MNYAMA MWENYE PEMBE KUMI NA VICHWA SABA
AKAMATWA
17TH JANUARY 2013.
UFUNUO WA YOHANA 13: 1-10
Ndugu msomaji nakusalimu kwa
jina la YESU KRISTO wa Nazareti, Mfalme wa wafalme;
Nitakuelezea kwa ufupi tu; umjue huyu mnyama ni nani, na
asili yake, na kazi yake, na aliyofanya hapa ulimwenguni na jinsi alivyotumika
kuwaongoza manabii wa uongo, mpaka hatima
yake 17.1.2013 , Nilipoongozwa na YESU kumkamata nikiwa na malaika
Mikaeli.
Kama wewe ni msomaji wa makala
/ unabii ambao mimi HEBRON nimekuwa nikiutoa katika ulimwengu huu sawasawa na anavyoniamuru YESU wa Nazareti, utakuwa
unaelewa hicho ninacho kuelezea. Soma katika makala ya Joka kuu kukamatwa
ambayo kazi hiyo niliifanya alivyoniamuru YESU na kwa uweza wake yeye mwenyewe.
Huyu mnyama mwenye mapembe na
vichwa saba,ni mmoja wa wale malaika
waliofukuzwa Mbinguni wakatupwa humu ulimwenguni na baba yao Joka kuu, au kwa
lugha nyingine ndiye baba yake shetani, mnyama huyu alipewa uwezo mkubwa sana na nguvu za kuwadanganya wanadamu na
hata kulichezea kanisa na
kulipoteza na kwenda kinyume 98% . Mnyama huyu ndiye aliyewawezesha wachawi kusafiri kwa ungo au kupaa, ndiye
aliyekuwa anawapa mabawa, mnyama huyu ndiye aliyekuwa anawekeza nguvu zake
kwenye pete ( zenye vito vya rangi) wanapozivaa hasa kwa watumishi zinakuwa na miujiza ya kipepo na
mtumishi anapokuwekea mkono lazima uanguke chini na wakristo wanapoanguka
wanaona ni nguvu za MUNGU hizo.
Ninachokuambia kitendo cha
wewe kuanguka chini, maana yake umepelekwa
kuzimu. Nikuulize swali, Je! Nguvu za MUNGU
zinakaa kwenye pete? Jibu ni
Hapana. Na wachawi , waganga wa kienyeji au mtu yeyote anayevaa hayo mapete ya
ajabu, tambua mtu huyo ni mshirikina na maisha yake, au utajiri wake, cheo,
huduma aliyonayo haongozwi na MUNGU aliye hai, na njia nyingine ili kuwapumbaza
wanaweka hiyo nguvu ya mnyama huyo kwenye cheni za shingoni. Kwa wanaume wanaoongozwa na mnyama huyu huvaa cheni
shingoni wanapo hubiri na pia hutoboa masikio na kuvaa hereni, haijalishi
anatenda miujiza, ujue asili yake ni huyu mnyama mwenye vichwa saba; Ila sasa
hivi hawana pa kupatia msaada
tena, maana huyu ndiye mungu wao, na sasa ufalme wake YESU ameubomoa.
Mnyama huyu ndiye kiongozi wa
miungu yote isiyo ya kweli, mfano
nitakutajia tu, baadhi ya miungu . Kuna mungu pembe, mungu jicho, mungu baali,
mungu wa kutoa vyeo vya kipepo, mungu dagon, freemason, mizimu na wengine wengi
tu.., nikisema kuwaandika itachukua siku nzima. Hawa wote wanaongozwa na mnyama huyu. Na mnyama huyu katika ufunuo
wa Yohana 13: 4-10, wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo
wake ; na wakamsujudu yule mnyama wakisema
ni nani afananaye na mnyama huyu ? Tena ni nani awezaye kufanya
vita naye? Tena akapewa kinywa cha kunena maneno. Maneno makuu ya makufuru, akapewa uwezo wa kufanya
kazi yake miezi ( 42). Akafunua kinywa chake amtukane MUNGU na kulitukana
jina lake, na maskani yake, nao wakaao Mbinguni. Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na
kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila
kabila na jamaa za lugha na Taifa, na
watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha
uzima cha mwana kondoo aliyechinjwa
tangu kuwekwa misingi ya Dunia.
Mtu akiwa na sikio na asikie
, mtu akichukua mateka. Atachukuliwa mateka. Mtu akiuwa kwa upanga,, atauwawa
kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na
Imani ya watakatifu.
Nimekuelezea kidogo kama
kitabu Kitakatifu kinavyoelezea ( BIBLIA
). Hivyo ndugu msomaji, wa nchi yoyote
na rangi yeyote wewe umeumbwa na MUNGU aliye Hai, MUNGU wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, Hawa miungu
mingine yote unayosikia au kuiona tofauti na MUNGU wa Ibrahimu , Isaka na Yakobo miungu hiyo
yote ni ya shetani, mfano waganga wote wanaongozwa na huyu mnyama mwenye vichwa saba, na ndiyo
maana mnao au mlio endaga kwa wanajimu,
waganga wa kienyeji, wapiga ramli, utaambiwa lete sadaka ya mungu wetu ndie
atende, au ajibu, nakufungua ufahamu wako,wacha
maana unakuwa connected ( kuunganishwa) na huyu mnyama aliyefukuzwa
pamoja na joka kuu nyakati zile, wewe mwenyewe unajua kabisa shetani hana
ushirika na MUNGU aliye hai, Je kwa nini wewe unajilinganisha na joka?
Madhara yake hautaurithi
ufalme wa MUNGU na mauti na kiama
inakusubiri, Tubu wachana na hayo.
Mnyama huyu alikuwa
amejificha baharini chini kilindini
kwenye bahari ya Atlantiki mahali
ambapo ni vigumu kumuona, na ndiye aliye
wazaa waganga, watumishi wa dini zote wanaotumia nguvu za uchawi na ndiye
aliyekuwa anawapandisha viwango ( Ngazi), baada ya kufanya kazi nzuri ya
shetani , mfano kutoa makafara, kuharibu maisha ya wanadamu na kufunga ndoa
nao.
Nitakueleza kwa upande wa
kanisa zaidi, watumishi wanavaa mapete tofauti na pete tofauti na pete za ndoa,
na vidole tofauti na wengine wanatoboa masikio halafu wanahubiri , ujue
huyo ni anaongozwa na huyu mnyama wa vichwa saba na macheni ya shingoni, na
wengine hutumia uchawi.
VYEO VYA KUZIMU KWA KANISA.
Vyeo hivi vyote vimeteketezwa
tarehe 17. 1. 2013. Kazi hii ilifanywa na wazee
24 , akiwepo MUSA na fimbo yake; Ngazi hizi zilikuwa zinawawezesha kufanya kazi ya Kanisa kwa njia za uongo na
kuwafanya wathaminike na kusikilizwa, na
watu huamini na kule kuamini kwao ndio kuangamizwa, mfano imeandikwa, usiabudu
sanamu, ila kanisa linaabudu sanamu au kuomba watakatifu, au kuleta
ubatizo usio wa YESU , ubatizo wa
kikombe, japo waumini wanajua ila hukiri tu. Huko ndiko kupotea .
Nitakueleza kwa ufupi tu
kuhusu hizi ngazi, Aliyekuwa ana ngazi
hizi idadi kubwa kuliko watumishi wote , alikuwa ana ngazi elfu
moja (1,000) ni kiongozi
wa dini kubwa kuliko zote
ulimwengu wote, pia alikuwa anao ukucha wa joka kuu, ambaye ameshakamatwa; na
wapili ni muhubiri maarufu kutoka Amerika
yeye ndiye wa pili alikuwa ana ngazi hamsini (50) inamaana aliyakamata
majimbo yote hamsini (50) ya Amerika na watu wake, ili awaangamize awapeleke kuzimu na mke wake aliyajua akamkimbia. Mwingine yupo Afrika Magharibi yeye alikuwa na ngazi kumi (10) za
shetani, Afrika ya Kusini walikuwa ni
wengi sana,, na Tanzania walikuwa wengi, Kenya,UK, Asia na Afrika wengi walikuwa na ngazi mbili, tatu, moja na tano.
Ujumbe huu
ninaokufikishia mimi HEBRON nimeambiwa niutume Ulimwengu mzima, na
itafika wakati nitaamriwa niwataje na nitawataja wala hakuna wa kunizuia na mimi siogopi
lolote na kila atakayefikiria tu jambo
baya huyo hataishi tena; Ndivyo nilivyoambiwa
na MUNGU na Neno lake halirudi bure lazima litimie.
Mtashangaa sasa watumishi
waliokuwa na miujiza na kujulikana sana Ulimwenguni wanaporomoka na kuacha kazi ,
Sababu hawana tena hizo nguvu na
mambo hayaendi, na hayataenda milele, na watumishi wa YESU wa Nazareti ndio mtawaona sasa, wakiukomboa
ulimwengu , na hao sasa mtawaona wanafariki vifo vya ajabu na kwa mfululizo ,
hii ni kwa ulimwengu wote, na dini zilizokuwa zinatumiwa na huyu mnyama mwenye vichwa saba,
zitasambaratika zote, mtakapo yaona hayo yametokea msiogope mjue serikali ya
mbinguni ipo kazini kufanya maandalizi
ya ujio wa YESU ili awapate wengi. Yawezekana
na wewe ni mmojawapo wa kuokolewa.
Na kwa wale watumishi wa
pesa ( Warumi 16 : 17 -18) . Ndugu zangu,
nawasihi waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kufuata kinyume cha
mafundisho mliyojifunza mkajiepushe nao. Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii
Bwana wetu KRISTO bali matumbo yao wenyewe
na kwa maneno ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu.
Mlizoea kuwanyang’anya kondoo
mali zao mkitumia jina la YESU na YESU amekataa, Ole wenu upanga wa MUNGU upo
juu ya kichwa chako. Mimi sipunguzi neno nasema kama ilivyo.
Ewe mwanadamu usitumie stika
ukipewa na mtumishi, na anakuambia inayo nguvu za mungu, ndugu msomaji nguvu za
MUNGU anakaa nazo yeye na hukupa kiroho, na nguvu za MUNGU hakuna
anayeweza kununua. Ila za shetani
zinanunuliwa, kama hirizi. MUNGU amechukia watoto wake wanapotezwa, hiyo ni
sanamu, tena mlio na hivyo vitu, stika, kalenda, picha vitambaa, ndio maisha
yenu yanazidi kuwa mabaya, inamaana
unapopewa na kuweka kwako baraka zako zinaibiwa na hizo stika zina
mapepo mfilisi na mbinguni hauendi, na hapa ulimwenguni ni shida tuu.. Mtafute YESU wa kweli, omba atakuongoza.
NOTE: Baada ya ngazi hizi za
kipepo, watumishi waliokuwa na nguvu hizo wameporomoka na mwisho ni kifo, na
hukumu . Haijawahi kutokea tokea kuumbwa
kwa misingi ya ulimwengu huu. Mnapo yaona msishangae ni YESU anafanya kazi hiyo
peke yake.
Na Freemason wote (Watumishi ) – Watakufa , kuumwa magonjwa
yasiyotibika na vifo vya ajabu.
MUNGU AMEKASIRIKA NA AMESHAAPA HATAGHAIRI TENA.
YATATIMIA , ASEMA BWANA WA MAJESHI.
NABII HEBRON