrika Mashariki (Tanzania).
MUNGU
amewafungua Waisraeli wote, na sasa watarudi na kukusanyika na pia watamwamini
kama BWANA na mwokozi wa mataifa yote. Aliyekuwa amewafunga hata wakamkataa
YESU na kumuita siyo Mfalme wa Wayahudi sasa akamatwa kuzimu na kuwaachia na
sasa mtashangaa wakianza kurejea nchini kwao kama ilivyotabiriwa na kuanza kuja
Tanzania, ambayo ndiyo Edeni ya sasa aliyoichagua MUNGU. Mtakapoyaona hayo,
msishangae; mjue ni YESU wa Nazarethi ndiye anayeyafanya na hakuna wa kuzuia.
Nitakueleza
kwa kifupi tu kuhusu huyu mfalme wa Wayahudi aliyekuwa kuzimu ni nani? Huyu ni
mzimu wa Wayahudi wa kizazi cha kwanza, uliokuwa unamilikiwa na shetani na joka
kuu, ulipewa nguvu na joka kuu yaani baba yake shetani ili kuwazuia Wayahudi
wasiwamini YESU na kumkubali, na pia swali hili watu wengi wamekuwa wakijiuliza
sana, kwa nini walimpinga; Ndugu msomaji, mahali popote na nchi yoyote, leo hii
jibu umelipata . Ile roho imetolewa ya kumpinga, na sasa wataokoka na kwa spidi
kubwa na nchi ya Israel itainuliwa sana kiuchumi na kijeshi kuliko ilivyo hivi
sasa. Ni MUNGU amesema, na mimi naitoa kama alivyoniambia; sipunguzi wala
siongezi neno langu.
NOTE:
Unabii wote nilioutoa soma katika blog hii, umeshaanza kutimia, na
lazima utimie wote. Ni YESU mwenyewe yupo kazini, msishangae mnapoona
mabadiliko, hata katika viongozi wa kanisa. Walio watumishi freemason watakufa
wote ulimwengu mzima na wengine wataiacha hiyo kazi kwa ajili ya kuogopa kifo.
Miaka
1000 (elfu moja) ya utawala wa YESU umetimia, aliye na sikio na asikie asema
BWANA wa majeshi, MUNGU wa Ibrahimu na Isaka. Mtayaona
matukio yasiyo ya kawaida, anakuja kulichukua kanisa lake yaani wateule tu.
Ujumbe
huu nimekufikishia wewe mimi Nabii Hebron.