HUYU NDIYE ALIYEMZAA MTUME NA NABII HEBRON KIROHO - MOSES KULOLA.
PROPHET HEBRON ALONGSIDE HIS DAUGHTER REBECCA AND WIFE NANCY.
Ndugu msomaji wa blogu hii, nakusalimu katika jina la BWANA YESU, ambaye ndiye BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE. Katika blogu hii, tutakuwa tunatoa habari za mafundisho ya YESU kama alivyokuwa akifanya ulimwenguni. Kwa sasa, kanisa limetekwa na shetani 98% ulimwenguni mwote, na macho ya rohoni ya kanisa yamekufa kabisa, na ROHO MTAKATIFU hayupo katika kanisa, ndio maana kondoo hawapati tena malisho, wametawanyika, na wanateseka.
Mafundisho mengi yanapatikana katika vitabu, cd's na dvd's kama zinavyoonekana pichani, na pia katika tovuti ya Nabii Hebron www.prophethebron.org. Pia, vipindi vya redio, Sunrise Radio 94.8FM kila Alhamisi saa tatu kamili usiku hadi saa nne usiku, na Radio 5 kila Alhamisi saa tatu kamili usiku hadi saa nne kamili usiku, kupata frequency kamili ya Radio 5 ingia katika website www.prophethebron.org.
Moses Kulola (Katikati), akiwa na Mtume na Nabii Hebron (kulia), mke wa Nabii Hebron (kushoto)
SHUHUDA NA MATUKIO YA WIKI HII - 25 November 2012
Shuhuda
Kijana huyu alikuwa na tatizo sugu la ugonjwa wa ngozi kwa
muda wa miaka kumi na nne (14), aliombewa hapa katika KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, na leo tarehe 25 November 2012, ameshuhudia kanisani katika ibada ya
jumapili (siku ya BWANA) amepona kama anavyoonekana kwenye picha.
MATUKIO
Mtume na Nabii Hebron akisisitiza jambo wakati wa mahubiri
katika ibada ya leo akifundisha tofauti kati ya nabii wa MUNGU Eliya (1WAFALME 18:21-40) na manabii wa Baali
(wa uongo), jinsi nabii Eliya alivyojenga madhabahu ya MUNGU iliyovunjika, na
akamuomba MUNGU wa Ibrahim, Isaka na Yakobo ashushe moto kutoka mbinguni
uteketeze dhabihu aliyomtengenezea MUNGU wa Ibrahim, Isaka na Yakobo, ili
kumdhihirisha MUNGU wa kweli ambaye yeye Eliya alimwabudu na kumtumikia baada
ya manabii wa Baali kushindwa kushusha moto toka kwa mungu wao waliyemtumainia
na kumtumikia. Na uwepo wa MUNGU ulidhihirishwa “live live” pale moto wa ELiya
uliposhuka kanisani, watu wakapata uponyaji, waliokuwa na vifungo walifunguliwa
kwa nguvu ya huo moto, na wenye mapepo yakawatoka. MUNGU wa Eliya akadhihirika
pia kwetu siku ya leo. Hakika jina la BWANA lihimidiwe milele, Amen.
Mama huyu amefunguliwa kifungo alichokuwa akitumikishwa na
nabii Baali, baada ya kumjua MUNGU wa kweli ambaye nabii Eliya alimwabudu na
kumtumikia. Na leo kupitia Mtume na
nabii Hebron ambaye moto wa Eliya ulikuwa ndani yake kuwaponya na kuwafungua
watu katika vifungo vyao, walivyotumikishwa na manabii wa Baali, hata mama huyu
aliponywa. Wengi wameponywa na kufunguliwa.
Mtume na Nabii Hebron alifafanua NENO na kusema kuwa, kwa
wakati huu watumishi wote waliokwenda kinyume na maagizo ya MUNGU ni manabii wa
mungu Baali, mungu mfu. Nabii Hebron akaendelea kwa kusema, mungu Baali haoni,
hazungumzi, hasikii, wala hana mikono inayosogea, ndiyo maana makanisani hakuna
majibu.
Siku hizi, waumini makanisani wamezungukwa na kujawa na
mateso, shida na kila taabu. Yote hayo yanatoka kwa mungu Baali. Pia nabii aliongeza kwa kusema “MUNGU ameniambia, katika
bara lote la Afrika, tofauti na watoto wadogo, watu wazima wanaofariki dunia
kila siku, kumi na tano tu (15) ndio wanaenda MBINGUNI.”
Ndugu msomaji wa blogu hii jiulize, unaishi kwa miaka
themanini (80) ulimwenguni, halafu mwisho wako unaingia jehanam kwa lusifa.
Haya makanisa na hizi dini zimekusaidiaje ili kuitengeneza njia yako ya kumwona
MUNGU siku yako ikifika?
+ 255 759 610 820
+ 255 759 253 593
+ 255 763 567 402
+ 255 764 042 149
+ 255 765 955 677
+ 255 759 253 593
+ 255 763 567 402
+ 255 764 042 149
+ 255 765 955 677
Email:
prophethebron@gmail.com