ALIYEMSALITI YESU AKAMATWA KUZIMU NA KUBOMOLEWA MAKAZI YAKE (YUDA ISKARIOTI) ALIYEKUWA MWANAFUNZI WA YESU KATI YA WALE MITUME 12.
Marko 14:(10-43)
Nakusalimu katika jina la YESU
KRISTO WA Nazarethi. Kama nilivyokwisha kukueleza katika vitabu, makala, CD na
DVD, YESU amenituma kuupindua ufalme wa shetani akiniongoza yeye na Malaika
mkuu na Wazee 24 na serikali yote ya mbinguni nikishirikiana nao. Katika maisha
yote, sikuwahi kuongea ma MUNGU, nilikuwa nkiongea na YESU tu, ila kwa mara ya
kwanza ni August 2012.
Niliogopa sana, nyumba
ikatetemeka, na watu wa nyumbani kwangu hata waliokuwa wakipika muda wa saa
mbili usiku walishukiwa na uwepo na kuhisi kuna jambo litatokea. Watu wote
walitetemeka kila mtu kivyake, na ndipo sauti ikasema nami. Usiogope, mimi ni
BWANA MUNGU wako, leo nimekuja kusema na wewe mwanangu usiogope. Ila wakati
anaongea, yaani ile sauti tu, niliumwa tumbo na wiki hiyo kwa ajili ya mshtuko
nilipungua mwili kama kilo tatu au nne. MUNGU anatisha ukuu wake, wala siwezi
elezea.
Akaniambia, nilikuumba ili uje
ufanye kazi hii ya mwisho. Akaniambia, mikono yako ni mikono yangu, na kinywa
chako kinachoongea au kutamka itakuwa hivyo hivyo, akaniambia, nimekuja kukutia
nguvu. Nakupenda maana nimemtii na nimekubali anitumie, kwa moyo mweupe,
akaniambia, nipo na wewe milele, mimi ni alfa na omega. Akaja tena siku
nyingine kuendelea kusema nami na kunipa maelekezo ya jinsi anavyotaka nifanye
na kuharibu kazi ya muovu.
Mpaka leo, ameongea na mimi mara
13 kwa muda mrefu. Muogopeni MUNGU siyo wa mchezo kama mnavyofikiria na hata
watumishi baadhi yao wanamchezea. Ole wako, na ninanukuu amesema NENO lake
halitapita, lazima litimie tu. Mnamo saa mbili usiku 10-12-2012, Yule aliyemsaliti
YESU yaani Yuda Iskarioti alikamatwa rasmi na ufalme wake aliopewa au kulipwa
na shetani ulibomolewa rasmi na sasa hayupo tena, yupo kifoni na amezikwa
pamoja na mke aliyepewa na shetani.
Yuda Iskarioti, iliandikwa ya
kuwa YESU atazaliwa, na atasalitiwa na ikatimia kama ilivyo NENO la MUNGU
lazima litimie. Huyu Yuda baada ya kufa, shetani alimpatia vyeo na ufalme, na
aliendeleza kazi ya usaliti kwa wanadamu. Kwa YESU kama ilivyo hivi leo,
alikuwa na jeshi kubwa la mapepo na anayaongoza na yanamtii yale anayotaka
aharibu kanisa kama alivyofanya kwa YESU. Alipokuwa mwanafunzi wa YESU,
alijifunza mengi kuhusu yale YESU aliyowafundisha waukomboe ulimwengu. Siri hizo
alizipeleka kwa shetani, na shetani akampa mamlaka na nguvu ili yale mafundisho
ambayo YESU ameagiza yafuatwe, yeye akawavuvia na kuwaibia watumishi na
kuwawekea kinyume, mfano ubatizo wa kikombe (maji) kichwani tu ni Yuda kauleta
ili kupinga ubatizo ya Yohana na mambo ya kufanya nyumba ya MUNGU soko na
machafu yote yeye ndiye aliyekuwa akifanya kazi hiyo na kutumia hizo roho na
kuwa mmiliki wa baadhi ya dini ulimwenguni mwote. Ukisoma kitabu cha Ufunuo wa
Yohana 22:(18-20) wote wanaokwenda kinyume na YESU, ole wao; yaliyompata Yuda
Iskarioti ujue na wewe ndivyo ilivyo. Angalia na ujiulize wewe wewe binafsi,
ubatizo wa maji ya kwenye kichwa umeandikwa kwenye Biblia? Jibu ni haupo. Nakujulisha wewe hujabatizwa,
haijalishi una cheo gani katika kanisa au eneo lolote. Tafuta kwenye kitabu cha
muongozo wa Mungu yaani Biblia au tuseme ndiyo katiba ya YESU. Ameniambia,
waambie wabatizwe kwa maji mengi, soma katika kitabu cha “UBATIZO WA KWELI KWA
LIMWENGU WOTE”, utafunguka vizuri.
Nimekueleza kwa kifupi tu, yaani
YUDA ndiye mharibifu wa kanisa na mpaka sasa, 98% YESU haonekani ulimwenguni
mwote imebakia 2% ndio anaonekana.
Huyu Yuda alizika Biblia na
kufanya watu wasiielewe wakiisoma, hata watumishi, ila wapo wanaojua wapo
ma-Yuda kuharibu kanisa na kuhakikisha watu wanaangamia kwa kupotea ili
wasiende pazuri Paradiso. YUDA alifanya kazi hii kama mzimu, na huyu nilikuta
anaongoza na kumiliki baadhi ya dini
kubwa za Kikristo na kuzipangia mafundisho kwa namna ya kubadili ukweli na
kwenda kinyume.
Kwa mfano, imeandikwa usiabudu
sanamu. Yuda ameingiza katika dini hizo ili kuwafanya wanadamu wapigwe kama
yeye. Jambo lingine ni kwa wale wanaobatiza kwa maji mengi, akawaongezea
wakubatize kwa jina la mchungaji, halafu BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU. Na wewe
uliyefanyiwa hivyo hujabatizwa, ni ubatizo feki, wala mbinguni haupo, upo
kwenye mafaili ya Yuda Iskarioti, na wewe hautaenda mbinguni, na pia
uliyebatizwa kwa jina la mchungaji wewe ni wa huyo mtumishi, na zaidi
amekushika maisha yako na fahamu zako, huendi popote!
Fuata ubatizo wa YESU, angalia
kama huo uchafu ulifanyika. Ole ya MUNGU juu yako unayetesa wana wa MUNGU. Huyu
Yuda baada ya YESU kufa, aliongozana na wale mafarisayo kushona lile pazia la
hekalu. Ilikuwa na maana kuwafungia watu wasimjue YESU ila pazia nimelipasua
upya na sasa watu wote, ulimwengu wote, hawatadanganyika tena, ni mwisho na
YESU anawapenda sana.
Mnaowaomba watakatifu waliokufa,
ni makosa. Hata wenyewe wanawashangaa! Nimeongea nao, yaani hawana furaha.
Imeandikwa, muabuduni MUNGU peke yake tu, usiabudu hata alichokiumba yeye. Yuda
akawabadilisha kanisa, likaanza kuwataja na kuwaomba baadhi “uniombee kwa baba”;
funguka ufahamu wako! YESU alitutumia msaidizi ambaye ndiye ROHO MTAKATIFU tu. Sasa
nikuulize swali, Je, hawa watu wanaowaomba si watu kama wewe? Niliongea na mama
yake YESU, analia sana watu wanapomwabudu yeye na kuacha kumwabudu YESU,
mnaofanya hivyo mmepotea, mwisho wenu ni kuzimu na kuchomwa moto. Ni mengi sana
nitaendelea kukufundisha ili umjue YESU ambaye ndiye njia ya uzima na ukweli
Yohana 14:6 (zaidi soma sura yote). Kwa huyo aliyekuwa msaliti, sasa amefungwa
na ufalme wake umebomolewa, na siri zote nimemnyang’anya , sasa mtafunguka. Ila
wachawi, freemason na wengineo mtambue hivi: yaliyompata Yuda Iskarioti
yanakuhusu wewe pia, asema BWANA MUNGU wa majeshi.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA IBADA YA LEO (SIKU YA BWANA) TAR. 23-12-2012.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA IBADA YA LEO (SIKU YA BWANA) TAR. 23-12-2012.
Dada huyu alikuwa akiumwa na viungo kwa muda mrefu akiwa anaombewa na Mtume na Nabii Hebron. |
Mtume na Nabii Hebron akiwa kwenye maombi ya kukagua waumini mmoja mmoja, kiti baada ya kiti kwa maombi kuhakikisha hakuna adui aliyeacha uovu ndani ya wana wa MUNGU. |
Kwa mawasiliano;
+ 255 759 610 820
+ 255 718 154 433
+ 255 718 916 864
+ 255 764 042 149
+ 255 718 154 433
+ 255 718 916 864
+ 255 764 042 149
Email:
maombi@prophethebron.org
publications@prophethebron.orgImeandaliwa na Priscus & Dorcas Macrine,
KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE.